Ali ni Walii wa Mungu

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Ali Walii wa Mungu)
Bendera ya Ali Walii Mwenyezi Mungu katika kaburi la Imam Ali (a.s) (1400)

Ali ni Walii wa Mungu (Kiarabu: علي ولي الله) ni nara na shaari za Waislamu wa madhehebu ya Shia kuhusiana na itikadi kwa Uimamu na Wilaya (uongozi) wa Imam Ali (a.s). Mashia wanaamini kuwa, Ukhalifa wa Imam Ali kwa umma wa Kiislamu ulikuwa baada tu ya kuaga dunia Bwana Mtume (s.a.w.w) na hilo lilitimia kwa amri na uteuzi wa Mwenyezi Mungu.

Katika adhana na iqama, baada ya kutoa shahada ya risala na Utume wa Mtume (s.a.w.w) ambayo hutanguliwa na shahada mbili, hutoa shahada pia kwamba, Ali Waliu Allah kwamba, Ali ni Walii wa Mungu, ingawa shahada hii kwa mujibu wa itikadi yao haihesabiwi kuwa ni sehemu ya adhana na iqama.

Mirza Qumi, alimu na mwanazuoni wa Kishia wa karne ya 13 Hijiria anatambua kusema: «علی ولی الله» baada ya «لا اله الا الله، محمد رسول الله» kuwa ni mustahabu. Kadhalika kwa mujibu wa mtazamo wa Sayyied Muhammad Hussein Husseini Tehrani ni kwamba, sentensi hizi kadhaa si zenye kutenganishika; akitumia hoja kwamba, tangu siku ya mwanzo ambapo Bwana Mtume (s.a.w.w) aliilingania Uislamu kaumu na jamaa zake wa karibu, alitoa amri pia ya kufuatwa Imam Ali (a.s).

Hii leo kuna sarafu zilizobakia ambazo zimeandikwa: «علی ولی الله» yaani Ali Walii wa Mungu ambazo ni mabaki ya zama za tawala za Kishia za Ismailia na Fatimiya ambapo sarafu ya kale zaidi miongoni mwazo inarejea katika nusu ya karne ya 14 Hijiria. Ibara hii inapatikana pia katika usanifu majengo wa Kishia na katika zama za Fatimiya; kama vile juu ya mihrabu ambayo iliongezwa mwaka 478 Hijria (1094 Miladia) katika msikiti wa Ibn Tulun huko Cairo Misri.


Daraja na utambuzi wa maana

Ali Walii wa Mungu «علی ولی الله» ni moja ya nara za wazi kabisa na Waislamu wa madhehebu ya Kishia kuhusiana na itikadi yao kwa Uimamu, Wilaya ya Imam Ali ambayo imechukuliwa katika Aya ya Wilaya na hadithi kama hadithi ya Wilaya na hotuba ya Ghadir. [3] Mashia wanaamini kwamba; «علی ولی الله» (Ali Walii wa Mungu) [4], uwalii huu ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu [5] na ukhalifa wake kwa umma wa Kiislamu baada tu ya kuaga dunia Mtume (s.a.w.w) nao ni uteuzi wa moja kwa moja kutoka kwa Mwenyezi Mungu. [6] Waislamu wa Kisunni wao wanaamini kwamba, Ali ni Khalifa wa Waislamu baada ya makhalifa watatu [7] na kama ilivyo kwa makhalifa wengine hawatambui kama ukhalifa wake ni kutoka kwa Mwenyezi Mungu. [8]

Ibara ya «علی ولی الله» (Ali Walii wa Mungu imekuja katika baadhi ya vitabu vinne vya Mashia (Kutub al-Ar'baa) ambapo imenukuliwa katika kitabu cha al-Kafi [9] na katika kitabu cha Man la yahdhuruh al-Faqih. [10] Aidha katika Ziyara zilizokuja katika vitabu hivi, Ali amehutubiwa na kutajwa kwa ibara ya « ولی الله» Walii wa Mungu) [11]. Katika baadhi ya hadithi katika vyanzo vya hadithi wa Kishia baada ya ibara ya «علی ولی الله» (Ali Walii wa Mungu) imetajwa ibara ya: «وَصیُّ رَسُولِ الله» (waasi na mrithi wa Mtume wa Allah), [12] na katika baadhi ya vyanzo Ali ametajwa kama: «خلیفةُ بعدِ رسولِ الله» (kiongozi baada ya Mtume wa Allah). [13] Baadhi ya masufi wa Kisunni pia, wametaja ibara ya «علی ولی الله» (Ali Walii wa Mungu) katika vitabu na athari zao. [14]

Katika hafla na kumbukumbu wanazofanya Mashia kwa ajili ya kuadhimisha Sikukuu ya Eidul Ghadir, hubandika mabango na bendera zenye ibara ya: «علی ولی الله» (Ali Walii wa Mungu). [15] Kadhalika huandika ibara hii katika pete. [16] Aidha kuandika ibara hii nyuma ya gari ni katika utamaduni wa baadhi ya Mashia nchini Iran. [17]

Shahada ya tatu

Makala asili: Shahada ya tatu

Mashia wakati wa kuadhini na kukimu Swala baada ya kushuhudia kwamba, Muhammad (s.a.w.w) ni Mtume na mjumbe wa Allah, hushuhudia pia kwamba, «علی ولی الله» (Ali ni Walii wa Mungu). [18] Hata hivyo mafakihi wa Kishia hawaitambui ibara hii kwamba, ni sehemu ya adhana na iqama; [19] kwa maana kwamba, kama usipoileta katika adhana na iqama, adhana na iqama yako havibatikili. Hata hivyo wengi miongoni mwao wameitambua kuwa inajuzu kwa ajili ya kupata thawabu. [20] Kadhalika Mashia kwa ajili ya kumsilimisha mtu na kumfanya aingie katika dini ya Kiislamu, baada ya shahada ya tawhidi na kumpwekesha Mwenyezi na shahada ya kwamba, Muhammad ni mjumbe na Mtume wa Allah humtamkisha mhusika, «علی ولی الله» (Ali Walii wa Mungu); hata hivyo shahada hii ya tatu si lazima ili mtu awe Muislamu, bali shahada mbili za awali zinatosheleza hilo. [22]

Katika hadithi zilizonukuliwa katika vyanzo na vitabu vya hadithi vya Kishia, ibara ya علی ولی الله imetajwa baada ya ibara «لا اِلٰهَ اِلّا الله، محمدٌ رسولُ الله» na inaaminika kwamba, kusema علی ولی الله baada ya ibara hiyo huwa sababu ya kusamehewa dhambi. [25] Sayyid Muhammad Hussein Husseini Tehrani mwanazuoni wa Kishia (aliaga duni 1374 Hijiria Shamsia) amesema kuwa, ibara hizi yaani: «لا اله الا الله، محمد رسول الله، علی ولی الله» si zenye kutenganishika. Anatumia hadithi ya Yaum al-Dar ambapo kwa mujibu wake katika siku ya kwanza Bwana Mtume (s.a.w.w) aliwalingania Uislamu kaumu na jamaa zake wa karibu, akawalingania kutamka shahada mbili na akawaamrisha kumfuata Imam Ali (a.s). [26]

Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, katika Siku ya Kiyama, juu ya mataji ambayo yatakuwa katika kichwa cha Mtume (s.a.w.w) [27] na Imam Ali (a.s) kutakuwa kumeandikwa ibara isemayo: «لا اله الا الله، محمد رسول الله، علی ولی الله». Mshabaha wa sifa kama hii umekuja na kunukuliwa katika baadhi ya hadithi nyingine kwenye vyanzo na vitabu vya Mashia. [29]

Aidha inaelezwa kuwa, ibara ya: «بسم الله الرحمن الرحیم، لا اله الا الله محمد رسول الله علی ولی الله» Ilikuwa imeandikwa katika bendera katika zama za utawala wa Fatimiya. [30]

Kuandikwa ibara ya «علی ولی الله» katika sarafu

Maneno Ali Waliyu-Allah kwenye dinari ijulikanayo kama Mostansarih dinar, ambayo ilitengenezwa na Arslan Basassiri mwaka 450 AD

Baadhi ya watawala wa tawala za Kishia, [32] Ismailiya [33] na Fatimiya [34] walitengeneza sarafu zikiwa zimeandikwa ibara ya: «علی ولی الله» yaani Ali Walii wa Mungu. Baadhi ya tawala hizo ni:

  • Utawala wa ukoo wa Bavand katika eneo la Tabaristan (leo ni sehemu ya Iran) katika nusu ya karne ya 14 Hijria. [45]
  • Daylami katika Gilan. [36]
  • Aal-Buweih, baada ya kuingia madarakani Basasiri (aliyeaga dunia 451 Hijria). [37]
  • Uljaytu, mtawala wa nane wa utawala wa Ilkhani, baada ya kubadilisha madhehebu yake na kuwa Shia. [38]
  • Sarbedaran (ulitawala 736-788 Hijiria). [39]
  • Ismailiya wa Alamut (walitawala 483-654). [40]
  • Safavi (utawala: 907-1135 Hijria). [41]

Aidha kumeripotiwa kuandikwa ibara ya «علی ولی الله» katika sarafu na watawala wasio wa Kishia kama Arghun mtawala wa nne wa ukoo wa Ilkhani (utawala: 683-690 Hijria), [42] na watawala wa Aq Qoyunlu (waliotawala 872-908 Hijria) [43]. Baadhi ya watafiti wa masuala ya historia wanasema kuwa, sababu ya hilo ni watawala hao kuwa na muelekeo wa madhehebu ya Shia [44] au kutaka kuwavutia Mashia. [45]

Katika majengo ya kihistoria na kidini

Maneno Ali Waliyu-Allah yaliandikwa kwenye moja ya madhabahu za msikiti wa Ibn Tulun huko Cairo, ambao ulijengwa wakati wa kipindi cha Fatimiya cha Moaz Mostansir (utawala wa 427-487 AH), Imam wa 18 wa Ismailia

Ibara ya «علی ولی الله» yaani Ali Walii wa Mungu ilikuwa ikiandikwa katika usanifu majengo wa Kishia [47] na katika kipindi cha utawala wa Fatimiyah. [48] Kwa mfano iliongezewa mihrabu katika mwaka 478 Hijiria (1904 Miladia) katika msikiti wa Ibn Tulun huko Cairo, ambayo ilikuwa imeandikwa ibara ya: «لا اله الا الله، محمد رسول الله، علی ولی الله»

Mihrabu hii ilitengenezwa katika zama za uukhalifa wa Muadh Mustansir Fatimi (utawala 427-487 Hijria), Imamu wa 18 wa Ismailiya. [50] Ibara ya «علی ولی الله» imeandikwa pia katika haram za baadhi ya Maimamu na watoto wa Maimamu; kama vile katika dharih ya Imam Ali (a.s) [54], dharih ya Imam Ridha (a.s) [55] na minara ya mnara wa haram ya Abul Fadh al-Abbas (a.s). [55]

Katika fasihi

Ibara ya « علی ولی الله» imeakisiwa pia katika fasihi ya lugha ya Kifarsi. Sayyid Ali Imaduddin Nasimi, mshairi wa Kisufi wa karne yay 8 Hijria ana beti za mashairi ambapo ametunia ibara hii. [57] Asiri Lahiji Nurbakhsi Sufi wa karne ya 9 Hijiria yeye pia ana beti za mashairi ambapo urari wake una ibara ya «علی ولی الله».


Rejea

Vyanzo