Nenda kwa yaliyomo

Vita vya Imamu Ali (a.s) Nchini Yemen

Kutoka wikishia

Sariyyah au Safari ya Kivita ya Imamu Ali (a.s) Ya Kuelekea Nchini Yemen (Kiarabu: سرية الإمام علي (ع) إلى اليمن), ilikuwa ni jukumu lililotolewa na bwana Mtume (s.a.w.w) kwa Imamu Ali (a.s), kwa ajili ya kueneza Uislamu katika eneo hilo. Ripoti kadhaa zinasema kuwa; Imamu Ali (a.s) alifanya safari mbili au tatu kwenda nchini Yemen. Katika safari hizi, Imamu aliweza kulingania kabila za Hamdan na Madh-hij na kuzifanya zikubali kuingia katika Uislamu.Jambo ambalo lilikuwa ndio msingi wa kabila zote za Yemen kusilimu. Baadaye, watu wa kabila za Hamdan na Madh-hij wakawa ni miongoni mwa wafuasi wa Imamu Ali (a.s), Imamu Hassan (a.s) na Imamu Hussein (a.s).

Katika ugawaji wa ngawira uliofanyika baada ya kumalizika kwa vita vya msafara huu, baadhi ya askari wa Imamu Ali (a.s) walilalamika kuhusu utendaji wa Imamu Ali mbele ya Mtume (s.a.w.w) kuhusiana na ugawaji huo wa ngawira, ambapo bwana Mtume (s.a.w.w) alijibu kwa kuelezea hadhi na sifa za Imamu Ali (a.s). Baadhi ya waandishi wa historia wa upande wa madhehebu ya Sunni, wanaamini kuwa Khutba ya Ghadir ilikuwa ni jibu kuhusiana na malalamiko hayo. Katika kujibu na kukabiliana na mtazamo wao huo, baadhi ya watafiti wameelezea tofauti kadhaa zilizopo katika malalamiko ya askari wa Ali (a.s) na maudhui ya Khutba ya Ghadir, mionngoni mwazo ni; tofauti za wakati, mahali, maudhui na sababu. Jambo ambalo linaonesha umbali wa kimaudhui kati ya maneno ya Mtume katika utetezi wake wa kumtetea Imamu Ali (a.s) na uhalisia wa Khutba ya Ghadir.

Katika moja ya safari hizi au katika jukumu lingine, bwana Mtume (s.a.w.w) alimtaka Imamu Ali (a.s) kutoa hukumu kati ya watu wa Yemen.

Kulinganiwa kwa Makabila ya Yemen

Safari ya kivita au kiukombozi ya Imamu Ali (a.s) nchini Yemen, imetambuliwa kuwa ni jukumu maalumu lililotolewa na bwana Mtume (s.a.w.w) kwa ajili ya kuwalingania na kuwaita watu wa Yemen kwenye Uislamu. [1] Ibnu Hisham na Ibnu Sa’ad, ambao ni waandishi wa historia wa upande wa madhehebu ya Sunni, wamezungumza juu ya safari mbili tofauti za Imamu Ali (a.s) nchini Yemen. [2] Baadhi pia wanadhani kuwa Imamu Ali (a.s) alifanya safari hizo mara tatu. [3] Kuna ripoti mbalimbali kuhusiana na safari za Imamu Ali (a.s) nchini Yemen, na namna ya mwaliko wake wa kuwaita watu wa Yemen kwenye Uislamu, ambapo baadhi ya mialiko hiyo inahusiana na kabila la Hamdan [4] na mengine inahusiana na kabila la Madh-hij. [5]

Mwaliko wa Imamu Ali (a.s) kwa Kabila la Hamdan

Kulingana na maelezo ya Tabari ni kwamba; Bwana Mtume (s.a.w.w) hapo awali alimtuma Khalid bin Walid kwenda Yemen; lakini baada ya miezi sita ya kutofanikiwa, katika mwezi wa Ramadhani mwaka wa 10 Hijiria, Imamu Ali (a.s) alitumwa akiwa na barua kwenda nchi hiyo. [6] Pale Imamu Ali (a.s) alipofika Yemen, aliwasomea barua hiyo aliyopewa na bwana Mtume (s.a.w.w) watu wote kabila la Hamdan, ambapo waliamua kuingia katika Uislamu siku hiyo hiyo. [7] Baadhi ya watafiti wanaamini kuwa; safari hii ilifanyika mwaka wa 8 Hijiria. [8]

Mwaliko wa Imamu Ali (a.s) kwa Kabila la Madh-hij

Waqidi, Ibnu Saad, na waandishi wengine wa historia wameutaja vitabuni mwao msafara huu wa Ali (a.s) kupitia amri ya bwana Mtume (s.a.w.w), akiwa pamoja na askari mia tatu kwenda Yemen, ambapo Imamu Ali (a.s) kwanza alikutana na kabila la Madh-hij na kuwaalika kwenye Uislamu. Kabila hilo lilipinga na wito huo, lakini baada ya mapigano yaliyo sababisha vifo vya takriban watu ishirini, waliamua kukubaliana na mwaliko huo wa Imamu Ali (a.s) na kuwa Waislamu. Safari hii imeripotiwa kufanyika katika mwezi wa Ramadhani mwaka wa 10 Hijiria. [12]

Imesemekana kuwa katika safari hii, Ka'abu al-Ahbar, mmoja wa wasomi wa Kiyahudi, alikutana na Imamu Ali (a.s) na baada kujibiwa maswali yake kuhusiana na Uislamu na bwana Mtume, alikubali kuwa Mwislamu, kisha akajaribu kuwaalika wasomi wengine wa Kiyahudi katika eneo lake kwenye Uislamu. [13]

Ugawaji wa Ngawira

Baada ya Imamu Ali (a.s) kukusanya ngawira katika vita dhidi ya Madh-hij, aliigawa sehemu iliyobaki kwa askari wake baada ya kutenga khumsi kutoka katika ngawira hiyo. [14] Kulingana na desturi ya maamiri wengine wa zamani, baadhi ya maamiri wa vita hivyo, walimuomba Imamu atoe sehemu maalumu ya khums kwa ajili yao. Imamu Ali (a.s) hakukubaliana na maombi hayo, na badala yake akawambia kuwa; Yeye atampeleka khumsi yote iliopo mikononi mwake kwa bwana Mtume (s.a.w.w) aliye kuwa kulekea Makka kwa ajili ya kuhiji, naye ndiye atakaye amua maamuzi yanayo faa kuhusiana na khumsi hiyo. [15] Kulingana na moja ya ripoti, Imamu Ali (a.s) aliandika barua kwa Mtume (s.a.w.w) akielezea utendaji wake, na Mtume wa Allah (s.a.w.w) akamtaka Imamu auangane na kushirikiane naye katika ibada hiyo ya Hija. [16]

Baada ya kufika Ta'if, Imamu Ali (a.s) alikabidhi uongozi wa jeshi na utunzaji wa khums kwa Abu Raafi na yeye mwenyewe akujiunga na Mtume (s.a.w.w) kuelekea Makkah. Baadhi ya watu walimwomba Abu Raafi awape sehemu ya khumsi naye akubali kuwatekelezea matwa hayo. Lakini baadaye pale Imamu Ali (a.s) alipokutana na askari wake, alimkemea Abu Rafi na kurejesha mali hizo alizowapa wafuasi wake, jambao ambalo lilisababisha malalamiko na kilio chao kwa bwana Mtume (s.a.w.w). [17] Inasemekana kuwa bwan Mtume (s.a.w.w) aliwashutumu askari hao walio mtuhumu Imamu Ali (a.s), na wakati huo huo akazungumzia sifa na hadhi ya Imamu Ali (a.s), akathibitisha uhalali utendaji wa Imamu Ali (a.s) kuhusiana na maamuzi yake juu yao. [18]

Ripoti ya malalamiko ya wafuasi wa Imamu Ali (a.s) kwa bwana Mtume (s.a.w.w) baada ya kutumwa Yemen na kushika nafasi ya Khalid bin Walid, pia ni miongoni mwa ripoti zilizoripotiwa kuhusiana na malalamiko ya askari dhidi ya Imamu Ali (a.s), ambapo jawabu ya bwana Mtume ilikuwa ni kumtetea Imamu Ali (a.s) na kuelezea hadhi na sifa zake. [19] Ibnu Hisham ameandika kuwa malalamiko hayo yalikuwa yanahusiana na jukumu la Imamu Ali (a.s) katika ukusanyaji wa zaka kutoka katika mji wa Najrani. [20]

Uhusiano wa Hotuba ya Ghadir na Malalamiko Dhidi ya Imamu Ali (a.s)

Ahmad bin Hussain Baihaki, [21] Ibn Kathir [22] na wengineo, [23] wanaamini kwamba; lengo la bwana Mtume (s.a.w.w) katika kutoa Hotuba ya Ghadeer, lilikuwa ni kujibu malalamiko ya baadhi ya Waislamu dhidi ya Imamu Ali (a.s) katika vita vya Yemen, hiyo basi baadhi wanazuoni wanaamini ya kwamba; hotuba hii haina uhusiano wowote na uongozi wa Imamu Ali (a.s) unaodaiwa baada ya kifo cha bwana Mtume (s.a.w.w). [24] Baadhi ya watafiti wamejibu shaka hii kwa kusema kwamba; masuala haya mawili ni masuala yasiyo na uhusiano wowote ule baina yake, si kihistoria, si kijiografia, si kimaudhui, wala kimafungamano. [25]

Tofauti ya Kiwakati na Kimahali Juu ya Matukio Mawili Hayo

Kulingana na baadhi ya watafiti ni kwamba; ripoti za malalamiko ya jeshi la Imamu Ali (a.s) huko Yemen, imeelezwa ya kwamba, bwana Mtume (s.a.w.w) alitoa jawabu ya wazi papo hapo kuhusisna na malalamiko hayo, na wala hakukua jambo gumu lililobaki kiasi ya kwamba, awajibike tena kutoa hotuba nyingine kwa ajili ya kutatua utata huo. [26] Kwa hiyo inasemekana kwamba; mahali pa tukio la Khutba ya Ghadeer Khum na malalamiko ya jeshi la Yemen hayalingani, yaani kuna umbali mkubwa baina ya matukio hayo mawili. Kulingana na waandishi wa historia, tukio la Ghadeer Khum lilifanyika katika eneo lililopo kati ya Makkah na Madinah. [27] Na kwa upande wa pili pia kuna Hadithi zisemazo kwamba; mahali pa malalamiko dhidi ya Imamu Ali (a.s) ilikuwa ni Madina, huku Hadihti nyingine zikisema kwamba tukio hilo lilitokea mjini Makkah. [28]

Tofauti ya Maudhui ya Matukio Mawili Hayo

Imesemekana kwamba tukio la Ghadeer Khum halina uhusiano na malalamiko ya jeshi la Yemen kwa upande wa maudhui; kwa sababu hakuna maelezo yoyote ya malalamiko katika hadithi ya Ghadeer, lakini kwenye ripoti za safari ya Imamu Ali (a.s) kwenda Yemen, kuna maneno kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) ambayo yana neno "malalamiko" kama vile "msilalamike juu ya Ali..." [29] Kama kukubaliwa na watu kwa imani ya uwezo wa Imamu juu ya waumini, na kutokuonyesha malalamiko dhidi ya Imamu Ali (a.s) na upendo wake kwake sio sawa. Zaidi ya hayo, ripoti za pongezi kwa Imamu na salamu kwake kwa maneno Amir al-Mu'minin na kiapo cha utii kwake, inaonyesha kwamba ufahamu wa wasikilizaji juu ya maneno ya Mtume, ilikuwa ni suala la ukhalifa. [30]

Ukadhi wa Imamu Katika Mji wa Yemen

Vyanzo kama vile Musnad Ibn Hanbal[32] na Al-Mustadrak Al-Sahihain[33] kutoka kwa Al-Hakim Nishaburi, vyote kwa pamoja vimenukuu uamuzi wa bwana Mtume (s.a.w.w) wa kumtaka Imamu Ali (a.s) kwenda Yemen na kutoa hukumu miongoni mwa watu wa nchi hiyo. Katika vyanzo hivyo imeelezwa ya kwamba; Imamu Ali (a.s) alionyesha wasiwasi juu ya uamuzi huo, na kusema kwamba, yawezekana watu hao kukataa na kuto kubaliana na hukumu zake kwa sababu ya ujana wake, ambapo baada ya bwana Mtume kumpa mashauri muhimu juu ya utendaji wake, alimtakia kila la kheri na kumwomba dua ili aweze kufanikiwa katika kazi hiyo. Baadhi wameihisabu safari yake hili kuwa ni moja ya safari iliyokuwa na nia ya kuzilingania Uislamu kabila ya Hamdan na Madh-hij, [34] na wengine wamefikiria kwamba; safari hii haikuwa na lengo la vita, na wakasema kwamba, safari hiyo ilitokea kati ya mwaka wa nane na wa tisa Hijiria. Kulingana na hukumu nyingi zilizotajwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s) alizotoa akiwa katika mji wa Yemen, inaonekana kwamba; Imamu Ali (a.s) alidumu kwa muda mrefu katika mji huo. [35]

Mafanikio ya Uwepo wa Imam Huko Yemen

Kulingana na moja ya ripoti ni kwamba; safari ya Imamu Ali (a.s) kwenda Yemen na iliyo pelekea watu wa kabila la Hamdan au Madhij kuingia katika Uislamu, ilipelekea kabila zingine za Yemen kujiunga na kuamini Uislamu kwa kufuata mfano wa utendaji wao katika kuamiliana na Imamu Ali (a.s). [36] Imesemekana kwamba watu wa Yemen, haswa kabila za Hamdan na Madh-hij, walionyesha nia ya kumfuata na kushikanmana na Imamu Ali tangu wakati huo, nao wakawa ni miongoni mwa washirika wake wa karibu huko mjini Kufa, [37] na wakamsaidia katika vita vya Siffin [38] na Nahrawan. [39] Baadaye, pia walimuunga mkono Imamu Hassan [40] na Imamu Hussein (a.s). [41] Baadhi wanaamini kuwa ukunjufu na utii wao ulikuwa ni matokeo ya ufahamu wao wa kina wa kuuelewa Uislamu na kuifahamu nafasi muhimu ya kiroho ya Imamu Ali (a.s), pamoja na urithi wa utawala wake baada ya bwana Mtume (s.a.w.w). [42]