Ammar bin Abi Salamah

Kutoka wikishia

Ammar bin Abi Salamah Dalani al-Hamdani (Kiarabu: عمّار بن أبي سلامة الدالاني الهمداني المعروف بعمار الدالاني) maarufu kwa jina la Ammar Dalani, alikuwa mmoja wa Maswahaba wa Mtume (s.a.w.w), askari wa Imam Ali (a.s) katika vita vya Jamal, Siffin, na Nahrwan, na ni katika mashahidi wa Karbala. [1]

Ammar anatokana na Bani Dalan moja ya kabila ya Hamdan. [2] Alijaribu kumuua Ibn Ziyad katika tukio la Karbala katika kambi ya Nakhila karibu na Kufa, lakini hakufanikiwa. Baada ya hapo, alijiunga na msafara wa Imamu Hussein (a.s.) [3] Katika baadhi ya vyanzo, pia ametajwa kwa jina la Amer [4].

Kwa mujibu wa riwaya ya Ibn Haiek Hamdani (aliyefariki mwaka 334 Hijiria) katika kitabu cha Al-Aklil minn Akhbar al-Yaman,, Ammar bin Abi Salamah alitoka Kufa kwa siri, alipigana na Zahar bin Qays na masahaba zake na akawashinda na akajileta kwa Imam Hussein (a.s). [5]

Ammar bin Abi Salamah aliuawa shahidi siku ya Ashura (10 Muharram), katika shambulio la kwanza (shambulio la jumla la jeshi la Omar bin Saad dhidi ya jeshi la Imam ). [6] Katika Ziyarah Nahiya isiyo maarufu, Ammar anasalijiwa kwa ibara hii: [7] «السَّلَامُ عَلَی عَمَّارِ بْنِ أَبِی سَلَامَةَ الْهَمْدَانِی ; Amani iwe juu ya Ammar bin Abi Salamahh al-Hamdani».

Muhammad bin Tahir Samawi (aliyefariki: 1370 Hijiria) amesimulia katika kitabu cha Ibsar al-Ain mazungumzo baina ya ammar na Imam Ali katika njia ya kutoka Dhi Qar kwenda Basra, akinukuuu hiilo kutoka katika kitabu cha Tarikh Tabari. Katika mazungumzo haya, Ammar anamuuliza Imam, utafanya nini utakapowafikia? Imam anajibu kwa kusema: "Nitawalingania kumtii Mwenyezi Mungu na wasipokubali, nitapigana nao." Ammar akasema: Katika hali hii, hawatamshinda mlinganiaji kwa Mungu. [8] Kwa mujibu wa vyanzo vya kihistoria, Imam Ali (a.s) alianza safari na jeshi lake kutoka Madina kwenda Iraq ili kukabiliana na Aisha, Talha na Zubeir alipokuwa njiani kuelekea katika vita hivyo vya Jamal alisimama katika eneo la Dhi Qar. [9]

Rejea

Vyanzo