Aya ya 23 ya Suratu Al-Ahzab
Sura Husika | Surat al-Ahzab |
---|---|
Namba ya Aya | 23 |
Juzuu | 21 |
Maudhui | Agano la Waumini na Mwenyezi Mungu Kuhusu Kuandamana na Mtume katika Vita |
Mada Yake | Hamza bin Abdul-Muttalib, Ja'afar bin Abi Talib na Imam Ali (a.s) |
Mengineyo | Mashahidi wa Vita vya Badr na Uhud |
Aya ya 23 ya Suratu Al-Ahzab (Kiarabu: الآية 23 من سورة الأحزاب) Ni Aya inayo husiana na waumini walio shikamana na ahadi yao wailiyo muahidi Mola wao, ambao baadhi yao walikuwa tayari wamesha bahatika kufa kishihidi, huku wengine wakingojea kupata bahati hiyo. Kwa mujibu wa maoni ya Allama Tabataba'i, ahadi inayo kusudiwa ndani ya Aya hiyo ni ahadi ya kwamba; Pale wanapokutana na maadui zao wasikimbie, bali na wasimame imara pamoja na bwana Mtume (s.a.w.w).
Kuna sababu mbali mbali zilizo tajwa kuhusiana na sababu ya kushuka Kwa Aya hii. Kulingana na maelezo ya mwandishi wa tafsiri ya Manhaju al-Sadiqina, ni kwamba; Wafasiri na wanahadithi wengi wanaamini kwamba; Aya hii ilishuka kuhusiana na Imamu Ali (a.s), Hamza bin Abdul-muttalib, Ja'far bin Abi Talib na Ubaidah bin Harith. Pia kuna Hadithi iliyo pokewa kutoka kwa Imam Ali (a.s) kuhusina na uhakika huu. Vyanzo vya tafsiri vya Ahlu-Sunna vimenukuu ya kwamba Aya hii ilishuka kuhusiana na Anas bin Nadhar, ambaye ni mmoja wa masahaba wa bwana Mtume (s.a.w.w).
Tafsiri za Kishia katika kuelezea maana ya ibara isemayo: مَنْ قَضى نَحْبَه (Waliokwisha fariki) zasema kwamba; ibara hii inawaelezea wale waliokufa kishahidi, kama vile Hamza na Ja'far bin Abi Talib. Ama kuhusiana na wale ambao wanasubiri kufikia kifo cha aina hiyo ni Ali (a.s). Vyanzo vya Kisunni navyo vimemtaja Hamza na mashahidi wa vita vya Badr na Uhud kama ni mifano hai ya ibara hiyo.
Kwa mujibu wa maelezo ya Nasir Makarim Shirazi ni kwamba; Hakuna mgongano kati ya tafsiri na mifano iliyotajwa chini ya Aya hiyo, kwa sababu Aya hii ina maana pana zaidi, kiasi ya kwamba inajumuisha mashahidi wote waliokwisha tangulia pamoja na wale wote wanaosubiri kufa mashahidi. Aya hii imetumiwa sana katika kuakisi nafasi na hadhi za mashahidi; kwa mfano, baada ya kuuawa kwa Muslim bin Awsaja na Muslim bin Aqil, Imamu Hussein (a.s) alisoma Aya hii. Pia, imetumiwa katika ujumbe wa rambirambi kuhusiana na mashahidi mbali mbali.
Matini na Tarjumi ya Aya
Aya ya 23 ya Suratu Al-Ahzab inarejelea kundi maalum la waumini ambao walikuwa ni mwanzo zaidi katika kumfuata bwana Mtume (s.a.w.w) kuliko wengine, ambao waliosimama imara katika ahadi zo walizo muahidi Mwenye Ezi Mungu (kujitoa muhanga hadi pumzi ya mwisho) katika kuuhami Uislamu. Baadhi yao walitimiza ahadi yao na kuuawa mashahidi, na wengine bado wanasubiri, bila kubadili au kugeuza ahadi zao, na bila kupotoka au kuyumba katika matendo yao. [1] Aya hii katika Qur’ani imekuja kama ifuatavyo:
﴾مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ ۖ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَىٰ نَحْبَهُ وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ ۖ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلًا﴿
Miongoni mwa Waumini wamo watu waliosadikisha (na kutimiza) waliyoahidiana na Mwenyezi Mungu. Basi kati yao wapo waliokwisha timiza ahadi yao (na wameuawa kishahidi), na kati yao wapo wanaongojea, na wala hawakubadili hata kidogo (ahadi zao).
(Surat al-Ahzab: Aya ya 23)
Sababu ya Kuteremka kwa Aya Hii
Kuna Sababu mbalimbali zilizo tajwa kuhusiana na sababu ya kuteremka kwa Aya ya 23 ya Surat Al-Ahzab. Kwa mujibu wa maelezo ya Mulla Fathullah Kashani (aliyefariki mwaka 988 Hijria) katika tafsiri yake ya Manhaju al-Sadiqin, ni kwamba; Wengi wa wafasiri na wapokezi wa Hadithi wanasema kwamba, Aya hii iliteremka kuhusiana na watu kadhaa, ambao ni: Imamu Ali (a.s), Hamza bin Abdul-Muttalib, Ja'far bin Abi Talib, na Ubaidah bin Harith. [2] Pia, katika sehemu nyingine, amenukuu akisema kwamba; sababu ya kuteremka kwa Aya hii inahusiana na kundi fulani la Masahaba kama vile; Hamza bin Abdul-Muttalib, Mus'ab bin Umair, na Anas bin Jabir. Ambao walikuwa wameweka nadhiri ya kwamba daima watakuwa pamoja na bwana Mtume (s.a.w.w) vitani na hawatakuwa na raha hadi wafe mashahidi. Waumini hawa walisifiwa na Mwenye Ezi Mungu katika Aya ya 23 ya Surat Al-Ahzab, kwa kukiri ya kwamba wao walikuwa ni waaminifu katika ahadi yao hiyo. [3] Kwa mujibu wa moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Ali (a.s), ni kwamba; Aya hii iliteremka kuhusiana na yeye mwenyewe, pamoja na Hamza, Ja'far, na Ubaidah bin Harith. [4]
Katika tafsiri ya Tabari, imeelezwa ya kwamba; Aya hii iliteremka kuhusiana na kundi la watu ambao hawakupata bahati ya kuuawa mashahidi katika vita vya Badr; kisha wakawekea ahadi Mwenye Ezi Mungu ya kwamba wao watapigana na bega kwa bega pamoja na bwana Mtume (s.a.w.w) dhidi ya washirikina. Kisha baadhi yao waliuawa mashahidi, huku wengine ambao hawakubahatika kuuawa wakiwa wamebaki wakisubiri shahada hiyo. [5]
Katika vyanzo vya Ahlus-Sunna, vimenukuu ya kwamba; Anas bin Malik amesimulia akisema kuwa Aya hii iliteremka kuhusiana na ami yake, ambaye ni Anas bin Nadhri. Anas, ambaye hakuwepo katika vita vya Badr, alisema ya kwamba; Mimi nilikosa kushiriki vita vya mwanzo vya Mtume (s.a.w.w) dhidi ya washirikina, hivyo basi, kama kutatokea vita vingine, nitapigana bega kwa bega pamoja na Mtume (s.a.w.w). Kisha akahudhuria vita vya Uhud na kupigana hadi naye akafa shahidi. [6]
Tafsiri
Kwa mujibu wa maoni ya Allama Tabataba'i, ibara isemayo: (صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَیْهِ ; Wametimiza yale waliyo muahidi Mwneye Ezi Mungu), inamaanisha kwamba; Waumini hao walithibitisha ukweli wao katika kile walichoahidiana na Mtume wa Alla (s.a.w.w). Na Ahadi hiyo ilikuwa kwamba; wakati watakapokutana na maadui zao, katu hawatakimbia wala kugeuka nyuma na kuwapa visogo maadui hao. [7] Ama ibara isemayo: (فَمِنْهم مَنْ قَضى نَحْبَه ; Miongoni mwao kuna waliouawa kishahidi). Inamaanisha kwamba; Baadhi ya waumini walifikwa na ajali zao na kufa au kuuawa katika njia ya Mwenye Ezi Mungu, na baadhi wengine (مَنْ يَنْتَظِر ; Wanaosubiri}}, ni wale wanasubiri kufikwa na ajali zao ambao pia nao hawajavunja ahadi zao. [8]
Neno (نَحْب) linaweza kuwa na maana kadhaa, kama vile; nadhiri, ahadi, kifo, na hatari. [9] Tabarsi, Mulla Fathullah Kashani, Raghib Isfahani na Allama Tabatabai wakinukuu kutoka kwa Raghib katika chake “Al-Mufradat”, wamesema kwamba; maana msingi ya neno (نَحْب ; nahbu}} ni nadhiri, na (قَضی نَحْبَه ; qadhaa nahbahu) inamaanisha kutimiza nadhiri; lakini wanakubaliana ya kuwa maana ya neno (نحب) katika aya ya 23 ya Suratu Al-Ahzab ni kufa au kuuawa katika njia ya Mwenye Ezi Mungu.
Mifano Hai na Lengwa ya Aya Hii
Kuna tofauti za maoni kati ya wafasiri kuhusiana na tafsiri ya Aya hii. Tafsiri ya Qumi [14] na tafsiri ya Al-Tibyan ya Sheikh Tusi, [15] wakinukuu kutoka kwa Imamu Baqir (a.s), wameeleza ya kwamba; Wale waliokufa mashahidi wanaokusudiwa katika Aya hii ni, Hamza na Ja'far bin Abi Talib, na wale wanaosubiri ni Ali (a.s). Hii pia imeelezwa na Hakim Hasakani (aliye fariki mano mwaka 490 Hijria), ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wa Ahlu-Sunna aliye nukuu habari hii katika chake Shawahid al-Tanzil kutoka kwa Ibn Abbas. [16] Katika moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Ali (a.s), imeelezwa ya kwamba; Aya hii ilishuka kuhusiana nasi; na ninaapa kwa jina la Mwenye Ezi Mungu, kwamba mimi bado nipo katika kungojea na hakuna mabadiliko yoyote yake yaliotokea katika subira yangu. [17]
Imepokewa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) kupitia Hadithi iliyo nukuliwa na Imam Swadiq (a.s), ya kwamba; Bwana Mtume alisema kumwambia Ali (a.s) ya kwamba: Yeyote anayekupenda kisha akufa katika hali hiyo, (فقد قَضى نَحْبَه ; Faqad qadhaa nahbahu), huyo atakuwa ametimiza ahadi yake, na yeyote anayekupenda ambaye bado hajafa, (فَهُوَ يَنْتَظِرُ ; Fahuwa yantadhiru) basi huyo yupo katika kungojea. [18]
Baadhi ya wafasiri wameeleza wakisema ya kwamba; ibara isemayo: «مَنْ قَضى نَحْبَه ; Man qadhaa nahbahu», inahusiana na mashahidi wa vita vya Badr na Uhud. [19]
Katika Tafsiri ya Muqatil bin Suleiman, moja ya tafsiri za karne ya pili Hijria, imeelezwa kuwa; Kutimiza ahadi kulikotajwa katika Aya hii, kunamaanisha ile ahadi ya usiku wa Aqaba (Baia ya Aqaba inayorejelea kiapo cha utii cha watu wa Yathrib kwa Mtume kabla ya hijra yake), na wale waliokufa mashahidi ni Hamza na wafuasi wake waliouawa katika vita vya Uhud. [20]
Pia imenukuliwa kutoka kwa Ibn Abbas kwamba; Maana ya «مَنْ قَضى نَحْبَه ; Man qadhaa nahbahu», ni Hamza na mashahidi wengine wa vita vya Uhud akiwemo Anas bin Nadhir na wenzake. [22] Katika baadhi ya vyanzo vya tafsiri, Talha bin Ubaydullah pia naye ameorodheshwa kama ni mfano hai wa «مَنْ قَضى نَحْبَه ; Man qadhaa nahbahu». [23]
Kwa mtazamo wa Ayatullah Makarem Shirazi, ni kwamba; Hakuna mgongano kati ya tafsiri na mifano tofauit iliyotajwa chini ya Aya hiyo. Hii ni kwa sababu ya kwamba Aya ina maana pana zaidi, inayowajumuisha ndani yake mashahidi wote wa Uislamu ambao walikufa kabla ya tukio la Vita vya Ahzab, pia inajumuisha kila shahidi wa zama na nyakati tofauti. Na kuhusisna na wanaosubiri, bila shaka Aya itakuwa inajumuisha wale wote waliokuwa wakisubiri kupata ushindi au kupata shahada. Bila shaka, watu kama Hamza na Ali (a.s) walikuwa ni watu wa kileleni mwa makundi mawili haya. [24]
Matumizi ya Aya
Aya hii imetumika mara kadhaa kuhusiana na mashahidi. Imenukuliwa ya kwamba; Imamu Hussein (a.s.) aliisoma Aya hii katika tukio la Karbala akiwa karibu na miili ya mashahidi wa Karbala, miongoni mwao akiwa ni Muslim bin Awsaja. [25] Pia inasemekana kwamba; aliisoma Aya hii wakati aliposikia habari za kuuawa kwa Muslim bin Aqil. [26] Imam Khomeini naye katika ujumbe wa rambirambi kufuatia kuuawa kwa Ata’ullah Ashrafi Esfahani, mmoja wa mashahidi wa mihadhara, aliitumia Aya hii akimwelezea kama mfano hai wa ibara ya Qur’ani isemayo: «رِجالٌ صَدَقُوا ما عاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ», akimaanisha kwambe; Yeye ni miongoni mwa waliotimiza ahadi za katika kuutetea Uislamu. [27] Pia Aya hii imeonekena kutumika katika kumbukumbu za mashahidi na ujumbe wa rambirambi kuhusiana na mashahidi, [28] pamoja na ujumbe wa rambirambi wa wanazuoni na viongozi wa kidini, kufuatia kuuawa kwa Kamanda Soleimani. [29]
Aya hii imeandikwa kwenye Haram ya Imamu Hussein (a.s) juu ya mlango uitwao Babu al-Shuhada [30] na Babu Ras al-Hussein (a.s). [31]
Maktaba ya Picha
-
آیه ۲۳ سور احزاب نصب شده در دیدار آیت الله خامنهای با خانواده سردار سلیمانی در اولین سالگرد شهادتش. ۱۳۹۹ش.
-
خوننامه یگان دیدبانی گردان ادوات لشکر ۳۲ انصارالحسین همدان در ۲ دی ۱۳۶۵ش.
-
پوستر تایپوگرافیکی آیه ۲۳ احزاب با استفاده از خط ثلث و ترکیب رنگ پرچم ایران از مسعود نجابتی، طراح و خوشنویس ایرانی.
-
آیه ۲۳ احزاب بر روی سنگ قبر حسن شحاته، از رهبران شیعیان مصر.
-
درج بخشی از آیه ۲۳ سوره احزاب در لوگوی بنیاد شهید و امور ایثارگران