Nenda kwa yaliyomo

Ta’abbud

Kutoka wikishia

Ta’abbud (Kiarabu: التَّعَبُّد) ni neno na istilahi y kidini yenye kumaana ya kufuata bila kudadisi na kusalimu amri kikamilifu mbele ya amri za Mwenye Ezi Mungu. Hii inamaanisha kwamba; waumini hua ni wenye kutii maagizo ya Mola wao bila kujua manufaa halisi ya maagizo hayo. Ibada zifanywanazo kwa msingi huu wa Ta’abbud, huhisabiwa kuwa ni aina fulani ya mitihani ya kimungu, yenye lengo la kutofautisha baina ya waumini wa kweli na wasio wa kweli. Hata hivyo, wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kuwa; Kuto kueleweka kwa sababu ya kuwekwa hukumu fulani, hakumaanishi kuwa hukumu hiyo haina sababu maalumu katika kuwekwa kwake mbele ya Mwenye Ezi Mungu. Ndiyo maana Sheikh Saduq katika kitabu chake cha ’Ilalu al-Shara'i’i alijaribu kuelezea falsafa ya hukumu mbali mbali za kisheria.

Kufuata sharia kita’abbud katika hukumu za kisheria, ni jambo linalokubalika mbele ya madhehebu yote ya Kiislamu, na dini haiwezi kuwa na sifa ya dini bila ya kuwepo kwa jambo hilo ndani yake. Suala la Ta’abbud ni suala msingi katika pembuzi za kifiqhi, ambalo ni moja ya kanuni kuu na asili za kifiqhi. Uhusiano kati ya akili na Ta’abbud ni miongoni mwa mada muhimu katika mjadala wa uhusiano kati ya sayansi na dini. Kwa mujibu wa watafiti wa Kiislamu, Ta’abbud haiwezi kumaanisha kusimamisha akili katika suala la kutafakari; hii kwa sababu ya kwamba; masuala ya msingi ya kidini hueleweka kwa msingi wa hoja na uyumkinikaji wake akili.

Kulingana na baadhi ya wanazuoni wa kisasa, tawhidi katika hatua ya mawazo inakinzana na akili na katika hatua ya vitendo inakinzana na uhuru. Baadhi ya watafiti wanasema kuwa maneno haya yanakinzana; kwa sababu kwa upande mmoja hayakanushi uhusiano kati ya dini na tawhidi na kwa upande mwingine yanajaribu kutoa tafsiri za dhana za kidini zisizokuwa za tawhidi. Pia wamesema kuwa kukubali maneno ya mitume kwa msingi wa tawhidi ni kama vile wajinga wanavyomrejea mwanazuoni, jambo ambalo halina shida kwa akili.

«Ta’abbud wa ‘Aqlaaniyyat»; ni kitabu kinachozungumzia mada ya Ta’abbud, kilichoandikwa na Muhammad Jafari.

Umuhimu wa Ta’abbud Katika Tafiti za Kiislamu

Ta’abbud ni istilahi ya kifiqhi na kimaadili, yenye maana ya kujisalimisha kwa waumini kikamilifu mbele ya amri za Mwenye Ezi Mungu. [1] Kulingana na istilahi hii, waumini hata kama hawajui sababu halisi au hekima ya amri za Mola wa, ila wa huzitimiza amri hizo bila ya udadisi wowote ule. [2] Imeelezwa kwamba; sheria na misingi ya dini haiwezi kufikirika wala kuyumkinika bila ya kuwepo kwa msingi wa ta’abbud ndani yake. [3] Kwa hivyo, katu haiwezi kupatikana utengano kati ya ta’abbud na tawhidi. [4] Ta’abbud na kujisalimisha mbele ya Mungu, [5] ndio roho ya Uislamu na ndio msingi mkuu wa dini hiyo, na dini isiyo na ta’abbud huhisabiwa kuwa ni dini isiyo na ukweli ndani yake. [6]

Ta’abbud katika hukumu za kisheria, ni jambo linalokubalika ndani madhehebu yote ya Kiislamu. [7] Kuvunjika kwa msingi huu wa ta’abbud ndiyo sababu ya kuangamia kwa dini fulani. Ta’abbud imezimama nguzo mbili: imani juu ya hekima ya amri za Mwenye Ezi Mungu, na shauku na upendo juu Mwenye Ezi Mungu. Kila mwanafikra mmonotheisti (mwabudu Mungu Mmoja), hana budi kujisalimisha na kuipa akili ya Mungu kipaumbele juu ya fikra zake yeye mwenyewe. [10]

Falsafa ya Ta’abbud

Kutokujua sababu za uwepo wa hukumu za kisheria hakumaanishi kuwa hukumu hizo zimewekwa bila ya sababu. [11] Kwa mujibu wa moja ya Hadithi kutoka kwa Imamu Ridha (a.s), Mungu amewaamrisha waja wake kuwa na ta’abbud katika utendaji wao wa ibada na ushikamanaji wao wa sheria, kwa sababu nyuma ya pazia la kila amri yake Allah kuna hekima, na nyuma ya pazia la kila makatazo kuna madhara fulani, na uwepo wake ni kwa ajili ya manufaa ya waja wake, ambapo uborekaji wa maisha ya wanadamu hutegemea namna ya mshikamano wao na utekelezaji wao wa sheria hizo. [12] Hata hivyo, kama dini nyingine za mbinguni zilivyo, Uislamu nao una hukumu kadhaa ambazo bado falsafa ya uwepo wake haijulikani mbele ya wanadamu. [13] Waumini hukubali na kutekeleza hukumu hizi kwa njia ya ta’abbud katika kumtii Mwenye Ezi Mungu. [14] Ibada zifanywanazo bila kujua falsafa ya uwepo wa hukumu hizo, ni aina ya mtihani wa kimungu wenye nia ya kutofautisha baina ya waumini wa kweli na wale wasiokuwa wa kweli. [15]

Sheikh Sadouq amejitahidi kueleza falsafa ya uwepo wa hukumu za Mwenye Ezi Mungu katika kitabu chake kiitwacho ʻIlal al-Shara-i'i. [16] Kwa mujibu wa maelezo ya Abbas-Ali ‘Amid Zanjani, mwandishi wa kitabu Fiqhe Siyasi (Fiqhi ya Kisiasa), ni kwamba; Yawezekana Sheikh Sadouq, aliyeaga dunia mwaka 381 Hijiria, ndiye mwanazuoni pekee aliyekusanya na kuandika falsafa ya uwepo hukumu hizo. [17] Amid Zanjani anaamini kuwa; Mafakihi wa Kishia hawakutilia maanani wala kujali tafiti za kitabu cha ‘Ilalu al-Shara-I’i, hii ni kwa sababu ya wao kuhofia kutumia mfumo wa qiyas (kutoa fatwa kwa kutumia makisio ya uwiano wa kimaudhui) katika tafiti za kifiqhi, na pia kwa sababu ya kutoidhoofisha hisia ya ta’abbud walionayo waja wa Mwenye Ezi Mungu. [18] Hata hivyo, Zanjani anauhisabu mtazamo huu ni kinyume na njia ya Qur'ani katika kuelezea sheria zake, kwani ndani ya Qur'ani kumeezewa hekima na manufaa au madhara ya uwepo wa baadhi ya hukumu fulani za kisheria. [19]

Muhammad Taqi Ja’afari, ambaye ni mwanafalsafa na mwanatheolojia wa Kishia, naye pia anaamini kwamba; Hukumu zote za kifiqhi zimesimama juu ya msingi madhubuti na ni zenye falsafa maalumu juu ya uwepo wake, pia sheria na hukumu zisizokuwa za kiibada nazo zaweza kufahamika na kueleweka falsafa yake kupitia akili salama. [20] Hata hivyo; wengine wanadhania kwamba, mengi miongoni mwa mafunzo ya Kiislamu yabidi kushikamana nayo kwa njia ya kita’abbud tu, kwa sababu mafunzo hayo katu hayawezi kudirikika kupitia welewa wa kiakili na kifalsafa. [21]

Ta’abbud na Akili

Kwa mujibu wa maelezo ya wanazuoni wa Kiislamu, ta’abbud inayopatikana katika dini ya Kiislamu, imesimama juu ya msingi wa akili; kama lilivyo suala la taqlidi (kufuata fatwa za mwanazuoni fulani) katika hukumu za kidini, kiuhalisia sula la taqlidii nalo limesimama juu msingi wa uchunguzi na akili. [22] Kwa hivyo, ta’abbud haimaanishi kuifunga akili na kuizuia kufikiri, kwani misingi mikuu ya dini (itikadi) yanajengwa juu ya msingi wa hoja madhubuti na akili yakinifu. [23] Kwa mujibu wa maoni ya Muhammad Hussein Tabataba'i, ambaye ni mwanafalsafa na mfasiri wa Qur'ani, ni kwamba; wafuasi wa baadhi ya dini wameibua masuala yasiyokuwa ya kiakili katika dini zao, na wakajaribu kuyatetea kwa hoja ya kwamba; ni hali ya kaida kuwepo kwa baadhi ya masuala ya ta’abbud (ushikamanaji wa ibada za kidini) yaendayo kinyume na akili. [24] Tabatabai, akiona tabia hii kuwa ni yenye mgongano ndani yake, anasema; Inawezekanaje kwa upande mmoja, ukweli wa dini kuthibitishwa na akili; lakini kwa upande mwingine, dini hiyo hiyo iwe na masuala ambayo akili haikubaliani nayo, bali ni yenye kusutwa na akili? [25]

Mada ya akili na taʻabbud ni mojawapo ya mijadala muhimu inayozungumzia uhusiano kati ya akili na ufunuo (Wahyi) au uhusiano kati ya sayansi na dini. [26] Kwa mujibu wa watafiti ni kwamb; Katika Nyanja za welewa na ufahamu twapaswa kutumia akili zetu, na katika nafasi ya utekelezaji twapaswa kuwa na taʻabbud (utekelezaji bila ya kuleta udadisi wala vikwazo). [27] Kwa hiyo, imeelezwa ya kwamba; misingi ya imani yapaswa kukubaliwa kupitia hoja za kiakili na haipaswi kukubaliwa kwa njia ya ta’abbud tu. [28] Watafiti wengine wanasema kwamba; Kipengele muhimu zaidi katika mjengeko na utafauti uliopo kati ya madhehebu manne ya Ahlu-Sunna, ni aina ya mitazamo yao kuhusiana na mwelekeo wa juu ya matumizi yao akili au kushikamana kwao na ta’abbud bila kujali akili. [29]

Ta’abbud na Uchopoaji au Uvuaji wa Hukumu za Kisheria (Istinbati)

Neno Ta’abbud, ni kinyume cha neno ta’aqqul (kutafakari na kudadisi kupitia hoja za kiakili). Ta’abbud ni mojawapo ya kanuni zinazotawala katika harakati za uchambuzi na upembezi kwa ajili ya uchopoaji na uibuaji wa kanuni za kifiqhi. [30] Kutambua mipaka ya akili na ya ta’abbud, ni mojawapo ya tafiti muhimu katika masuala yanayo ambatana na hukumu za kisheria. [31] Kwa mujibu wa baadhi ya mafaqihi, nyanja ya ta’abbud katika dini inajumuisha ibada peke yake, na katu haijumuishi miamala ndani yake. [32] Kwa hivyo, katika suala la miamala, mafaqihi wanapaswa kuainisha nguzo zinazo dhamini uhalali wa miamala au visababishi vya uhalali wa miamala kutoka katika Hadithi, na sio kuanisha hukumu za kifiqhi. [33] Kwa mujibu wa maelezo ya ‘Amid Zanjani, ni kwamba; migogoro na vizingiti vilivyopo kati ya ta’abbud na akili katika fiqh ya Kishia, ni masuala ambayo yamesha patiwa ufumbuzi, kwani mafaqihi wa Kishia huihisisha ta’abbud na nyanja za hukumu zenye ushahidi kutoka Qur'ani au hadithi, huku nyanja ya akili ikiwa ni maalum kwa ajili ya hukumu zisizo anzilishwa kupitia Qur’ani na Hadithi pamoja na hukumu za kiserikali. [34] [Maelezo 1]

Mtazamo wa Wanamageuzi

Wasiwasi mkubwa wa wasomi wa kisasa ni kuhusiana mgongano kati ya akili na kushikamana na msingi wa ta’abbud katika dini. [35] Imeelezwa kuwa; Kujiepusha na ta’abbud ni mojawapo ya mafanikio muhimu ya mfumo wa kimamboleo (Modernism). [36] Mustafa Malikian ambaye ni mtaalamu na mwalimu wa fani ya falsafa, anaamini kuwa; Katika ngazi ya kinadharia ta’abbud inapingana na akili, na katika ngazi au hatua ya vitendo, ni yenye kupingana na uhuru. [37] Hata hivyo, Malikian anaamini kwamba; ta’abbud yenye msingi wa kiakili haina tatizo na hiana aina kama hiyo ya migongano. [38]

Abdul-karim Soroush, ambaye ni mmoja wa watafiti wa Kiislamu; anaamini kwamba; sehemu ya ibada katika fiqh ni mchanganyiko siri khadhaa ndani yake, na yapaswa kukubaliwa kwa njia ya ta’abbud; ila sehemu ya miamala katika fiqh haina siri kama hizo ndani yake. [39] Muhammad Mujtahidi Shabestari, pamoja na kuamini juu ya kuto kuwepo kwa siri fulani ndani ya sehemu ya miamala, pia anaamini kwamba, sehemu ya fiqhi ya ibada nayo haina siri yoyote ile ndani yake. [40] Kwa mujibu wa imani ya Shabestari, ni kwamba; fatwa nyingi za mafaqihi katika masuala ya siasa hazina msingi wa kiakili, na husababisha kupotea kwa maslahi kadhaa ya Waislamu. [41]

Ukosoaji wa Maoni ya Wanamageuzi

Kulingana na baadhi ya watafiti, ni kwamba; wanamageuzi wako njia panpa kati ya imani ya dini na ulumwengu wa kimamboleo (Modernism), na njia panda hii ndio iliyo wasababishia mkanganyiko wa maneno; kwa sababu, kwa upande mmoja, wao huwa hawakanushi uhusiano kati ya ta’abbud na dini, lakini kwa upande mwingine, wanajaribu daima kutoa tafsiri za mafundisho ya kidini ambazo hazihusishi msingi wa ta’abbudi ndani yake. [42] Muhammad-Taqi Ja’afari anaamini kwamba; Kule wanamageuzi kuiweka ta’abbudi kuwa ni kinyume na mantiki, hili ndilo lililo pelekea wao kuiona dini kuwa na mantiki kama vitu viwili vinavyopingana. [43]

Kitabu chenye jina la Ta’abbud wa Aqlaniyat, kilichoandikwa na Muhammad Ja'afar

Kulingana na watafiti mbali mbali ni kwamba; Kukubaliana na ta’abbudi pamoja na imani ya uwepo wa siri maalumu katika dini, kumesimama kwenye misingi ya kimantiki; hii ni kwa sababu ya kwamba, kwa upande mmoja dini ina uhusiano wa moja kwa moja na ulimwengu wa ghaibu na imefungamana na siri za ulimwengu huo, na manabii hufikisha ujumbe wa ulimwengu wa ghaibu kwa ajili ya wokovu wa wanadamu. Kwa upande mwingine ni kwamba; Kukubali maneno ya manabii kwa ajili ya wokovu, ni mojawapo ya hukumu za kimantiki zimuamurizo asiyejua kumtafuta mwenye kujua ili kumkidhia haja zake. [44] Baadhi ya watafiti wameona kuwa; Si sahihi kuvuka mipaka katika kutoa tafsiri dhidi ya imani ya ta’abbudi. Pia, watafiti hao wamesema kuwa; Wanamageuzi wanapokutana na mafundisho ya kidini huwa na hukumu za mapema; wamesema hivyo kwa sababu ya kule kuyahisabu kwao maandiko ya kidini kuwa ni maandiko yasio na siri ndani yake wala yasio na hadhi ya kupewa tahamani ya ta’abbud. [45] Muhammad-Taqi Misbah Yazdi anaamini kuwa; kufikiri kwa njia ya kimamboleo katika masuala ya kita’abbudi, ndio mwanzo wa kupatikana kwa aina fulani za upotovu katika baadhi ya vikundi vya kisiasa vinavyodai kushikamana na Uislamu. [46]

Bibliografia (Vitabu Maalumu)

Vitabu vifuatavyo ni miongoni mwa vitabu vilivyoandikwa kuhusu ta’abbud:

  • «Ta’abbud wa Ta’aqqu Dar Fiqh ya Islami»: ni kitabu kilichoandikwa na Muhammad Taqi Jafari: Kitabu hichi kilichapishwa mwaka 1373 Shamsia na Kongresi ya Kumbukumbu ya Sheikh Ansari huko Qom.
  • «Ta’abbud wa Aqlaaniyyat»: ni kitabu kilichoandikwa na Muhammad Jafari: Kitabu hichi kilichapishwa na Kituo cha Mawazo ya Vijana mwaka 1402 Shamsia, katika kurasa 168. Miongoni mwa tafiti za kitabu hichi ni: Dhana ya ta’abbud, vipengele vyake mbalimbali, na uhusiano kati ya ta’abbud na akili.

Maelezo

  1. Kikawaida hukumu huwa zimegawika katika sehemu mbili: A. Hukumu zipatikanzo moja kwa moja katika Qur’ani na Hadithi. B. Hukumu zizalishwajo kupitia kupitia jopo la wanasheria maalumu.

Rejea

Vyanzo