Dua ya Kumi na Moja ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa katika Sha'ban 1102 AH. | |
Mtoaji / Mwandishi | Imamu Sajjad (a.s) |
---|---|
Lugha | Kiarabu |
Msimulizi / Mpokezi | Mutawakkil ibn Harun |
Mada | Maombi ya kupata hatima njema katika maisha ya duniani pamoja na maisha ya Akhera. |
Chanzo | Sahifa Sajjadiyah |
Tafsiri kwa Lugha ya | Kifarsi |
Dua ya Kumi na Moja ya Sahifa Sajjadiyyah (Kiarabu: الدعاء الحادي عشر من الصحيفة السجادية) ni sehemu mojawapo ya maombi yaliyonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), ikilenga kutafuta hatima njema katika maisha haya na yajayo. Miongoni mwa mambo yaliotajwa na Imamu Sajjad (a.s.) katika dua hii, ni kuwepo kwa mahusiano maalumu kati ya amali za mwanadamu na hali (khulka) za kiroho za Malaika (katika kuamiliana na waja wa Mungu), uhakika wa majibu ya Mwenye Ezi Mungu katika kujibu dua za waja wake, Pamoja na umuhimu wa kuomba dua ya kupata fursa ya kutumia vyema nyakati za mapumziko.
Ufafanuzi wa Dua ya kumi na moja unapatikana katika vitabu mbali mbali vya tafsiri za Sahifatu Sajjadiyya. Baadhi ya vitabu vya tafsiri vilivyoandikwa katika kuchambua dua zilizomo katika kitabu Sahifatu Sajjadiyya, ni Pamoja na; Diyare Asheghan (Ardhi au Nyumba za Wapenzi), kilichoandikwa na Hussein Ansarian, na Shuhud wa Shenakht (Uoni na Utambuzi) cha Hassan Mamduhi Kermanshahi, vitabu viwili hivi vimeandikwa kwa lugha ya Kiajemi. Kadhalika, kuna vitabu vyengine kadhaa vya tafsiri ya kitabu Al-Sahifatu al-Sajjadiyya, vilivyoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu kiitwacho Riyadhu al-Salikin (Bustani za Wasafiri wa Kiroho), kilichoandikwa na Sayyid Ali Khan Madani.
Misingi ya Mafunzo ya Dua ya Kumi na Moja
Kiini na mada kuu ya Dua ya Kumi na Moja iliyomo katika kitabu cha Sahifatu ya Sajjadiyya inahusiana na ombi la kupata hatima njema katika maisha ya duniani pamoja na maisha yajayo (maisha ya Akhera). Miongozo ya kiroho ya dua hii, kama ilivyopokewa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s), imegawika katika vifungu vitano.[1] Vifungu vitano vya dua hii vimeku katika miktadha inayofafanua vipengele vifuatavyo:
- Dhikri ya Mwenye Ezi Mungu ni msingi wa kuifikia hadhi na utukufu; shukrani Kwake ndiyo chimbuko la kufaulu na kupata uokovu, na kumtii Yeye ndiyo njia ya kunusurika na maangamizi.
- Dua ya kuomba taufiki ya kumkumbuka Mola kwa njia ya kuwa Naye moyoni (utajo wa moyoni).
- Dua ya kuomba taufiki ya kuweaza kutumia ipasavyo nyakati za faragha na nyakati za mapumziko.
- Uhusianao wa moja kwa moja kati ya amali za binadamu na hisia za Kimalaika (katika mahusiano na waja); mfano wake, ni ile furaha ya wale Malaika wasajili wanofurahi kutokana na matendo mema ya mwanadamu.
- Dua ya kuomba taufiki ya kupata mwisho mwema (husnu al-khatima).
- Dua ya kuomba hifadhi ya kuepukana na karipio na lawama za Mwenye Ezi Mungu, hifadhi ambayo haiwezi kupatikana bila ya amali ya kuomba toba.
- Dua ya kuomba stara Siku ya Hesabu (Kiyama), kutokana na makosa na mapungufu.
- Ahadi ya Mwenye Ezi Mungu ya kuyaitikia maombi ya waja Wake.[2]
Tafsiri Chambuzi za Dua ya Kumi na Moja
Kuna tafsiri nyingi zilizoandikwa kwa lugha tofauti katika kufasiri Dua ya kumi na moja ya Sahifa Sajjadiya. Tafsiri za lugha ya Kiajemi zilizoandikwa na wanazuoni mbali mbali ni Pamoja na; Diyare Asheqan cha Hussein Ansarian,[3] Shuhud wa Shenakht cha Muhammad Hassan Mamdouhi Kermanshahi,[4] na Sharhe wa Tarjomeh Sahifehe Sajjadiyye (Ufafanuzi na Tafsiri ya Sahifa Sajjadiya) cha Sayyid Ahmad Fahri.[5]
Pia Dua hii ya kumi na moja imefafanuliwa kwa lugha ya Kiarabu kupitia tafsiri za waandishi mbali mbali, ikiwemo; Riyadh as-Salikin kitabu kilicho andikwa na Sayyid Ali Khan Madani,[6] Fi Dhilal al-Sahifati al-Sajjadiyya (Katika Vivuli vya Sahifa Sajjadiya), kitabu cha Muhammad Jawad Mughniyya,[7] Riyadhu al-Arifin (Bustani za Watambuzi) kilichoandikwa na Muhammad bin Muhammad Darabi, [8] na Afaq al-Ruh (Upeo wa Roho) kilichoandikwa na [[Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Pia msamiati wa dua hii umeelezwa katika ufafanuzi wa kilugha kwenye kitabu kiitwacho Ta'liqat ala al-Sahifati al-Sajjadiyya, (Maelezo Chambuzi juu ya Sahifa Sajjadiya), kitabu kilichoandikwa na Faydh Kashani.[10]
Matini na Tafsiri ya Dua ya Kumi na Moja
وَ کانَ مِنْ دُعَائِهِ علیهالسلام بِخَوَاتِمِ الْخَیرِ
یا مَنْ ذِکرُهُ شَرَفٌ لِلذَّاکرِینَ، وَ یا مَنْ شُکرُهُ فَوْزٌ لِلشَّاکرِینَ، وَ یا مَنْ طَاعَتُهُ نَجَاةٌ لِلْمُطِیعِینَ، صَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اشْغَلْ قُلُوبَنَا بِذِکرِک عَنْ کلِّ ذِکرٍ، وَ أَلْسِنَتَنَا بِشُکرِک عَنْ کلِّ شُکرٍ، وَ جَوَارِحَنَا بِطَاعَتِک عَنْ کلِّ طَاعَةٍ.
فَإِنْ قَدَّرْتَ لَنَا فَرَاغاً مِنْ شُغْلٍ فَاجْعَلْهُ فَرَاغَ سَلَامَةٍ لَا تُدْرِکنَا فِیهِ تَبِعَةٌ، وَ لَا تَلْحَقُنَا فِیهِ سَأْمَةٌ، حَتَّی ینْصَرِفَ عَنَّا کتَّابُ السَّیئَاتِ بِصَحِیفَةٍ خَالِیةٍ مِنْ ذِکرِ سَیئَاتِنَا، وَ یتَوَلَّی کتَّابُ الْحَسَنَاتِ عَنَّا مَسْرُورِینَ بِمَا کتَبُوا مِنْ حَسَنَاتِنَا
وَ إِذَا انْقَضَتْ أَیامُ حَیاتِنَا، وَ تَصَرَّمَتْ مُدَدُ أَعْمَارِنَا، وَ اسْتَحْضَرَتْنَا دَعْوَتُک الَّتِی لَا بُدَّ مِنْهَا وَ مِنْ إِجَابَتِهَا، فَصَلِّ عَلَی مُحَمَّدٍ وَ آلِهِ، وَ اجْعَلْ خِتَامَ مَا تُحْصِی عَلَینَا کتَبَةُ أَعْمَالِنَا تَوْبَةً مَقْبُولَةً لَا تُوقِفُنَا بَعْدَهَا عَلَی ذَنْبٍ اجْتَرَحْنَاهُ، وَ لَا مَعْصِیةٍ اقْتَرَفْنَاهَا.
وَ لَا تَکشِفْ عَنَّا سِتْراً سَتَرْتَهُ عَلَی رُءُوسِ الْأَشْهَادِ، یوْمَ تَبْلُو أَخْبَارَ عِبَادِک.
إِنَّک رَحِیمٌ بِمَنْ دَعَاک، وَ مُسْتَجِیبٌ لِمَنْ نَادَاک.
Na miongoni mwa maombi yake (Amani iwe juu yake) kuhusiana hatima njema likuwa ni dua yenye ibara zisemazo:
Ewe ambaye utajo Wake ni heshima kwa wanaomkumbuka, na Ewe ambaye kumshukuru Yeye uokovo wa wanaomshukuru, na Ewe ambaye kumtii Yeye ndio uokovu na amani kwa wanaomtii! Mrehemu Muhammad na Aali zake, na uzishughulishe nyoyo zetu zishikamane na kazi ya utajo Wako na kuachana na kumbukumbe nyengine (zinazohusiana na wasiokuwa Wewe), na uzitwike (uzishughulishe) ndimi zetu na kazi ya kukushukuru Wewe badala ya kuwashukuru wengine (wote wasiokuwa Wewe), na uvitumie viungo vyetu katika kazi ya utiifu Wako badala ya utiifu wa mwingine wote (wasiokuwa Wewe).
Basi, iwapo Utajaalia(utatukadiria) wakati wa mapumziko kutoka kwenye shughuli fulani, basi yajaalie mapumziko yetu yawe ni mapumziko ya salama, ambayo hatutapatwa na udhi (ovu) lolote lile ndani yake, wala hatutafikwa na uchovu wowote ule ndani yake. Hadi waandishi (wasajili) wa matendo maovu waachane nasi hali ya kuwa daftari halina na andishi lolote lile ovu kuhusiana nasi, na waandishi wa matendo mema waachane nasi huku wakiwa na furaha kwa yale waliyoandika kutokana na matendo yetu mema.
Na kitakapofika kipindi cha hitima ya maisha yetu, na kumalizika kwa muda wa umri wetu, na tukajiwa na wito Wako usiokwepeka, ambao ni wa lazima na wala hatuna budi kuupokea, hapo basi mshushie rehema Zako Muhammad na Aali zake. Na uijaalie toba iliokubalika, kuwa ndio hitimisho la mwisho la amali zetu zilizoandikia na waandishi Wako wanaosajili matendo yetu, ambapo baada yake Hutatuwajibisha kwa dhambi tuliyoifanya, wala kwa uasi tulioutenda.
Na usitukunjulia pazia ulilotusitiri nalo mbele ya mashahidi, Siku utakapozipeleleza na kuzisasambua habari za waja Wako.
Hakika, Wewe ni Mwingi wa Rehema kwa anayekuomba, na Mwenye Kumwitikia anayekuelekea.
Rejea
- ↑ Tarjume wa Sherh Duaye Yozdahome Sahifa Sajjadiyah, Tovuti ya Erfan.
- ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1993, juz. 5, uk. 101-122; Mamduhi, Shuhud va Shanakhte, 1999, juz. 1, uk. 485-500
- ↑ Ansarian, Diyar Ashiqan, 1372 S, juz. 5, uk. 97-122.
- ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shanakhte, 1388 S, juz. 1, uk. 485-500.
- ↑ Fihri, Sherh wa Tafsir al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1388 S, juz. 1, uk. 529-560.
- ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 2, uk. 441-463.
- ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 165-169.
- ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 141-143.
- ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 1, uk. 285-298.
- ↑ Faydh Kashani, Taqaqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 35.
Vyanzo
- Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
- Khalji, Muhammad Taqi, Asrar al-Khamushan, Qom, Parto Khorshid, 1383 S.
- Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
- Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
- Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
- Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
- Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
- Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
- Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.