Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Tatu ya kitabu cha Sahiifatu Al-Sajjaadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Tatu ya kitabu cha Sahiifatu Al-Sajjadiyyah
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, iliyoandikwa na Abdullah Yazdi, Sha'ban 1102 AH.

Mtoaji / MwandishiImamu Sajjad (a.s)
LughaKiarabu
Msimulizi / MpokeziMutawakkil ibn Harun
MadaKuelezea sifa za Malaika, nafasi zao mbele ya Mola wao, makundi yao, pamoja maombi ya kuwatakia rehema na amani Malaika hao.
ChanzoSahifa Sajjadiyah
Tafsiri kwa Lugha yaKifarsi

Dua ya Tatu ya kitabu cha Sahiifatu Al-Sajjaadiyyah (Kiarabu: الدعاء الثالث من الصحيفة السجادية) ni moja kati ya dua adhimu iliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Muktadha wa dua hii unahusiana na uchambuzi wa sifa pekee walizopambika Malaika wa Mwenyezi Mungu, wakiwemo: Wahamili wa Arshi (wabebaji wa kiti cha enzi cha Mwenye Ezi Mungu) pamoja na Malaika wote walio katika ngazi mbalimbali huko mbinguni. Imamu Sajjad (a.s) anazungumzia sifa kadhaa za Malaika wa Mungu ikiwa ni pamoja na; Kutochoka kwao katika kumtakasa Mola wao, upole na unyeyekevu wao mbele ya Mola wao, pamoja na kushikamana na amri za Mola bila upinzani wa aina yoyote ile katika uwajibikaji wao.

Dua ya Tatu ya Sahiifatu Sajjadiyyah, inapatikana katika vitabu mbali mbali vilivyo andikwa kwa ajili ya kutoa tafasiri na uchambuzi sahihi wa kitabu hicho. Miongoni mwa tafsiri zilizotolewa kuhusiana na kitabu hicho ni pamoja na: Diyaare-‘Aashiqaan (Nyumba za Wapenzi), kilichoandikwa kwa Kifarsi na Hujjatul-Islam Hussein Ansaariyaan na Riyaad al-Saalihiin fi Sharhi Sahifati Sayyidi al-Saajidiin, kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na Sayyid ‘Ali Khan al-Madani.

Mafunzo Yaliomo katika Dua ya Tatu

Mada na maudhui kuu ya Dua ya Tatu ya kitabu Sahifatu Sajjadiyya imejikita katika kuelezea sifa za Malaika wa Mwenye Ezi Mungu, nafasi zao mbele ya Mola wao, makundi yao, pamoja maombi ya kuwatakia rehema na amani Malaika hao. Mafunzo yaliyomo katika dua hii yanatufunza yanatufunza kwamba:

  • Malaika wanaobeba Arshi ya Mwenye Ezi Mungi hawachoki wala kudhoofiki katika kumsifu, kumtakasa, na kumuabudu Mwenye Ezi Mungu.
  • Malaika wa Mungu hawafanyi uzembe katika kutekeleza amri za Mola wao, na wala hawana sifa ya kusahau.
  • Siku ya Kiyama, watu watafufuliwa kupitia sauti ya tarumbeta ya Israfil.
  • Mikaili ni Maika mwenye nafasi tukufu mbele ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Jibril ni mwaminifu wa Wahyi na ni mmoja wa Malaika wa karibu kabisa na Mwenye Ezi Mungu.
  • Ruhu Al-Amin ni kiongozi wa Malaika waliopo katika hifadhi ya utukufu wa ufalme wa Mungu.
  • Malaika hawana hisia za matamanio wala hawaghafiliki.
  • Malaika ni watiifu na wanyenyekevu mbele ya utukufu wa Mungu, na ni wenye kukiri mapungufu yao katika kumwabudu Mola wao.
  • Malaika ndio wawashushaji wa Wahyi kwa Mitume wa Mwenye Ezi Mungu.
  • Malaika ni wenye kuuwasalimu watu wa Peponi.
  • Malaika wa Mungu wamegawika katika Makundi mbalimbali, wakiwemo: Malaika maalumu wa Mungu, Malaika waliopangwa kwenye pembe za mbingu (visusi vya mbingu), washika hifadhi ya hazina ya mvua, waongozaji (wasukumaji) mawingu, walinzi au wasimamizi wa upepo, waangalizi wa milima, waandishi wa matendo ya watu, Malaika wa Mauti na wasaidizi wake, Nakir na Munkar, Malaika wa mitihani ya kaburi (Ruman), wanaoizunguka Bayt al-Ma’mur, Malaika na walinzi wa Jahannam, Ridhwan na wasimamizi wa Pepo, Malaika wengine wa motoni ambao hawakutawajua kwa majina na wala hatujui majukumu yao, pamoja na wale wanaoandamana na mwanadamu (Saa'iq na Shahid).
  • Sala na salamu za Mungu ziwe juu ya Malaika hawa na ziwe ni nyongeza ya usafi na heshima yao.[1]

Tafisiri za Dua

Kuna tafsiri kadhaa zilizokuja kuichambua Dua ya hii ya tatu ilioko katika kitabu Sahifatu Sajjadiyya. Miongoni mwa fafanuzi zilizokuja kufafanua zinapatana katika lugha ya Kifarsi. Vitabu vya Kifarsi vyenye tafsiri ya dua hii ni pamoja na; Diyāre-Āshiqān, kilichoandikwa na Hussein Ansarian,[2] Shuhūd wa Shenaakht, cha Muhammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi,[3] Asrāre-Khāmushān, cha Muhammad Taqi Khalaji,[4] na Sharhe wa Tarjume ya Sahife Sajjadiyye cha Sayyid Ahmad Fahri.[5]

Aidha, dua hii imeelezewa na kuchambuliwa kwa undani kabisa katika vitabu vilivyo andikwa kwa lugha ya Kiarabu, ikiwa ni pamoja na; Riyāḍ al-Sālikīn fī Sharḥ Ṣaḥīfa Sayyidifatu al-Sājidīn, cha Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fī Dhilāli al-Ṣaḥīfa al-Sajjādiyya, cha Muhammad Jawād Mughniyah,[7] Riyāḍhu al-‘Ārifīn, cha Muhammad bin Muhammad Darabi,[8] pamoja na Āfāq al-Rūḥ, cha Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Vilevile, orodha ya misamiati na maneno ya dua hii yamefafanuliwa vya kutosha katika vitabu vya fasihi ya lugha ya Kiarabu, kama vile; Ta‘liqāt ‘ala al-Ṣaḥīfati al-Sajjādiyya kilichoandikwa na Faidhu Kashani.[10]

Matini ya Dua na Tafsiri Yake

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الصَّلَاةِ عَلَي حَمَلَةِ الْعَرْشِ وَ كُلِّ مَلَكٍ مُقَرَّبٍ

اللَّهُمَّ وَ حَمَلَةُ عَرْشِكَ الَّذِينَ لَا يَفْتُرُونَ مِنْ تَسْبِيحِكَ، وَ لَا يَسْأَمُونَ مِنْ تَقْدِيسِكَ، وَ لَا يَسْتَحْسِرُونَ مِنْ عِبَادَتِكَ، وَ لَا يُؤْثِرُونَ التَّقْصِيرَ عَلَى الْجِدِّ فِي أَمْرِكَ، وَ لَا يَغْفُلُونَ عَنِ الْوَلَهِ إِلَيْكَ

وَ إِسْرَافِيلُ صَاحِبُ الصُّورِ، الشَّاخِصُ الَّذِي يَنْتَظِرُ مِنْكَ الْإِذْنَ، وَ حُلُولَ الْأَمْرِ، فَيُنَبِّهُ بِالنَّفْخَةِ صَرْعَى رَهَائِنِ الْقُبُورِ.

وَ مِيكَائِيلُ ذُو الْجَاهِ عِنْدَكَ، وَ الْمَكَانِ الرَّفِيعِ مِنْ طَاعَتِكَ.

وَ جِبْرِيلُ الْأَمِينُ عَلَى وَحْيِكَ، الْمُطَاعُ فِي أَهْلِ سَمَاوَاتِكَ، الْمَكِينُ لَدَيْكَ، الْمُقَرَّبُ عِنْدَكَ

وَ الرُّوحُ الَّذِي هُوَ عَلَى مَلَائِكَةِ الْحُجُبِ.

وَ الرُّوحُ الَّذِي هُوَ مِنْ أَمْرِكَ، فَصَلِّ عَلَيْهِمْ، وَ عَلَى الْمَلَائِكَةِ الَّذِينَ مِنْ دُونِهِمْ مِنْ سُكَّانِ سَمَاوَاتِكَ، وَ أَهْلِ الْأَمَانَةِ عَلَى رِسَالاتِكَ

وَ الَّذِينَ لَا تَدْخُلُهُمْ سَأْمَةٌ مِنْ دُؤُوبٍ، وَ لَا إِعْيَاءٌ مِنْ لُغُوبٍ وَ لَا فُتُورٌ، وَ لَا تَشْغَلُهُمْ عَنْ تَسْبِيحِكَ الشَّهَوَاتُ، وَ لَا يَقْطَعُهُمْ عَنْ تَعْظِيمِكَ سَهْوُ الْغَفَلَاتِ.

وَ الَّذِينَ يَقُولُونَ إِذَا نَظَرُوا إِلَى جَهَنَّمَ تَزْفِرُ عَلَى أَهْلِ مَعْصِيَتِكَ سُبْحَانَكَ مَا عَبَدْنَاكَ حَقَّ عِبَادَتِكَ.

فَصَلِّ عَلَيْهِمْ وَ عَلَى الرَّوْحَانِيِّينَ مِنْ مَلَائِكَتِكَ، وَ أَهْلِ الزُّلْفَةِ عِنْدَكَ، وَ حُمَّالِ الْغَيْبِ إِلَى رُسُلِكَ، وَ الْمُؤْتَمَنينَ عَلَى وَحْيِكَ

وَ قَبَائِلِ الْمَلَائِكَةِ الَّذِينَ اخْتَصَصْتَهُمْ لِنَفْسِكَ، وَ أَغْنَيْتَهُمْ عَنِ الطَّعَامِ وَ الشَّرَابِ بِتَقْدِيسِكَ، وَ أَسْكَنْتَهُمْ بُطُونَ أَطْبَاقِ سَمَاوَاتِكَ

وَ الَّذِينَ عَلَى أَرْجَائِهَا إِذَا نَزَلَ الْأَمْرُ بِتَمامِ وَعْدِكَ

وَ خُزَّانِ الْمَطَرِ وَ زَوَاجِرِ السَّحَابِ

وَ الَّذِي بِصَوْتِ زَجْرِهِ يُسْمَعُ زَجَلُ الرُّعُودِ، وَ إِذَا سَبَحَتْ بِهِ حَفِيفَةُ السَّحَابِ الْتمَعَتْ صَوَاعِقُ الْبُرُوقِ.

وَ مُشَيِّعِي الثَّلْجِ وَ الْبَرَدِ، وَ الْهَابِطِينَ مَعَ قَطْرِ الْمَطَرِ إِذَا نَزَلَ، وَ الْقُوَّامِ عَلَى خَزَائِنِ الرِّيَاحِ، وَ الْمُوَكَّلِينَ بِالْجِبَالِ فَلَا تَزُولُ

وَ الَّذِينَ عَرَّفْتَهُمْ مَثَاقِيلَ الْمِيَاهِ، وَ كَيْلَ مَا تَحْوِيهِ لَوَاعِجُ الْأَمْطَارِ وَ عَوَالِجُهَا

وَ رُسُلِكَ مِنَ الْمَلَائِكَةِ إِلَى أَهْلِ الْأَرْضِ بِمَكْرُوهِ مَا يَنْزِلُ مِنَ الْبَلَاءِ وَ مَحْبُوبِ الرَّخَاءِ

وَ السَّفَرَةِ الْكِرَامِ الْبَرَرَةِ، وَ الْحَفَظَةِ الْكِرَامِ الْكَاتِبِينَ، وَ مَلَكِ الْمَوْتِ وَ أَعْوَانِهِ، وَ مُنْكَرٍ وَ نَكِيرٍ، وَ رُومَانَ فَتَّانِ الْقُبُورِ، وَ الطَّائِفِينَ بِالْبَيْتِ الْمَعْمُورِ، وَ مَالِكٍ، وَ الْخَزَنَةِ، وَ رِضْوَانَ، وَ سَدَنَةِ الْجِنَانِ.

وَ الَّذِينَ «لَا يَعْصُونَ اللَّهَ مَا أَمَرَهُمْ، وَ يَفْعَلُونَ مَا يُؤْمَرُونَ، وَ الَّذِينَ يَقُولُونَ : «سَلَامٌ عَلَيْكُمْ بِمَا صَبَرْتُمْ، فَنِعْمَ عُقْبَى الدّارِ

وَ الزَّبَانِيَةِ الَّذِينَ إِذَا قِيلَ لَهُمْ «خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ» ابْتَدَرُوهُ سِرَاعاً، وَ لَمْ يُنْظِرُوهُ.

وَ مَنْ أَوْهَمْنَا ذِكْرَهُ، وَ لَمْ نَعْلَمْ مَكَانَهُ مِنْكَ، و بِأَيِّ أَمْرٍ وَكَّلْتَهُ.

وَ سُكَّانِ الْهَوَاءِ وَ الْأَرْضِ وَ الْمَاءِ وَ مَنْ مِنْهُمْ عَلَى الْخَلْقِ

فَصَلِّ عَلَيْهِمْ يَوْمَ يَأْتِي «كُلُّ نَفْسٍ مَعَهَا سَائِقٌ وَ شَهِيدٌ» وَ صَلِّ عَلَيْهِمْ صَلَاةً تَزِيدُهُمْ كَرَامَةً عَلَى كَرَامَتِهِمْ وَ طَهَارَةً عَلَى طَهَارَتِهِمْ

اللَّهُمَّ وَ إِذَا صَلَّيْتَ عَلَى مَلَائِكَتِكَ وَ رُسُلِكَ وَ بَلَّغْتَهُمْ صَلَاتَنَا عَلَيْهِمْ، فَصَلِّ عَلَيْنَا بِمَا فَتَحْتَ لَنَا مِنْ حُسْنِ الْقَوْلِ فِيهِمْ، إِنَّكَ جَوَادٌ كَرِيمٌ.

Na miongoni mwa dua zake – amani iwe juu yake – ilikuwa ni dua ya kuwatakia rehema na mamani Wachukuzi wa Arshi (kiti cha enzi cha Mungu) pamoja na kila Malaika aliye karibu zaidi na Mwenye Ezi Mungu.

Ewe Mola! (Wabariki) wachukuzi wa Arshi yako—ambao hawachoki kukusabihi (kukutakasa na kukuadhimu), wala hawapotezi hamasa ya kukutakasa, wala hawachoki katika amali yao ya kukuabudu, wala hawapendelei uzembe dhidi ya bidii katika kutekeleza amri zako, na wala hawasahau kuonesha mapenzi yao ya kina kwako.

Na (mbariki) Israfili, mshika (mmiliki) baragumu, ambaye macho yake yanaangaza akisubiri idhini kutoka kwako na kuwadia kwa amri Yako; hapo atawazindua waliolala makaburini kwa mlio wa baragumu hilo, ambao wamelala wakiwa ni watekwa wa vifungo vya makaburi.

Na (pia mbariki) Mikaili, mwenye cheo kikubwa mbele Yako, na (mwenye) nafasi adhimu aliyotokana na utiifu wake kwako.

Na (mbariki) Jibrilu mwaminifu juu ya ufunuo Wako, anayetiiwa na walioko mbingu Kwako, mwenye nafasi thabiti mbele Yako, mwenye ukaribu nawe (kwa ukaribu wa kipekee kabisa).

Na (umbariki) Roho ambaye ni msimamizi wa Malaika wa Mapazia la kizuizi (pazia la siri za Mwenye Ezi Mungu).

Na (pia mbariki) Roho ambaye anatokana na amri yako (anatoka na neno lako); mshushie baraka zako juu yake, na juu ya Malaika walio chini yake, (ambao ni) wakaazi wa mbingu zako, na wale wahisika wa dhamana za ujumbe wako kwa kiuaminifu.

Na (wambariki) wale (Malaika) ambao bidii zao hazikatiwishi na uchovu wa aina yeyote ile, wala hawashikwi na udhaifu wala mnyong’onyeo na ulegevu; na hawazuiliwi na matamanio wala hawapatwi na hali ya kughafilika katika kulitakasa Jina Lako Tukufu, wala hawasimamishi kazi kukuadhimisha kutokana na kusahau kwa akili (zao).

Na (wambariki) ni wale ambao wanapouona Moto wa Jahannamu ikivuma kwa ghadhabu dhidi ya waliokuasi husema: ‘Utakatifu ni Wako, Ee Mola! Hakika hatukukuabudu kwa kikweli kama inavyostahiki Ibada Yako (kutendwa).

Basi wateremshie rehma (na baraka) zako wao, pamoja na Malaika (wengineo ambao ni) wenye maumbile ya kirohoni (wasio na miili) miongoni mwa Malaika Wako, na wale wenye cheo cha ukaribu Naye, na wachukuzi wa siri (ujumbe) wa ghaibu kwa ajili Mitume Wako, na waliokabidhiwa amana za Wahyi Wako.

Na (teremshie rehma na baraka zako) juu ya makundi ya Malaika uliowateua (na kuwaweka makhususi) kwa ajili ya Nafsi Yako, ukawatosheleza (na kuwafanya) wasihitajie chakula wala kinywaji kwa sababu ya utakaso Wako, na ukawaweka katika tabaka za ndani za mbingu Zako.

Na (wateremshie rehma na baraka zako) wale walioko pembezoni mwake, wakati wa kushuka amri Yako kwa ukamili wa ahadi yako (wakati wa kushuka ahadi yako kikamilifu kama ulivyo ahidi).

Na (wateremshie rehma na baraka zako) wahifadhi wa hazina za mvua na waongozaji wa mawingu (waliowekwa kwa amri Yako).

Na (mteremshie rehma na baraka zako) yule ambaye sauti yake ya kuonya (ya kuyaongoza mawingu) hupelekea kusikika sauti ya milipuko ya radi, (sauti ambayo pia husikika) pale mawingu yanaposokotana kwa kasi kupitia amri yake, kisha (mawingu hayo) kung'aa kupitia umeme wa radi.

Na (wateremshie rehma na baraka zako) wale wanaoisindikiza theluji na mvua ya mawe, na wanaoshuka pamoja na matone ya mvua wakati yanapoteremka, na (wale) walinzi wa hazina za Pepo, na waliowekwa kusimamia milima ili isitikisike wala kuondoka mahali pake.

Pia (wateremshie rehma na baraka zako) wale uliowafunza na kuwajuza vipimo vya uzani wa maji, na vipimo cha yale yote yanayobebwa na maforiko na miminiko ya mvua.

Na (wateremshie rehma na baraka zako) Mitume Wako miongoni mwa Malaika wanaotumwa kwa watu wa ardhini (ili kufikisha) yale yasiyopendeza kwa ajili ya majaribio (mitihani), na yale yanayopendeza yenye neema na ustawi.

Pia (rehema na baraka Zako) ziwe juu ya mabalozi (wawakilishi Wako) wema (Kirama Kaatibina), ambao ni waandishi wanaohifadhi (wanaosajili na kurikodi) matendo ya wanadamu; na pia ( rehema na baraka Zako) ziwashukie Malaika wa Mauti na wasaidizi wake; Munkar na Nakir; Ruman, mtahini wa walio makaburini; na ( rehema na baraka Zako) ziwe juu ya wanaozunguka Baitu al-Ma’mur; na kwa Malik (msimamizi wa Moto) pamoja na walinzi wa Jahannam; na (rehema na baraka Zako) zimuendee Ridwan (Malaika) na watumishi wa Peponi.

Na (rehema na baraka Zako) ziwashukiewale wasiomuasi Mwenye Ezi Mungu katika yale Aliyowaamrisha, bali hutekeleza ipasavyo yote wanayoamrishwa. Na wale wasesemao (katika kuwakaribisha watu wa Peponi): “Amani iwe juu yenu kwa sababu ya subira yenu; basi makazi haya ya milele ni malipo bora mno.

Na Malaika wakali wa adhabu – Mazabania – ambao pale wanapoamrishwa kwa kuambiwa: “Mkamate! Mfungeni kwa pingu! Kisha mtupeni motoni mwa Jahannam!” — hujitokeza kwa haraka bila kuchelewa hata kidogo, na wala hawampi fursa hata ndogo mhukumiwa wao.

Na (mshushie rehema na umbariki) yule ambaye tumemsahau kumtaja, na wala hatujui ana nafasi yake mbele Yako, wala hatufahamu amemuwakilishwa kufanya jambo gani (wala hatutambui kazi yake).

Pia (waheremu na wabariki) wakaazi wa angani, wa ardhini na wa majini, na wale ambao miongoni mwao mna waliowekwa kwa ajili ya viumbe kwa amri ya Mwenyezi Mungu.

Basi warehema Siku ambayo kila nafsi itakuja ikiwa imeandamana na mshika shemere na shahidi wake; na uwarehemu rehema zitakazowazidishia utukufu wa ziada juu ya utukufu wao, na usafi wa ziada juu ya usafi wao.

Ee Mola! Plae Unapowaswalia Malaika Wako na Mitume Yako, na ukawafikishia salamu zetu kwa, basi nasi pia turehemu kwa rehma zako kutokana na maneno mema uliotujaalia ambayo tumeyatumia katika kuwataja wao (kuwataja Malaika na Mitume hao). Hakika Wewe ni Mkarimu wa hali ya juu, na ni Mwingi wa fadhila.

🌞
🔄

Rejea

  1. Ansarian, Diyar Ashiqan, 1372 S, juz. 3, uk. 19-149; Khalji, Asrar Khamooshan, 1383 S, 131-235.
  2. Ansarian, Diyar Ashiqan, 1372 S, juz. 3, uk. 19-149
  3. Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 289-317.
  4. Khalji, Asrar Khamooshan, 1383 S, juz. 1, uk. 131-234.
  5. Fihri, Sharh wa Tafsir Sahifa Sajjadiyah, 1388 S, juz. 1, uk. 205-250.
  6. Madani Shirazi, Riadh al-Salikiin, 1435 AH, juz. 2, uk. 5-80.
  7. Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 83-93.
  8. Darabi, Riadh al-Arifiin, 1379 AH, uk. 65-82.
  9. Fadlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 69-96.
  10. Faidh Kashani, Taaliqat Ala Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 22-26.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.