Nenda kwa yaliyomo

Tashbihi katika Qur’ani

Kutoka wikishia

Tashbihi katika Qur’ani (Kiarabu: الأمثال القرآنية) (matumizi ya lugha ya taswira) uliotumika katika Qur'ani, ni moja ya sanaa muhimu katika kufafanua na kuwasilisha dhana za Qur'ani, na ni moja ya sehemu za miujiza ya kiisimu (linguistics) ya kitabu hichi kitukufu. Kipengele hichi kimepewa umuhimu maalum katika Riwaya za Kishia, huku watu wakihimizwa kuzingatia na kutafakari juu ya maana na ukweli juu ya tashbihi zilizomo ndani ya Qur’ani. Kwa mujibu wa wafasiri wa Qur'ani, madhumuni ya kutoa mifano kwa njia ya tashbihi (matumizi ya lugha ya taswira), ni kurahisisha mafundisho magumu ili yawafikie watu wa kawaida kwa urahisi zaidi, kwani madhumuni ya kushuka kwa Qur’ani ni kufikisha ujumbe wa Mungu kwa kila mtu. Wafasiri wa Qur'ani wakibainisha lengo la uwepo wa tashbihi ndani ya Qur'ani sambamba na hoja za kiakili, mijadala yenye busara na mawaidha, wamesema kwamba; lengo la kutumia tashibihi hizo, ni kufanikisha uelewa wa watu kwa njia rahisi na sahihi. Imeelezwa kwamba; tashbihi (matumizi ya lugha ya taswira) za Qur’ani zimekuja kwa malengo ya kimalezi (kimaadili), zikilenga kuhimiza maadili tabia na mema, sambamba na kutoa mifano ya vitendo na vigezo ambavyo vinaweza kueleweka kirahisi na kuigwa na wanajamii.

Kuna mitazamo miwili tofauti Katika kujadili tashbihi na matumizi ya lugha ya taswira za Qur'ani. Mmoja kati ya mitazamo hii inasema kuwa: tashibihi za Qur’ani haziwakilishi kitu chengine chochote kile zaidi ya kurahisisha dhana fulani katika akili ya msikilizaji. Kwa upande mwingine, kuna wale wanaodai kwamba; hakuna aina yoyote ile ya tashbihi au matumizi ya lugha ya taswira katika matumizi ya lugha za Qur'ani, na badala yake, tashibihi hizo zinaakisi uwepo wa mfano hai na wa ukweli juu ya jambo fulani. Kwa mujibu wa wafasiri wa Qur'ani, tashbihi za Qur'ani zinaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kulingana na vigezo tofauti. Haya ni pamoja na uwazi katika kubainisha nyenzo za tashbihi, idadi ya vishabihishwavyo, pamoja na mnasaba ambao umetumika katika tashbihi hizo. Kila kundi lina umuhimu wake katika kuelezea mifano na dhana mbalimbali za kiakili zinazopatikana ndani ya Qur'ani, na hivyo kuchangia katika uelewa wa kina wa mafundisho yake. Wafasiri wametaja sifa kadhaa muhimu kuhusiana na tashbihi za Qur'ani, zikiwemo "uwenevu na upana wa mtando wake," ambao unaonyesha uwezo wa tashbihi hizo katika kufafanua kwa kina dhana mbalimbali. Pia nyengine iliyotajwa na wafasiri hao ni sifa ya «wepesi na urahisi wa welewa wake mbele ya watu mbali mbali», sifa yenye kuonesha jinsi ya Qur’ani inavyotoa kipaumbele, kwenye masuala ya kuwasilisha dhana zake mbali mbali kwa wahusika wake njia rahisi na kuepuka vikwazo katika ufukishaji huo.

Kuna kazi mbalimbali za kiuandishi zilizofanywa katika uwanja wa lugha za mafumbo na tashbihi zilizomo ndani ya Qur'ani Tukufu. Miongoni mwa kazi hizi ni kitabu kiitwacho "Rudhatu al-Amthal, Fi al-Amthalil al-Qur'an al-Karim", kilichoandikwa na Ahmad bin Abdullah al-Kozkanani al-Najafi. Kitabu hichi kinachambua kwa kina matumizi ya lugha za mafumbo na tashbihi katika Qur'ani, kikilenga kufafanua siri na maana zilizofichika ndani ya lugha hii, ambazo ni sehemu ya miujiza ya kiisimu ya kitabu hicho kitukufu.

Tashbihi Ikiwa ni Moja ya Mitindo Mitano ya Qur’ani

Mtindo ya kutumia lugha ya tashbihi katika uliotumiwa na Qur’ani katika ubainishaji na uwasilishaji, unatambuliwa kama ni mojawapo ya mitindo yake mitano muhimu ya uwasilishaji wake. Kwa mujibu wa Riwaya ya bwana Mtume (s.a.w.w), lugha ya mafumbo na tashbihi ni sehemu ya mitindo mitano ya kipekee inayotumiwa katika Qur'ani. [1] Kwa mujibu wa watafiti, mtindo huu wa lugha ya tashbihi na mafumbo ndani ya Qur'ani unaweza kufunika nyanja mbalimbali, zikiwemo za kisayansi, kimaadili, kielimu, na kijamii. [2] Baadhi ya watafiti wa Qur'ani wanaona kuwa matumizi ya lugha ya tashbihi katika Qur'ani ni moja ya ishara za miujiza yake, ikionesha uwezo wa hali ya juu wa kuelezea dhana ngumu kwa namna inayoeleweka kwa watu wote bila ya pingamizi. [3]

Dua ya Imamu Sajaad (a.s) Kuhusiana na Lugha ya Tashbihi

Ewe Mola, mteremshie rehema Muhammad na Aali zake, na ijaalie Qur'ani iwe mliwaza wetu katika mausiku yeneye giza zito... ili mioyo yetu ipate kuelewa vyema maajabu yake, na ili lugha za tashbibi zilizomo ndani yake zitulie nyoni mwetu, lugha ambazo hata milima madhubuti haiwezi kuhimili uhalisia wa lugha hizo. [4]

Hadith za Shia zinaliangalia kwa jicho la ndani kabisa suala la matumizi ya lugha ya taswira na tashibihi lililopo katika Qur'ani Tukufu. Kwa mfano, katika riwaya iliyosimuliwa kutoka kwa Imamu Ali (a.s), imeeleawa kuwa; moja ya faida za matumizi ya lugha za tashbihi katika Qur'an ni kuwapa somo na mazingatio watu mbai mbali. [5] Katika sehemu nyingine, matimizi ya lugha za taswira katika Qur'ani yamewekwa sambamba na sifa nyengne za Qur'ani, kama vile sifa ya hidaya na sifa ya kutoa mwongozo wazi kwa wahusika wake. [6] Pia kulingana na Riwaya iliyopokewa kutoka kwa Imamu Baqir (a.s), ni  kwamba; Qur'ani imekuja katika sura nne katika uwasilishaji wake, ambapo lugha ya mifano na tashbihi, na mfumo wa sunna za Mwenye Ezi Mungu ni miongoni mwa sura nne hizo. [7] Na Imamu Swadiq (a.s), katika moja ya Hadithi zake anasema kwamba; lugha za mifano zilizomo ndani ya Qur'ani zina faida mno; Kwa hiyo ziangalieni kwa makini na mufikirie maana zake kwa kina na wala msizipite bila ya kuzijali. [8]

Nafasi ya Lugha za Tashbihi katika Kuelewa Dhana za Qur'ani

Jawadi Amuli, mfasiri wa Qur'ani, anabainisha ya kwamba; jukumu kuu la Qur’ani ni kufikisha ujumbe wake wa kimataifa kwa wanadamu wote, nakuendelea kufanya hivyo hadi Siku ya Kiama, kwa kutumia njia zote zinazowezekana katika kufanikisha jambo hilo. Hivyo basi, pamoja na hoja, mijadala kwa kutumia njia njema, pamoja na mawaidha kwa njia mbali mbali, pia matumizi ya lugha ya mifano na tashbihi ni moja ya njia zenye umuhimu mkubwa katika kuelewa na kufafanua dhana zake kwa wanadamu. [9] Kama alivyoeleza Allama Tabatabai, ya kwamba; Mwenye Ezi Mungu hana budi kutumia lugha ya tashbihi ili kufafanua elimu za viwango vya juu, kwa sababu watu wa kawaida wana kawaida ya kuelewa zaidi mambo ya kihisia (kimaada) kuliko dhana za juu za kiakili. Hivyo basi lugha za mifano na tashbihi inawasaidia watu kutafsiri na kuelewa kwa urahisi zaidi maudhui ngumu. [10]

Jawadi Amuli, akirejelea Aya isemayo: (وَ تِلْکَ الْأَمْثَالُ نَضْرِبُهَا لِلنَّاسِ ۖ وَمَا یَعْقِلُهَا إِلَّا الْعَالِمُونَ ; Na hii ni mifano tunaitoa kwa ajili ya watu, lakini hakuna mwenye kutia akilini (kuielewa) isipokuwa wenye maarifa). [11] Anasisitiza ya kwamba; mfano ni kama daraja linalomvusha mwanadamu kutoka kwenye maarifa ya kihisia hadi kwenye maarifa ya kiakili. Kisha, mfano huo humuwezesha mtu kuhama kutoka kwenye maarifa ya kiakili hadi kwenye maarifa ya kiroho ya moyo (ya kushuhudia uhalisia wa mbamo moja kwa moja bila ya kutumia nyenzo fulani). [12] Hivyo, mifano inafanya kazi kama ni nyenzo muhimu kati ya viwango tofauti vya maarifa, ikimsaidia mtu kufikia uelewa wa kina wa mambo ya kiroho na kiirfani.

Tafiti za Welewa wa Dhana ya Lugha za Mifano (Conceptology)

Allama Tabatabai anaeleza kwamba; mifano ima huwa ni kisa cha tukio halisi au ya kubuni ambayo msemaji huitumia kutokana na mfanano wake na mazungumzo yake, ili kuleta uelewa wa kina zaidi katika akili ya msikilizaji. [13] Jawadi Amuli akichambua lugha ya mifano na tashibihi kusema kwamba; sifa ya mfano ni kubeba maarifa mazito ya kiakili hadi kiwango cha maudhui ya kihisia yalio rahisi, ili kuyafanya yaeleweke na kila mtu. [14] Kwa mtazamo wake, matumizi ya lugha za mifano sio tu njia ya kimantiki, bali ni njia ya kurahisisha uelewa, ikiyafanya maarifa yapatikane kwa urahisi na kila mmoja wetu, bila kujali kiwango chao cha elimu au uzoefu walionao. [15]

Mitazamo Miwili Tofauti Kuhusu Matumizi ya Lugha Mifano Katika Qur'ani

Kuna mitazamo miwili tofauti miongoni mwa wataalamu na watafiti mbali mbali katika uchambuzi wa mifano hai ya lugha za tashbihi katika Qur'ani. Mitazamo hii miwili ni kama ifuatavyo: [16]

  1. Lugha za mifano na tashbihi katika Qur'ani ni tashbihi tu zilizotumika kwa ajili ya kuwe wazi dhana za Qur’ani mbele ya msikilizaji kwa nia ya kumrahisishia welewe wa dhana hizo.
  2. Hakuna tashbihi yoyote ile katika matumizi ya lugha za taswira na mifano ya Qur'ani; Bali matumizi ya lugha hizo yanaakisi uwepo halisi wa masuala hayo yaliyozungumzwa kwa njia hizo. [Maelezo 1]

Baadhi ya wafasiri wa Kishi’a, kama vile Allama Tabatabai [17] na Abdullah Jawadi Amuli, [18] sambamba na baadhi ya wafasiri wa upande wa Ahl al-Sunna, kama vile Muhammad Abdu, [19] wanaamini kuwa; Aya zinazohusiana na Ufufuo na mwanzo wa uumbaji, kama vile Aya za uumbaji wa mwanadamu, kusujudu kwa malaika na kuasi kwa Iblisi, zina msingi halisi katika ukweli wa kimaumbile na zinaonekana kuwa na maelezo ya wazi bila ya kuwa ni nia ya kutumia lugha ya kitashbihi ndani yake. Hata hivyo, pia Aya hizo ni zenye kufunua taswira ya mifano ya ukweli wa kimaumbile ulio nyuma ya pazia (ulio jificha) mbele ya dhahiri ya wanadamu. Tunaweza kuita nadharia hii kwa jina la «Lugha ya Mifano ya Kimaumbile», ambayo si tu inachora picha na kuwakilisha taswira maalumu, bali pia inabeba maana na ukweli wa kina kuhusu uhalisia wa mambo yalivyo. [20]

Sifa za Mifano ya Qur'ani

Miongoni mwa na sifa zilizotajwa kuhusiana na lugha za tashbihi zilizomo ndani ya Qur’ani, ni pamoja na; «wenevu wa mtando wake» , «urahisi na uelewa uso na mashaka», «ujengaji taswira ya dhana na kuyapa uhai maneno yaliotika ndani ya lugha hiyo la kitaswira», na pia «matumizi ya vitu dhahiri na matukio asilia». [21]

Kwa mfano, Qur'ani imetumia mifano na tashibihi kadhaa katika kujenga «wepesi na kurahisisha ufahamu wa dhana mbali mbali za Qur’ani». Miongoni mwayo ni pamoja na; «mfano umuhali wa ngamia kutokuwa na uwezo wa kupenya katika tundu ya shidano» unaomaanisha umuhali wa makafiri kuingia Peponi, [22] mfano wa «kula nyama ya ndugu aliyekufa», uliotumika katika kujenga taswira ya ubaya wa kusengenya, [23] na mfano wa «punda anayebeba vitabu», wenye lengo la kujenga taswira ya ubaya wa mtu  asiyetenda kwa kuzingatia elimu aliyo nayo. [24] [25].

Malengo na Athari za Kimaadili za Matumizi ya Lugha za Mifano Katika Qur'ani

Kitabu Tamthili Qur'an, kilichoandikwa na Hamid Muhammad Qassimy

Mifano ya Qur'ani ina malengo na athari muhimu za kimaadili katika kijamii. Baadhi ya malengo na athari hizo ni kama ifuatavyo:

  1. Kutoa Malezi kwa Njia ya Kukuza Thamani za Maadili: Lugha za mifano huwatia watu moyo katika kuthamini za kimaadili mema, ikiwasisitizia umuhimu wa tabia njema katika maisha yao ya kila siku.
  2. Kuchora Taswira na Picha ya Ukweli kwa Njia ya Kihisia: Lugha ya mifano inatoa taswira ya ukweli wa kiroho na wa kiimani katika sura ya mambo ya hisia na yanayoweza kushikika kwa njia za hisia, hivyo kusaidia watu kuelewa zile dhana ngumu za kiroho na kiimani.
  3. Kutoa Mifano Mifano Hai na Halisi: Lugha za mifano huwasilisha mifano halisi na ya kivitendo ambayo inaweza kufuatwa na wengine, na kuwasaidia katika kujenga mitazamo chanya na tabia bora katika jamii.
  4. Kuchochea Fikra na Mawazo ya Mwanadamu: Lugha za mifano huwatia watu hamasa ya kujitahmini na kutafakari, ikiimarisha uwezo wao wa kiakili na kuwasaidia kuelewa changamoto mbalimbali zinazowakabili. [26]

Kwa mfano, kuhusiana na suala la kumzindua mwanadamu kwa lengo la kumlea kimaadili, katika Aya ya 261 ya Surat Al-Baqara, Mwenye Ezi Mungu amemlinganisha mtoaji sadaka na mbegu ipadwayo na kutoa matunda kadhaa, ila kwa kuzingatia madhara ya masimbulizi yanayofuatia baada ya utoaji sadaka yanayoweza kufanya na baadhi ya watoa sadaka, Mwenye Ezi Mungu katika Suratu Al-Aya ya 264 Baqara, ameilinganisha sadaka ya mtu wa aina hii, na vumbi jepesi lillopo juu ya jiwe. Vumbi ambalo halina uwezo wa kuvumilia upepo wala mvua,  ambapo mvua chache tu huliacha jiwe hilo likiwa safi bila vumbi. [27] Allamah Tabatabai, mwandishi wa Tafsir al-Mizan, akielezea malengo ya lugha za mifano katika Qur'ani, katika tafsir ya Aya ya 39 ya Surat Furqan, isemayo; «وَكُلًّا ضَرَبْنا لَهُ الْأَمْثالَ ; Na kila kundi tulilifahamisha kupia lugha ya tashbihi (mifano)», anasema kwamba; Aya hii inakusudia kusema kuwa; Mwenye Ezi Mungu hutumia lugha za mifano na tashibihi kwa nia ya; kukumbusha, kuhubiri na kutoa onyo. [28]

Bibliografia

Katika uwanja wa mifano ya Qur'ani, kumekuwepo na maandiko mbalimbali yaliyoandikwa. Baadhi ya maandiko haya ni:

  • «Ahmad bin Abdallah al-Kawzkanani/ Rawdhatu-l-Amthal» (Fi Al-mthali al-Qur'an al-Karim) kilichoandikwa na Ahmad bin Abdallah al-Kawzkanani al-Najafi, kilichochapishwa mwaka 1325 Hijria. [29] (Kitabu hichi kilifanyiwa uchambuzi wa kina kwenye makala ya "Uchambuzi na ukosowaji wa Kitabu cha Tafsiri 'Rawdhatu-l-Amthal'," iliyowasilishwa na Muhammad Ali Rida'i Kirmani.) [30]
  • Amthaalu al-Qur'an kilichoandikwa na Ali-Asghar Hikmati. (Kitabu hichi kilichapishwa na Taasisi ya Qur'ani huko Tehran.)
  • Amthaalu al-Qur'an kilichoandikwa na Ismail Ismaili. (Toleo la kwanza la kitabu hichi lilichapishwa mwaka 1369 Hijria na shirika la Uswa, kitabu ambacho kimeandikwa kwa kutegemea kitabu cha "Amthal al-Qur'an" cha Hikmat na maelezo ya Suyuti ya kitabu cha "Itqan.")
  • Tamthilat Qur'an, Vijegiha, Ahdaaf wa Aathaa Tarbiyatiye Aan “Sifa, Malengo na Athari za Kimaadili kilichoandikwa na Hamid Muhammad Qasimi. (Sifa ya kitabu hichi, kilichochapishwa mwaka 1382 Shamsia, ni kwamba; kinajumuisha ndani yake mtazamo wa mifano ya Qur'ani kupitia mmtazamo wa kimaadili.)

Maelezo

  1. Tofauti kati ya mitazamo hii miwili inaonekana katika mfano wa Qur'ani ambapo baadhi ya watu wanalinganishwa na «punda» au «mbwa». Kulingana na mtazamo wa kwanza, watu hawa wana sifa zinazofanana na sifa za wanyama hao. Hata hivyo, kulingana na mtazamo wa pili, mfano huu unawakilisha ukweli wao wa kimsingi ambao utaonekana kwa ukamilifu Siku ya Kiama. (Jawadi Amuli, Tafsiri ya Tasnim, 1378 SH, juz. 2, uk. 332.)

Rejea

Vyanzo