Nenda kwa yaliyomo

Dua ya ishirini na moja ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia

Dua ya ishirini na moja ya Sahifa Sajjadiyya: ni dua iliyopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), na ni dua inayo husiana na maombi yake aliyiokuwa akiomba katika nyakati za huzuni na unyonge. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anawasilisha na kufafanua dhana ya kitheolojia juu ya Tawhidu al-Af'ali (Umoja wa Mungu Kiutendendaji au Upweke wa Mungu katika matendo mbali mbali), akibainisha kuwa Mwenye Ezi Mungu ndiye Muathiri pekee na halisi katika ulimwengu huu wa uwepo. Kwa mujibu wa mtazamo wa Imamu Sajjad (a.s) ni kwamba; Rehema ya Mungu ndiyo kimbilio pekee la kweli kwa mwanadamu. Aidha, dua hii inamtaja Mwenye Ezi Mungu kuwa ndiyo njia au ndiyo eneo pekee lenye dhamana ya utulivu na mani kwa mwanadamu. Imamu huyu wa Nne anatoa wito wa kutokata tamaa kwa wanadamu, hata kama kutatokea ucheleweshaji katika kujibiwa dua zake. Imamu Sajjad (a.s) anasisitiza kwamba; utiifu kamilifu ndiyo mbinu pekee ya kufikia daraja za juu na kupata ukuruba na Mwenye Ezi Mungu.

Maelezo fafanuzi ya dua ya ishirini na moja ya Sahifa Sajjadiyya yanapatikana katika tafsiri mbali mbali chambuzi za kitabu Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwazo ni kama vile; Diyare Asheqan, kitabu kilichoandikwa na Hussein Ansarian, [1] na Shuhud wa Shenakht, kichoandikwa na Hassan Mamduhi Kermanshahi, vitabu ambavyo vinatoa ufafanuzi wake kwa lugha ya Farsi. Pia kuna vitabu kadhaa vilichambua dua hii kwa lugha ya Kiarabu, miongoni mwavyo ni; Riyadh al-Salikin, kitabu chambuzi cha Sahifa Sajjadiyya kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani kwa lugha ya Kiarabu.


Mafundisho ya Dua ya Ishini na Moja

Dua ya ishirini na moja katika Sahifa Sajjadiyya ni dua inayosemwa wakati wa huzuni kutokana na matatizo na matukio yatokeayo ulimwenguni, pia ni dua iombwayo wakati wa kukubwa na huzuni kutokana na dhambi mbali mbali, mitelezo pamoja na kughafilika. [1] Mafunzo ya dua hii ni kama ifuatavyo:

·  Mungu humwezesha yule asiye na uwezo.

• Ufafanuzi juu ya masomo yanayopatikana katika Tawhid ya upwekeshaji wa Mungu kwenye ngazi ya matendo.

• Kukosekana kwa usalama bila ya Mungu (rehema ya Mungu ndiyo eneo pekee la usalama kwa mwanadamu).

• Hakuna msaidizi wala mtetezi bila ya Mungu.

• Unyonge wa mwanadamu mbele ya hasira za Mwenye Ezi Mungu.

• Uwezo na nguvu hupatikana tu kupitia msaada wa Mungu.

• Kutowepo kimbilio jengine la kukimbilia zaidi ya kumrudia Mwenye Ezi Mungu.

• Mungu ndiye mwenye nguvu pekee za kuleta mageuzi ulimwenguni, na ndiye Bwana (Mlezi), Msaidizi na mwenye haki ya kudai madai yote maisha humu.

• Utawala wa Mungu juu ya ulimwengu.

• Vitu vyote viko chini ya uamuzi wa Mwenye Ezi Mungu.

• Mungu ndiye njia pekee ya kutimiza ndoto mbali mbali.

• Uamuzi wa Mungu kwa mja wake ni uadilifu kamili.

• Utii ni njia pekee ya kupata ukuruba wa Mwenye Ezi Mungu.

• Kukiri udhaifu wa mwanadamu (mbele ya Mola Wake).

• Ibada ndio njia ya kufikia yale yaliyoko kwa Mwenye Ezi Mungu.

• Kukiri udhaifu, unyonge, uduni na uhitaji (mele ya Mwenye Ezi Mungu).

• Kumtii Mwenye Ezi Mungu pake yake, ndio njia pekee ya kupata radhi na upendo wa Mwenye Ezi Mungu.

• Kutokata tamaa mele ya Mwenye Ezi Mungu, kutokana na kuchelewa au kutojibiwa kwa maombi fulani.

• Kutomsahau Mungu wakati wa kuneemeka kwa neema Zake.

• Kuomba taudiki ya kupata uwezo wa kujishughulisha na ibada za kimwili pamoja na roho.

• Siri ya kwa nini sifa zote njema zamlazimu Mwenye Eiz Mungu pekee.

• Kuomba moyo uwe tupu ili kufaraghika na mapenzi ya kumpenda Mungu na kumkumdhukuru Yeye Subhanahu wa Ta’ala.

• Kuomba moyo uwe na nguvu kupitia hamu na shauku (raghba) ya kumuelekea Mwenye Ezi Mungu.

• Kuomba moyo utulie katika maisha yote kwa mategemeo ya kumtegemea Mungu.

• Kuomba taufiki ya kupata radhi za Mungu katika kila jambo.

• Kuomba ulinzi dhidi ya watu wabaya na kupata ukuruba wa kuwa karibu na Mwenye Ezi Mungu na utukufu wake.

• Kuomba sifa kuhimidiwa na Mwenye Ezi Mungu katika hali zote.

• Kuomba uchaji Mungu uwe ndiyo akiba yetu kwa ajili ya maisha ya yanayofuata baada ya kifo.

• Kupata radhi za Mungu na kuepuka hasira yake kupitia umtiifu wa daima.

• Kuepukana na dhambi kwa kumcha Mungu.

• Kuomba urafiki na Mungu pamoja na waja wake wema.

• Kuomba amani ya moyo na kutotegemea viumbe vya Mungu.

• Kuomba neema ya kuwa na shauku na upendo kwa Mungu.

• Kuomba kuwa pamoja na Muhammad (s.a.w.w) pamoja na familia yake. [2]


Tafsiri Chambuzi za Dua ya Ishini na Moja

Ufafanuzi wa dua ya ishirini na moja unapatika katika tafsiri chambuzi mbalimbali za kitabu Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa tafsiri hizo chambuzi zinapatika katika vitabu vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiajemi (Kifarsi au Kipashia), kati ya vyo ni kama vile; Diyare Asheqan, [3] kilichoandikwa na Hussein Ansarian, Shuhud wa Shenakht, kilichoandikwa na Muhammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi, [4] na Sherh Sahife Sajjadiyye, kilichoandikwa na Sayyid Ahmad Fahri. [5]

Pia kuna waandishi kadhaa waliofafanua dua hii ya ishirini na moja ya Sahifa Sajjadiyya kwa lugha ya Kiarabu. Miongoni mwa vitabu vya tafsiri chambuzi za Sahifa Sajjadiyya vilivyochambua dua hii kwa lugha ya Kiarabu, ni kama vile; Riyadhu al-Salikin, cha Sayyid Ali Khan Madani, [6] Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyya, cha Muhammad Jawad Mughniyya, [7] Riyadhu al-Arifina, kilichoandikwa na Muhammad bin Muhammad Darabi, [8] na Afaqi al-Ruh, kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [9] Pia msamiati au istilahi za dua hii zimefafanuliwa katika baadhi ya vitabu kwa mtindo wa kiistilahi. Miongoni mwavyo kama vile; Ta'liqat Ala al-Sahifa al-Sajjadiyya, cha Fayd Kashani [10] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, kilichoandikwa na Izzu al-Din al-Jaza'iri. [11]


Matini ya Dua na Tafsiri Yake

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِذَا حَزَنَهُ أَمْرٌ وَ أَهَمَّتْهُ الْخَطَايَا

Na (ifuatayo) ilikuwa miongoni mwa dua zake (rehema za Mungu ziwe juu yake) anayoomba pale alipohuzunishwa na jambo fulani na akalemewa na makosa:


اللَّهُمَّ يَا كَافِيَ الْفَرْدِ الضَّعِيفِ، وَ وَاقِيَ الْأَمْرِ الَْمخُوفِ، أَفْرَدَتْنِي الْخَطَايَا فَلَا صَاحِبَ مَعِي، وَ ضَعُفْتُ عَنْ غَضَبِكَ فَلَا مُؤَيِّدَ لِي، وَ أَشْرَفْتُ عَلَى خَوْفِ لِقَائِكَ فَلَا مُسَكِّنَ لِرَوْعَتِي

Ee Mungu wungu! Ewe Mtoshelezaji wa yule kiumbe duni (aliyejitengake), na Mkingaji (Mwepushaji) wa tukio linalotisha. Maasi yamenisababishia upweke, hivyo sina wa kuniunga mkono (sina rafiki aliye pamoja nami). Nami sina uwezo wa kustahimili ghadhabu zako, (kwa mantiki hiyo) mimi sina wa kuniunga mkono. Na niko ukingoni mwa khofu ya makutano nawe, hivyo basi hakuna cha kuipoza hofu yangu.


وَ مَنْ يُؤْمِنُنِي مِنْكَ وَ أَنْتَ أَخَفْتَنِي، وَ مَنْ يُسَاعِدُنِي وَ أَنْتَ أَفْرَدْتَنِي، وَ مَنْ يُقَوِّينِي وَ أَنْتَ أَضْعَفْتَنِي

Na ni nani atakayenidhaminia usalama dhidi yako, ilhali Wewe umenitia khofu? Na ni nani atakayenipa usaidizi, ilhali Wewe umenitenga? Na ni nani atakayeniimarisha, ilhali Wewe umenidhoofisha?


لَا يُجِيرُ، يَا إِلَهِي، إِلَّا رَبٌّ عَلَى مَرْبُوبٍ، وَ لَا يُؤْمِنُ إِلَّا غَالِبٌ عَلَى مَغْلُوبٍ، وَ لَا يُعِينُ إِلَّا طَالِبٌ عَلَى مَطْلُوبٍ.

Ee Mola wangu! Hakuna anayetoa hifadhi isipokuwa Bwana kwa anayemilikiwa, na hakuna anayetoa hifadhi isipokuwa mshindi juu ya aliyeshindwa, na hakuna anayetoa msaada isipokuwa msasakaji kwa anayesakwa.


وَ بِيَدِكَ، يَا إِلَهِي. جَمِيعُ ذَلِكَ السَّبَبِ، وَ إِلَيْكَ الْمَفَرُّ وَ الْمَهْرَبُ، فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ أَجِرْ هَرَبِي، وَ أَنْجِحْ مَطْلَبِي.

Na yote hayo, Ee Mola wangu Mlezi, yako mikononi mwako, na kwako Wewe ndio kimbilio na maficho (ya kuepukana na hatari). Basi, mrehemu Muhammad na Aali zake, na unihifadhi katika kimbio langu hili, na uikubalie haja yangu (na ifaulishe hayangu).


اللَّهُمَّ إِنَّكَ إِنْ صَرَفْتَ عَنِّي وَجْهَكَ الْكَرِيمَ أَوْ مَنَعْتَنِي فَضْلَكَ الْجَسِيمَ أَوْ حَظَرْتَ عَلَيَّ رِزْقَكَ أَوْ قَطَعْتَ عَنِّي سَبَبَكَ لَمْ أَجِدِ السَّبِيلَ إِلَى شَيْءٍ مِنْ أَمَلِي غَيْرَكَ، وَ لَمْ أَقْدِرْ ‌ عَلَى مَا عِنْدَكَ بِمَعُونَةِ سِوَاكَ، فَاِنِّي عَبْدُكَ وَ فِي قَبْضَتِكَ، نَاصِيَتِي بِيَدِكَ.

Ee Mulo wangu, hakika iwapo utanigeuzia uso (iwapo utanitenga na dhati Yako tukufu), au ukaninyima neema Zako adhimu, au ukanizuilia riziki zako, au ukanizuilia na njia ya uwezeshaji Wako, katu katika hali hiyo sitaweza kupata njia ya kufikia matarajio yangu yoyote yale nje yako (bila Wewe). Na katu sitaweza kupata vilivyoko kwako kwa msaada wa mwengine asiyekuwa Wewe, bila shaka mimi ni mja wako na nimo katika mamlaka Yako, hatima yangu imo mikononi Mwako.


لَا أَمْرَ لِي مَعَ أَمْرِكَ، مَاضٍ فِيَّ حُكْمُكَ، عَدْلٌ فِيَّ قَضَاؤُكَ، وَ لَا قُوَّةَ لِي عَلَى الْخُرُوجِ مِنْ سُلْطَانِكَ، وَ لَا أَسْتَطِيعُ مُجَاوَزَةَ قُدْرَتِكَ، وَ لَا أَسْتَمِيلُ هَوَاكَ، وَ لَا أَبْلُغُ رِضَاكَ، وَ لَا أَنَالُ مَا عِنْدَكَ إِلَّا بِطَاعَتِكَ وَ بِفَضْلِ رَحْمَتِكَ.

Sina amri yoyote ile mbele ya amri yako; hukumu Yako yapita juu yangu bila pingamizi; uamuzi Wako kwangu ni wa haki. Sina nguvu za kutoka katika mamlaka Yako, wala siwezi kuukiuka uwezo Wako, na wala sina uwezo wa kujivutia upende Wako, na sina uwezo wa kufikia radhi Zako, wala siwezi kupata kilichoko kwako isipokuwa kwa kukutii na kwa kupitia fadhila za rehema Zako.

إِلَهِي أَصْبَحْتُ وَ أَمْسَيْتُ عَبْداً دَاخِراً لَكَ، لَا أَمْلِكُ لِنَفْسِي نَفْعاً وَ لَا ضَرّاً إِلَّا بِكَ، أَشْهَدُ بِذَلِكَ عَلَى نَفْسِي، وَ أَعْتَرِفُ بِضَعْفِ قُوَّتِي وَ قِلَّةِ حِيلَتِي، فَأَنْجِزْ لِي مَا وَعَدْتَنِي، وَ تَمِّمْ لِي مَا آتَيْتَنِي، فَإِنِّي عَبْدُكَ الْمِسْكِينُ الْمُسْتَكِينُ الضَّعِيفُ الضَّرِيرُ الْحَقِيرُ الْمَهِينُ الْفَقِيرُ الْخَائِفُ الْمُسْتَجِيرُ.

Ee Mungu! Nimepitisha mchana pamoja na usiku hali nikiwa ni mja wako duni asiye na hadhi; sina mamlaka ya kujipatia manufaa au kujikinga na madhara yoyote yale isipokuwa kwa uwezesho wako. Ninathibitisha kile nilichokitamka kunihusiana na nafsi yangu; ninakiri uhafifu wa nguvu zangu na upungufu wa busara zangu. Hivyo basi, tekeleza ahadi yako kwangu; na kitimiza kile ulichonikirimu; kwani mimi ni mja wako mhitaji, duni, hafifu, mwenye dhaifu, mnyonge (mwenye matatizo), asiye na thamani (asiye na kima), fukara, mwenye khofu, na mwenye kutafuta himaya yako.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ لَا تَجْعَلْنِي نَاسِياً لِذِكْرِكَ فِيما أَوْلَيْتَنِي، وَ لَا غَافِلًا لِإِحْسَانِكَ فِيما أَبْلَيْتَنِي، وَ لَا آيِساً مِنْ إِجَابَتِكَ لِي وَ إِنْ أَبْطَأَتْ عَنِّي، فِي سَرَّاءَ كُنْتُ أَوْ ضَرَّاءَ، أَوْ شِدَّةٍ أَوْ رَخَاءٍ، أَوْ عَافِيَةٍ أَوْ بَلَاءٍ، أَوْ بُؤْسٍ أَوْ نَعْمَاءَ، أَوْ جِدَةٍ أَوْ لَأْوَاءَ، أَوْ فَقْرٍ أَوْ غِنًى.

Ewe Mola wangu, zishushie rehema na amani Muhammad na Aali zake. Na usinijaalie kuwa ni mwenye kusahau utajo Wako katika (shukurani za kushukuru) yale uliyonitunukia; wala (usinijaalie kuwa) kuwa ni mwenye kughafilika juu ya hisani Zako katika yale uliyonitahini nayo; wala mwenye (usinifanye kuwa ni mwenye) kukata tamaa ya majibu Yako kwangu, hata kama yatachelewa. Iwe nipo katika hali ya furaha au dhiki, au katika hali ya ukunjufu au ya dhiki, ya siha au maradhi, ya shida au neema, ya wasaa au ufinyu, au iwe ni katika hali ya ufukara au utajiri.


اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْ ثَنَائِي عَلَيْكَ، وَ مَدْحِي إِيَّاكَ، وَ حَمْدِي لَكَ فِي كُلِّ حَالَاتِي حَتَّى لَا أَفْرَحَ بِمَا آتَيْتَنِي مِنَ الدُّنْيَا، وَ لَا أَحْزَنَ عَلَى مَا مَنَعْتَنِي فِيهَا، وَ أَشْعِرْ قَلْبِي تَقْوَاكَ، وَ اسْتَعْمِلْ بَدَنِي فِيما تَقْبَلُهُ مِنِّي، وَ اشْغَلْ بِطَاعَتِكَ نَفْسِي عَنْ كُلِّ مَا يَرِدُ عَلَيَّ حَتَّى لَا اُحِبَّ شَيْئاً مِنْ سُخْطِكَ، وَ لَا أَسْخَطَ شَيْئاً مِنْ رِضَاكَ.

Ewe Mola! Mshushie rehema na amani Muhammad na Aali zake. Na jaalia tungo za sifa zangu zangu ziwe kwa ajili Yako, na upambaji wangu uwe kwa ajili ya kukupamba Wewe, na shukurani zangu ziwe kwako katika hali zangu zote, ili nisifurahikie yale ya kidunia uliyonipatia, na wala nisihuzunikie yale uliyonizuilia duniani humu. Na uufundishe (au) uufungamanishe moyo wangu na takua Yako, na uutumikishe mwili wangu katika yale unayoafiki kutoka kwangu. Na iajiri nafsi yangu kwe kazi ya twaa Yako dhidi ya yote yale yanayonikabili, ili nisipende chochote kile kilisababisha ghadhabu Zako, na wala nisichukie chochote kile kilichomo ndani ya ridhaa Yako.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ فَرِّغْ قَلْبِي لَِمحَبَّتِكَ، وَ اشْغَلْهُ بِذِكْرِكَ، وَ انْعَشْهُ بِخَوْفِكَ وَ بِالْوَجَلِ مِنْكَ، وَ قَوِّهِ بِالرَّغْبَةِ إِلَيْكَ، وَ أَمِلْهُ إِلَى طَاعَتِكَ، وَ أَجْرِ بِهِ فِي أَحَبِّ السُّبُلِ إِلَيْكَ، وَ ذَلِّلْهُ بِالرَّغْبَةِ فِيما عِنْدَكَ أَيَّامَ حَيَاتِي كُلِّهَا.

Ewe Mola wangu! Mshushie rehema na amani Muhammad pamoja na Aali zake. Na utenge moyo wangu kwa ajili ya mahaba Yako tu, na uushughulishe (moyo wangu huu) na dhikri Yako. Uimarishe (moyo huu) kupitia khofu Yako na kupitia woga utokao Kwako. Uutie nguvu kwa shauku ya kukutamani, na uelemeze kwenye utiifu wako. Uuelekeze kwenye njia uzipendazo zaidi miongoni mwa zile njia zielekazo Kwako, na uutiishe kwa raghba ya kupata vilivyoko Kwako, katika kipindi chote cha uhai wangu.


وَ اجْعَلْ تَقْوَاكَ مِنَ الدُّنْيَا زَادِي، وَ إِلَى رَحْمَتِكَ رِحْلَتِي، وَ فِي مَرْضَاتِكَ مَدْخَلِي، وَ اجْعَلْ فِي جَنَّتِكَ مَثْوَايَ، وَ هَبْ لِي قُوَّةً أَحْتَمِلُ بِهَا جَمِيعَ مَرْضَاتِكَ، وَ اجْعَلْ فِرَارِيَ إِلَيْكَ، وَ رَغْبَتِي فِيما عِنْدَكَ، وَ أَلْبِسْ قَلْبِيَ الْوَحْشَةَ مِنْ شِرَارِ خَلْقِكَ، وَ هَبْ لِيَ الْأُنْسَ بِكَ وَ بِأَوْلِيَائِكَ وَ أَهْلِ طَاعَتِكَ.

Na jaalia uchamungu wangu Kwako uwe ndiyo zawadi (maandalizi) yangu ya hapa duniani (kwa ajili ya Akhera), na safari yangu iwe ni kuelekea kwenye rehema Zako, na kiingilio changu kiwe ni kwenye maridhawa Yako. Na jaalia makao yangu ya kudumu yawe ni katika Janna Yako. Na unihibie (unizawadie) nguvu nitakayoweza kuhimili kwayo mambo yote yenye ridhaa Yako. Jaalia makimbilio yangu yawe ni Kwako, na raghba yangu iwe katika vile vilivyoko Kwako. Na uvishe moyo wangu hofu (hisia au hamu ya kutengana) na viumbe Wako waovu, na unipe utulivu utokanao na kufaraghika Nawe, pamoja na wapenzi wako, na wale wanaoshiokamana na taa (utiifu) Yako.

وَ لَا تَجْعَلْ لِفَاجِرٍ وَ لَا كَافِرٍ عَلَيَّ مِنَّةً، وَ لَا لَهُ عِنْدِي يَداً، وَ لَا بِي إِلَيْهِمْ حَاجَةً، بَلِ اجْعَلْ سُكُونَ قَلْبِي وَ أُنْسَ نَفْسِي وَ اسْتِغْنَائِي وَ كِفَايَتِي بِكَ وَ بِخِيَارِ خَلْقِكَ.

Wala usimjaalie muovu wala kafiri yeyote yule kuwa na fursa ya kunisimbulia au fursa ya kunifadhili. Na wala usinifanye niwategemee katika haja zangu. Bali, jaalia utulivu wa moyo wangu, faraja ya roho yangu, kujitosheleza kwangu, na utimilifu wa mambo yangu, (vyote) viwe chini ya jukumu Lako (au viwe mkononi mwako) pamoja na waja Wako wema.

اللَّهُمَّ صَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْنِي لَهُمْ قَرِيناً، وَ اجْعَلْنِي لَهُمْ نَصِيراً، وَ امْنُنْ عَلَيَّ بِشَوْقٍ إِلَيْكَ، وَ بِالْعَمَلِ لَكَ بِمَا تُحِبُّ وَ تَرْضَى، إِنَّكَ عَلَى كُلِّ شَيْ‌ءٍ قَدِيرٌ، وَ ذَلِكَ عَلَيْكَ يَسِيرٌ.

Ewe Mola wangu! Mshushie rehema na amani Muhammad pamoja na Aali zake. Na unijaalie niwe karibu nao, na unifanye niwe msaidizi wao. Na unipe neema ya kuwa na shauku Kwako, pamoja na taufiki kuwa na shauku ya kutenda kwa ajili Yako (miongoni mwa) yale unayoyapenda na kuyaridhia. Hakika Wewe ni Muweza juu ya kila kitu, na jambo hilo ni rahisi mno Kwako.