Seif bin Harith al-Hamdani

Kutoka wikishia

Seif bin Harith bin Sari'i al-Hamdani (alikufa shahidi 61 H) ni miongoni mwa mashahidi wa Karbala ambaye aliuawa shahidi katika siku ya Ashura akiwa pamoja na Malik bin Abdallah bin Suray binamu yake na kaka yake wa kuchangia mama. Seif alitokana na kabila la Hamdan kutoka katika ukoo wa Bani Jabir na ni kutokana na sababu hiyo yeye na binamu yake wanafahamika kama wa mashahidi wa Kijabiri. Katika vyanzo vya historia kumeripotiwa mazungumzo yake yeye na na Malik pamoja na Imamu Hussein (a.s). Imekuja katika ripoti hiyo kwamba, wawili hao walikwenda kwa Imamu Hussein (a.s) siku ya Ashura hali ya kuwa wanalia na katika kumjibu Imamu Hussein ambaye aliwauliza sababu ya kulia kwao walisema: Hawawezi kufanya chochote kwa ajili ya Imamu Hussein mkabala wa adui.


Jina na asili

Seif bin Harith bin Suray ni mmoja wa mashahidi wa Karbala [1] ambaye baadhi wanaamini kwamba, jina lake limekuja kwa sura tofauti katika vitabu na vyanzo vya historia kama vile "Shabib bin Harith bin Suray" [2] na "Sufyan bin Suray. [3] Baadhi wamezungumzia uwezekano kwamba Seif bin Harith, ambaye katika baadhi ya vyanzo anahesabiwa kuwa ni miongoni mwa mashahidi wa Karbala [4] ndio huyo huyo Seif bin Harith [5].

Seif bin Harith ametajwa katika Ziyara ya Rajabiya ya Imamu Hussein (a.s.) [6], lakini katika Ziraya ya Shuhadaa (Ziyara Nahiyah isiyo mashuhuri) amesalimiwa kwa jina la Shabib bin Harith bin Suray. [7] Baadhi wanaona kuwa, huyu ni mtu mmoja na sio watu wawili. [8] Baadhi wamemhesabu Seif kuwa miongoni mwa mashahidi vijana wa Karbala. [9] Katika vyanzo vya historia pia Seif bin Harith ametajwa kuwa ni kijana.

Asili Seif bin Harith alitokana na kabila la Hamdan [11] na kutoka ukoo wa Bani Jabir [12]. Baadhi wamemchukulia kuwa anatoka katika ukoo wa Bani Faish. [13] Yeye na binamu yake Malik bin Abdullah bin Suray, ambao walikuwa ni ndugu kutoka upande wa mama yao, [14] wametajwa kwa jina la "Mashahidi wa Kijabiri." [15]

Kufa shahidi

Seif na binamu yake Malik pamoja na mtumwa wao Shabib bin Abdullah Nahshali waliungana na Imamu Husein (a.s.) [16]. Inaelezwa kuwa, watu hawa watatu walikwenda kwa Imamu wakitokea katika mji wa Kufa. [17] Muhammad bin Jarir Tabari (aliaga duni 310 H) mwandishi wa historia wa Kisuni anazingatia kuuawa shahidi kwa Seif na Malik kuwa ni mchana wa siku ya Ashura. Kwa mujibu wa Tabari, masahaba wa Imamu Hussein (a.s.) walipotambua kwamba ushindi haukuwezekana kutokana na kuongezeka kwa maadui, waliamua kushindana wao kwa wao katika kutoa maisha yao kwa ajili ya Imamu Hussein. [18]


Mazungumzo ya vijana wawili mashahidi wa Kijabiri na Imamu Hussein (a.s)

Imamu Hussein (a.s) aliwaambia: Enyi ndugu zangu! Mnalia nini? Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu nataraji sasa hivi muwe na furaha. Vijana wale wakasema: Mwenyezi Mungu atufanye tuwe fidia kwako, hatujilii sisi wenyewe, tunakulilia wewe tunapoona wamekuzingira na hatuna uwezo wa kukutetea. (Imam) akasema: Enyi ndugu zangu! Mwenyezi Mungu wenu akulipeni malipo bora zaidi ya wachamungu katika huzuni hii na kwa msaada mnaotoa kwa maisha yangu. [19]

Inasemekana kwamba Seif bin Harith na Malik walikuja kwa Imam huku wakitokwa na machozi [20] walipomwona adui akiikaribia hema ya Imamu Husein (a.s.) [20]. Imamu aliwauliza sababu ya kulia kwao. Walisema, walilia kwa sababu ya kuona hali ya Imamu na kushindwa kwao kumsaidia ambapo Imamu Hussein aliwasifu na kuwaombea dua kwa msimamo wao. [21] Vyanzo vya historia vinasema, Seif na Malik walikimbia kuelekea katika uwanja wa vita baada ya kuzungumza na Imamu, huku wakashindana [22] wao kwa wao katika vita na kusaidiana. [23] Baada ya muda, Seif na Malik walimsalimia Imam Husein (a.s.) na Imam akajibu salamu yao. [24]

Mazungumzo kama haya yamenukuliwa pia kuhusiana vijana wawili wa Ghiffari, Abdullah na Abd al-Rahman bin Urwa Ghiffari. [25] Hata hivyo, baadhi wanaamini kwamba katika baadhi ya vyanzo, kama vile Maqtal al-Hussein Khwarazmi, kumechanganywa mazungumzo ya vijana wawili wa Jabiri na vijana wawili wa Ghiffari. [26] Katika kitabu cha Maqtal cha Khwarazmi, mazungumzo yaliyotajwa yanahusishwa na vijana wawili wa Ghiffari, na kwa upande wa vijana wawili wa Jabiri, ni salamu yao tu kwa Imamu Husein (a.s.) na jibu la Imamu ndilo lililoelezwa na mwandishi kutosha na hilo tu. [27]

Ikhlasi (nia njema) na kujitolea kwa Seif na Malik kumezingatiwa na baadhi ya waandishi wa sira. [28] Hawa wawili baada ya mapigano makali na wapanda farasi na askari wa miguu waliuawa shahidi [29] kutokana na kupigwa kwa upanga na mikuki karibu na Imam [30] katika eneo moja. [31] Alipoiona miili yao, Imamu alilia na kuwaombea msamaha na maghfira, na huku akionyesha kusalimu amri kwa majaaliwa na qadari kwamba, kila mtu atarejea kwa Mungu. [32]

Wanahistoria wameandika tarehe tofauti za kufa shahidi Seif na Malik. Baadhi wamesema kifo chao cha kishahidi kilikuwa baada ya Hajjaj bin Masrouq, [33] na wengine wamesema kilikuwa baada ya kifo cha kishahidi cha Hanzalah bin Qays [34] au Hanzalah bin As’ad [35]. Baadhi ya watu wametambua kuuawa kwao shahidi kuwa ni baada ya Abdullah na Abd al-Rahman bin Urwa Ghiffari. [36]