Nenda kwa yaliyomo

Sayyidat Nisa’ al-Alamin

Kutoka wikishia

Sayyidat Nisa’ al-Alamin (Kiarabu: سَیّدَةُ نِساءِ الْعالَمین) ina maana ya kiongozi wa wanawake wote duniani. Sayyidat Nisa’ al-Alamin ni katika lakabu na fadhila za Bibi Fatima (a.s). Kwa mujibu wa vyanzo vya hadithi vya Waislamu wa madhehebu ya Shia [2] na Ahlu-Sunna [3], Mtume (s.a.w.w) ndiye aliyempatia Fatima lakabu hii. Kwa mujibu wa Ibn Abil al-Hadid ni kuwa, ibara hii imepokewa kwa sura ya mutawatir kilafudhi au kimaanawi kutoka kwa Bwana Mtume (s.a.w.w). [4]

Katika maneno ya Imamu Ali (a.s) aliyoyasema wakati anamzika Fatima ambayo yamenukuliwa katika kitabu cha al-Kafi vilevile ibara hii imetumiwa kwa ajili ya Fatima (a.s). [5] Kadhalika lakabu hii imetajwa katika baadhi ya maandiko ya Ziyara kama Ziyara ya Imamu Ali (as), [6] Zitayar ya Bibi Fatima Zahra (a.s), [7] Ziyarat Waritha, [8] Ziyarat Ashura [9] na Ziyarat Ridha (a.s) [10] kwa anuani ya lakabu ya Zahra (a.s).

Katika hadithi zingine katika vyanzo vya Ahlul-Sunna imenukuliwa ya kwamba, Mtume (s.a.w.w) amemtaja Fatima kuwa ni kiongozi wa wa wanawake waumini, kiongozi wa wanawake wa Umma wa Kiislamu na kiongozi wa wanawake wa peponi.

Katika baadhi ya hadithi kando ya Fatima (a.s) kuna wanawake ambao wametajwa kuwa ni viongozi wa wanawake wote duniani [12] ambao ni Maryam bint Imran mama yake Nabii Issa (a.s), Asia mke wa Firauni na Khadija bint Khuwailidi mke wa Mtume (s.a.w.w). Hata hivyo kwa mujibu wa hadithi, Maryam ni kiongozi wa wanawake katika zama zake na Fatima hi kiongozi wa wanawake wa mwanzo na wa mwisho yaani wanaweake wote duniani. [13] Aidha ili kuthibitisha kwamba, Fatima ni mwanamke bora zaidi ya wanawake wengine, kumetumiwa kama hoja maneno ya Mtume (s.a.w.w) ambayo anamtaja Fatima kuwa ni pande la nyama yake. [14]

Katika kumbukumbu ya kuzaliwa na kufa shahidi Bibi Fatima (a.s), Waislamu wa madhehebu ya Shia hutumia vitambaa na maberamu kwa ajili ya kupamba maeneo yao ya maombolezo au sherehe ambayo huwa yameandikwa ibara hii. [15]

Vyanzo

  • Ibn al-Mashhadī, Muḥammad. Al-Mazār al-kabīr. 1st edition. Qom: Daftar-i Intishārāt-i ʿIslamī, 1419 AH.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Tehran: al-Maktaba al-Islāmīyya, 1388 AH.
  • Muntakhab faḍāʾil al-nabīyy wa Ahl Baytih min al-ṣiḥāḥ al-sitta wa ghayrihimā min al-kutub al-muʿtabara ʿind ahl al-sunna. Beirut: al-Ghadīr, 1423 AH.
  • Rājī Kannāṣ, Muḥammad al-. Ḥayāt nisāʾ Ahl al-Bayt. Beirut: Dār al-Maʿrifa, 1429 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. ʿUyūn akhbār al-Riḍā. Edited by Mahdī Lājiwardī. Tehran: Nashr-i Jahān, 1378 AH.
  • Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-. Man lā yaḥḍuruh al-faqīh. Edited by ʿAlī Akbar Ghaffārī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1413 AH.
  • Ṭūsī, Muḥamamd b. al-Ḥasan al-. Miṣbāḥ al-mutahajjid. 1st edition. Beirut: Muʾassisat Fiqh al-Shīʿa, 1411 AH.