Nenda kwa yaliyomo

Siyanati Maashita, Mke wa Hazkili

Kutoka wikishia

Ṣiyaanati Maashṭa Mke wa Hazqil (Mu’min Aali Fir’aun) Taarifa za Jumla • Ukaribu wa Kifamilia: Mke wa Mu’min Aali Fir’aun • Kuzaliwa: Kipindi cha Utawala wa Farao (Firauna) • Mahali Alipoishi: Misri • Kifo: Aliuawa pamoja na watoto wake kwa amri ya Firauna kwa sababu ya imani yake kwa Mwenye Ezi Mungu Taarifa Nyingine • Asili: Msusi wa binti ya Farauna • Mhusika: Moja ya wanawake watakaofufuliwa baada ya kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.s)

Siyanati Maashita, Mke wa Hazkili Siyana Mashita, mke wa Hazkili (Muumini wa Aalu Firauni), aliuawa yeye pamoja na wanawe kupitia amri ya Firauna, kutokana na imani yake thabiti kwa Mwenye Ezi Mungu. Kulingana na masimulizi ya vyanzo mbali mbali, yeye ni mmoja wa wanawake wanaotarajiwa kurudi tena duniani baada ya kudhihiri Imamu Mahdi (a.f). Kwa mujibu wa baadhi ya Riwaya, mke wa Hazkili, anayejulikana kama "Siyanati Maashita," alikuwa mrembeshaji (msusi) wa binti ya Firauna. Siku moja, alipokuwa akimpamba binti wa Firauna, alitamka jina la Mwenye Ezi Mungu mbele ya binti huyo. Binti wa Firauna akaenda kwa baba yake (Firauna), na kumjulisha kwamba Siyana alikuwa ni miongoni mwa waumini wanaoamini juu ya kuwepo kwa Mwenye Ezi Mungu, na wala hamtambui Firauna kama ni Mungu. Hapo Firauna akachukuwa uamuzi wa kuteketeza wanawe mbele ya macho yake kupitia tanuri ya shaba, lakini Siyana alikataa kubadili imani yake. Baadae, Firauna akaamua mteketeza msusi huyo muumini wa Mungu Mmoja. [1] Nafasi ya Siyanati Maashita na wanawe katika Riwaya imetajwa kama ifuatavyo: • Pale bwana Mtume (s.a.w.w) alipokuwa katika safari yake ya Mi‘raj, alisikia harufu inayovutia mno, baada ya bwana Mtume (s.a.w.w) kumuuliza Jibrilu kuhusiana na harufu hiyo, Jibrilu alimjibu na kumweleza kuwa ni harufu inayotokana na majivu ya Siyana na wanawe. [2] • Siyana ni miongoni mwa wanawake wanaotabiriwa kurudi tena duniani wakati wa kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.f), ili kuwahudumia na kuwatibu majeruhi. [3] • Ibn Abbas anamhisabu mtoto wa mwisho wa familia hii kama ni mmoja wa watoto wanne walioweza kunena wakiwa bado ni wachanga. Kwa mujibu ya maelezo ya Ibnu Abbas ni kwamba; Pale Firauna alipokuwa anakaribia kumteketeza mtoto wa mwisho wa mama huyo, mtoto huyu alitamka na kumwambia mama yake akisema: "Ewe Mama, kuwa na subira, kwani wewe uko katika njia ya haki". [4]