Nenda kwa yaliyomo

Abdallah bin Abil-Husayn al-Azdi al-Bajali

Kutoka wikishia

Abdallah bin Abil-Huswayn al-Azdi al-Bajali (Kiarabu: عبد الله بن أبي الحُصين الأَزدي البجلي) alikuwa ni katika maaskari wa Jeshi la Omar bin Sa’d katika tukio la Karbala na aliokuwa miongoni mwa askari waliokuwa chini ya amri Amr bin Hajjaj ambao walimfungia na kumzuia maji Imamu Hussein (a.s). Inaelezwa kuwa, Imamu Hussein alimlaani bwana huyu.

Jina na Nasaba

Abdallah bin Abil-Husayn ametajwa kuwa anatokana na kabila la Bajilah. [1] Jina lake katika vyanzo na vitabu mbalimbalio limetajwa kuwa ni Abdallah bin Husayn [2] na Abdallah bin Abil-Hussein al-Azdi. [3]

Kuweko Kwake katika Jeshi la Ibn Sa'ad

Abdallah bin Abi Husayn alikuwa mmoja wa askari wa Omar bin Sa'ad na katika kundi la Amr bin Hajjaj, ambaye alimnyima na kumzuia maji Imamu Hussein (a.s) na masahaba zake katika tukio la Karbala. Mnamo tarehe 7 Muharram, Ubaidullah bin Ziyad alimuandikia barua Omar bin Sa'ad na kumtaka amtenganishe Imam Husein (a.s) na maji. Barua hii ilipomfikia Omar bin Sa'ad, alimuamuru Amr bin Hajjaj kumzuia Imamu Hussein (a.s) na masahaba zake kufikia maji ya mto Furati. Kwa mujibu wa vyanzo, Abdullah bin Abi Husayn Azdi alimwambia Imamu Husein (a.s):

«Ewe Hussein, je, huoni maji kana kwamba, ni moyo wa mbingu! Wallahi hutakunywa hata fumba moja hadi ufe kwa kiu».

Imamu Hussein (a.s) alisema: «Ewe Mungu! Mfishe kwa kiu wala usimsamehe kamwe». [4] Kwa mujibu wa Hamid bin Muslim Azdi ni kuwa, Abdullah bin Abi Husayn Azdi aliugua baada ya tukio la Karbala, na haijalishi ni kiasi gani cha maji alichokunywa, lakini kiu yake haikuwa ikikatika mpaka alipofariki dunia. [5]

Rejea

Vyanzo