Nenda kwa yaliyomo

Sayyid Mohammad Ali Al-Hashim

Kutoka wikishia
Sayyid Muhammad Ali Aal-Hashim

Sayyid Muhammad Ali Aal-Hashim (aliyezaliwa mwaka 1341 na kufariki 1403 Shamsia) alikuwa ni Imamu na khatibu wa Sala ya Ijumaa katika mkoa wa Tabriz na mwakilishi wa Walii Faqih (Mtawala Mkuu wa Kidini) katika jimbo la Azerbaijan ya Mashariki. Pia Sayyid Muhammad Ali Aal-Hashim alikuwa ni mwakilishi wa watu wa Azerbaijan ya Mashariki katika Baraza la Wanazuoni Watalaamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu. Pia alikuwa na majukumu ya katika kitengo cha kiitikadi katika jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mnamo tarehe 30 ya mwezi wa Urdibeheshti, mwaka 1403 Shamsia, sawa na tarehe 20 May 2024, yeye pamoja na Sayyid Ibrahim Raisi, ambaye ni rais wa Iran, wote kwa pamoja walipatwa na umauti katika ajali ya helikopta wakitokea mkoa wa Azerbaijan ya Mashariki.

Maisha Yake

Sayyid Muhammad Ali Al-Hashim, mwana wa Sayyid Muhammad Taqi Al-Hashim, alikuwa ni mmoja wa viongozi mashuhuri wa kidini wa mjini Tabriz. Sayyid Muhammad alisoma elimu ya msingi hadi sekondari huko huko Tabriz. Al-Hashim alianza masomo ya dini katika chuo kikuu cha elimu ya kidini cha Tabriz kabla ya kuelekea mjini Qom kwa masomo ya ngazi za juu zaidi. Yeye alipiga magoti kwa muda wa miaka 14 akishiriki masomo ya ngazi za juu ya Sayyid Ali Khamenei.[1]

Nyadhifa Rasmi na Majukumu ya Kisiasa

Ayatullah Khamenei mnamo 10 Khordad 1396 Shamsia sawa na 31 May 2018 alimteua Al-Hashim kama mwakilishi wa Wilayatu Al-Faqih (Utawala Mkuu wa Kidini) huko Azerbaijan na pia kuwa ni Imamu mkuu wa Ijumaa wa Tabriz.[2] Wakati wa uongozi wake kama Imamu wa Ijumaa wa Tabriz, kuliondolewa vizuizi maalumu vya vyuma vilivyokuwa vikiwekwa msikitini wakati wa sala kwa ajili ya kuwatenganisha safu za viongozi na watu wa kawaida ibadani humo, jambo ambalo lilitekelezwa kufuatia ombi lake la kutaka kuondolewa kwa vizuizi hivyo.[3]

Kuanzia tarehe 28 mwezi wa Tiir 1388 Shamsia sawa na 19 July 2009[4] hadi tarehe 11 Tiir 1396 Shamsia sawa na 2 July 2017,[5] Al-Hashim alikuwa na jukumu la uwakilishi wa Wilayatu Al-Faqih (Utawala Mkuu wa Kidini) na uenyekiti wa Shirika la Imani na Itikadi za Kisiasa ndani ya jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.[6] Katika kipindi hicho, yeye alifanikiwa kwa mara tatu mfululizo kushika nafasi ya kwanza kati ya mashirika yanayo jishughulisha na masuala ya itikadi za kisiasa za vikosi vya kijeshi.[7]

Al-Hashim alishika nafasi ya ubunge ndani ya Bunge la Sita la Walinzi Wakuu wa Sheria wa Majlis Khubregan akiwa ni mwakilishi wa watu wa Azerbaijan ya Mashariki. Kwa kupata idadi ya kura 834,108, yeye alikuwa na idadi kubwa zaidi ya kura katika mihula mbalimbali ya uchaguzi wa Walinzi Wakuu wa Sheria wa Majlis Khubregan katika jimbo la Azerbaijan ya Mashariki.[8] Baadhi ya nyadhifa zake rasmi alizowahi kushika ni:[9]

  • Mkuu wa Kitengo cha Sala za Ijumaa mjini Tabriz
  • Mkuu wa Imani na itikadi za Kisiasa wa Kituo cha Mafunzo ya Jeshi la Nchi Kavu
  • Mkuu wa Imani na Itikadi za Kisiasa wa Kikosi cha Jeshi la 21 la Hamza la Azerbaijan
  • Mkuu wa Idara ya Imani na Itikadi ya Mkoa wa Azerbaijan
  • Naibu wa Uhamasishaji na Uhusiano wa Umma wa Shirika la Imani na Itikadi za Kisiasa katika Mkoa wa Azerbaijan
  • Naibu wa Idara ya Imani na Itikadi za ya Jeshi la Majini
  • Naibu wa Idara ya Imani na Itikadi za ya Kisiasa ya Jeshi la Nchi Kavu
  • Naibu wa Ushirikiano wa Shirika la Imani ya Kisiasa ya Jeshi
  • Naibu wa Shirika la Imani na Itikadi za Kisiasa la Jeshi kwa idhini ya Amri Mkuu wa Majeshi
  • Mjumbe wa Baraza la Azerbaijan la Kutathmini Maslahi ya Serikali
  • Mkuu wa Idara ya Imani na Itikadi za Kisiasa ya Jeshi la Nchi Kavu.

Rejea

  1. «Zindeginame», Site Hadharat Ayatullah Sayyid Muhammad Ali Al-Hashim.
  2. «Intikhab Namayande Waliyu al-Faqih Dar Ustan Azerbaijan Sharqi wa Imam Jum-e Tabriz», Khamenei.ir.
  3. «Imam Jum-e Tabriz Hamchinan Azarbaijan-ha Ra Ghafligir Mikonad»، Mashriqnews.
  4. «Intikhab Hujatul-Islam Sayyid Muhammad Ali Al-Hashi Be Riyasat Sazman Aqidati Siyasi Artesh» Khamenei.ir.
  5. «Intikhab Hujatul-Islam Muhammad Hassani Be Riyasat Sazman Aqidati Siyasi Artesh» Khamenei.ir.
  6. «Intikhab Hujatul-Islam Sayyid Muhammad Ali Al-Hashi Be Riyasat Sazman Aqidati Siyasi Artesh» Khamenei.ir.
  7. «Zindeginame», Site Hadharat Ayatullah Sayyid Muhammad Ali Al-Hashim.
  8. «"Al-Hashim" Rukurdi Khabargan Ra Shekast, Khabarionline».
  9. «Zindeginame», Site Hadharat Ayatullah Sayyid Muhammad Ali Al-Hashim.

Vyanzo