Dua al-Hazin

Kutoka wikishia

Dua al-Hazin (Kiarabu: دعاء الحَزین) ni minong’ono inayonasibishwa kwa Imamu Ali bin Hussein al-Sajjad (a.s). Imeusiwa na kukokotezwa kusoma dua hii baada ya Sala ya usiku.[1] Katika dua hii kumeashiriwa mafahimu na maana mbalimbali kama majuto kunako amali mbaya na utendaji dhambi mkabala wa msamaha na adhama ya Mwenyezi Mungu ya kuwa msamehevu, wasiwasi wa upweke baada ya kifo na kuomba msamaha kutoka kwa Mwenyezi Mungu.[2] Baadhi ya wasomi na watafiti wanaamini kwamba, madhumuni na maana zilizoko katika dua hii, zinaakisi baadhi ya mafahimu na maana za kimsingi katika mtazamo wa Shia kuhusu ulimwengu kama huzuni, ghamu na masaibu ya mwanadamu, upweke, kutokuwa na matumaini na watu wengine na kuomba hifadhi na kimbilio kwa Mwenyezi Mungu.[3]

Hassan bin Fadhl Tabarsi mmoja wa wasomi na wanazuoni wa hadithi wa karne ya 6 Hijria anasema, Imamu Sajjad (a.s) alikuwa akiisoma dua hii baada ya Sala ya usiku.[4] Hata hivyo Sheikh Tusi (aliyeaga dunia: 460 H) hajaleta katika kitabu cha Misbah al-Mutahajjid maneno yoyote ya kuinasibisha dua hii na Imam Sajjad (a.s).[5] Dua hii haijajapia katika kitabu cha Sahifa Sajjadiyya na kwa mujibu wa baadhi ya watafiti ni kwamba, dua hii haijaandikwa katika kitabu chochote miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kwa ajili ya kukamilisha kitabu cha Sahifa al-Sajjadiya vilivyoandikwa kabla ya karne ya 14.[6]

Sheikh Baha’i katika Miftah al-Falaah ametoa sherh na ufafanuzi wa dua hii na kueleza kwamba, inadhamini adabu za Sala ya Witr.[7] Sayyid Abbas Shushtari Lucknowi fakihi wa India (aliaga dunia: 1306 H) pia ametunga mashairi ya minong’ono ambayo ametoa katika dua hii.[8]

Rejea

  1. Qummīy, Mafātīḥ al-jinān, uk. 873.
  2. Ṭūsī, Miṣbāḥ al-mutahajjid, uk. 160.
  3. Mihrwash, Ḥazīn, Duʿā, uk. 442.
  4. Ṭabrasī, Makārim al-akhlāq, uk. 295.
  5. Ṭūsī, Miṣbāḥ al-mutahajjid, uk. 160.
  6. Mihrwash, Ḥazīn, Duʿā, uk. 442.
  7. Sheikh Bahāʾī, Miftāḥ al-falāḥ, uk. 701.
  8. Nushāhī, Kitābshināsī-yi āthār-i Fārsī-yi chāp shuda dar shibh-i qārra, juz. 3, uk. 1965.

Vyanzo

  • Mihrwash, Farhang. Ḥazīn, Duʿā. In Dāʾirat al-maʿārif buzurg-i Islāmī. Tehran: Markaz-i Dāʾirat al-Maʿārif Islāmī, 1391 Sh.
  • Nushāhī, ʿĀrif. Kitābshināsī-yi āthār-i Fārsī-yi chāp shuda dar shibh-i qārra (Hind, Pākistān, Bangilādish). Tehran: 1391 Sh.
  • Qummīy, Abbās. Mafātīḥ al-jinān. [n.p]:Markaz-i Taḥqīqāt-i Ḥajj, [n.d].
  • Shaykh Bahāʾī, Muḥammad b. Ḥusayn. Miftāḥ al-falāḥ fī ʿamal al-yawm aw al-layla. Qom: Jāmiʿa Mudarrisīn, 1415 AH.
  • Ṭabrisī, Ḥassan bin al-Faḍhl al-. Makārim al-akhlāq. Qom: al-Sharif al-Raḍī, 1370 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥamamd bin al-Ḥassan al-. Miṣbāḥ al-mutahajjid wa silāḥ al-mutaʿabbid. Beirut: Muʾassisat Fiqh al-Shīʿa, 1411 AH.