Dua ya Kumi na Tano ya Sahifa Sajjadiyya
Dua ya Kumi na Tano iliyoko katika Sahifa Sajadiyya: ni miongoni mwa dua zilizopokewa kutoka kwa Imamu Sajad (a.s), dua aliyokuwa akiiomba wakati wa kuugua au kukutana na shida fulani. Katika dua hii, Imamu Sajad (a.s) anamshukuru Mwenye Ezi Mungu kwa kumjaalia afya njema au kwa kumsafisha kupitia magonjwa hayo. Kwani magonjwa ni miongoni mwa nyenzo za kumtakasa mwanadamu kutokana na dhambi mbali m bali. Aidha, anasisitiza kwamba ugonjwa ni moja ya misukumo inayomsukuma mwanadamu kuelekea toba, na kwamba kumtegemea Mungu ndio ufunguo wa kuondoa vizuizi au pingamizi zote za kiroho pamoja na kidunia.
Dua hii pia imechambuliwa kwa kina kabisa katika vitabu mbali mbali vilivyofasiri dua za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa tafsiri chambuzi zilizochambua dua hii kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; Diyare Ashaqaan, kilichoandikwa na Hussein Ansarian na Shahud na Shnakht, kilichoandikwa na Hassan Mamdouhi Kirmanshahi. Ama kwa upande wa lugha ya Kiarabu, kitabu kitabu kiitacho Riyadhu al-Salikina, kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.
Mafunzo ya Dua ya Kumi na Tano
Dhamira kuu ya dua ya kumi na tano katika Sahifa Sajjadiyya ni kutpa tafakuri ya maombi mbele ya changamoto za maradhi, matatizo na majaribu mbali mbali ya kidunia. Hata hivyo, mtazamo wa kina wa Imamu Sajjad (a.s.) katika dua hii, unalenga zaidi juu ya athari za ya maisha baada ya kifo (Akhera), zinzopatikana kupitia janga la maradhi, mabalaa na misiba mbali mbali. [] Dhana za dua ya kumi na tano, zimeangazwa na Imamu Sajjad (a.s) katika dondoo zifuatazo:
· Kumshukuru Mungu kwa neema ya afya na mtihani wa ugonjwa (Kuona hali zote mbili, siha na maradhi, kuwa ni sawa mbele ya wajibu wa kutoa shukrani).
· Thamani adhimu ya hali ya kua na afya njema na uzuri wa kiutu wa kuwa na subra katika kukabiliana na maradhi.
· Kuthamini (kushukuru) nguvu na ustawi wa kiafya katika ibada (Kuelekeza nishati ya mwili katika kutafuta radhi za Mwenye Ezi Mungu).
· Maradhi ni kafara ya madhambi na kizuizi kinachozuia mghafala wa nafsi (usahaulifu wa kumsahau Mola).
· Kutakasika na athari za madhambi kupitia toba na maradhi.
· Kutafakari juu ya matunda na hekima iliyojificha nyuma ya pazia la udhaifu.
· Maradhi ni tanbihi inayomwelekeza mja kwenye toba.
· Kupokea fidia (thawabu) kwa kuvumilia magonjwa,na kurekodiwa kwake katika kumbukumbu za Malaika waandishi wa amali waitwao (Raqib na Atid).
· Ujira wa Allah katika maradhi unatokana na Fadhila na Ihsani Yake. [3]
· Kuidiriki kuitambua thamani ya afya wakati wa mtihani wa maradhi.
· Ombi la kuwa na ridhaa kutokana majaaliwa (ya Mungu) na kupata wepesi katika kukabiliana na changamoto tofauti. [4]
· Kumtegemea Mungu ndiyo funguo ya kufungulia milango yote iliyokomewa.
· Neema za Allah hazina masimango wala ujira
·
Tafsiri Chambuzi za Dua ya Kumi Tano
Kuna tafsiri chambuzi kadhaa za kina na kimantiki juu ya Dua ya Kumi na Tano zilizowasilishwa kwa lugha ya Kiajemi kupitia maandiko yanayochambua dua za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa maandiko hayo ni pamoja na Diyare Asheqan (Ardhi ya Wenye Mapenzi ya Dhati), kazi iliyofanywa na Hossein Ansarian, [6] Shohud wa Shenakht (Uoni wa Kiroho na Welewa) kazi ya Mohammad-Hassan Mamduhi Kermanshahi, [7] na Sharh wa Tarjomeh Sahifeh Sajjadiyeh (Ufafanuzi na Tafasiri ya Sahifa Sajjadiyya), kazi andishi ya Sayyid Ahmad Fahri. [8]
Zaidi ya hayo, pia kuna uchambuzi wa kina wa Dua ya Kumi na Tano uliowasilishwa kwa lugha ya Kiarabu na waandishi mbai mbali. Miongoni mwake ni pamoja na; Riyadhu al-Salikin, kazi iliyofanywa na Sayyid Ali Khan Madani, [9] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi andishi ya Muhammad Jawad Mughniyya, [10] Riyadhu al-Arifin, kazi ya Muhammad bin Muhammad Darabi, [11] na Afaq al-Ruh, kitabu kichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah. [12] Isitoshe, pia dhana za kimsamiati za dua hii zimefafanuliwa ki-istilahi kupitia uchambuzi wa kilugha. Miongoni vitabu vilivyochambua msamiati wa dua hii ni kama vile; Ta'liqat 'ala al-Sahifa al-Sajjadiyya, ambayo ni kazi andishi ya Faidhu Kashani [13] na Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya, ambayo ni kazi ya Izz al-Din al-Jaza'iri. [14]
Matini ya Dua na Tafsiri Yake
وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ إِذَا مَرِضَ أَوْ نَزَلَ بِهِ كَرْبٌ أَوْ بَلِيِّةٌ
Na ifuatayo ni miongoni mwa maombi yake (Amani iwe juu yake) pindi alipokuwa akikabiliwa na hali ya maradhi, au alipokuwa akipatwa na msongo wa moyo au janga au mtihani.
اللَّهُمَّ لَكَ الْحَمْدُ عَلَى مَا لَمْ أَزَلْ أَتَصَرَّفُ فِيهِ مِنْ سَلَامَةِ بَدَنِي ، وَ لَكَ الْحَمْدُ عَلَى مَا أَحْدَثْتَ بِي مِنْ عِلَّةٍ فِي جَسَدِي
Ewe Mola wangu, shukrani na sifa stahiki ni Zako kwa ajili ya siha ya mwili wangu katika kipidi chote ambacho bado nitakuwa nikiendelea kujinufaisha nayo, na pia shukrani na sifa stahiki ni Zako Wewe kwa maradhi uliyoyazusha katika mwili wangu.
فَمَا أَدْرِي ، يَا إِلَهِي ، أَيُّ الْحَالَيْنِ أَحَقُّ بِالشُّكْرِ لَكَ ، وَ أَيُّ الْوَقْتَيْنِ أَوْلَى بِالْحَمْدِ لَكَ.
Ee Mola wangu, kwa kweli mimi sielewi ni ipi katika hali mbili hizi iliyo na haki zaidi ya Shukrani kwako, na ni upi katika nyakati mbili hizi inayopasa kuhimidiwa zaidi Kwako.
أَ وَقْتُ الصِّحَّةِ الَّتِي هَنَّأْتَنِي فِيهَا طَيِّبَاتِ رِزْقِكَ ، وَ نَشَّطْتَنِي بِهَا لِابْتِغَاءِ مَرْضَاتِكَ وَ فَضْلِكَ ، وَ قَوَّيْتَنِي مَعَهَا عَلَى مَا وَفَّقْتَنِي لَهُ مِنْ طَاعَتِكَ
Je (wakati unaopaswa kushukuriwa zaidi), ni (ule) wakati wa afya njema ambao ulinineemesha ndani yake, na ukanifurahisha kwa riziki Zako njema, kisha ukanipa uchangamfu ndani yake, ili kutafuta radhi na fadhila Zako, kisha ukaniwezesha ndani yake juu ya yale uliyoniwafikisha katika utiifu Wako?
أَمْ وَقْتُ الْعِلَّةِ الَّتِي مَحَّصْتَنِي بِهَا ، وَ النِّعَمِ الَّتِي أَتْحَفْتَنِي بِهَا ، تَخْفِيفاً لِمَا ثَقُلَ بِهِ عَلَيَّ ظَهْرِي مِنَ الْخَطِيئَاتِ ، وَ تَطْهِيراً لِمَا انْغَمَسْتُ فِيهِ مِنَ السَّيِّئَاتِ ، وَ تَنْبِيهاً لِتَنَاوُلِ التَّوْبَةِ ، وَ تَذْكِيراً لِمحْوِ الْحَوْبَةِ بِقَدِيمِ النِّعْمَةِ
Au ni wakati wa mtihani wa maradhi ambao umenitakasa nao, na Neema ulizoniruzuku, kama takhfifu (upunguzo) kwa yale yaliyolemisha mgongo wangu kwa madhambi, na kama twahara (utakaso) kwa yale maasi niliyozama ndani yake, na kama tanbihi ya kunizindua kuelekea kwenye Toba, na ukumbusho wa kufuta dhambi kubwa kwa Neema yako ya kale?
وَ فِي خِلَالِ ذَلِكَ مَا كَتَبَ لِيَ الْكَاتِبَانِ مِنْ زَكِيِّ الْأَعْمَالِ ، مَا لَا قَلْبٌ فَكَّرَ فِيهِ ، وَ لَا لِسَانٌ نَطَقَ بِهِ ، وَ لَا جَارِحَةٌ تَكَلَّفَتْهُ ، بَلْ إِفْضَالًا مِنْكَ عَلَيَّ ، وَ إِحْسَاناً مِنْ صَنِيعِكَ إِلَيَّ .
Na (miongoni mwa niniloyapata) wakati huo (wa kipindi cha maradhi yangu), ni amali njema zilizoniandikia na Malaika Wawili (wanao); amali ambazo wala moyo haukuwahi kuzitaraji, na katu hazikutamkwa na ulimi (wangu), wala hazikutendwa kwa juhudi za kiungo (changu) chochote. Bali, ni ukarimu Wako kwa juu yangu, na kunifanyia hasani ndiyo kwaida Yako.
اللَّهُمَّ فَصَلِّ عَلَى مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ ، وَ حَبِّبْ إِلَيَّ مَا رَضِيتَ لِي ، وَ يَسِّرْ لِي مَا أَحْلَلْتَ بِي ، وَ طَهِّرْنِي مِنْ دَنَسِ مَا أَسْلَفْتُ ، وَ امْحُ عَنِّي شَرَّ مَا قَدَّمْتُ ، وَ أَوْجِدْنِي حَلَاوَةَ الْعَافِيَةِ ، وَ أَذِقْنِي بَرْدَ السَّلَامَةِ ، وَ اجْعَلْ مَخْرَجِي عَنْ عِلَّتِي إِلَي عَفْوِكَ ، وَ مُتَحَوَّلِي عَنْ صَرْعَتِي إِلَى تَجَاوُزِكَ ، وَ خَلَاصِي مِنْ كَرْبِي إِلَى رَوْحِكَ ، و سَلَامَتِي مِنْ هَذِهِ الشِّدَّةِ إِلَى فَرَجِكَ
Ewe Mola wangu, mrehema Muhammad na Aa zake. Na unijalie kuyapokea kwa upendo yale uliyoniridhia, na uyasahilishe kwangu yale (magumu) uliyoniletea. Na nitakase kutokana na uchafu wa matendo yangu ya awali, na uniondoshee athari hasi za matendo yangu niliyotanguliza. Na niwafikishe kupata ladha ya ustawi kamili (afya njema) na unionjeshe Ladha ya afya njema. Na ujaalie mwondoko wangu wa kutoka katika maradhi yangu haya, uwe ni njia ya kuelekee kwenye afua Yako (msamaha Wako); na (jaalia) mabadiliko yangu ya kutoka kwenye shida (mtihani huu), iwe ni ndiyo njia ya kuelekea kwenye msamaha Wako, na (ujaalie) ukombozi wangu wa kutoka kwenye msukosuko wangu huu, iwe ni mwelekeo wa kuelekee kwenye faraja yako, kisha jaalia salimiko langu la kutoka kwenye jaribu hili iwe ni njia ya kuelekee kwenye ukombozi wako.