Siyanati Maashita
Jina | Siyana Mashita |
---|---|
Jamaa Maarufu | Mke wa Hazkili (Muumini wa Aalu Firauni) |
Mahali pa Makazi | Misri |
Kifo cha Kishahidi | Aliuwawa pamoja na watoto wake kwa amri ya Firauni |
Shughuli | Msusi wa binti ya Firauna |
Mahusiano | Yeye ni mmoja wa wanawake ambao watarejea baada ya kudhihiri kwa Imam al-Zaman (a.s). |
Siyana Mashita (Kiarabu: صيانة الماشطة), mke wa Hazkili (Muumini wa Aalu Firauni), aliuawa yeye pamoja na wanawe kupitia amri ya Firauna, kutokana na imani yake thabiti kwa Mwenye Ezi Mungu. Kulingana na masimulizi ya vyanzo mbali mbali, yeye ni mmoja wa wanawake wanaotarajiwa kurudi tena duniani baada ya kudhihiri Imamu Mahdi (a.j.t.f).
Kwa mujibu wa baadhi ya Riwaya, mke wa Hazkili, anayejulikana kama "Siyanati Maashita", alikuwa mrembeshaji (msusi) wa binti ya Firauna. Siku moja, alipokuwa akimpamba binti wa Firauna, alitamka jina la Mwenye Ezi Mungu mbele ya binti huyo. Binti wa Firauna akaenda kwa baba yake (Firauna), na kumjulisha kwamba Siyana alikuwa ni miongoni mwa waumini wanaoamini juu ya kuwepo kwa Mwenye Ezi Mungu, na wala hamtambui Firauna kama ni Mungu. Hapo Firauna akachukuwa uamuzi wa kuteketeza wanawe mbele ya macho yake kupitia tanuri ya shaba, lakini Siyana alikataa kubadili imani yake. Baadae, Firauna akaamua mteketeza msusi huyo muumini wa Mungu Mmoja.[1]
Nafasi ya Siyanati Maashita na wanawe katika Riwaya imetajwa kama ifuatavyo:
- Pale bwana Mtume (s.a.w.w) alipokuwa katika safari yake ya Mi‘raj, alisikia harufu inayovutia mno, baada ya bwana Mtume (s.a.w.w) kumuuliza Jibril kuhusiana na harufu hiyo, Jibrilu alimjibu na kumweleza kuwa ni harufu inayotokana na majivu ya Siyana na wanawe.[2]
- Siyana ni miongoni mwa wanawake wanaotabiriwa kurudi tena duniani wakati wa kudhihiri kwa Imamu Mahdi (a.j.t.f), ili kuwahudumia na kuwatibu majeruhi.[3]
- Ibn Abbas anamhisabu mtoto wa mwisho wa familia hii kama ni mmoja wa watoto wanne walioweza kunena wakiwa bado ni wachanga. Kwa mujibu ya maelezo ya Ibnu Abbas ni kwamba; Pale Firauna alipokuwa anakaribia kumteketeza mtoto wa mwisho wa mama huyo, mtoto huyu alitamka na kumwambia mama yake akisema: "Ewe Mama, kuwa na subira, kwani wewe uko katika njia ya haki".[4]
Rejea
- ↑ Jazairi, Al-Nur al-Mubin, 1404 AH, uk. 260; Majlisi, Bihar al-Anwar, 1362 AH, juz. 13, uk. 163; Majlisi, Hayat al-Qulub, 1384 AH, juz. 1, uk. 243.
- ↑ Majlisi, Bihar al-Anwar, 1362 S, juz. 13, uk. 163.
- ↑ Tabari, Dalail al-Imamah, 1383 S, uk. 260; Mahallati, Riyahin al-Shari’a, Dar al-Kutub al-Islamiyya, juz. 5, uk. 41.
- ↑ Tha’labi, Qasas al-Anbiya, 1414 AH, uk. 188.
Vyanzo
- Al-Jazairi, Niʿmat Allah bin Abd Allah, Al-Nur al-mubin Fi Qisas al-anbiyaʾ wa al-Mursalin, Qom: Maktabat Ayatullah al-Marʿashi, 1404 AH.
- Majlisi, Muhammad Baqir, Bihar al-Anwar, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyya, 1362 Sh.
- Majlisi, Muhammad Baqir, Al-Hayat al-Qulub, Qom: Sarwar, 1384 Sh.
- Mahallati, Dhabih Allah, Riyahin al-shari'a, Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyya.
- Thaʿlabi, Abi Ishaq Ahmad bin Muhammad, Qasas al-anbiya, Beirut: 1414 AH.
- Tabari, Muhammad bin Jarir al-Dalaʾil al-Imama, Qom: Dar al-Dhakhaʾir, 1383 AH.