Aya ya 62 ya Suratu Al-Namli

Kutoka wikishia
Aya ya Amman Yujiibu

Aya ya 62 ya Suratu Al-Namli (Kiarabu: الآية 62 من سورة النمل) Ni Aya imuelezaye Mwenye Ezi Mungu, kuwa Yeye ndiye anayejibu maombi ya mwanadamu na kumwondolea dhiki zake, pale yeye anapokabiliwa na hali ngumu au dhiki maalumu. Pia, Aya hii inaashiria mamlaka na uongozi wa Mwenye Ezi Mungu uliotanda juu ya ardhi. Kulingana na mila na mazoea ya jamii za Kiislamu (hasa Mashia), Aya hii huwa inatambuliwa kwa jina la آیه اَمَّن یُجیب «Aya ya Amman Yujiibu». Jina hilo limezoeleka kutokana na sehemu ya mwanzo ya ibara ya Aya hii ilivyo. Waislamu wa madhehebu ya Shia huihisabu Aya hii kuwa dua yenye umuhimu mkubwa katika jamii zao. Pia wakati wa dhiki watu hupendekezwa kusomaji wa Aya hii ili kumwomba Mungu wao takhfifu ya kuondokewa na matatizo pamoja na dhiki walizonazo.

Baadhi ya wanazuoni wa Kishia, wakitegemea riwaya kutoka kwa Ahlul-Bait (a.s), wanaamini kwamba; Aya hii imeshuka kuhusiana na Imamu Mahdi (a.s), ambaye wanamwona yeye kuwa ndiye akisiko la halisi la mwenye dhiki «مُضطَر» aliyetajwa katika Aya hiyo, na hivyo Mwenye Ezi Mungu atajibu dua zake na hatimae kumfanya kuwa ndiye Khalifa (mtawala) wa ardhini humu. Allama Tabatabai, mmoja wa wafasiri mashuhuri wa Kishia, ametoa maelezo na ufafanuzi usemao kwamba; Imamu Mahdi (a.f) ni mmoja wa walengwa katika kushuka Aya hii, ila yeye siye mtu pekee aliyekusudiwa ndani ya Aya hii. Akiendelea na maelezo yake anasema kwamba; neno mudhtarru «مُضطَر» lililotumika kwenye Aya hii linawahusu watu wote wanaopitia dhiki na matatizo mbali mbali.

Moja ya mambo muhimu yenye misiguano ya tafakuri baina ya wafasiri mbali mbali wa Qur’ani, ni ibara isemayo «خُلَفاءَ الاَرض» (warithi au makhalifawa ardhi). Wafasiri wengi wa Kishia na Kisunni wametoa nadharia zao wakisema kuwa; ibara hiyo inamaanisha kuwa, katika kila kizazi (cha zama fulani), Mwenye Ezi Mungu huwa ana kawaida ya kuwapa baadhi ya watu fulani mamlaka ya kurithi na kuwaongoza wengine juu ya ardhi yake. Hata hivyo, kuna wafasiri wengine wanaoamini kuwa; urithi huu unahusu wanadamu wote kwa ujumla, ikimaanisha kwamba Mwenye Ezi Mungu amewapa wanadamu nguvu na uwezo wa kusimamia mambo yote yaliyomo duniani humu, pamoja na kutumia rasilimali zilizomo ndani yake.

Nafasi ya Aya Ndani ya Utamaduni wa Wanamii wa Kiislamu

Vilevile tazama: Aya Aman Yujiib

Aya ya 62 ya Surat Al-Naml inaanza kwa ibara isemayo: «اَمَّن یُّجیبُ المُضطَرَّ اِذا دَعاهُ وَ یَکشِفُ السُّوءَ» ikimaanisha maana isemayo; Basi ni [Nani] anaye mwitikia mwenye dhiki pale amuombapo na kumuondolea shida zake? Watu wa kawaida miongoni mwa Mashia, huifasiri Aya hii kwa maana ya dua, na watu wamejengeka desturi ya kufanya ibada maalumu ya dua inayoitwa «Khitma ya Amman Yujuubu». [1] Hata hivyo, ni vyema kufahamu kwamba muktadha wa Aya yenyewe hauhusiani moja kwa moja na masuala ya dua, bali ni ushauri wa wanazuoni ndio unaotoa pendekezo la kutumia Aya hiyo katika kuomba dua. Hivyo watu hutumia ibaza za Aya hiyo kwa kusema: «یا مَنْ یجیبُ الْمُضْطَرَّ إِذا دَعاهُ [2]» au «يَا مَنْ يُجِيبُ دُعَاءَ الْمُضْطَرِّ», ili kuomba msaada kutoka kwa Mola wao. [3]

Mirza Jawad Maliki Tabrizi ushauru wa maelezo yasemayo kwamba; Ni vyema kwa mtu aliyemaliza mwezi wa Ramadhani bila kuona mabadiliko yoyote katika hali yake, kutumia Aya hii na kumlilia Mwenyezi Mungu kwa nia safi na kuomba msaada ili aondokewe matatizo na matatizo aliyonayo na kuboresha hali ya nafsi yake. [4]

Matni ya Aya na Tafsiri Yake

Katika Aya ya 62 ya Surat Al-Naml, swali la tatu kati ya maswali matano yanayouliza Mwenyezi Mungu kuwauliza washirikina, linawekwa wazi katika Aya hii pamoja na Aya zilizo tangulia kabla yake. Swali hili, ambalo linaendana na muktadha wa Aya zilizotangulia na zinazofuata baada yake, linatoa changamoto kwa wale wanaomshirikisha Mwenye Ezi Mungu. Hapa Mwenye Ezi Mungu anawauliza washirikina hao kwa kusema; Je ni nani anayestahili kuabudiwa: ni yule anayejibu dua ya mwenye dhiki na kuondoa shida zake, au miungu yenu isiyoweza kufanya chochote? Swali hili linakuja kama onyo na kielelezo cha uwezo wa Mwenye Ezi Mungu pekee juu ya viumbe vyake, huku likitoa msisitizo wa kutofautisha kati ya uwezo wa Mwenye Ezi Mungu na unyonge wa miungu bandia. [5]

اَمَّن یُّجیبُ المُضطَرَّ اِذا دَعاهُ وَ یَکشِفُ السُّوءَ وَ یَجعَلُکُم خُلَفاءَ الاَرضِ ءَاِلهٌ مَّعَ اللهِ قَلیلاً مَا تَذَکَّرُونَ


Ni nani anayemjibu mwenye dhiki pale ammwombapo, na kumwondolea matatizo yake, kisha akakufanyeni nyinyi kuwa ni warithi wa ardhi hii? Je, kuna Mungu mwingine (anayestahili kuabudiwa) pamoja na Mwenye Ezi Mungu? Shukurani zenu ni chache.



(Surat al-Namli: 62)


Sababu ya Kushuka kwa Aya

Wanazuoni kadhaa wa Kishia, akiwemo Sharfuddin Istrabadi (aliyefariki mwaka 965 Hijria), [6] Sharif Lahiji, [7] na Nu'mani (aliyefariki mwaka 360 Hijria), [8] wakitegemea Riwaya kutoka kwa Ahlul-Bayt (a.s), wanaamini kwamba; Aya ya 62 ya Suratu Al-Naml iliteremshwa kuhusiana na Imamu Mahdi (a.t.f.s). Katika moja Hadithi iliyosimuliwa na Imamu Swadiq (a.s) na kunukuliwa kwenye Tafsiri ya Qummi, ni kwamba; Aya hii inahusiana na Qaimu Aali Muhammad (Imamu Mahdi), ambaye ni mkombozi wa haki kutoka katika kizazi cha Mtume Muhammad (s.a.w.w), ambaye wanazuoni hawa wanamchukulia kuwa ndiye mudhtarr (mwenye dhiki) hasa aliyetajwa kwenye Aya husika. Imeelezwa kwamba baada ya yeye kusali akiwa kwenye eneo la Maqamu Ibrahim (ndani ya msikiti wa Makka) na kuomba dua, Mwenye Ezi Mungu ataitikia dua yake, atamwondolea dhiki zake, na hatimae kumfanya kuwa Khalifa juu ya ardhi hii. [9]

Nu'mani, naye akitoa tafsiri ya Aya hii katika kitabu chake Al-Ghaybah, akitegemea Hadithi kutoka Muhammad bin Muslim kutoka kwa Imamu Baqir (a.s) amebainisha akisema kuwa; Aya ya 62 ya Suratu Al-Naml iliteremshwa kwa ajili ya Imamu Mahdi (a.t.f.s), ambaye baada ya kudhihiri kwenye Kaaba, ataungwa mkono na Malaika Jibril huku akiwa pamoja na wafuasi wa kibinadamu wapatao 313 ambao watamkubali na kushikamana naye kisawa sawa. [10]

Allama Tabatabai (aliyefariki mwaka 1360 Shamsia), na Makarem Shirazi ambaye ni mfasiri wa Qur’ani, wanaeleza kwamba; kule kutajwa kwa sababu ya kushuka kwa Aya hii katika Hidithi hizo, ni moja tafsiri zinazo ashiria mfano hai ya Aya hiyo. Nao wanasema kwamba; Aya hii inajumuisha watu wote walioko katika hali ya dhiki, bila kujali wakati au nafasi walizo nazo. [11] Ali bin Ibrahim Qummiy, kwa upande wake, ameongeza akisema kuwa; kutoa mfano huo ni aina ya ta’wil, yaani kufasiri Qur'ani kwa kutumia maana ya ndani (batini) ya Qur'ani, na maana pana zaidi ya Aya hiyo inajumuisha muktadha wa maisha ya wanadamu wote. [12]

Uhusiano kati ya Dhiki na Kujibiwa kwa Dua

Vilevile tazama: Aya Aman Yujiib

Wafasiri wamejadili kwa kina maana ya ibara isemayo: «اَمَّن یُّجیبُ المُضطَرَّ اِذا دَعاهُ وَ یَکشِفُ السُّوءَ» yaani: Ni nani anayemuitikia mwenye dhiki anapomwomba na kuondoa shida zake (ispokuwa Mungu)? Katika kueleza uhusiano kati ya dhiki (idhtiraar) na kujibiwa kwa dua, wafasiri wamefafanua wakisema kuwa; mudhtarru ni yule mtu ambaye, kutokana na hali ya dhiki kali aliyo nayo, huwa hana chaguo jengine ila kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu peke yake. Kikawaida mtu huyu huwa amekata tamaa kabisa kuhusiana na msaada kutoka kwa viumbe wa Mungu, kwa hiyo akaamua kijisalimisha kwa Mwenye Ezi Mungu kwa dhati na kwa moyo mmoja. Hali hiyo ya kujisalimisha kikamilifu na kumtegemea Mwenye Ezi Mungu pekee ndiyo chanzo cha kujibiwa dua yake. Kwa mtazamo wa wafasiri wa Qur’ani, ni kwamba; mwenye dhiki (mudhtarru) ni yule mwenye dhiki kubwa mno, ambaye amekimbilia kwa Mola wake kwa lengo la kukidhiwa haja yake. [13]

Kulingana na wafasiri mashuhuri kama Fadhlu bin Hassan Tabarsi (aliyefariki mwaka 548 Hijria), Fat-hullah Kashani (aliyefariki mwaka 988 Hijria), na Makarim Shirazi, ni kwamba; Mwenye Ezi Mungu hujibu maombi ya kila mmoja bila ubaguzi. Hata hivyo, wamebainisha wakisema kuwa; dua ya mtu aliye katika dhiki (mudhtarru) huwa ina nguvu zaidi, hii ni kwa sababu mwombaji wake huomba dua yake huku akiwa na unyenyekevu wa hali ya juu kabisa, na maombi yake huwa yanatoka katika kina cha moyo wake. Kwa hiyo, hali ya dhiki imewekwa kama ni mojawapo wa masharti na sifa inayopelekea dua hiyo kupokelewa. [14] Muhammad Sabzewari (aliyefariki mwaka 1368 Shamsia) na Allama Tabatabai nao wameeleza wakesima kwamba; dhiki iliyotajwa katika Aya hii inawakilisha maombi ya kweli, ambayo yanatoka katika undani wa moyo wa mwombaji. [15] Hii inamaanisha kuwa dua iyombwayo kwa uhalisia wa kiroho na unyenyekevu kamili, hupata thamani maalumu mbele ya Mwenye Ezi Mungu.

Tafsiri Tofauti Kuhusiana na Warithi wa Ardhi

Wafasiri wametoa maoni mbalimbali kuhusu maana ya kifungu cha Aya hii kisemacho: khulafaa' al-ardh (warithi wa ardhi). Wafasiri wengi wa Kishia na Kisunni wameifasiri ibara hii wakisema kwamba; hii inaashiria kuwa, katika kila zama Mwenye Ezi Mungu, huwa na kawaida ya kuwapa baadhi ya watu nafasi ya kurithi nafasi za wale waliowatangulia, ili waendeleze maisha na washike nafasi za za uongozi ardhini humu. Miongoni mwa wafasiri wenye maoni haya ni: Sheikh Tusi, [16] Tabarsi, [17] Abul-Futuh Razi, [18] Faydhu Kashani, [19] Muhammad bin Jarir Tabari, [20] Ibn Kathir, [21] Tha'alibi, [22] Zamakhshari, [23] na Fakhr Razi. [24] Kwa mujibu wa tafsiri hii, urithi wa ardhi unawakilisha mwendelezo wa kizazi kimoja baada ya chengine, ambapo kila kizazi hupewa nafasi na jukumu la kuongoza, kutawala, na kuendeleza matakwa ya Mwenye Ezi Mungu ardhini humu. Ufafanuzi huu unaweka msisitizo juu ya mpango wa Mungu wa kuwakabidhi wanadamu nafasi ya usimamizi wa ardhi, huku kila kizazi kikiwa na jukumu la kuhakikisha haki, uadilifu, na ustawi wa dunia.

Kwa upande wa pili, Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai akieleza maana ya neno khalifa katika Aya hiyo, anasema kwamba; Ibara hii inasisitiza uwezo wa mwanadamu wa kusimamia ardhi na kuleta mageuzi juu ya kila kilichomo ardhini humo. Kwa mtazamo huu, kama dhiki na matatizo yanayomkumba mwanadamu humpelekea kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu kwa maombi ya kumtaka msaada. Basi kule Mwenye Ezi Mungu kumjibu dua yake, ni moja ya hatua ya kumkamilishia mwanadamu huyo ukhalifa na urithi wa ardhi hii, jukumu ambalo Mwenye Ezi Mungu amempa yeye kwa lengo la kusimamia viumbe na mazingira yake. Kulingana na mtazamo wa Allama Tabatabai, tafsiri nyingine za khalifa ambazo zinaashiria mwendelezo wa utawala kizazi kwa kizazi, hazilingani moja kwa moja na muktadha wa Aya hii. Kwa hiyo, anasisitiza kuwa; maana ya khalifa iliyokusudiwa hapa inaohusiana na nafasi ya mwanadamu kama msimamizi wa ardhi, mwenye jukumu la kuhakikisha uadilifu na utawala sahihi.  [25]

Tabarsi, katika moja ya tafsiri ambayo ameitaja kuwa ni dhaifu, amenukuu Riwaya kutoka kwa Ibnu Abbas isemayo kwamba; maana ya khalifa, inamaanisha kuwa Mwenye Ezi Mungu anawafanya Waislamu kuwa warithi wa nafasi zilizoshikwa na makafiri, na kuwapa makazi katika ardhi na miji yao, ili waweze kumtii Mwenye Ezi Mungu badala ya kuendeleza ukafiri uliokuwa ukitendwa na makafiri hao. [26] Hata hivyo, Allama Tabatabai amepinga tafsiri hii, na kusema kwamba; Aya iliyobeba neno khalifa lilioko katika Aya hiyo, imekuja kuwazungumza makafiri, haikuwa na mazungumzo na waumini. Hivyo basi kulingana maoni ya na Allama, kama tafsiri hiyo ingekuwa ni sahihi, basi ingebidi kuwalenga waumini badala ya makafiri, basi ni wazi kuwa lengo la Aya hii si kubadili utawala wa kidunia, bali ni kufafanua jukumu na nafasi ya mwanadamu katika ardhi hii. [27]

Je, Kulingana na Aya Hii, ni Wajibu Mtu Kumtiifu kwa Mtawala Wake?

Al-Suyuti (aliyeishi kati ya mwaka 849-911 Hijria), ambaye ni mfasiri wa kutoka upande wa madhehebu ya Kisunni, akitoa ufafanuzi kuhusiana na kipengele cha Aya husika kisemacho: «Kigezo:وَ یَجعَلُکُم خُلَفاءَ الاَرضِ» chenye maana isemayo kwamba; “Na (ni nani yule) anaye kufanyeni nyinyi kuwa viongozi (warithi) wa ardhi”. Amenukuu Riwaya kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w), ambayo kwa mujibu wake ni kwamba; ni wajibu kwa wanajamii kumtii khalifa (mtawala) aliyeko madarakani. Na kwamba iwapo mtawala huyo atakuwa ni mtu mzuri, basi hapatakuwa na matatizo juu ya suala hilo; lakini ikiwa ni yeye n mtu mbaya, basi Mwenye Ezi Mungu atamchukulia hatua na kumhukumu siku ya Kiyama. [28]

Hata hivyo, Allama Tabatabai ameipinga Riwaya hiyo, akieleza kwamba maana ya neno urithi (utawala) katika Aya hiyo, halina maana ya uongozi wa mtu fulani, bali ni mamlaka ya mwanadamu kama mwanadamu juu ya ardhi, pamoja na vitu vyote vilivyomo ndani yake. Zaidi ya hayo, ikiwa suala la mtu fulani kupewa mamlaka na uongozi, hupelekea wajibu wa kumtii mtu huyo bila masharti, basi wito na malinganio ya kidini hayatakuwa na maana; kwani Mwenye Ezi Mungu katika Qur'ani amewataja baadhi ya wafalme kama vile Nimrodi na Farao (Firauna) kuwa ni miongoni mwa wale aliowaneemesha kwa neema ya uongozi. Hivyo, inabidi kukubali kwamba ni wajibu kuwatii wafalme hao, jambo ambalo haliwezekani wala haliingii akilini. [29]

Rejea

Vyanzo