Nenda kwa yaliyomo

U’mratul al-Qadha

Kutoka wikishia

Umratu al-Qadha au Umratu al-Qadhiyyah au Umratu al-Qasas (Kiarabu: عُمْرَةُ الْقَضاء أو عمرة القضیة أو عُمْرَةُ الْقَصاص) ni ibada (amali) ya Hijja ya Umra ambayo Mtume Muhammad (s.a.w.w) na wafuasi wake Waislamu waliifanya katika mwezi wa Dhul-Qa'dah mwaka wa saba wa Hijiria. Iliitwa Umratu al-Qadhaa kwa sababu watukufu Waislamu walipanga kufanya Hijja hiyo ya Umra mwaka uliotangulia katika mwezi wa Dhul-Qa’da; Lakini kwa sababu washirikina wa Makkah waliwazuia Waislamu wasifanye ibada hiyo, hatimae kwa kuzingatia mapatano na makubaliano waliyoafikiana katika Sulhu Hudaybiyah, Waislamu waliruhusiwa kuhiji Umra mwaka mmoja baada ya makubaliano waliyoafikiana katika Sulhu Hudaybiya.

Katika Umra hii, Mtume alifanya Tawaf na Sa'i ya Swafa na Marwa akiwa amepanda ngamia na akaligusa Jiwe jeusi kwa fimbo yake. Kwa mujibu wa baadhi ya wafasiri, dalili ya kuteremshwa Aya ya 144 ya Surah Al-Baqarah ni kuhusu Umratu al-Qadha. Pia, wengine wanaamini kwamba aya ya 27 ya Surah al- Fat'h ilietrmshwa katika safari hii na ndoa ya Mtume na Bibi Maimuna pia ilifanyika katika safari hii.

Dalili za kuitwa Umratu Al-Qadhaa

Hijja hii imeitwa Umratu Al-Qadhaa kwa sababu Katika mwaka wa saba wa Qamari[1], Mtume wa Uislamu alikwenda Makka pamoja na idadi ya Waislamu kutekeleza Hijja ya Umra. Hijja ambayo ilikuwa ni Qadhaa ya mwaka uliopita ambao hawakufanikiwa kuitekeleza ibada hiyo. Katika mwaka uliotangulia, mwaka wa sita wa Hijrah, Waislamu walikuwa wamehamia Makka kufanya Umra;Ibnu Kathir,[2] lakini washirikina wa Makka wakawazuia wasiingie Makka. Hatimaye, mkataba wa amani uliandikwa baina ya Waislamu na washirikina wa Makka, ambao ulijulikana kama Amani ya Hudaybiyah. Kwa mujibu wa Makubaliano ya Amani ya Hudaybiyah, Waislamu hawakuruhusiwa kuhiji katika mwaka wa sita; Lakini katika mwaka uliofuata (mwaka wa saba), wangeweza kuingia Makka kwa siku tatu na kufanya Umra.[3]

Umratu al-Qadhaa pia inajulikana kwa majina mengine kama Umratu al-Qadhiyyah, Ghazawatu al-Qadhaa, Umratu al-Sulh, na Umratu al-Qasas. Umra hiyo imeitwa Umratu al-Qasas kwa sababu Mtume (s.a.w.w) alilipiza kisasi kwa washirikina waliozuia Umra yake katika mwezi wa (Dhul-Qa'dah mwaka wa 6). Hijiria[4] Baadhi ya Wafasiri wamethibitisha kuwa aya;{الشَّهْرُ الْحَرَامُ بِالشَّهْرِ الْحَرَامِ وَالْحُرُمَاتُ قِصَاصٌ ۚ فَمَنِ اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ فَاعْتَدُوا عَلَيْهِ بِمِثْلِ مَا اعْتَدَىٰ عَلَيْكُمْ ۚ وَاتَّقُوا اللَّهَ وَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ ; Mwezi mtakatifu kwa mwezi mtakatifu, na vitu vitakatifu vimewekewa kisasi, basi anaye kushambulieni nanyi pia mshambulieni kwa kadiri alivyo kushambulieni}[5]. Aya hii iliteremshwa kuhusu tukio hili.

Kuondoka kuelekea Makka

Kwa mujibu wa amri ya Mtume (s.a.w.w) , watu (Waislamu) wote waliokuwepo katika Mkataba wa Hudaybiya mwaka wa saba Qamari, walielekea Makka na wengine pia wakajiunga nao na idadi ya Waislamu ikafikia watu elfu mbili.[6] Waislamu walichukua ngamia 60 pamoja nao kwa ajili ya kuchinja.Tabary, Tarekhu Al-Umamu wal-Muluk, juzuu ya 3, kurasa ya 25 Katika safari hii Mtume (s.a.w.w) alimteua Abu Dharri al-Ghafary kama kiongozi wake mteule katika mji wa Madina. [7]

Kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba wa Hudaybiya, Waislamu waliruhusiwa kuingia katika mji wa Makka na silaha zao walizokuwa nazo katika safari tu[8] . hata hivyo, Mtume (s.a.w.w.) aliwaweka Waislamu 200 nje ya mji wa Makka wakiwa na farasi na silaha za kivita ili kama washirikina wa Makka wangetaka kuanza vita na kupigana, Waislamu waweze kujilinda.[9]

Kuingia kwa Waislamu katika mji wa Makka

Waislamu walipoingia ndani ya mji wa Makka, baadhi ya viongozi wake waliuacha mji huo.[10] Wengine walibaki ili kumlinda Mtume (s.a.w.w) na Waislamu. Mtume (s.a.w.w) alitoa mkono wake wa kulia kutoka katika vazi lake la Ihram na wafuasi wake Waislamu wakafanya vivyo hivyo ili kuonyesha uwezo wao kwa watu wa Makka.[11] Mtume akiwa amepanda ngamia alilizunguka Al-Kaaba na akakimbia baina ya Swafa na Mar-wa[12] Pia akaligusa jiwe jeusi kwa fimbo yake. [18] Baada ya Hijja, Mtume (s.a.w.w) aliingia kwenye Al-Kaaba na akamuamrisha Bilali asome Adhana ya adhuhuri juu ya Al-Kaaba.[13]

Matukio mengine

Mbali ya matukio hayo yaliyoashiriwa , vile vile Kulikuwa na matukio mengine yaliyotokea wakati wa Umratu al-Qadhaa, baadhi yake ni kama haya yafuatayo:

Rejea

  1. Al Baladhiriy, Ansabul-Ashraf, juzuu ya 1, kurasa ya 353
  2. Al-Bidaya wa Al-Nihaya,juzuu ya 4, kurasa ya 164.
  3. Al Bayhaqiyu, Dalail Al-Nubuwah,juzuu ya 4 kurasa ya 145
  4. Ibnu Hisham, Siratu Al-Nabawiyah, juzuu ya 2, kurasa ya 370
  5. Surah al-Baqarah, Aya ya 194
  6. Al Waaqidi, Al-Maghazy, juzuu ya 2, kurasa ya 731
  7. Al Baladhiry, Ansabul-Ashraaf. juzuu ya 1, kurasa ya 353
  8. Al Bayhaqiyu, Dalail Al-Nubuwah, juzuu ya 4, kurasa ya 145
  9. Al Maqriizy, Imtaul-Asmau, juzuu ya 1, kurasa ya 331
  10. Ibnu Khaldun, Tarekh Ibnu Khaldun,juzuu ya 2, kurasa ya 455
  11. Al Maqriizy, Imtaul-Asmau, juzuu ya 1, kurasa ya 331
  12. Al Waqidiyu, Al maghazy, juzuu ya 2, kurasa ya 736
  13. Al Waqidiyu, Al maghazy, juzuu ya 2, kurasa ya 737
  14. Ibnu Hisham, Siratu Al-Nabawiyah, juzuu ya 2, kurasa ya 372
  15. Ibnu Hisham, Siratu Al-Nabawiyah, juzuu ya 2, kurasa ya 372
  16. Ibnu Hisham, Siratu Al-Nabawiyah, juzuu ya 2, kurasa ya 372-373
  17. Ibnu Hisham, Siratu Al-Nabawiyah, juzuu ya 2, kurasa ya 372-373
  18. Al Waqidiyu, Al maghazy, juzuu ya 2, kurasa ya 738-739

Vyanzo

  • Ibn Hisham, A’bdul Malik Ibn Hisham, Al-Siyratu Al-Nabawiyyah, Utafiti: Mustafa Al-Saqqa, Ibrahim Al-Abyari, na Abdul Hafidh- Shalabi, Beirut, Dar Al-Ma’arifah, Bita.
  • Ibn Khaldun, Abdul al-Rahman ibn Muhammad, Diwan al-Mubtada wa al-Khabar fi Taarikh al-A’rab wa al-Barbar na Man A’serham Man Zawi -Shaan al-Akbar, iliyotafitiwa na Khalil Shahadah, Beirut, Dar al-Fikr. , chapa ya pili, 1408 AH.
  • Ibn Kathir Damascus, Isma’il Ibn O’mar, al-Badaiya wa al-Nahaiya, Beirut, Dar al-Fikr, 1407 AH.
  • Balazri, Ahmad bin Yahya, Ansab al-Ashraf, Utafiti: Suheil Zakar, Riadh Zarkali, Beirut, Dar al-Fikr, chapa ya kwanza, 1417 AH.
  • Beyhaqi, Ahmad bin Hussain, Dalail N-Nubuwwat Wa Ma’arifat Ahwal Saahib Shariya’t, utafiti: Abdul Mu’ti Qala’aji, Beirut, Dar al-Kitab Al-Alamiya, chapa ya kwanza, 1405 AH.
  • Tabari, Muhammad bin Jureyr, Taarikh Al-umam wa Al-Muluk, utafiti: Muhammad Abulfadhl Ibrahim, Beirut, Dar al-Turath, chapa ya pili, 1387 AH.
  • Muqrizi, Taqi al-Din, Imtaa al-Ismaa, Bima l-Nabiyi min al-Ahwal wal al-Am-wali wa al-Hafda wa al-Mataa, utafiti: Muhammad Abdul Hamid Namiysi, Beirut, Dar al-Katb al-Alamiyya, chapa ya kwanza, 1420 Hijria.
  • Makarem Shirazi, Nasser, Tafsir al-Namune, Tehran, Dar al-Kutub al-Islamiyya, chapa ya kwanza, 1374.
  • Wahidi Neishabouri, Ali bin Ahmad, Asbab al-Nuzul, Beirut, Dar al-Katb al-Islamiya, 1411 AH.
  • Waqidi, Muhammad bin Omar, Kitab Al-Maghazi, utafiti: Jones Marsden, Beirut, Al-Alemi Foundation, toleo la tatu, 1409 AH.