Dua ya Arobaini na Moja ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya maandishi ya "Sahifa Sajjadiya", kwa mwandiko na hati za Sheikh Abdullah Yazdi, iliandikwa mnamo mwezi Shaaban mwaka 1104 Hijria Taarifa kuhusu Dua na Ziara • Mada: Kuomba stara kutokana na aibu ya dhambi na kuepukana nazo • Kutoka kwa Maasumu / Si kutoka kwa Maasumu: Kutoka kwa Maasumu • Imetoka kwa: Imam Sajjad (a.s) • Msimulizi: Mutawakkil bin Harun • Vyanzo vya Kishia: Sahifa Sajjadiya Maombi na Ziara Maarufu
Dua ya Arobaini na Moja ya Sahifa Sajjadiyya: Ni mojawapo ya dua zilizonukulia kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Nayo ni ile dua inayomwomba Mwenye Ezi Mungu stara na ulinzi dhidi ya kutenda dhambi. Katika maombi ya dua hii, Imamu anaomba rehema za Mwenye Ezi Mungu ili asiangamie kwenye la kisasi na adhabu ya Mwenye Ezi Mungu. Dua ya Arobaini na Moja, imefafanuliwa kwa kina katika tafsiri za Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vilivyofasiri dua hii, ni kitabu kiitwacho Shuhud wa Shinakht (Mwangazo na Utambuzi) kilichoandikwa na Hassan Mamduhi Kermanshahi kwa lugha ya Kiajemi, pamoja na Riyadh al-Salikin ambayo ni kazi ya Sayyid Ali-Khan Madani, ilioandikwa kwa lugha ya Kiarabu.
Mafundisho ya Dua Dua ya Arobaini na Moja, ni mojawapo ya nyiradi tukufu zilizomo katika kitabu kiitwacho Sahifa Sajjadiyya, na ni ombi maalumu la kumnyenyekea Mwenye Ezi Mungu ili alete stara ya kufunika madhambi na ampe mja wake kinga dhidi ya dhambi na makossa mbali mbali. [1] Kwa mujibu wa ufafanuzi wa Kermanshahi ni kwamba; kuanikwa hadharani kwa makossa ya mwanadamu, katika maisha haya pamoja na huko Akhera, ni moja ya maumivu makubwa yanayomsibu binadamu. Kwa hivyo, Imam Sajjad (a.s), kupitia dua hii, anamtaka Mwenye Ezi Mungu afiche na kustiri dhambi za waja Wake na asiwadhalilishe mbele ya viumbe wengine. [2] Mafundisho muhimu yanayopatikana katika dua hii ni kama yafuatayo: • Kuomba heshima na fadhila za Mwenye Ezi Mungu ili mja asikataliwe mbele ya Mola wake. • Maombi ya kuepushwa na kutumbukia katika uwanja kisasi na adhabu ya Mwenye Ezi Mungu kwa sababu ya dhambi. • Kuomba stara ya madhambi na kuepushwa na fedheha. • Maombi ya kuingizwa miongoni mwa waja waliobarikiwa kwa Pepo. • Madhara ya kufichua siri za watu na athari zake kwa maisha ya mtu binafsi. • Kukamilika kwa heshima na hadhi ya mwanadabu kupitia radhi na msamaha wa Mwenye Ezi Mungu. • Kuomba kupata daraja za watu wa daraja tukufu na wenye taqwa. • Dua ya kuwafakishwa na kuwa miongoni mwa watu wa kulia (As-hab al-Yamin). [3]
Tafsiri Mbali Mbali Dua ya Arobaini na Moja ya Sahifa Sajjadiyya imetathminiwa na kufasiriwa kwa kina kupitia waandishi mbalimbali. Katika muktadha wa maandiko ya Kifarsi, dua hii imefasiriwa katika vitabu vifuatavyo: • Shohood wa Shenaakht: cha Mohammad Hasan Mamdouhi Kermanshahi [4] • Sharhe wa Tarjume Sahifa Sajjadiya, cha Seyyed Ahmad Fahri [5] Kwa upande wa lugha ya Kiarabu, ufafanuzi na tafsiri ya dua hii unapatikana katika kazi zifuatazo: • Riyadh al-Salikeen: cha Seyyed Ali Khan Madani [6] • Fi Dhilaal al-Sahifa al-Sajjadiyya: cha Mohammad Javad Moghniyeh [7] • Riyadhu al-Arifiin: kilichoandikwa na Mohammad bin Mohammad Darabi [8] • Afaaqu al-Rouh: cha Seyyed Mohammad Hossein Fadhlullah [9] Vilevile, istilahi na maneno yaliyotumika katika dua hii yamfasiriwa na kufafanuliwa wa kitaalamu kupitia mfumo wa lugha fasihi, kama inavyoonyeshwa katika: • Taliqaatu Ali al-Sahifa al-Sajjadiyya: cha Fayz Kashani [10] • Sharhu al-Sahifa al-Sajjadiyya: cha Ezzaldin Jazairi [11]
Tafsiri ya Dua Na mojawapo ya dua zake (a.s), katika kuomba stara na ulinzi kutokana na dhambi, ni kama ifuatavyo: Ee Mola wangu!
Mpe amani (sala) Muhammad na Aali zake, na unitandikie zulia la heshima yako, unifikishe kwenye chemchemi za rehema zako, uniingiza katikati ya pepo yako, usinionjeshe adhabu ya kukataliwa kutoka kwako, wala usininyime kwa njia ya kukosa matumaini kutoka kwako.
Ee Mola wangu! Usinilipe (usiniadhibu na kuniangamiza) kwa dhambi nilizozitenda, wala usinipekue kwa yale niliyoyachuma. Usiyafichue niliyoyaficha rohoni, wala usiyadhihirishe niliyoyasitiri. Usiyapime matendo yangu kwa mizani yako adilifu, wala usizimwage habari zangu hadharani.
Ee Mola wangu! Sitiri na usiyaanike hadharani, yale ambayo kuukinitangazia yataniletea fedheha, na yaweke mbali na macho ya wanadamu, yakunje na uyaweke mbali na macho (ya watu) yale yanayonifedhehesha mbele yako.
Ee Mola wangu! Vinjari (tukuza) cheo changu kwa ridhaa yako, kamilisha utukufu wangu kwa msamaha wako, niunge kwenye kundi la mkono wa kulia (wenye kustahiki), uniongoze katika njia za waliokoka, nijaalie (niwe) miongoni mwa waliofaulu, yashughulishe (yajenge) maisha yangu na kazi ya kuhudhuria vikao vya watu wema. Amini, Ee Mola wa walimwengu wote!