Dhawil Qurba

Kutoka wikishia

Dhawil-Qurba (Kiarabu: ذوي القربى) ina maana ya kizazi, ndugu na jamaa wa karibu na Mtume (s.a.w.w) wameashiriwa katika kitabu kitakatifu cha Qur'an na kuarifishwa kuwa kuwapenda watu hao basi ni kama ujira wa risala ya Bwana Mtume (s.a.w.w). Kwa mujibu wa riwaya na hadithi zilizopokolewa kwa upande wa Mashia na hata Masuni Imam Ali bin Abi Talib (a.s), Bibi Fatma Zahra (a.s), Imam Hassan(a.s) na Imamu Hussein (a.s) ndio vielelezo vya Dhawil-Qurba wa Bwana Mtume (s.a.w.w).

Utambuzi wa maana(conceptology)

Maana ya Dhawil Qurba ni ndugu na jamaa wa karibu katika familia na kinasaba. Neno al-Qurba limekuja katika Qur'an mara kadhaa likiwa liomeambatana na neno Dhi kama ilivyokuja kwenye Dhil-Qurba , Dhawi kama ilivyo kwenye Dhawil-Qurba , au Uuli katika Uuli-Qurba na vile vile imekuja katika aya: ((قُل لّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلاَّ الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَى)) Katika Aya hii tunaona kwamba, hapa neo hili limekuja bila ya ziada na bila ya kutanguliwa na dhi, dhawi na kadhalika. Zamakhshari ambaye ni mfasiri wa Kisuni na mtambuzi mahiri wa lugha anasema: Makusudio ya al-Qurba katika Aya hii ni ndugu na jamaa wa karibu.

Neno al-Qurba katika Qur'an tukufu limetumiwa kwa maana ya jamaa, ndugu na watu wa karibu katika familia. Qurb katika lugha ya Kiarabu ina maana ya ukuruba katika nasaba, zama na wakati. Kwa mujibu wa hadithi, katika Aya ya Mawaddah (kuwapenda Ahlul Bait), na katika aya ya khumsi , na aya ya 7 ya Surat al-Hashr ambayo inasema: Mali aliyo leta Mwenyezi Mungu kwa Mtume wake kutoka kwa watu wa hivi vijiji ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na kwa ajili ya Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na msafiri, ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu. Na anacho kupeni Mtume chukueni, na anacho kukatazeni jiepusheni nacho, na mcheni Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu ni mkali wa kuadhibu. Aya hizi zimefasiriwa kwamba, jamaa wa karibu waliokusudiwa na aya hizo ni ndugu, kizazi na jamaa wa Bwana Mtume (s.a.w.w).

Misdaqi ya utambuzi

Makala asili: Aya ya Mawaddah

Kwa mujibu wa mtazanmo wa waislamu wa madhehebu ya Shia ni kwamba, makusuduio ya Dhil-Qurba katika Aya ya: ((...قل لّا أَسْأَلُكُمْ عَلَيْهِ أَجْرًا إِلاَّ الْمَوَدَّةَ فِي الْقُرْبَى)); Sema, sikuomnbeni ujira isipokuwa kuuwapenda watu wangu wa karibu, ni Imamu Maasumu(a.s) na inamjumuisha pia Bibi Fatma Zahra(a.s). Vile vile katika riwaya na hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo vya tafsiri na hadithi vya Ahlul Sunna, Imamu Ali (a.s), Bibi Fatma (a.s), Imamu Hassan na Hussein (a.s) wametajwa na kuarifishwa kuwa ni vielelezo wa al-Qurba yaani watu wa karibu.

Baadhi ya wafasiri wa Ahlu-Sunna wanasema kuwa: Aya hii inawahutubu Makureshi. Mwenyezi Mungu ameamuamrisha Mtume (s.a.w.w) ya kwamba awatake Makureshi kama hawataki kuamini kutokana na kuwa na nasaba na Mtume, basi wasimfanyie uadui. Aidha kwa mujibu wa nukuu, Aya hii inawahutubu Ansari kutoka upande wa Salma bint Zeid Najar mama wa Abdul-Mutallib na wajomba wa Amina mama wa Mtume (s.a.w.w) ambao walikuwa na ukuruba na undugu. Watu hao walileta mali kwa ajili ya Mtume (s.a.w.w), lakini Aya hii ikashuka na Mtume akakataa mali yao.

Hukumu za fikihi

Baadhi ya hukumu za fikihi zinazohusina na jamaa wa karibu (Dhawil Qurba):

  • Fungu (hisa) la Dhawil Qurba katika Khumsi: Wanazuoni wa fikihi wa madhehebu ya Shia wanaamini kwamba, hisa ya Dhawil Qurba iliyokuja katika Aya ya Khumsi ni mali ya Imam Maasumu na wameiweka hisa hiyo kando ya fungu na hisa ya Mwenyezi Mungu na hisa ya Mtume na kuitaja kuwa hisa na fungu la Imam. Na kuna wakati pia fungu la Imam hutajwa pia kuwa ni hisa na fungu la Dhawil-Qurba.
  • Fungu la Dhawil-Qurba katika Aya ya ((...مَّا أَفَاء اللَّهُ)): Dhawil Qurba ni katika matumizi ya mafungu sita (ghanima ambazo zinameangukia mikononi mwa waislamu bila ya kupigana vita).

Vyanzo

  • Alusi, Sayyid Mahmoud, Ruhul Maani Fi Tafsir al-Qur'ani al-Adhim, kimehakikiwa na Ali Abdallah Atiyah, Beirut, Darul Kutub al-Ilmiyah, 1415 Hijria.
  • Ibn Barraj Tarabulusi, Al-Muhadhib, Qum, Ofisi ya Uchapishaji ya Kiislamu, yenye mfungamano na Jumuiya ya Mudarrisin katika Hawza (Chuo Kikuu cha Kiislamu) ya Qum, 1406 Hijria.
  • Ibn Hanbal, Ahmad, Fadhail al-Sahabah, Cairo, Darul Ibn al-Jawzi, 1330 Hijria.
  • Ibn Faris, Maqayis al-Lugha, Qum, Maktab al-I'lam al-Islam, 1404 Hiria.
  • Ibn Kathir, Ismail bin Omar, Tafsir Ibn Kathir, kimehakikiwa na Yusuf Abdul Rahman, Mar'ashi, Beirut, Darul Maarifah Lil-Tabaa Wanashr Watauzii, 1412 Hijria/1999 Miladia.
  • Bukhari, Muhammad bin Ismail, Sahih al-Bukhari, uhakiki umefanywa na: Muhammad Zuheir bin Nassir al-Nassir, Beirut, Dar Tauq Najat, 1422 Hijria.
  • Hakim Neishabouri, Muhammad bin Abdallah, al-Mustadrak Alaa Sahihein, Cairo, Darul-Haramein Lil-Nashr Watibaa, 1417 Hijria.
  • Hurr Amili, Muhammad bin Hassan, Wasail al-Shia, Qum, Taasisi ya Aal Beit (as), 1409 Hijria.
  • Khui, Sayyid Abul-Qassim, Mustanad al-Ur'wat, Qum Lutfi, 1364 Hijria Shamsia.
  • Raghib Isfahani, Hussein bin Muhammad, al-Mufradat Fi Gharib al-Qur'an, Beirut, Dar al-Shamiah, 1412 Hijria.
  • Zamakhshari, Mahmlud, al-Kashaaf An Haqaiq Ghawamidh al-Tanzil, Beirut, Darul-Kutb al-Arabi, 1407 Hijria.
  • Sayyid Murtadha, Ali bin Hussein, Rasail al-Sharif al-Murtadha, Msahihishaji: Sayyid Mahdi Rajai, Qum, Darul-Qur'an al- Karim, 1405 Hijria.
  • Suyut, Jalal al-Din, Dur al-Manthur Fi Tafsir Bil-Maathur, Qum, maktaba ya Ayatullahil-Udhma Mar'ashi Najafi, 1404 Hijria.
  • Qurtubi, Muhammad bin Ahmad, al-Jamiul Ahkamil Qur'an, Tehran, Nasser Khosrow, 1364 Hijria Shamsia.
  • Qumi, Ali bin Muhammad, Jamiul Khilaf Wal-Wifaq, Qum, Waandaaji wa mazingira ya kudhihiri Imamu wa Zama 1379 Hijria Shamsia.
  • Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam, Beirut, Dar Ihyaa Turath al-Arabi, 1362 Hijria.