Umra ya mufrad
- Makala hii inahusiana na wasifu kuhusu mafuhumu na maana ya kifikihi na hivyo haiwezi kuwa kigezo cha amali na matendo ya kidini. Kwa ajili ya amali za kidini, rejea katika vyanzo vingine.
Al-Umra al-Mufrada (Kiarabu: العمرة المفردة) ni katika aina za Umra na mjumuiko wa amali (matendo) ambayo hufanywa kwa ajili ya kuzuru al-Kaaba (nyumba ya Mwenyezi Mungu). Umra al-Mufrada sio sehemu ya amali (matendo) ya Hija na ni kwa namna hiyo ndio maana iko mkabala (kinyume) na Umra al-Tamatui ambayo ni sehemu ya Hajj al-Tamatui.
Umra
- Makala asili: Umra
Umra ni mkusanyiko wa matendo (amali) ya kisheria kama kuvaa ihram, tawafu na [[kufanya sa'ayi baina ya swafa na marwa][1] ambayo hufanywa kwa lengo la kuzuru nyumba ya Mwenyezi Mungu.[2] Kuna aina mbili za Umra: Umra al-Tamatui na Umra al-Mufrada.[3] Umra al-Tamatui hufanywa pamoja na Hajj al-Tamatui na ni sehemu yake (ni sehemu ya Hajj al-Tamatui).[4] Umra al-Mufrada inajitegemea peke yake. Kwa maana kwamba, iko kando na Hajj al-Tamatui[5] Mafakihi wanasema, kutekeleza Umra kama ilivyo Hija ni wajibu kwa muislamu mara moja katika umri wake kwa yule aliyetimiza masharti[6] na kufanya zaidi ya mara moja ni mustahabu.[7]
Kupewa jina na vigawanyo vyake
Umra al-Mufrada imeitwa mufrada kutokana na kuwa siyo sehemu ya Hija na hufanywa peke yake.[8] Umra Qiraan na Ifraad ni katika vigawanyo vya Umra Mufrada. Umra Qiraan ni Umra ambayo ni ya mtu ambaye anapaswa kutekeleza Hajj Qiraan.[9] Umra ifrad ni Umra ya mtu ambaye anapaswa kutekeleza Hajj Ifrad (ni makhsusi kwa wakazi wa Makka).[10]
Amaali (matendo) ya Umra al-Mufrada ni
Umra al-Mufrada ina amali (matendo saba), ambayo ni kama ifuatavyo:
- Ihram
- Kufanya tawafu
- Sala ya tawafu
- Sa'ayi
- Kupunguza au kunyoa nywele
- Tawafu ya Nisaa
- Sala ya tawafu ya Nisaa.[11]
Kwa mujibu wa hadithi na kauli za mafakihi, Umra al-Mufrada inayofanyika katika mwezi wa Rajab ina fadhila kubwa sana kuliko Umra al-Mufrada inayofanyika katika miezi mingine.
Tofauti baina ya Umra Mufrada na tamatui
Umra Mufrada na Umra al-Tamatui zinatofautiana katika mambo kadhaa yafuatayo:
- Umra al-Mufrada ina tawafu nisaa na swala ya tawafu nisaa lakini Umra al-Tamatui haina.
- Ihram katika Umra al-Tamatui inapaswa kufungwa (kuvaliwa) katika miezi maalumu ya Hija (Shawwal, Dhul-Qaadah na Dhul-Hijja) lakini katika Umra al-Mufrada inawezekana kuvaa ihram katika miezi yote.
- Katika Umra al-Tamatui baada ya kufanya sa'ayi baina ya swafa na marwa ni lazima kupunguza kiwango fulani cha nywele au kucha; lakini katika Umra al-Mufrada inawezekana badala ya mtu kupunguza akanyoa nywele zote za kichwa (kunyoa kipara).[12]
- Katika Umra al-Tamatuui, miqat inapaswa kuwa katika moja ya vituo vitano; lakini katika Umra al-Mufrada mbali na miqati hizo tano inawezekana kufunga ihram sehemu ya karibu kabisa nje ya haram.[13]
Umra yenye fadhila zaidi
Kwa mujibu wa vitabu vya fiqh, Umra katika mwezi wa Rajab ina fadhila na thawabu nyingi zaidi ikilinganishwa na miezi mingine.[14] Jambo hili limebainishwa pia katika hadithi mbalimbali. Katika kitabu cha Wasail al-Shiah kuna hadithi zimenukuliwa kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w) na Imam Swadiq (a.s) ambazo zinabainisha kwamba, kufanya Umra katika mwezi wa Rajab ni Umra Mufrada yenye fadhila nyingi zaidi.[15][Maelezo 1]
Maelezo
- ↑ یادداشت
Rejea
- ↑ Muhaqqiq Hilli, Shara'i al-Islam, juz. 1, uk. 275
- ↑ Sheikh Tusi, al-Mabsut, juz. 1, uk. 296; Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 2, uk. 441
- ↑ Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh,juz. 5, uk. 479
- ↑ Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh,juz. 5, uk. 481
- ↑ Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh,juz. 5, uk. 485
- ↑ Tazama: Muhaqqiq Hilli, Shara'i al-Islam, juz. 1, uk. 274; Najafi, Jawahir al-Kalam, juz. 2, huk. 441
- ↑ Sheikh Tusi, al-Mabsut, juz. 1, uk. 297; Tim peneliti Bi'tsah Aytullah Khomenei, Muntakhab Manasik Haj, uk. 59
- ↑ Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 485
- ↑ Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 485
- ↑ Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 485
- ↑ Muhaqiq Hili، Shara'i al-islam، 1408 H، juz. 1، uk. 275.
- ↑ Muhaqiq Hili، Shara'i al-islam، 1408 H، juz. 1، uk. 275-276.
- ↑ Muassasah Dairah al-Ma'arif fiqh Islami, Farhang Fiqh, juz. 5, uk. 488
- ↑ Tazama: al-Durus al-Shariiya, 1417 H, ju. 1, uk. 337; Muhaqqiq Hilli, Shar'i al-Islam, 1408 H, juz. 1, uk. 276.
- ↑ Hur Amuli, Wasail al-Shiah, juz. 14, uk. 302
Vyanzo
- Hur Amuli, Muhammad bin Hassan, Tafshil Wasail al-Shi'ah ila Tahshil Masail al-Shari'ah, Qom: Muassasah Al Al-Bait, cet. I, 1409 H.
- Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqhi Islami, Farhang Fiqh Muthabeqe Mazhab Ahlibait (a.s), Qom: Muassasah Dairah al-Ma'arif Fiqhi Islami, cet. I, 1392 HS.
- Muhaqqiq Hilli, Ja'far bin Hassan, Sharayi' al-Islam fi Masail al-Halal wa al-Haram, Diteliti dan direvisi oleh: Abdul Hussein Muhammad Ali Baqqal. Qom: Ismailiyan, cet. II, 1408 H.
- Najafi, Muhammad Hassan, Jawahir al-Kalam fi Sharh Sharayi' al-Islam. Beirut: Dar Ihya al-Turats al-Arabi, cet. VII, 1404 H.
- Shahid Awal, Muhammad bin Makki al-Amuli. Al-Durus al-Shar'iyah fi al-Fiqh al-Imamiyah, Qom: Penerbit Islami, cet. II, 1417 H.
- Sheikh Tusi, Muhamamd bin Hassan. Al-Mabsuth fi al-Fiqh al-Imamiyah, Diteliti dan direvisi oleh Sayyied Muhammad Taqi Kashfi. Teheran: al-Maktabah al-Murtadhawiyah li Ihya' al-Athar al-Ja'fariyah, cet. III, 1387 HS.
- Tim peneliti Bi'tsah Ayatullah Khomenei. Muntakhab Manasik Hajj. Pnerbit Mash'ar, cet. II, 1426 H.