Nenda kwa yaliyomo

Abd al-Nabi al-Jazairi

Kutoka wikishia

Abd al-Nabii al-Jazairi (Kiarabu: عبد النبي الجزائري) (aliaga dunia 1021 Hijiria) alikuwa msomi wa Ilm al-Rijaal (elimu wa kuwatambua wapokezi wa hadithi) na msomi wa Kishia wa karne ya 11 Hijiria. Msomi huyu anahesabiwa kuwa aligawa watambuzi wa wapokezi wa hadithi katika makundi ya waasisi, wakamilishaji, wakusanyaji na wahakiki na alikuwa wa kwanza katika hilo. Pia alikuwa mbunifu katika kuwagawa wapokezi wa hadithi katika msingi wa migawanyo minne ya hadithi (sahihi, ya kutegemewa, nzuri na dhaifu).

Swahib Madarik na Muhaqqiq Karaki ni miongoni mwa maustadhi na walimu wake na vitabu vya: Hawi al-Aqwal katika elimu ya Rijaal na al-Mabsut fil Imamah katika maudhui ya Uimamu ni katika athari zake.

Historia Yake

Hakuna taarifa kuhusiana na tarehe aliyozaliwa Abd al-Nabi Jazairi. Baadhi wametambua tarehe yake ya kuzaliwa kwamba, takriban ni nusu ya karne ya 10 Hijiria wakitegemea ishara za walimu na wanafunzi wake.[1] Jina la baba yake limetajwa kuwa ni Sa’ad;[2] hata hivyo Abdallah bin Issa al-Afandi mwandika wasifu ametilia shaka kuhusiana na kwamba, jina la baba yake ni Sa’ad.[3]

Asili ya Abd al-Nabi Jazairi ni Jaza’ir.[4] Jaza’ir ni eneo lililoko nchini Iraq upande wa kaskazini magharibi mwa mji wa Basra na linatambulika kwa jina la Jibayish.[5] Abd al-Nabi Jazairi alisoma Najaf[6] na katika kipindi cha miongo miwili ya mwisho wa uhai wake alikuwa akiishi Karbala.[7] Aliishi katika zama moja na Swahib Maalim (aliyeaga dunia 1011 Hijiria), Swahib Madarik (aliyefariki dunia (1009 Hijiria) na Sheikh Bahai (ambaye aliaga dunia 1031 Hijiria) ambao ni miongoni mwa wanazuoni wa Kishia.[8]

Jazairi aliaga dunia 18 Jamadil Awwal 1021 Hijiria katika kijiji kilichoko baina ya mji Isfahan na Shiraz (miji ya Iran). Kaburi lake linapatikana katika mji wa Shiraz, Iran.[9]

Kusoma na Kufundisha

Abd al-Nabi Jazairi alisoma elimu za Kiislamu katika Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Najaf (Hawza) kinachopatikana katika mji wa Najaf, Iraq. Swahib Madarik[10] na Muhaqqiq Karaki[11] walikuwa miongoni mwa walimu wake; hata hivyo Abdallah bin Issa al-Afandi mwandishi wa wasifu, ametilia shaka kama Muhaqqiq Karaki ni mwalimu wake kutokana na tofauti ya umri baina yao.[12] Pamoja na hayo, Muhadith Nuri, msomi na mwanazuoni wa Kishia amemtambua Muhaqqiq Karaki kuwa ni mwalimu wa Abd al-Nabi Jazairi kwa kuzingatia ijaza (idhini) alioitaja Allama Majslisi katika kitabu chake cha Bihar al-Anwar, licha ya kuwa yumkini wakati Jazairi alipokuwa mwanafunzi wake alikuwa na umri mdogo.[13]

Jazairi alipata idhini pia kutoka kwa Swahib Madarik.[14]

Wanafunzi Wake:

Mwanzo wa Mageuzi Katika Ilm al-Rijaal

Baadhi wamewatambua Abd al-Nabi al-Jazairi na Sayyid Mustafa Tafrishi kuwa ni waanzishi wa zama za uchunguzi wa kina wa wapokezi wa hadithi na elimu ya Rijaal.[25] Suleiman bin Abdallah al-Mahuzi amemtambua msomi huyu kuwa ndiye aliyegawa watambuzi wa wapokezi wa hadithi katika makundi ya waasisi, wakamilishaji, wakusanyaji na wahakiki na aliyekuwa wa kwanza katika hilo,[26] ambapo alijihusisha na elimu ya Rijaal kiuhakiki na aliwatazama wapokezi wa hadithi kwa mtazamo wa jarh na taadil (kutokuwa na uadilifu na kuwa mwaminifu).[27] Hata hivyo kabla ya Jazairi, baadhi ya wanazuoni kama Shahidi Thani alijihusisha kuwatathmini wapokezi wa hadithi kwa njia ya ukosoaji ingawa hilo halijumuishi wapokezi wote wa hadithi na pande tofauti za elimu ya Rijaal.[28]

Al-Nabi Jazairi ni mtu wa kwanza ambaye aliwagawa wapokezi wa hadithi kwa misingi minne (sahihi, ya kutegemewa, nzuri na dhaifu).[29][30] Kabla yake hakukuwa na mgawanyo wa wapokezi wa hadithi kwa mgawanyo au kulikuwa kumefanyika mgawanyiko kwa mujibu wa misingi miwili ya hadithi (sahihi na dhaifu).[31]

Kwa mujibu wa Abu Ali Hairi mtambuzi wa wapokezi wa hadithi wa karne ya 13 Hijiria, Jazairi kama alivyokuwa Ibn Ghadhairi akthari ya watu ambao hawakustahiki sifa ya udhaifu aliwahesabu kuwa ni dhaifu.[32] Ahmad Bahrani msomi wa Kishia wa karne ya 11 Hijiria amenukuliwa pia akisema kuwa, Jazairi alikuwa mkali sana katika kuwadhoofisha wapokezi wa hadithi;[33] hata hivyo ukali wake huu ulipelekea kutumiwa kauli zake kwa ajili ya kuthibitisha uaminifu wa baadhi ya wapokezi wa hadithi ambao watu walihitalifiana.[34][35]

Kwa mujibu wa Sayyid Muhammad Baqir Khwansari ni kwamba, Jazairi alikuwa mahiri pia katika elimu za Fiqhi, Usul, theolojia, hadithi na kadhalika.[36]

Athari

Abd al-Nabi Jazairi ana athari mbalimbali katika nyanja na elimu za Rijaal, fiq’h, usul-fiq’h na teolojia.

Hawi al-Aqwal

Makala asili:Hawi al-Aqwal fi ma'arifat al-Rijaal (kitabu)
Hawi al-Aqwal

Hawi al-Aqwal fi ma’arifat al-Rijaal,[37] ni kitabu katika elimu ya Rijaal ambacho kutokana na ubunifu katika kukiandika, kimezingatiwa na wataalamu wa elimu ya Rijaal.[38] Katika kitabu hiki, msomi huyu amewagawa wapokezi wa hadithi kwa msingi wa migawanyo minne ya hadithi (sahihi, ya kuaminika, nzuri na dhaifu).[39] Kadhalika katika utangulizi na hitimisho la kitabu kuna maudhui kama fasili na maana ya Ilm al-Rijaal, utambuzi wa lakabu za Maimamu (a.s), kubainisha makundi saba ya Kishia[40] na As’hab Rijaal (kundi maalumu la wapokezi wa hadithi ambao kwa mujibu wa wasomi na wataalamu wa elimu hii, lina daraja ya juu zaidi katika uaminifu).[41]

Athari Zingine

Rejea

  1. Jazāʾirī, Hāwi l-aqwāl fī maʿrifat al-rijāl, juz. 1, uk. 11.
  2. Khāwnsārī, Rawḍāt al-jannāt, juz. 4, uk. 269.
  3. Afandī Iṣfahānī, Taʾlīqiyya amal al-ʾāmil, uk. 183.
  4. Khāwnsārī, Rawḍāt al-jannāt, juz. 4, uk. 268.
  5. Jazāʾirī, Hāwi l-aqwāl fī maʿrifat al-rijāl, juz. 1, uk. 39.
  6. Khāwnsārī, Rawḍāt al-jannāt, juz. 4, uk. 268.
  7. Jazāʾirī, Hāwi l-aqwāl fī maʿrifat al-rijāl, juz. 1, uk. 36.
  8. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 159.
  9. Afandī Iṣfahānī, Riyāḍ al-ʿulamāʾ, juz. 3, uk. 275.
  10. Ḥakīm, al-Mufaṣṣal fī tārīkh al-Najaf al-ashraf, juz. 4, uk. 261
  11. Ḥurr al-ʿĀmilī, ʾAmal al-āmil, juz. 2, uk. 165.
  12. Afandī Iṣfahānī, Riyāḍ al-ʿulamāʾ, juz. 3, uk. 273.
  13. Nūrī, Mustadrak al-wasāʾil, juz. 20, uk. 179.
  14. Ḥakīm, al-Mufaṣṣal fī tārīkh al-Najaf al-ashraf, juz. 4, uk. 261.
  15. Qummī, al-Kunā wa l-alqāb, juz. 2, uk. 331.
  16. Afandī Iṣfahānī, Riyāḍ al-ʿulamāʾ, juz. 7, uk. 139.
  17. Āqā Buzurg Tihrānī, al-Dharīʿa, juz. 5, uk. 252.
  18. Khāwnsārī, Rawḍāt al-jannāt, juz. 4, uk. 271.
  19. Jazāʾirī, Hāwi l-aqwāl fī maʿrifat al-rijāl, juz. 1, uk. 16, Utangulizi.
  20. Hurri Amili, Amalu al-amiliin, Maktabat al-Andolis, juz. 2, uk. 48.
  21. Ismailiyan, Rawdhat al-jannat, 1390 H, juz. 2, uk. 171.
  22. Hurri Amili, Amalu al-amiliin, Maktabat al-Andolis, juz. 2, uk. 48.
  23. Āqā Buzurg Tihrānī, al-Dharīʿa, juz. 1, uk. 207.
  24. Āqā Buzurg Tihrānī, Ṭabaqāt aʿlām al-Shīʿa, juz. 8, uk. 48.
  25. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 24.
  26. Baḥrānī, Miʿrāj ahl al-kamāl, Utangulizi wa mwandishi, uk. 7-24.
  27. Baḥrānī, Miʿrāj ahl al-kamāl, Utangulizi wa mwandishi, uk. 18-24.
  28. Baḥrānī, Miʿrāj ahl al-kamāl, Utangulizi wa mwandishi, uk. 23.
  29. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 159.
  30. Mazandarānī Ḥāʾirī, Muntahā al-maqāl, Utangulizi wa mwandishi, uk. 31.
  31. Mazandarānī Ḥāʾirī, Muntahā al-maqāl, Utangulizi wa mwandishi, uk. 31.
  32. Mazandarānī Ḥāʾirī, Muntahā al-maqāl, Utangulizi wa mwandishi, uk. 31.
  33. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 160.
  34. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 160.
  35. Kunturī, Kashf al-ḥujub, uk. 192.
  36. Khāwnsārī, Rawḍāt al-jannāt, juz. 4, uk. 269.
  37. Kunturī, Kashf al-ḥujub, uk. 192.
  38. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 164.
  39. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 159.
  40. Rabbānī, Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth, uk. 164.
  41. Ṭalāʾiyān, Maʾkhadh-shināsī-yi rijāl-i Shī'a, uk. 91.
  42. Āqā Buzurg Tihrānī, al-Dharīʿa, juz. 2, uk. 329.
  43. Āqā Buzurg Tihrānī, al-Dharīʿa, juz. 19, uk. 53.
  44. Khāwnsārī, Rawḍāt al-jannāt, 1390 H, juz. 4, uk. 271.
  45. Āl Maḥbūba, Māḍī l-Najaf wa ḥāḍiruhā, juz. 2, uk. 90.
  46. Āl Maḥbūba, Māḍī l-Najaf wa ḥāḍiruhā, juz. 2, uk. 90.
  47. Āl Maḥbūba, Māḍī l-Najaf wa ḥāḍiruhā, juz. 2, uk. 91.
  48. Āqā Buzurg Tihrānī, Ṭabaqāt aʿlām al-Shīʿa, juz. 8, uk. 358.
  49. Khāwnsārī, Rawḍāt al-jannāt, juz. 4, uk. 271.
  50. Āl Maḥbūba, Māḍī l-Najaf wa ḥāḍiruhā, juz. 2, uk. 91.

Vyanzo

  • Afandī Iṣfahānī, ʿAbd Allāh. Taʾlīqiyya amal al-ʾāmil. Edited by Aḥmad Ḥusaynī Ashkwarī. Qom: Kitābkhāna-yi Ayatullāh Marʿashī Najafī, 1410 AH.
  • Afandī Iṣfahānī, ʿAbd Allāh. Riyāḍ al-ʿulamāʾ wa ḥiyāḍ al-fuḍalāʾ. Edited by Aḥmad Ḥusaynī Ashkwarī. Beirut: Muʾassisa Tārīkh al-ʿArabī, 1431 AH.
  • Āqā Buzurg al-Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Al-Dharīʿa ilā taṣānīf al-shīʿa. Edited by Aḥmad b. Muḥammad Ḥusaynī. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1403 AH.
  • Āqā Buzurg Tihrānī, Muḥammad Muḥsin. Ṭabaqāt aʿlām al-Shīʿa. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1430 AH.
  • Āl Maḥbūba, Jaʿfar. Māḍī l-Najaf wa ḥāḍiruhā. Beirut: Dār al-Aḍwāʾ, 1406 AH.
  • Baḥrānī, Sulaymān b. ʿAbd Allāh. Miʿrāj ahl al-kamāl ilā maʿrifat al-rijāl. Edited by Mahdī Rajāʾī and ʿAbd al-Zahrāʾ ʿUwaynātī. [n.p], 1412 AH.
  • Dihkhudā, ʿAlī Akbar. Lughatnāma. Edited by Akram Sulṭānī and others. Tehran: Dānishgāh-i Tehrān, 1385 Sh.
  • Ḥurr al-ʿĀmilī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. ʾAmal al-āmil. Edited by Aḥmad Ḥusaynī Ashkwarī. Baghdad: Maktabat al-Andalus, [n.d].
  • Ḥakīm, Ḥasan ʾIsā. Al-Mufaṣṣal fī tārīkh al-Najaf al-ashraf. Qom: al-Maktaba al-Ḥaydarīyya, 1427 AH.
  • Jazāʾirī, ʿAbd al-Nabī. Hāwi l-aqwāl fī maʿrifat al-rijāl. Edited by Muʾassisa al-Hidāya li-Iḥyāʾ al-Turāth. Qom: Riyād al-Nāṣirī, 1418 AH.
  • Kunturī, Iʿjāz Ḥusayn b. Muḥammad Qulī. Kashf al-ḥujub wa al-astār ʿan asmāʾ al-kutub wa al-asfār. with an introduction by Shahab al-Dīn Marʿashī. Qom: Kitābkhāna-yi Ayatullāh Marʿashī Najafī, 1409 AH.
  • Khāwnsārī, Muḥammad Bāqir. Rawḍāt al-jannāt fī aḥwāl al-ʿulamā wa al-sādāt. Edited by Asadullāh Ismāʿīlīyān. Qom: Intishārāt-i Ismāʿīlīyān, 1390 AH.
  • Mazandarānī Ḥāʾirī, Muḥammad b. Ismāʿīl. Muntahā al-maqāl fī aḥwāl al-rijāl. Edited by Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1416 AH.
  • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Mustadrak al-wasāʾil wa musṭanbit al-wasā'il. [n.p], [n.d].
  • Qummī, Shaykh ʿAbbās. Al-Kunā wa l-alqāb. with an introduction by Muḥammad Hādī Amīnī. Tehran: Maktabat al-Ṣadr, 1368 SH.
  • Rabbānī, Muḥammad Ḥasan. Sabkshināsī dānish-i rijāl al-hadīth. Qom: Markaz-i Fiqh-i al-aʾimma al-Aṭhār, 1385 SH.
  • Ṭalāʾiyān, Rasūl. Maʾkhadh-shināsī-yi rijāl-i Shī'a. Qom: Muʾassisa ʿIlmī Farhangī Dār al-Ḥadīth, 1381 SH.