Nenda kwa yaliyomo

Dua ya Pili ya Sahifatu Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Pili ya Sahifatu Sajjadiyyah
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika mwandiko wa Ahmad Nayrizi, iliyoandikwa mwaka 1145 Hijria.

Mtoaji / MwandishiImamu Sajjad (a.s)
LughaKiarabu
Msimulizi / MpokeziMutawakkil ibn Harun
MadaInahusiana na kumswalia bwana Mtume (s.a.w.w), kufafanua sifa zake, pamoja na kutoa ufafanuzi juu ya jitihada na subira zake katika kuwaongoza watu kuuelekea uadilifu na kushikamana na imani ya Uislamu
ChanzoSahifa Sajjadiyah
Tafsiri kwa Lugha yaKifarsi

Dua ya Pili ya Sahifatu Sajjadiyyah (Kiarabu: الدعاء الثاني من الصحيفة السجادية) ni miongoni mwa dua mashuhuri zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), nayo ni dua inajumuisha maombi maalumu ya kumwombea pamoja na kusalia bwana Mtume (s.a.w.w). Pia dua inatoa maelezo juu ya juhudi kubwa alizozifanya na bwana Mtume (s.a.w.w), katika kuwalingania watu na kuwataka waelekea kwenye haki na kushikamana na mwongozo wa Mwenye Ezi Mungu. Katika dua hii, Imamu Sajjad (a.s) anamshukuru Allah Mtukufu kwa kumtuma Mtume wake wa mwisho ndani ya umma huu wa Kiislamu, na kumwomba Mwenye Ezi Mungu amtunuku Mtume Muhammad (s.a.w.w) daraja ya juu kabisa, kutokana na juhudi zake zisizo na kifani katika kueneza Uislamu na kusimamisha haki katika jamii ya mwanadamu. Vilevile, ndani ya dua hii kunapatikana maelezo muhimu kuhusiana na sifa tukufu za Bwana wa Mitume Muhammad Al-Mustafa (s.a.w.w), zikibainisha nafasi yake kama kiigizo bora kwa walimwengu wote duniani humu.

Kuna tafsiri kadhaa zilizoandikwa kuhusiana na kitabu kilichokusanya dua mbali mbali za Imamu Sajjad (a.s), ambapo Dua hii ya Pili, imeonekana kuchambuliwa ndani ya tafsiri hizo mbalimbali za kitabu hicho kijulikanacho kwa jina la Sahifatu Sajjadiyya. Miongoni mwa tafsiri mbalimbali za kitabu hichi ni pamoja na; Diyāre-‘Āshiqān, kilichoandikwa kwa lugha ya Kifarsi na Hussein Ansarian, pamoja na Riyādh al-Sālikīn fī Sharh-e Sahīfa Sayyid al-Sājidīn, kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu na Sayyid Ali Khān al-Madani.

Mafunzo ya Dua ya Pili ya Sahifatu Sajjadiyyah

Mandhari kuu ya dua ya pili katika Sahifa ya Sajjadiyyah inahusiana na kumswalia bwana Mtume (s.a.w.w), kufafanua sifa zake, pamoja na kutoa ufafanuzi juu ya jitihada na subira zake katika kuwaongoza watu kuuelekea uadilifu na kushikamana na imani ya Uislamu. Miongoni mwa mafunzo ya kiimani yanayopatikana ndani ya dua hii ni:

  • Kumhimidi na kumtukuza Mwenye Ezi Mungu kutokana na kuwaneemesha Waislamu kupitia ujio wa mjumbe wa mwisho kutoka kwa Mola wao.
  • Taswira ya uweza wa Mwenye Ezi Mungu wa katika kutenda chochote kile akipendacho, hata kama ni kikubwa kupita kiasi, na ujuzi wake wa kuelewa kila kitu, ambapo hakuna chochote kile kinachofichika mbele yake, hata kama kitakuwa ni kidogo kupita budi.
  • Nafasi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) kama ni hitimisho la utume, na nafasi ya Uislamu kama ni toleo la mwisho la sheria za Kimungu.
  • Ushuhuda wa Imamu juu ya vitendo vya jumuiya ya Waislamu.
  • Taswira ya sifa za Mtume Muhammad (s.a.w.w), zinazomtathimini yeye kama ni; mlinzi wa wahyi wa Mwenye Ezi Mungu, kiumbe mwenye hadhi ya juu zaidi miongoni mwa viumbe wote, mteule miongoni mwa watumishi wa Mungu, chanzo cha rehema, akisiko la wema, ufunguo wa baraka.
  • Jitihada za bwana Mtume (s.a.w.w) na kudumu katika kuwahimiza watu kuielekea haki, mtekelezaji wa amri za Mwenye Ezi Mungu, na mvumilivu katika kuvumilia misukosuko katika kazi yake takatifu, ambapo mara kadhaa alihatarisha maisha yake huku akikabiliwa na migogoro ya kiudugu katika kabila lake kwa sababu ya kuikataa kwao haki aliyokuwa akiitangaza, jitihada zake za kuwaunganisha watu waliokuwa wametengana, jambo ambalo liliwezekana kupitia imani ya Kiislamu, kuhama kwenda ardhi ya mbali, kupambana na maadui wa Mwenyezi Mungu, n.k).
  • Dua ya kumwombea bwana Mtume (s.a.w.w) daraja ya juu kabisa huko Peponi.
  • Kukubaliwa kwa shufaa ya bwana Mtume (s.a.w.w), kwa ajili ya watu wa nyumba yake pamoja na wafuasi na waumini[1] maalumu, kupitia ukuruba wake na Mola wake.
  • Ithibati ya uhakika usio na shaka wa ahadi ya Mungu kwa waja wake.
  • Kumtangaza Mwenye Ezi Mungu kuwa ni mwenye uwezo wa kuyabadilisha mabaya na kuyafanya yawe mema.

Matini ya Dua na Tafsiri Yake

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

:وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ بَعْدَ هَذَا التَّحْمِيدِ فِي الصَّلَاةِ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ

وَ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي مَنَّ عَلَيْنَا بِمُحَمَّدٍ نَبِيِّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ دُونَ الْأُمَمِ الْمَاضِيَةِ وَ الْقُرُونِ السَّالِفَةِ، بِقُدْرَتِهِ الَّتِي لَا تَعْجِزُ عَنْ شَيْ‌ءٍ وَ إِنْ عَظُمَ، وَ لَا يَفُوتُهَا شَيْ‌ءٌ وَ إِنْ لَطُفَ، فَخَتَمَ بِنَا عَلَى جَمِيعِ مَنْ ذَرَأَ، وَ جَعَلَنَا شُهَدَاءَ عَلَى مَنْ جَحَدَ، وَ كَثَّرَنَا بِمَنِّهِ عَلَى مَنْ قَلَّ.

اللَّهُمَّ فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ أَمِينِكَ عَلَى وَحْيِكَ، وَ نَجِيبِكَ مِنْ خَلْقِكَ، وَ صَفِيِّكَ مِنْ عِبَادِكَ، إِمَامِ الرَّحْمَةِ، وَ قَائِدِ الْخَيْرِ، وَ مِفْتَاحِ الْبَرَكَةِ.

كَمَا نَصَبَ لِأَمْرِكَ نَفْسَهُ وَ عَرَّضَ فِيكَ لِلْمَكْرُوهِ بَدَنَهُ وَ كَاشَفَ فِي الدُّعَاءِ إِلَيْكَ حَامَّتَهُ وَ حَارَبَ فِي رِضَاكَ أُسْرَتَهُ وَ قَطَعَ فِي إِحْيَاءِ دِينِكَ رَحِمَهُ. وَ أَقْصَى الْأَدْنَيْنَ عَلَى جُحُودِهِمْ وَ قَرَّبَ الْأَقْصَيْنَ عَلَى اسْتِجَابَتِهِمْ لَكَ. وَ وَالَى فِيكَ الْأَبْعَدِينَ وَ عَادَى فِيكَ الْأَقْرَبِينَ و أَدْأَبَ نَفْسَهُ فِي تَبْلِيغِ رِسَالَتِكَ وَ أَتْعَبَهَا بِالدُّعَاءِ إِلَى مِلَّتِكَ.

وَ شَغَلَهَا بِالنُّصْحِ لِأَهْلِ دَعْوَتِكَ وَ هَاجَرَ إِلَى بِلَادِ الْغُربَةِ، وَ مَحَلِّ النَّأْيِ عَنْ مَوْطِنِ رَحْلِهِ، وَ مَوْضِعِ رِجْلِهِ، وَ مَسْقَطِ رَأْسِهِ، وَ مَأْنَسِ نَفْسِهِ، إِرَادَةً مِنْهُ لِإِعْزَازِ دِينِكَ، وَ اسْتِنْصَاراً عَلَى أَهْلِ الْكُفْرِ بِكَ. حَتَّى اسْتَتَبَّ لَهُ مَا حَاوَلَ فِي أَعْدَائِكَ وَ اسْتَتَمَّ لَهُ مَا دَبَّرَ فِي أَوْلِيَائِكَ.

فَنَهَدَ إِلَيْهِمْ مُسْتَفْتِحاً بِعَوْنِكَ، وَ مُتَقَوِّياً عَلَى ضَعْفِهِ بِنَصْرِكَ فَغَزَاهُمْ فِي عُقْرِ دِيَارِهِمْ، حَتَّى ظَهَرَ أَمْرُكَ، وَ عَلَتْ كَلِمَتُكَ، وَ لَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ.

اللَّهُمَّ فَارْفَعْهُ بِمَا كَدَحَ فِيكَ إِلَى الدَّرَجَةِ الْعُلْيَا مِنْ جَنَّتِكَ حَتَّى لَا يُسَاوَى فِي مَنْزِلَةٍ، وَ لَا يُكَافَأَ فِي مَرْتَبَةٍ، وَ لَا يُوَازِيَهُ لَدَيْكَ مَلَكٌ مُقَرَّبٌ، وَ لَا نَبِيٌّ مُرْسَلٌ. وَ عَرِّفْهُ فِي أَهْلِهِ الطَّاهِرِينَ وَ أُمَّتِهِ الْمُؤْمِنِينَ مِنْ حُسْنِ الشَّفَاعَةِ أَجَلَّ مَا وَعَدْتَهُ يَا نَافِذَ الْعِدَةِ، يَا وَافِيَ الْقَوْلِ، يَا مُبَدِّلَ السَّيِّئَاتِ بِأَضْعَافِهَا مِنَ الْحَسَنَاتِ إِنَّكَ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ.

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ بَعْدَ هَذَا التَّحْمِيدِ فِي الصَّلَاةِ عَلَى رَسُولِ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ:
Na miongoni mwa dua na nyiradi za Imamu Sajjad (a.s) baada ya kumaliza kumhimidi Mola wake, ni kumtakia rehema na amani Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w). Dua ambayo imekuja kwa ibara zifuatazo:
وَ الْحَمْدُ لِلَّهِ الَّذِي مَنَّ عَلَيْنَا بِمُحَمَّدٍ نَبِيِّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَ آلِهِ دُونَ الْأُمَمِ الْمَاضِيَةِ وَ الْقُرُونِ السَّالِفَةِ، بِقُدْرَتِهِ الَّتِي لَا تَعْجِزُ عَنْ شَيْ‌ءٍ وَ إِنْ عَظُمَ، وَ لَا يَفُوتُهَا شَيْ‌ءٌ وَ إِنْ لَطُفَ، فَخَتَمَ بِنَا عَلَى جَمِيعِ مَنْ ذَرَأَ، وَ جَعَلَنَا شُهَدَاءَ عَلَى مَنْ جَحَدَ، وَ كَثَّرَنَا بِمَنِّهِ عَلَى مَنْ قَلَّ.
Na shukurani zote ni zake Mwenye Ezi Mungu, aliyetuneemesha kwa kutuletea Muhammad (s.a.w.w), ambaye ni Nabii wake, neema ambayo tumeipata sisi na na wala hakuna umma wowote ule uliobahatika kama sisi katika karne zilizopita. Hili limewezekana kupitia nguvu zake ambazo hazishindwi na chochote kile ulimwenguni humu, hata kiwe ni kikubwa kiasi gani, na wala hakuna kinachoweza kumponyoka na kukaa nje ya milki yake, hata kama kitakuwa ni kidogo kiasi gani. Ametufanya sisi kuwa ndio hitimisho la wale wote waliokuja kabla yetu, kisha akatuweka kuwa ni mashahidi juu ya wale waliokataa (kufuata uongofu wake), na akaikithirisha idadi yetu juu ya wengine walio wachache kwa neema yake.
اللَّهُمَّ فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ أَمِينِكَ عَلَى وَحْيِكَ، وَ نَجِيبِكَ مِنْ خَلْقِكَ، وَ صَفِيِّكَ مِنْ عِبَادِكَ، إِمَامِ الرَّحْمَةِ، وَ قَائِدِ الْخَيْرِ، وَ مِفْتَاحِ الْبَرَكَةِ.
Ewe Mola! Basi umshushie rehema Muhammad – mwaminifu wako kwa Wahyi wako, mteule wako miongoni mwa viumbe wako, mchaguliwa wako miongoni mwa waja wako, kiongozi wa rehema, nembo ya kheri na ufunguo wa baraka.
كَمَا نَصَبَ لِأَمْرِكَ نَفْسَهُ وَ عَرَّضَ فِيكَ لِلْمَكْرُوهِ بَدَنَهُ وَ كَاشَفَ فِي الدُّعَاءِ إِلَيْكَ حَامَّتَهُ وَ حَارَبَ فِي رِضَاكَ أُسْرَتَهُ وَ قَطَعَ فِي إِحْيَاءِ دِينِكَ رَحِمَهُ. وَ أَقْصَى الْأَدْنَيْنَ عَلَى جُحُودِهِمْ وَ قَرَّبَ الْأَقْصَيْنَ عَلَى اسْتِجَابَتِهِمْ لَكَ. وَ وَالَى فِيكَ الْأَبْعَدِينَ وَ عَادَى فِيكَ الْأَقْرَبِينَ و أَدْأَبَ نَفْسَهُ فِي تَبْلِيغِ رِسَالَتِكَ وَ أَتْعَبَهَا بِالدُّعَاءِ إِلَى مِلَّتِكَ.
(Mrehemu) Kama vile yeye alivyojitolea kwa juhudi zote kwa ajili ya kutekeleza amri zako tukufu, kisha akavumilia mateso na maudhi ya kimwili kwa ajili yako. Alifuta mipaka ya ujamaa (alikabiliana na jamaa zake), katika kuilingania dini yako, hadi akajitwika mzigo wa mapambano dhidi ya jamaa zake mwenyewe kwa ajili ya radhi zako. Alivunja nasaba na jamaa zake kwa azma ya kufufua na kuhuisha dini yako. Aliwakataa (aliwaweka mbali) jamaa zake wa karibu kwa sababu ya ukafiri wao, na akawakaribisha waliokuwa mbali kinasaba, kwa sababu ya kuitikia kwao wito wako. Aliunda udugu na watu wa mbali, na akajenga uadui na jamaa zake wa karibu kwa ajili yako. Aliichosha nafsi yake usiku na mchana kwa ajili ya kufikisha ujumbe wako, na aliukalifisha mwili wake katika juhudi za kuwaita watu kwenye njia yako ya haki.
وَ شَغَلَهَا بِالنُّصْحِ لِأَهْلِ دَعْوَتِكَ وَ هَاجَرَ إِلَى بِلَادِ الْغُربَةِ، وَ مَحَلِّ النَّأْيِ عَنْ مَوْطِنِ رَحْلِهِ، وَ مَوْضِعِ رِجْلِهِ، وَ مَسْقَطِ رَأْسِهِ، وَ مَأْنَسِ نَفْسِهِ، إِرَادَةً مِنْهُ لِإِعْزَازِ دِينِكَ، وَ اسْتِنْصَاراً عَلَى أَهْلِ الْكُفْرِ بِكَ. حَتَّى اسْتَتَبَّ لَهُ مَا حَاوَلَ فِي أَعْدَائِكَ وَ اسْتَتَمَّ لَهُ مَا دَبَّرَ فِي أَوْلِيَائِكَ.
Na aliishughulisha (nafsi yake) kwa kuwapa nasaha wale walioitikia wito wako. Kisha akahama kuelekea katika ardhi ya ugenini, mahali ambapo mbali na makaazi yake, mbali na eneo la nyayo zake, mbali na mji wa kuzaliwa kwake, mbali na mahala pa utulivu wa moyo wake, (alifanya hivyo) akiwa na azma ya kuitukuza dini yako, na kwa nia ya kutafuta msaada dhidi ya waliokukanusha. (Aliendelea) hadi akafaulu katika aliyoyakusudia dhidi ya maadui zako, na akakamilisha liyoyapanga kwa ajili ya vipenzi vyako.
فَنَهَدَ إِلَيْهِمْ مُسْتَفْتِحاً بِعَوْنِكَ، وَ مُتَقَوِّياً عَلَى ضَعْفِهِ بِنَصْرِكَ فَغَزَاهُمْ فِي عُقْرِ دِيَارِهِمْ، حَتَّى ظَهَرَ أَمْرُكَ، وَ عَلَتْ كَلِمَتُكَ، وَ لَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُونَ.
Hivyo akainuka dhidi yao huku akiwa ni mtegemezi wa ushindi kupitia msaada wako, na akaitia nguvu nafsi yake dhaifu akiuegemea msaada wa nusura yako. Akaingia vitani dhidi yao na kupigana nao hali wakiwa ndani ya miji yao, mpaka amri yako ikapata nguvu, na neno lako likatukuka (hata kama washirikina walilichukiza na jambo hilo).
اللَّهُمَّ فَارْفَعْهُ بِمَا كَدَحَ فِيكَ إِلَى الدَّرَجَةِ الْعُلْيَا مِنْ جَنَّتِكَ حَتَّى لَا يُسَاوَى فِي مَنْزِلَةٍ، وَ لَا يُكَافَأَ فِي مَرْتَبَةٍ، وَ لَا يُوَازِيَهُ لَدَيْكَ مَلَكٌ مُقَرَّبٌ، وَ لَا نَبِيٌّ مُرْسَلٌ. وَ عَرِّفْهُ فِي أَهْلِهِ الطَّاهِرِينَ وَ أُمَّتِهِ الْمُؤْمِنِينَ مِنْ حُسْنِ الشَّفَاعَةِ أَجَلَّ مَا وَعَدْتَهُ يَا نَافِذَ الْعِدَةِ، يَا وَافِيَ الْقَوْلِ، يَا مُبَدِّلَ السَّيِّئَاتِ بِأَضْعَافِهَا مِنَ الْحَسَنَاتِ إِنَّكَ ذُو الْفَضْلِ الْعَظِيمِ.
Ewe Mola! Basi mwinue (Mtume Muhammad) na umpe daraja ya juu kabisa katika Pepo Yako kwa sababu ya juhudi alizozifanya kwa ajili Yako, mpaka asilinganishwe na mwengine yeyote yule kidaraj, wala asilingane na yeyote katika cheo, hadi si Malaika aliyekaribu Nawe, wala nabii asiweze kukaribiane naye kwa heshima alioipata mbele Yako. Na uitangaze nafasi ya uombezi wake kwa watu wa nyumbani yake waliotakasika pamoja na umma wa walioamani, na uutangaze ubora wa shufaa yake hiyo kuliko vile ulivyomuahidi. Ewe Mtimiza ahadi! Ewe Mkamilishaji wa kauli Zake! Ewe Ugeuzaye mabaya kuwa mema mara dufu!

Na miongoni mwa dua na nyiradi za Imamu Sajjad (a.s) baada ya kumaliza kumhimidi Mola wake, ni kumtakia rehema na amani Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w). Dua ambayo imekuja kwa ibara zifuatazo:

Na shukurani zote ni zake Mwenye Ezi Mungu, aliyetuneemesha kwa kutuletea Muhammad (s.a.w.w), ambaye ni Nabii wake, neema ambayo tumeipata sisi na na wala hakuna umma wowote ule uliobahatika kama sisi katika karne zilizopita. Hili limewezekana kupitia nguvu zake ambazo hazishindwi na chochote kile ulimwenguni humu, hata kiwe ni kikubwa kiasi gani, na wala hakuna kinachoweza kumponyoka na kukaa nje ya milki yake, hata kama kitakuwa ni kidogo kiasi gani. Ametufanya sisi kuwa ndio hitimisho la wale wote waliokuja kabla yetu, kisha akatuweka kuwa ni mashahidi juu ya wale waliokataa (kufuata uongofu wake), na akaikithirisha idadi yetu juu ya wengine walio wachache kwa neema yake.

Ewe Mola! Basi umshushie rehema Muhammad – mwaminifu wako kwa Wahyi wako, mteule wako miongoni mwa viumbe wako, mchaguliwa wako miongoni mwa waja wako, kiongozi wa rehema, nembo ya kheri na ufunguo wa baraka.

(Mrehemu) Kama vile yeye alivyojitolea kwa juhudi zote kwa ajili ya kutekeleza amri zako tukufu, kisha akavumilia mateso na maudhi ya kimwili kwa ajili yako. Alifuta mipaka ya ujamaa (alikabiliana na jamaa zake), katika kuilingania dini yako, hadi akajitwika mzigo wa mapambano dhidi ya jamaa zake mwenyewe kwa ajili ya radhi zako. Alivunja nasaba na jamaa zake kwa azma ya kufufua na kuhuisha dini yako. Aliwakataa (aliwaweka mbali) jamaa zake wa karibu kwa sababu ya ukafiri wao, na akawakaribisha waliokuwa mbali kinasaba, kwa sababu ya kuitikia kwao wito wako. Aliunda udugu na watu wa mbali, na akajenga uadui na jamaa zake wa karibu kwa ajili yako. Aliichosha nafsi yake usiku na mchana kwa ajili ya kufikisha ujumbe wako, na aliukalifisha mwili wake katika juhudi za kuwaita watu kwenye njia yako ya haki.

Na aliishughulisha (nafsi yake) kwa kuwapa nasaha wale walioitikia wito wako. Kisha akahama kuelekea katika ardhi ya ugenini, mahali ambapo mbali na makaazi yake, mbali na eneo la nyayo zake, mbali na mji wa kuzaliwa kwake, mbali na mahala pa utulivu wa moyo wake, (alifanya hivyo) akiwa na azma ya kuitukuza dini yako, na kwa nia ya kutafuta msaada dhidi ya waliokukanusha. (Aliendelea) hadi akafaulu katika aliyoyakusudia dhidi ya maadui zako, na akakamilisha liyoyapanga kwa ajili ya vipenzi vyako.

Hivyo akainuka dhidi yao huku akiwa ni mtegemezi wa ushindi kupitia msaada wako, na akaitia nguvu nafsi yake dhaifu akiuegemea msaada wa nusura yako. Akaingia vitani dhidi yao na kupigana nao hali wakiwa ndani ya miji yao, mpaka amri yako ikapata nguvu, na neno lako likatukuka (hata kama washirikina walilichukiza na jambo hilo).

Ewe Mola! Basi mwinue (Mtume Muhammad) na umpe daraja ya juu kabisa katika Pepo Yako kwa sababu ya juhudi alizozifanya kwa ajili Yako, mpaka asilinganishwe na mwengine yeyote yule kidaraj, wala asilingane na yeyote katika cheo, hadi si Malaika aliyekaribu Nawe, wala nabii asiweze kukaribiane naye kwa heshima alioipata mbele Yako. Na uitangaze nafasi ya uombezi wake kwa watu wa nyumbani yake waliotakasika pamoja na umma wa walioamani, na uutangaze ubora wa shufaa yake hiyo kuliko vile ulivyomuahidi. Ewe Mtimiza ahadi! Ewe Mkamilishaji wa kauli Zake! Ewe Ugeuzaye mabaya kuwa mema mara dufu!

🌞
🔄

Rejea

  1. Ansarian, Diyar Ashiqan, 1373 S, juz. 2, uk. 17-356; Khalji, Asrar Khamooshan, 1383 S, juz. 2, uk. 16-131.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Husseini Madani, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah Sayyid al-Sajjadin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1409 AH.
  • Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Sultan Moradi, Muhammad, Simaye Payambar Adham Dar Sahifa Sajjadiyah, Qom, Intisharat Sibt al-Nabi, 1385 S.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.
  • Hashimi Nejad, Sayyid Jawad, Muhammad Raz Afarinesh, Qom, Intisharat Ayaat Bayyinat Ayat Baynat, 1385 S.