Nenda kwa yaliyomo

Sikukuu za mwezi wa Sha'ban

Kutoka wikishia
Sherehe ya nusu-Sha'ban katika Msikiti wa Jamkaran

Sikukuu za mwezi wa Sha'ban (Kiarabu: الأعياد الشعبانية) ni kumbukumbu ya kuzaliwa Maimamu kadhaa wa Kishia na watoto wao katika mwezi wa Sha'ban. Kwa mujibu wa vyanzo, Imamu Hussein bin Ali (a.s) alizaliwa 3 Sha'ban [1] na kwa mujibu wa kauli nyingine alizaliwa tarehe 5 Sha'ban mwaka wa 3 Hijria [2], Imamu Sajjad (a.s) amezaliwa tarehe 5 [3] au 9 Sha'ban [4] na Imamu Muhammad Mahdi (a.t.f.s) amezaliwa tarehe 15 Sha'ban [5]. Pia, baadhi ya vyanzo vinachukulia kuzaliwa kwa Hadhrat Abbas (a.s) kuwa ni tarehe 4 Sha'ban [6] na kuzaliwa Hadhrat Ali Akbar mnamo tarehe 11 Sha'aban. [7]. Hata hivyo katika baadhi ya vyanzo tarehe zingine zimeandikwa za kuzaliwa kwa Imam Sajjad [8] na Imam Mahdi (a.s) [9]. Pia, siku za kuzaliwa za Hazrat Abbas [10] na Ali Akbar [11] hazijaandikwa katika vyanzo vilivyotangulia.

Katika siku hizi, Waislamu wa madhehebu ya Shia husherehekea kwa kupamba mitaa, misikiti na Haram, za Ahlul-Bayt (a.s), kuimba na kuwasifu Maimamu (a.s) pamnoja na kutoa nadhiri. Nchini Iran, sherehe kubwa zaidi kati ya hizi hufanyika katika Msikiti wa Jamkaran, Qom katikati ya Sha'ban. [12] Nchini Iraq, Waislamu wa madhehebu ya Shia huenda kumzuru Imamu Hussein (a.s) kwa miguu huku wakisherehekea nusu ya Sha'ban. Sherehe za nusu ya Sha'ban (15 Sha'ban) pia hufanywa na Mashia katika nchi za Kiislamu kama vile Bahrain, Misri na India. [13]

Katika kalenda ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, tarehe 3 Sha'ban ni siku ya kuzaliwa Imam Hussein imepewa jina la "Siku ya Mlinzi", tarehe 4 Sha'ban ni siku ya kuzaliwa Hazrat Abbas inafahamika kama "Siku ya Vilema wa Vita" na tarehe 5 Sha'ban ambayo ni siku ya kuzaliwa imamu Sajjad inajulikana kama Siku ya Sahifa Sajjadiya, tarehe 11 Sha'ban ni siku ya kuzaliwa Ali Akbar, na tarehe 15 Sha'ban ambayo ni siku yake ya kuzaliwa Imam Mahdi (a.j.t.f) imeitwa "Siku ya Kimataifa ya Wastadhaafu (Wanyonge)".[14]

Rejea

Vyanzo