Maneno ya Imamu Ali (a.s) alipokuwa akimzika Fatima (a.s)

Kutoka wikishia

Maneno ya Imamu Ali (a.s) wakati wa kumzika Fatima Zahra (a.s) binti mtukufu wa Bwana Mtume (s.a.w.w) yanajumuisha matamshi ya uchungu ya kutoka moyoni ya Ali (a.s) ya kuliwazana na Mtume (s.a.w.w) katika maombolezo ya Fatima. Maneno haya yamekuja katika kitabu cha Nahaj al-Balagha. Katika maneno haya, Imamu Ali (a.s) anazungumzia uzito wa msiba na kuwa ya daima ghamu na huzuni yake kutokana na kufa shahidi Bibi Fatima na anamtaka Mtume (s.a.w.w) amuulize Bibi Fatima kuhusiana na matukio yaliyotokea baada ya yeye (Mtume) kuaga dunia na kurejea kwa Mola wake. Wafafanuzi wa Nahaj al-Balagha wanaamini kuwa, Imamu Ali kwa kutumia ibara jumla ya "Muulize Fatima" kuhusiana na matukio yaliyotokea baada ya wewe kuaga dunia anaashiria matukio kama kupokonywa Fadak na tukio la kushambuliwa na kuvamiwa nyumba ya Fatima na kuharibika mimba ya Muhsin (a.s). Kadhalika kupitia ibara za hotuba hii kumefikiwa natija nyingine kama kuzikwa Fatima karibu na kaburi la Bwana Mtume (s.a.w.w).

Maneno haya yamekuja katika vitabu mbalimbali vya hadithi vya Mashia kama vile al-Kafi na al-Amali Sheikh Tusi na vitabu vya Ahlu-Sunna kama Tadhkirat al-Khawas.

Mazingira ya kutolewa hotuba hii na umuhimu wake

Maneno ya Imam Ali (a.s) kwa Mtume (s.a.w.w) wakati wa kumzika Bibi Fatima (a.s) yanachukuliwa kuwa yanaashiria huzuni ya Imamu kwa kutengana na mke wake na yanadhihirisha adhama na utukufu wa Fatima (a.s). [1] Kwa mujibu wa Ayatullah Makarim Shirazi katika kutoa ufafanuzi wa maneno haya katika Nahaj al-Balagha ni kuwa, maneno haya yanaakisi baadhi ya mambo muhimu ya ukweli wa kihistoria mwanzoni mwa Uislamu kwa njia isiyo ya moja kwa moja, lakini kwa uwazi na kwa maana kubwa. [2]

Wafafanuzi wa Nahaj al-Balagha wamewashiria chini ya hotuba na maneno haya masuala kama tukio la Fadak, kuporwa Ukhalifa Imamu Ali (a.s), sababu ya kufichwa na kutotambulika kaburi la Fatima, wakati wa kufa kwake shahidi, [3] muda wa maisha yake [4] na lakabu za Fatima. [5]

Maudhui

Maneno ya Imam Ali (a.s) kwa Mtume (s.a.w.w) wakati wa kumzika Bibi Fatima (a.s) yanatathminiwa kuwa yanaashiria huzuni ya Imamu kwa kutengana na mke wake Fatima (a.s). [6] Anazungumzia uzito na kuwa ya daima ghamu na huzuni yake kutokana na kufa shahidi Bibi Fatima na anamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie subira. Imamu Ali (a.s) anamtaka Mtume (s.a.w.w) amuulize Bibi Fatima kuhusiana na matukio yaliyotokea baada ya yeye (Mtume) kuaga dunia na kurejea kwa Mola wake. Katika maneno haya Imamu Ali anamtambulisha Fatima kuwa ni amana iliyokuwa mikononi mwaka ambayo sasa inarejeshwa kwa Mtume (s.a.w.w). [7]

Uelewa wa kimaudhui

Katika ufafafanuzi wa Nahaj al-Balagha chini ya hotuba hii, kumeelezwa nukta zilizofahamika kuhusiana na hotuba hii. Baadhi ya nukta hizo ni:

  • Mfungamano mkubwa wa kihuba baina ya Ali na Fatima: Wafafanuzi wa Nahaj al-Balagha wanasema kuhusiana na ibara hii: ((أَمَّا حُزْنِی فَسَرْمَدٌ وَ أَمَّا لَیلِی فَمُسَهَّدٌ ; Ama ghamu na huzuni yangu ni ya daima na usiku wangu ni wa mkesha)) kwamba, ni ishara ya kwamba, ghamu na huzuni kubwa ya Imamu Ali ya kutengana na Fatima (a.s). [8]
  • Kuwa karibu kaburi la Fatima na la Mtume (s.a.w.w): Wafafanuzi wa Nahaj al-Balagha wanaitumia ibara ya ((النَّازِلَةِ فِي جِوَارِكَ)) yaani anayeshuka jirani yako (karibu na wewe) kama hoja ya kuonyesha kuwa kaburi la Bibi Fatima (a.s) liko jirani na kaburi la Mtume (s.a.w.w). [9] Ayatullah Makarim Shirazi anasema kuwa, ibara hii inaipa nguvu dhana na nadharia ya watu wanaosema kuwa, Fatima amezikwa katika nyumba yake. [10]
  • Kudhulumiwa Fatima: Ibn Maytham Bahrani (aliaga dunia 679 au 699 Hijiria) anasema kuwa: Ibara ya: ((فَأَحْفِهَا السُّؤَالَ)) yaani muulize bila kificho inaashiria kuwa, Fatima alidhulumiwa na Ali (a.s) anashtakia. [11] Ayatullah Makarim Shirazi anasema kuwa, ibara hii iko jumla na inaashiria matukio kama kushambuliwa nyumba ya Fatima, kuharibika mimba ya Muhsin na kumchukua Imamu Ali na kupelekwa msikitini ili akatoe bai ana kiapo cha utiifu kwa Abu Bakr. [12]

Andiko na tarjumi

وَ مِنْ كَلَامٍ لَهُ رُوِيَ عَنْهُ أَنَّهُ قَالَهُ عِنْدَ دَفْنِ سَيِّدَةِ النِّسَاءِ فَاطِمَةَ كَالْمُنَاجِي بِهِ رَسُولَ اللَّهِ عِنْدَ قَبْرِهِ:



Na katika maneno yake amenukuliwa kwamba, aliyasema wakati wa kumzika kiongozi wa wanawake Bibi Fatima Zahra kana kwamba, alikuwa akizungumza na Mtume maneno ya kuliwazana.

السَّلَامُ عَلَيْكَ يَا رَسُولَ اللَّهِ عَنِّي وَ عَنِ ابْنَتِكَ النَّازِلَةِ فِي جِوَارِكَ وَ السَّرِيعَةِ اللَّحَاقِ بِكَ. قَلَّ يَا رَسُولَ اللَّهِ عَنْ صَفِيَّتِكَ صَبْرِي وَ رَقَ عَنْهَا تَجَلُّدِي، إِلَّا أَنَّ فِي التَّأَسِّي لِي بِعَظِيمِ فُرْقَتِكَ وَ فَادِحِ مُصِيبَتِكَ مَوْضِعَ تَعَزٍّ، فَلَقَدْ وَسَّدْتُكَ فِي مَلْحُودَةِ قَبْرِكَ وَ فَاضَتْ بَيْنَ نَحْرِي وَ صَدْرِي نَفْسُكَ، فَإِنَّا لِلَّهِ وَ إِنَّا إِلَيْهِ راجِعُونَ. فَلَقَدِ اسْتُرْجِعَتِ الْوَدِيعَةُ وَ أُخِذَتِ الرَّهِينَةُ، أَمَّا حُزْنِي فَسَرْمَدٌ وَ أَمَّا لَيْلِي فَمُسَهَّدٌ، إِلَى أَنْ يَخْتَارَ اللَّهُ لِي دَارَكَ الَّتِي أَنْتَ بِهَا مُقِيمٌ. وَ سَتُنَبِّئُكَ ابْنَتُكَ بِتَضَافُرِ أُمَّتِكَ عَلَى هَضْمِهَا، فَأَحْفِهَا السُّؤَالَ وَ اسْتَخْبِرْهَا الْحَالَ، هَذَا وَ لَمْ يَطُلِ الْعَهْدُ وَ لَمْ يَخْلُ مِنْكَ الذِّكْرُ. وَالسَّلَامُ عَلَيْكُمَا سَلَامَ مُوَدِّعٍ، لَا قَالٍ وَ لَا سَئِمٍ، فَإِنْ أَنْصَرِفْ فَلَا عَنْ مَلَالَةٍ، وَ إِنْ أُقِمْ فَلَا عَنْ سُوءِ ظَنٍّ بِمَا وَعَدَ اللَّهُ الصَّابِرِينَ.



Amani iwe juu yako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kutoka kwangu na kwa binti yako ateremkaye karibu yako, na wa haraka mno kukutana na wewe. Subira yangu ni haba kumhusu mteule wako ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na uwezo wangu wa subira umedhoofu, isipokuwa kwa kujifunza ukubwa wa kutengana na wewe na uzito wa msiba wako, na ni mahali pa kuvuta subira. Kwa hakika nimekuweka kwenye mwandani wa kaburi lako na ilitiririka kati ya shingo yangu na kifua changu nafsi yako. Kwa hakika sisi tunatoka kwa Mwenyezi Mungu na kwake tutarejea. Sasa amana imerejeshwa, na kilichotolewa kimechukuliwa na rehani imechukuliwa. Lakini huzuni yangu ni ya milele, na usiku wangu ni wa mkesha mpaka Mwenyezi Mungu atakapoichagulia nyumba yako ambayo wewe unakaa humo. Binti yako atakupa habari juu ya kuungana kwa umma wako katika kumdhulumu, mdadisi na mtake akupe habari, hii ikizingatiwa kuwa haukuwa muda mrefu na wala hukuachana na kumbukumbu yako. Na amani iwe juu yenu, ni maamkizi ya muagaji siyo ya aliyekasirika wala aliyechoka. Ni kuondoka sio kutokana na kuchoka, na endapo nitabakia siyo kwa sababu ya dhana mbaya kwa yale aliyoahidi Mwenyezi Mungu kwa wenye kusubiri. [26]