Nenda kwa yaliyomo

Ummu Dawud

Kutoka wikishia

Ummu Dawud (Kiarabu: أم داوود) ni mke wa Hassan Muthanna na mama kunyonyesha wa Imam Swadiq (a.s). Kuniya yake imechukuliwa kutoka katika jina la mtoto wake Dawud bin Hassan. Jina lake lilikuwa Habiba au Fatima. Alinukuu amali za Ummu Dawud na dua ya Istiftah (Dua ya Ummu Dawud) kutoka kwa Imam Sadiq (a.s).

Ummu Dawud alijifunza amali hizi na dua kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) kwa ajili ya kuachiliwa mtoto wake kutoka gerezani kutoka. Kulingana na yeye, baada ya kufanya amali za Ummu Dawud, mwanawe Dawud alitolewa gerezani na kurudi nyumbani.

Jina na Kuniya

Habiba au kwa mujibu wa mtazamo wa wengine Fatima maarufu kwa jina la Ummu Dawud ni binti ya Abdallah bin Ibrahim na alikuwa mke wa Hassan al-Muthanna. [1] Aliondokea kuwa mashuhuri kwa jina la Ummu Dawud kutokana na jina la mwanawe aliyejulikana kama Dawud bin Hassan. [2] Katika kitabu cha A'yan al-Shia, kuniya yake nyingine imetajwa kuwa ni Ummu Khalid ali-Barbariyah. [3]

Ummu Dawud alikuwa mama wa kunyonyesha wa Imamu Swadiq (a.s) (83-148 H). [4] Mwanawe Dawud ametambuliwa kuwa miongoni mwa masahaba wa Imamu Baqir (a.s) au Imamu Swadiq (a.s). [5]

Amali na Dua ya Ummu Dawud

Makala kuu: A'mal Ummu Dawud na Dua ya Ummu Dawud

Katika vyanzo vya hadithi kuna hadithi iliyonujkuliwa kutoka kwa Imamu Swadiq (a,s) ambamo ndani yake inamuagiza Ummu Dawud kufanya a'amali katika masiku meupe (Ayyam al-Bidh). Amali hiizi zimeondokea kuwa mashuuhuri kwa jina la A'mali za Ummu Dawud. Kadhalika kuna dua iliyonukuliwa ambayo inajulikana kwa jina la Dua al-Istiftah au Dua Ummu Dawud ambayo husomwa mwishoni mwa A'amali za Ummu Dawud. [6] Mpokezi wa hadithi hii ni Ummu Dawud mwenyewe. [7]

Dua ya Ummu Dawud imetajwa pia katika kitabu cha Fadhail Shahr Rajab (Fadhila za Mwezi wa Rajab), kilichoandikkwa na Hakim Haskani, mmoja wa Maulamaa wa Kisunni wa karne ya 5 Hiijria. [8]

Amali za Ummu Dawud hutekelezwa namna hii: Kwanza, kufunga Saumu katika masiku meupe (tarehe 13,14 na 15 Rajab), katika siku ya 15 Rajab inapowadia adhuhuri utaoga, baada ya kuswali Sala za Adhuhuri na Alasiri, husomwa baadhi ya Sura za Qur’ani na amali ya mwisho ni kusoma Dua Ummu Dawud au Istiftah. [9]

Maulamaa wa Kishia kama Sheikh Tusi, Sayyib bin Tawus na Allama Majlisi wanasema, Dua ya Ummu Dawud ina taathira katika kuondolewa mtu matatizo na kutakabaliwa haja. [10]

Mkasa wa A'amal Ummu Dawud

Mkasa na tukio la kubaishwa na Imamu Swadiq (a.s) A'mali Ummu Dawud katika muundo na fremu ya kisa chenye maelezo mapana na marefu limeandikwa na kusimuliwa katika vitabu vya Fadhail al-Ash'hur al-Thalatha (Fadhila za Miezi Mitatu), kilichoandikwa na Sheikh Swaduq na Iqbal al-A'mal kilichoandikwa na Sayyid bin Tawus. [11]

Kwa mujibu wa ripoti ya vitabu hivi viwili, Dawud, mtoto wa Ummu Dawid, alitekwa na kupelekwa Iraq wakati wa ukhalifa wa Mansur Dawaniqi, na kwa muda mrefu Ummu Dawud hakuwa na habari za mwanawe huyo. Anafanya maombi na kuuomba sana dua, ili mwanawe aachiliwe, lakini hapati habari yoyote kutoka kwake. Pia anatawasali kwa waja, lakini maombi yao pia hayasuluhishi tatizo; [12] kiasi kwamba, anafikia hatua ya kukata tamaa ya kumwona tena mtoto wake.[13]

Hadi siku moja, alipokwenda kumtembelea Imamu Swadiq (a.s) ambaye alikuwa mgonjwa. Imamu Swadiq anamuuliza kuhusu Dawud, na Ummu Dawud anamsimulia kisa chenyewe na kilichomkuta mwanawe Dawud.Imamu Swadiq akamwambia: Kwa nini husomi Dua ya Istiftah? (Dua Ummu Dawud) Kisha anamtaka afunge katika masiku meupe (Ayyam al-Bidh) na katika siku ya mwisho yaani tarehe 15 ya Rajab), afanye A'amali za Ummu Dawud na kisha aisome ile dua. [14]

Ummu Dawud anasema, baada ya kuwa ametekeleza amali za Ummu Dawud, baada ya kulala, usiku anaota ndoto na kumuona Mtume (s.a.w.w) akimbashiria kuachiliwa huru Dawud. Baada ya muda Dawud anarejea nyumbani na kusema kuwa, aliachiliwa huru usiku ule ule. [15]

Rejea

Vyanzo