Nenda kwa yaliyomo

Asadu Llahi (Lakabu)

Kutoka wikishia

Asadu Llahi (Kiarabu: أسد الله): Ni lakabu ya Imamu Ali (a.s)[1] na Hamza bin Abdu al-Muttalib.[2] Ibara hii ya “Asadu Llahi” yenye maana ya simba wa Mwenye Ezi Mungu, ni lugha ya kiistiari yenye kuashiria ushujaa wa watu wawili hawa.

Mtume wa Mwenye Ezi Mungu (s.a.w.w) alimwita Ali bin Abi Talib kwa jina la Asadu Llahi na Asadu al-Rasuli.[3] Pia katika baadhi ya vyanzo vya dini, Imamu Ali (a.s) ameonekana kupewa jina la Asadu Llahi al-Ghalib «اسدالله الغالب», lenye maana ya simba mshindi wa mwenye Ezi Mungu.[4]

Mashia wanaamini kwamba; jina hili ni jina tuuzi kwa ajili ya Imamu Ali peke yake (a.s). Jina hili lenye maana ya simba wa Mwenye Ezi Mungu, limeakisiwa na fasihi mbali mbali za lugha ya Kiajemi (Kifarsi). Jina hili linapatikana ndani ya mashairi ya washairi kadhaa wa Kifursi, akiwemo; Kisai Marwi,[5] Sa’adi,[6] ‘Attari Nishaburi[7] na ‘Ubaidu Zakani.[8]

Said Muhammad Hussein Shahriyar kuhusiana na Imamu Ali (a.s) anasema:

علی آن شیر خدا شاه عرب * اُلفتی داشته با این دل شب


شب ز اسرار علی آگاه است * دل شب محرم سرّالله است[9]

Ali ndiye yule simba wa Mungu na mfalme wa Warabu * Mwenye fungamano la upendo na huu usiku * Usiku ndio wenye kuelewa siri za bwana huyu wa ajabu * Siri zake Mungu zesitiriwa moyoni mwa usiku


Kwa upande mwengi; Hamza bin Abdu al-Muttalib naye alikuwa akijulikana kwa jina la Asadu Llahi[10] na Leithu Llahi (chui wa Mungu),[11] kutokana na ushujaa wake vitani. Bwana Mtume (s.a.w.w) alimtambulisha bwana Hamza kwa jina la Asadu Llahi na Asadu Rasuli llahi.[12] Kulingana na moja ya Riwaya zilizo nukuliwa katika moja ya vitabu maarufu vinne vya Kishia kiitwacho Al-Kafi, ni kwamba; hata kwenye Arshi ya Allah pia kumeandikwa ya kwamba, Hamza ni simba wa Mungu na simba wa mtume wake (s.a.w.w).[13]

Katika vita vya Badri bwana Hamza akiwa katika hamasa za mashairi ya kujinasibu vitani, alionekana akijinadi na kujitapa kwa jina la Asadu Llahi na Asadu Rasuli Llahi.[14] Katika moja ya sala na salamu alizosalimiwa nazo bwana Hamza na Maimamu Maasumu, ndani yake ametajwa kwa jina hili la Asadu Llahi.[15]

Kulingana na moja ya taarifa za idara ya usajili wa majina ya watoto, ni kwamba; jina la Asadu Llahi ni miongoni mwa majina 100 yashikayo nafasi ya kwanza miongoni mwa wanaume walio zaliwa nchi Iran kati ya mwaka 1297 hadi 1380 Shamsia.[16]

Rejea

  1. Ibnu Shahr Ashub, Manaqib Āli Abi Talib, 1379 S, juz. 3, uk. 259.
  2. Ibnu Abdul-Barr, al-Isti'ab, juz. 1, uk. 369.
  3. Ibnu Shahr Ashub, Manaqib Āli Abi Talib, 1379 S, juz. 3, uk. 259.
  4. Majlisi, Bihar al-Anwar, juz. 35, uk. 268.
  5. Kasai Marvazi, Divan Ash'ar. Mad-h Hadhrat Ali.
  6. Sa'di, Mawa'idh, Qasaid, Qasideh.
  7. Attar Neishaburi, Mantiq al-Tair, Fi Fadhilat Amir al-Mu'minin Ali bin Abi Talib Radhiyallahu Anhu.
  8. Ubaid Zakani, Divan Ash'ar.Tarkibat, dar Tauhid wa Munaqebat.
  9. Shahriyar, Divan Shahriyar, 1385 S, juz. 2, uk. 938.
  10. Ibnu Hayyun Maghribi, Sharh al-Akhbar, 1409 H, juz. 3, uk. 228.
  11. Ibnu Hajar, al-Isabah, 1415 H, juz. 5, uk. 512.
  12. Majlisi, Bihar al-Anwar, 1404 H, juz. 8, uk. 5.
  13. Kulaini, al-Kafi, 1407 H, juz. 1, uk. 224.
  14. Waqidi, al-Maghazi, 1409 H, juz. 1, uk. 68; Mufid, al-Irshad, 1413 H, juz. 1, uk. 74.
  15. Ibnu Qulawaih Qummi, Kamil al-Ziyarat, uk. 22.
  16. Guzareshi Jalib Az Yeksad Name Bartar Iraniyan Dar Qarne Hadhir.

Vyanzo

  • Ibn Ḥajar al-ʿAsqalānī, Aḥmad bin ʿAlī. Al-Iṣāba fī tamyīz al-ṣaḥāba. Mhariri: ʿĀdil Aḥmad ʿAbd al-Mawjūd & ʿAlī Muḥammad Muʿawwaḍ. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1415 AH.
  • Ibn Ḥayyūn, Nuʿmān bin Muḥammad. Sharḥ al-akhbar fī faḍāʾil al-aʾimma al-aṭhār. Mhariri: Muḥammad Ḥussein Ḥusseinī Jalālī. Qom: Daftar-i Nashr-i Islāmī, 1409 AH.
  • Ibn Qūlawayh, Jaʿfar bin Muḥammad. Kāmil al-zīyārāt. Mhariri: ʿAbd al-Ḥussein Amīnī, Najaf: Dār al-Murtaḍawīyya, 1356 Sh.
  • Kulaynī, Muḥammad bin Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Mhariri: ʿAlī Akbar Ghaffārī & Muḥammad Ākhūndī. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1407 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1403 AH.
  • Mufīd, Muḥammad bin Muḥammad al-. Al-Irshād. Mhariri: Muʾassisat Āl al-Bayt. Qom: Kungira-yi Sheikh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Wāqidī, Muḥammad bin ʿUmar al-. Al-Maghāzī. Mhariri: Marsden Jones. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī, 1409 AH.