Wakuu wa Bani Israil
Wakuu wa Bani Israil au watawala wa jadi (watemi) (Kiarabu: نُقَباء بني إسرائيل) ni wawakilishi na wajumbe 12 kutoka katika makabila 12 ya Bani Israil (watoto wa Nabii Ya’qub) ambao walichaguliwa na Nabii Mussa (a.s) kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Jukumu lao lilikuwa ni kulinda agano na ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyoichukua na kuiweka kwa Bani Israil. Watemi na viongozi hao wa jadi walikuwa na jukumu la kukusanya taarifa za kaumu dhalimu katika safari ya kuelekea Baytul-Muqaddas. Nabii Mussa (a.s) aliwataka taarifa watakazopata wasizitoe kwa kaumu zao. Hata hivyo akthari yao walikiuka na kukiuka agizo hilo.
Katika vyanzo vya pande mbili (Masuni na Mashia) kumenukuliwa hadithi kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ambayo imetambua idadi ya warithi na viongozi baada yake ni 12 na wametambuliwa kuwa idadi yao ni sawa na idadi ya watemi na viongozi wa jadi wa Bani Israil. Hadithi hizi ni mashuhuri kwa jina la hadithi za makhalifa 12. Maulamaa wa Kishia huzitumia hadithi hizi kwa ajili ya kuthibitisha Uimamu wa Maimamu Kumi na Mbili.
Wakuu 12; Wawakilishi wa Nabii Mussa (a.s)
Wakuu 12 au viongozi wa jadi ni wawakilishi wa Nabii Mussa (a.s) katika kaumu zao [1] ambapo kwa mujibu wa baadhi ya hadithi waliteuliwa na Nabii Mussa 9as) kwa amri ya Mwenyezi Mungu. [2] Wafasiri wanasema kuwa, watemi hao ni kutoka katika makabila 12 ya Bani Israel au Mitume kutoka Bani Israel (watoto wa Nabii Ya’qub) [3] ambapo alichaguliwa mwakilishi mmoja kutoka katika kila kabila. [4]
Wawakilishi hao ni watemi na shakhsia wakubwa wa kaumu zao [5] na wana satwa na ushawishi kama ambavyo wana nafasi maalumu baina ya watu na katika makabila yao. [6] Katika baadhi ya vitabu vya tafsiri watu hawa wametambulishwa kuwa ni viongozi wa kaumu zao, [7] mkuu [8] na hata mfalme. [9] Kuna kundi pia ambalo linaamini kwamba, shakhsia na viongozi hao 12 baadaye waliteuliwa kuwa Mitume. [10] Kuna wengine ambao wametaja daraja yao kuwa ni kubwa zaidi, wamewatambua kuwa watu waliokuwa na kitabu zaidi ya Mtume wa kawaida na chini ya Ulul Azm (Mitume watukufu watano). [11]
((وَلَقَدْ أَخَذَ اللَّهُ مِيثَاقَ بَنِي إِسْرَائِيلَ وَبَعَثْنَا مِنْهُمُ اثْنَيْ عَشَرَ نَقِيبًا وَقَالَ اللَّهُ إِنِّي مَعَكُمْ لَئِنْ أَقَمْتُمُ الصَّلاةَ وَآتَيْتُمُ الزَّكَاةَ وَآمَنتُم بِرُسُلِي وَعَزَّرْتُمُوهُمْ وَأَقْرَضْتُمُ اللَّهَ قَرْضًا حَسَنًا لّأُكَفِّرَنَّ عَنكُمْ سَيِّئَاتِكُمْ وَلأُدْخِلَنَّكُمْ جَنَّاتٍ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ فَمَن كَفَرَ بَعْدَ ذَلِكَ مِنكُمْ فَقَدْ ضَلَّ سَوَاء السَّبِيلِ
Na Mwenyezi Mungu alifanya agano na Wana wa Israili. Na tukawateulia kutokana nao wakuu kumi na mbili. Na Mwenyezi Mungu akasema: Kwa yakini Mimi ni pamoja nanyi. Mkisali, na mkatoa Zaka, na mkawaamini Mitume wangu, na mkawasaidia, na mkamkopesha Mwenyezi Mungu mkopo mwema, hapana shaka nitakufutieni maovu yenu na nitakuingizeni katika mabustani yapitayo mito kati yake. Lakini atakaye kufuru miongoni mwenu baada ya hayo bila ya shaka atakuwa amepotea njia iliyo sawa.
Surat al-Maida(۱۲)
Imekuja katika Aya ya 12 ya Surat al-Maida: Katika Aya hii Mwenyezi Mungu anaonyesha kuwa, wakuu hawa 12 waliteuliwa miongoni mwa Bani Israil. Hata hivyo Qur’an haijabainisha wazi nafasi na daraja yao. [12] Wafasiri wana mitazamo tofauti kuhusiana na hili. [13]
Kufananisha Viongozi wa Baada ya Mtume na Wakuu wa Bani Israil
Katika hadithi iliyonukuliwa kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) imetambua idadi ya warithi na viongozi baada yake ni 12 na wametambuliwa kuwa idadi yao ni sawa na idadi ya watemi na viongozi wa jadi wa Bani Israil. [14] Majimui ya hadithi hizi ni mashuhuri kwa jina la Hadithi za makhalifa 12 na wote wametambulishwa kuwa ni kutoka kwakabila la kureshi. [15 Maulamaa wa Kishia huzitumia hadithi hizi kwa ajili ya kuthibitisha Uimamu wa Maimamu Kumi na Mbili. [16] Kwa mujibu wa hadithi nyingine, Mtume ametambua hatima ya kaumu yake kama ya kaumu ya Bani Israil. [17] Kadhalika katika bai ya Aqaba,m Mtume (s.a.w.w) aliteua wakuu 12 miongoni mwa ansar ili wawe wawakilishi wake mjini Madina. [18]
Sayyid Muhammad Hussein Tabatabai katika tafsiti yake ya al-Mizan ameshabihisha Nuqaba (wakuu) na Ulul-amri (wenye mamlaka) katika dini ya Uislamu na kuwatambua kuwa wao ni marejeo ya masuala ya dini na dunia ya Bani Israil. [19]
Jukumu la Wakuu 12 wa Bani Israil
Kwa mujibu wa Aya za Qur’an, nuqabaa (wakuu) na watemi wa Bani Israel walikuwa na jukumu la kulinda agano na ahadi ambayo Mwenyezi Mungu aliichukua kutoka kwa Bani Israil. [20] Kadhalika waliamrishwa na Nabii Mussa (a.s) kusafiri na kwenda Baytul-Muqaddas [21] ili wakakusanye taarifa za kaumu dhalimu [22] ambazo zilikuwa zikishi katika ardhi ya Kan’an, [23] Shamat au Sham [24] (eneo kubwa lililokuwa likijumuisha Syria, Lebanon, Jordan na sehemu ya ardhi ya Palestina, au eneo la Ariha katika Sham. [25] Baada ya kusajili kile walichokishuhudia walirejea kwa Nabii Mussa (a.s) na kuzungumzia adhama ya wakazi wa maeneo hayo, [26] nabii Mussa aliwataka wasisimulie hayo kwa kaumu zao na wajiepushe na kuwatisha, [27], lakini ukiondoa wawili tu miongoni mwao, [28] au watano, [29, waliobakia wote walikengeuka agizo na amri ya Nabii Mussa (a.s).
Majina ya Wakuu wa Bani Israil
Tha’alabi, mmoja wa wafasiri wa Qur’an tukufu wa Ahlu-Sunna ametaja katika tafsiri yake majina ya wakuu 12 wa Bani Israel ambao ni:
- Shamil bin Ran.
- Shaqat bin Huri.
- Caleb bin Jephunneh.
- Maqail bin Yusuf.
- Jishua bin Nun.
- Qantum bin Arqun.
- Madi bin Adi.
- Jadi bin Qamin.
- Bianun bin Mulkia.
- Naftali Mahar bin Vaqsi.
- Hama’il bin Haml.
- Sabur bin Mulkia.[30]
Katika baadhi ya vyanzo vingine majina ya wakuu 12 wa Bani Israil yamenukuliwa yakiwa na tofauti kidogo. [31].
Vyanzo
- Abū l-Futūḥ al-Rāzī, Ḥusayn b. ʿAlī. Rawḍ al-Jinān wa Rawḥ al-Janān fī Tafsīr al-Qurʾān. Mashhad: Āstān-i Quds-i Raḍawī, 1408 AH.
- Abū ʿUbayda, Muʿammar b. Muthannā. Majāz al-Qurʾān. Cairo: Maktabat al-Khānjī, 1381 Sh.
- Abū Yaʿlī al-Mawsilī, Aḥmad b. ʿAlī. Musnad Abi Yaʿlī. Edited by Ḥusayn Sulaym Asad. Damascus: Dār al-Maʾmūn li-Turāth, 1404 AH.
- Ālūsī, Maḥmūd b. ʿAbd Allāh al-. Rūḥ al-maʿānī fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Edited by ʿAlī ʿAbd al-Bārī al-ʿAṭiyya. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1415 AH.
- ʿĀmilī, Ibrāhīm. Tafsīr ʿĀmilī. Tehran: Katābfurūshī-yi Ṣadūq, 1360 Sh.
- Bazār, Aḥmad b. ʿAmr al-. Musnad al-Bazār. Edited by Maḥfūz al-Raḥmān Zayn Allāh. Medina: Maktabat al-ʿUlūm wa al-Ḥikam, 1993.
- Bayḍāwi, ʿAbd Allāh b. ʿUmar. Anwār al-tanzīl wa asrār al-taʾwīl. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1418 AH.
- Deobandī, Maḥmūd Ḥasan. Tafsīr-i kābulī. 11th edition. Tehran: Nashr-i Iḥsān, 1385 Sh.
- Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muḥammad. Al-Wāḍiḥ fī tafsīr al-Qurʾān al-karīm. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1424 AH.
- Ḥasanī Wāʿiz, Maḥmūd b. Aḥmad. Daqāʾiq al-taʾwīl wa ḥaqāʾiq al-tanzīl. Tehran: Markaz-i Pazhūhishī Mīrāth-i Maktūb, 1381 Sh.
- Ibn Ḥanbal, Aḥmad b. Muḥammad. Musnad al-Imām Aḥmad b. Ḥanbal. Beirut: Muʾassisa al-Risāla, 1416 AH.
- Ibn Sulaymān, Muqātil. Tafsīr muqātil Ibn sulaymān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1423 AH.
- Ibn Qutayba al-Dīnawarī, ʿAbd Allāh b. Muslim . Tafsīr gharīb al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Hilāl, 1411 AH.
- Ibn Hāʾim, Aḥmad b. Muḥammad. Al-Tibyān fī tafsīr gharīb al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Gharb al-Islāmī, 1423 AH.
- Ibn Hammūsh, Makkī. Al-Hidāya ila bulūgh al-nihāya. Shārja: Jāmiʿat al-Shārqa, 1429 AH.
- Irbilī, ʿAlī b. ʿĪsā al-. Kashf al-ghumma fī maʿrifat al-aʾimma. Edited by Sayyid Hashim Rasūlī Maḥallātī. Tabriz: Maktabat Banī Hāshimī, 1381 AH.
- Jurjānī, ʿAbd al-Qāhir b. ʿAbd al-Raḥmān. Darj al-durar fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Jordan: Amman: Dār al-Fikr, 1430 AH.
- Khazzāz al-Qummī, ʿAlī b. Muḥammad b. ʿAlī al-. Kifāyat al-athar fī l-naṣṣ ʿalā l-aʾimmat al-ithnā ʿashar. Edited by ʿAbd al-Laṭīf Ḥusaynī Kūhkamaraʾī Khoeī. Qom: Bīdār, 1401 AH.
- Khalīl b. Aḥmad. Kitāb al-ʿayn. 2nd edition. Qom: Nashr-i Hijrat, 1409 AH.
- Mughnīya, Muḥammad Jawād al-. Tafsīr al-Kāshif. Qom: Dār al-Kitab al-Islāmī, 1424 AH.
- Makārim Shīrāzī, Nāṣir. Tafsīr-i nimūna. 10th edition. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1371 Sh.
- Maybudī, Aḥmad b. Muḥammad. Kashf al-asrār wa ʿuddat al-abrār. 5th edition. Tehran: Amīr Kabīr, 1371 Sh.
- Mudarrisī Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Ḥusyan. Maktab dar farāyand-i takāmul. Translated to Farsi by Hāshim Īzadpanāh. Tehran: Intishārāt-i Kawīr, 1386 Sh.
- Muʾassisa-yi Maʿārif Islāmī. Muʿjam al-aḥādīth al-Imām al-Mahdī (a). Qom: Intishārāt-i Masjid Muqaddas-i Jamkarān, 1428 AH.
- Nuʿmanī, Muḥammad b. Ibāḥīm al-. Kitāb al-ghayba. Tehran: Nashr-i Ṣadūq, 1397 AH.
- Suyūṭī, ʿAbd al-Raḥmān b. Abī Bakr al-. Al-Durr al-manthūr fī tafsīr al-maʾthūr. Qom: Maktabaṭ Āyat Allāh al-Marʿashī, 1404 AH.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
- Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Al-Khiṣāl. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Jāmiʿat al-Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmiyya, 1362 Sh.
- Samarqandī, Naṣr b. Muḥammad al-. Tafsīr al-samarqandī al-musammā baḥr al-ʿulūm. Beirut: Dar al-Fikr, 1416 AH.
- Shaʿrānī, Abu l-Ḥassan. Pazhūhishha-yi Qurʾānī ʿAllāma Shaʿrānī dar tafāsīr majmaʿ al-bayān. Qom: Būstān-i Kitāb, 1386 Sh.
- Ṣāḥib, Ismāʿīl b. ʿAbbād. Al-Muḥīṭ fī al-lugha. Edited by Muḥammad Ḥasan Āl-i Yāsīn. Beirut: Ālam al-Kutub, 1414 AH.
- Ṣādiqī Tihrānī, Muḥammad. Tarjumān-i furqān: tafsīr mukhtaṣar al-Qurʾān al-karīm. Qom: Shukrāna, 1388 Sh.
- Ṭabāṭabāʾī, Sayyid Muḥammad Ḥusayn al-. Al-Mīzān fī tafsīr al-Qurʾān. 2nd edition. Beirut: Muʾassisat al-Aʿlamī li-l-Maṭbūʿāt, 1390 AH.
- Thaʿālibī, ʿAbd al-Raḥmān b. Muḥammad al-. Tafsīr al-thaʿālibī al-musammā bi l-jawāhir al-ḥisan fī tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1418 AH.
- Thaʿlabī, Aḥmad b. Muḥammad al-. Al-Kashf wa l-bayān ʿan tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1422 AH.
- Ṭabarānī, Sulaymān b. Aḥmad. Tafsīr al-kabīr: tafsīr al-Qurʾān al-ʿazīm. Irbid, Jordan: Dār al-Kitāb Thiqāfī, 2008.
- Ṭabarānī, Sulaymān b. Aḥmad. Al-Muʿjam al-kabīr. Edited by Ḥamdī ʿAbd al-Majīd Salafī. 2nd edition. Mosul: Maktabat al-ʿUlūm wa al-Ḥikam, 1404 AH.
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Tafsīr-i jawāmiʾ al-jāmiʾ. 1st Edition. Qom: Markaz-i Mudīrīyat-i Ḥawza-yi Ilmīya-yi Qom, 1412 AH.
- Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-. Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. 3rd edition. Tehran: Intishārāt-i Nāṣir Khusraw, 1372 Sh.
- Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-. Jāmiʾ al-bayān fi tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʾrifa, 1412 AH.
- Ṭayyib, ʿAbd al-Ḥusayn. Aṭyab al-bayān fi tafsīr al-Qurʾān. 2nd edition. Tehran: Intishārāt-i Islām, 1369 Sh.
- Zamakhsharī, Maḥmūd b. ʿUmar al-. Al-Kashshāf ʿan ḥaqāʾiq ghawāmiḍ al-tanzīl wa ʿuyūn al-aqāwīl fī wujūh al-tʾawīl. 3rd edition. Beirut: Dār al-Kitāb al-ʿArabī, 1407 AH.