At-Taliqah

Kutoka wikishia

At-Taliqah maana yake ni wale walioachwa huru, ikimaanisha kundi la wapinzani wa Mtume (SAW) ambao, baada ya Mtume Muhammad (s.a.w) kuitangaza na kuipigania dini ya haki ya Mwenyeezi Mungu kundi hilo halikukubali maamrisho ya Mtukufu Muhammad. Abu Sufiyani na mwanawe Mu'awiya ni miongoni mwa kundi hili mashuhuri. Katika vita vya Saffain, Imam Ali (a.s.) aliwatambulisha watu wa kundi hilo kuwa ni wale ambao daima walikuwa maadui waliouchukia Uislamu na hawakuwa na Imani thabiti juu ya dini ya Kiislamu. Talqaa ni neno la dharau ambalo lilitumika kwa Bani Umayyah, na kwa msingi huu, hawakuhesabiwa kuwa wanastahiki ukhalifa na uongozi.

UFAFANUZI WA MSAMIATI (NENO) T’ALIQAA

T’aliqa maana yake ni mateka aliyeachiliwa huru. [1] Mtume (SAW) alitumia neno hili baada ya ushindi wa Makka, akimaanisha kundi la watu wa Makka. [2] watu ambao walikuwa ni miongoni mwa wapinzani wa Mtume, watu hao hawakuwa na Imani thabiti ya dini ya kiislamu, bali waliikubali dini ya Kiislamu baada ya kutekwa katika mji wa Makka. Mtume (s.a.w.w.) hakuwafanya watu hao kuwa ni watumwa na akawaita taliqaa, ambayo ina maana ya watu waliyoachwa huru.[3] Kwa mujibu wa maelezo ya Sayyed Mohammad Hussein Tehrani, mwanazuoni wa Kishia wa karne ya 14, Yeye alisema kabla ya kutekwa kwa Makka, watu wa kundi hilo walisema muacheni Muhammad na wafuasi wake, ikiwa atawashinda tutasilimu, na wakimshinda Muhammad, watu wake watatuokoa kutoka kwake. . 4] Talqaa, kwa maana nyengine pia hukusudiwa "Waislamu wa ushindi wa Makka"

Idadi na watu wa kundi la T’aliqaa

Kwa mujibu wa baadhi ya ripoti za kihistoria, kundi hilo la watu walioachiwa huru walikuwa zaidi ya watu elfu mbili. [6] Pia, katika vyanzo vya kihistoria, imethibitishwa kuwa miongoni mwa watu hao hao walioachiwa huru ni hawa wafuatao: Abu Sufyan, Mu’awiyah bin Abiy Sufiyani, Yazid bin Abu Sufiyani, Suhail bin Amr, Huwaytab bin Abdul Uzzai, [7] Jabir bin Matam, Ikramah bin Abi Jahl, Atab bin Asaid, Safwan bin Umayyah, Muti bin Aswad, Hakim bin Hizam, Harith bin Hisham na Hakem bin Abi al-As[8] .

Hasan bin Farhan Maliki (aliyezaliwa mwaka 1390 Hijiria), mwanazuoni wa Kisunni, ameligawa kundi la watu wa Talqaa katika makundi matatu kulingana na vyeo na nafasi zao:

  • Kundi ambalo Mtume alikuwa anaamini katika usahihi wa imani zao na hakuwapa chochote katika mali na zaka.; miongoni mwa watu wa kundi hilo ni Kama Ikramah bin Abi Jahl, Atab bin Asaid na Jubeir bin Mut'am.
  • Kundi ambalo Mtume aliwapa mali na zaka ili kuhamasisha nyoyo zao waikubali dini ya Kiislamu; watu hao walijulikanwa kam (مؤلفةالقلوب)mualliffatul Quluwb, miongoni mwao ni Abu Sufyan, Mua’wiya, Safwan bin Umayya na Mut’ii bin Aswad. Kundi hili linachukuliwa kuwa ni kundi la chini kabisa la Talqaa.

muallifatul-Quluwb

Ili kufahamu maana ya muallifatul-Quluwb na tuisome ibara hii ifuatayo: Katika istilahi Muallifatul-Qluwb ni makafiri ambao, Mtume aliwahamasisha kuikubali dini ya Kiislamu kuwa ni dini ya haki, na ili kuwafanya wawe na Imani thabiti aliwagaia mali katika sehemu ya zaka ili nyoyo zao zivutiwe na kuelekea kwenye Uislamu.

  • Kundi la tatu ni kati ya kundi la kwanza na la pili, Harith bin Hisham, Suhail bin Amr na Hakim bin Hizam, walitambulishwa kutoka kwa watu wa kundi hili.[9]

Bani Ummayyah

Kulingana na baadhi ya wanadharia wa kisasa, wamesema’ tafsiri ya Taliqaa ina maana ya aina ya unyanyapaa, [10] na kwa msingi huu, Bani Ummayyah walijulikana kama ni kikundi cha watu, au wanachama wenye wazo moja fikra moja, na wana wafuasi wanaowafuata. Hadhrat Ali (a.s.) alimwita Mu’awiyah, kuwa ni mmoja wa watu wa kundi la Taliqaa kwa hiyo, hakumwona kuwa anastahiki ukhalifa, uimamu, uongozi au kumtaka ushauri. [12] Imam Ali (a.s.) pia katika vita vya Safein aliwachukulia watu wa kundi la Taliqaa kuwa ni wale ambao hawakuwa na Imani thabiti ya dini ya kiislamu, walisilimu lakini daima walikuwa katika vita na Uislamu. [13] Ali bin Abi Talib (a.s.) aliwatambulisha watu wa kundi hilo kuwa ni maadui wa Qur’ani, Sunna za Mtume, na ni watu waliokuwa wakitowa au kupokea rushwa na hongo.

Hadhrat Zainab (pbuh), katika khutuba aliyoitowa alipokuwa mateka wa Yazid bin Muawiyah, alimwita Yazid kuwa ni mwana wa Talqaa.[15] Kwa mujibu wa kile ambacho Ahmad bin Yahya Balazri, mwanahistoria wa karne ya 3 Hijiria, alichotoa katika kitabu chake Ansab al-Ashraf, alithibtisha kuwa Umar bin Khattab alikuwa miongoni mwa kundi la Taliqa na kizazi na watoto wao hawakustahiki kupewa ukhalifa wala uongozi.

VYANZO

  • Balazri, Jamal Min Ansab al-Ashraf, 1417 AH, Juz. 10, uk. 434-435; Ibn Hajar Asqlani, the injury, 1415 AH, juzuu ya 4, uk.70.
  • Ibn Hajar Asqlani, Al-isaba fi Tamiyiz Sahabah, Utafiti: Adel Ahmed Abd al-Mawat na Ali Muhammad Maawad, Beirut, Dar al-Kitab Al-Alamiya, 1415 AH/1995 AD.
  • Ibn Qutaibiyya al-Din Nuuri, Abdullah bin Muslim, Uimamu na siasa, utafiti: Ali Shiri, Beirut, Dar al-Audhaa, chapa ya kwanza, 1410 AH.
  • Ibn Mandhur, Muhammad Ibn Mukram, Lisanul-A’rab, kilichohaririwa na Ahmad Fars, Beirut, Dar al-Fikr, 1414 AH.
  • Ibn Hisham, Al-Sirah al-Nabawiyya, Abdul Malik Ibn Hisham, utafiti: Mustafa al-Saqqa, Ibrahim al-Abiari na Abdul Hafiz Shibli, Beirut, Dar al-Marafa, Bita.
  • Balazri, Ahmed bin Yahya, Kitabu cha Jamal Min Ansab al-Ashraf, utafiti: Sohail Zakar na Riaz Zarkali, Beirut, Dar al-Fikr, 1417 AH/1996 AD.
  • Jawadi, Seyyed Mahdi, "T’aliqaa na nakshi yao katika historia ya Uislamu", katika jarida la utafiti wa historia, nambari 12, vuli 2007.
  • Husseini Tehrani, Seyyed Mohammad Hossein, Imamshinasi, Mashhad, Allamah Tabatabai uchapishaji, 1426 AH.
  • Tabarsi, Ahmad bin Ali, Al-Ihtijaj Ali Ahlul al-Jajj, Mashhad, chapa ya Murtadha Publishing House, 1403 AH.
  • Tabari, Muhammad bin Jurayir, Taarikh Al-Umam wa Al-Muluk, Beirut, Dar al-Tarath, 1378.
  • Maliki, Hasan bin Farhan, Swahbatu na Sahaba Al- it’laq ya Lughawi wa Al-Tahsis Shari’i, O’man, Kituo cha Mafunzo ya Al-Tarikhiya AD,
  • Maghdasi, Mutahari bin Taaher, al-Mashad na al Bus-I wa-Tarikh, Bursa'id, Al-Thaqafah Al-Diniyyah School, B.T.A.
  • Moqrizi, Ahmad bin Ali, Imta'a al-Isma'a ikijumuisha maneno ya Mtume, Ahwal wa Al-Amwal, Al-Hafdihi wa al-Mata'u, utafiti: Muhammad Abdul Hamid al-Namisi, Beirut, Dar al-Katb. al-Alamiya, 1420 AH/1999 AD.
  • Man-qari, Nasr bin Muzahim, Waaqqiat Saffain, utafiti: Abd al-Salam Muhammad Harun, Al-Arabiyyah al-Haditha, 1382 AH/ Offset: Qom, Uchapishaji al-Mar-ashi al-Najafi, 1404 AH.