Nenda kwa yaliyomo

Said bin Abdullahi Hanafi

Kutoka wikishia

Said bin Abdullahi Hanafi (Kiarabu: سعد بن عبد الله الحنفي), ambaye aliyeuawa shahidi manamo mwaka 61 Hijria, ni mmoja wa mashahidi wa Karbala. Alijulikana kwa uaminifu wake mkubwa na kujitolea kwake muhanga kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s). Said ni mfuasi wa Ahlul-Bait (a.s) kutoka mji wa Kufa. Said ndiye aliye chukua jukumu muhimu la kuwasilisha barua za watu wa Kufa kwa Imamu Hussein (a.s), akionyesha imani yake thabiti juu ya nafasi ya uongozi wa Imamu (a.s). Pia, yeye ndiye beba jukumu la kuuwasilisha ujumbe wa Muslim bin Aqil kwa Imamu Hussein (a.s), nayo ni ishara ya kujitolea kwake kwa ajili ya harakati za kutetea Haki. Said bin Abdullahi alijiunga na msafara wa Imamu Hussein (a.s) baada ya kuikabidhi barua ya Muslim bin ‘Aqil kwa Imamu (a.s). Usiku wa Ashura, Said alitoa hotuba yenye msisimko mkubwa, akisisitiza mshikamano na uaminifu wake kwa Imamu Hussein (a.s), ambapo aliahidi ya kuwa; hata kama angekufa na kufufuliwa mara sabini, bado asinge thubutu kumsaliti Imamu (a.s). Ahadi hii inaonesha uzito wa imani yake na dhamira yake ya kusimama kwenye mstari wa haki hadi mwisho.

Uwasilishaji wa Barua Katika Tukio la Karbala

Said bin Abdullah Hanafi bin Lajim; alikuwa ni mmoja wa wajumbe muhimu na mashujaa wa tukio la Karbala. Alitoka katika kabila la Bani Hanifa bin Lajim, ambalo ni tawi la Bani Bakar bin Wa'il, sehemu ya matawi ya kabila kubwa la Adnan. [1] Said alikuwa akiishi katika mji Kufa, na alikuwa ni maarufu kwa ushujaa wake na ucha Mungu wake, [2] sifa ambazo zimeelezwa na mwanahistoria Muhammad Samawi katika kitabu chake Absar al-Ain. Katika vitabu vya ziara, ambavyo ni sehemu muhimu ya fasihi ya Kiislamu ya madhehebu ya Shia, Said bin Abdullah ametajwa kwa heshima kubwa. Katika Ziaraat Al-Shuhadaa (Ziara za Mashujaa), ametajwa kwa jina la Sa’ad, [3] na katika Ziarat Al-Rajabiyya ya Imamu Hussein (a.s), ametajwa kwa jina la Said, [4] ambapo hupewa salamu maalum kwa heshima ya mchango wake wa kipekee katika tukio hilo la kihistoria la Karbala. Uaminifu na mshikamano wake kwa Imamu Hussein (a.s) na mchango wake katika harakati za Karbala vilimpatia nafasi ya kipekee katika historia ya Kiislamu.

Said bin Abdullah Hanafi na Hani bin Hani Sabii'i walikuwa ni wajumbe muhimu waliochaguliwa kuwasilisha barua ya tatu kutoka kwa watu wa Kufa kwenda kwa Imamu Hussein (a.s). Barua hizi zilibeba maombi na matumaini ya watu wa Kufa, zikionesha nia yao ya kumkaribisha Imamu Hussein (a.s) na kumpa msaada na ulinzi. [5] Waandishi wa barua hizo walikuwa Shabath bin Rib'i, Hajjaj bin Abjar, Yazid bin Harith, Yazid bin Ruwaim, Azra bin Qais, Amru bin Hajjaj na Muhammad bin Umair. [6] Kulingana na baadhi ya Riwaya, Said bin Abdullah ndiye aliyepewa jukumu la kupeleka barua hizo, hii ni kwa kutokana na heshima yake kubwa na nafasi yake katika jamii ya Waislamu wa mji wa Kufa. Heshima hii ilitarajiwa kumshawishi Imamu Hussein (a.s) na kumfanya azingatie kwa makini zaidi barua za watu wa Kufa na kumpa motisha wa kuelekea huko. Watafiti waamini ya kwamba; watu Kufa waliamini kuwa; ushawishi wa mjumbe kama Said ungemshawishi Imamu Hussein (a.s) katika kuchukua hatua hiyo muhimu. [7]

Imamu Hussein (a.s) alijibu barua za maombi ya watu wa Kufa kupitia Said bin Abdullah, akisema kwamba; alimtuma Muslim bin Aqil kama ni mjumbe wake maalumu kwa ajili ya watu mji wa Kufa. Kulingana na chanzo cha kihistoria cha Tarikh Tabari, kitabu kilichoandikwa mnamo mwaka wa 303 Hijiria, ni kwmaaba; pale Muslim bin Aqil alipofika mji wa Kufa na kuzungumza na watu wa mji huo, Abas bin Abi Shabib Shakiri, Habib bin Mudhahir na Said bin Abdullah walithibitisha ukweli wa nia za msaada wao kwa ajili ya Imamu Hussein (a.s). [8] Katika mkutano wao, Muslim bin Aqil alimchagua Said bin Abdullah kumwalika Imamu Hussein (a.s) kuingia mji wa Kufa. Said alifunga safari na kuelekea Makka, akamkabidhi Imamu Hussein barua kutoka kwa Muslim bin Aqil, kisha akaondoka mjini Makka sambamba na msafara wa Imamu Hussein (a.s) wakielekea Kufa. Uteuzi wa Said kwa ajili ya majukumu kama haya, ni ushahidi wa heshima yake na uaminifu wake katika harakati za kumuunga mkono Imam Hussein (a.s) katika safari yake kuelekea Kufa. [9]

Bayana za Said bin Abdullah Juu ya Uaminifu Wake kwa Imam Hussein (a.s) Usiku wa Ashura

Ulipofika usiku wa Ashura, Said bin Abdullah alijitokeza kwa imani thabiti na ujasiri wa kipekee katika kumsaidia Imamu Hussein (a.s). Katika mazungumzo na Imamu Hussein, Said alieleza kuwa hata kama watamchoma moto mara sabini kisha kupeperusha jivu la maiti yake, bado katu hataacha kumsaidia na kumhami Imamu Hussein (a.s). Kauli hii ilikuwa jibu la maneno ya Imam Hussein (a.s), ambaye aliwaambia wafuasi wake kwamba; kila mmoja wao achukue mkono wa rafiki yake na kutumia nafsi ya giza la usiku ili kuondoka na kukimbia matokeo ya Karbala. Said bin Abdullah alithibitisha azimio lake na kujitolea kwa hali ya juu, akionyesha uaminifu na msimamo wake wa dhati katika kutimiza ahadi yake kwa Imamu Hussein (a.s). Msimamo huu shujaa na thabiti wa Said, ni wa kupigiwa mfano na ni kiwango cha uaminifu na kujitolea kilichooneshwa na mashujaa wa Karbala katika kipindi hicho kigumu. [10]

Kuwalinda Waumini Wakati wa Sala Siku ya Ashura

Kwa mujibu wa Riwaya kutoka kwa waandishi wa matukio ya kihistoria ya Karbala, wakati Imamu Hussein (a.s) alisimama kwa ajili ya sala ya hofu mchana wa siku ya Ashura, Said bin Abdullahi na Zuhair bin Qain walijitolea kwa ujasiri mkubwa kumlinda Imamu dhidi ya mishale kutoka upande wa maadui zao. Walijitahidi kumlinda kwa kutumia nyuso zao, vifua, mbavu, na mikono yao dhidi ya mashambulizi hayo. [11] Imeripotiwa katika vyanzo mbali mbali ya kwamba; mwili wa Said bin Abdullahi baada ya kufariki kwake, ulikutwa ukiwa na mishale 13 iliyo ambatana na majeraha ya upanga. [12] Ujasiri wake katika kumlinda Imamu Hussein (a.s) umempa maarufu wa jina la shahidi wa sala. [13] Nukuu zinasema; pale Said bin Abdullahi alipoanguka chini akiianga dunia, alionekana akisoma dua ifuatayo kwa unyenyekevu kabisa akisema:

Ee Mola! Lilaani jeshi la watu wa mji Kufa, kama ulivyowalaani watu wa ‘Aad na Thamud. Ee Mola! Fikisha salamu zangu kwa Mtume wako na uwasilishe maumivu niliyovumilia kutokana na majeraha yangu kwake; kwani msaada wangu kwa Mtume ni wenye lengo la kupata malipo yako. [14]

Baada ya kusema dua hiyo, alimwelekea Imamu Hussein (a.s) na kumuuliza: "Ee mwana wa Mtume wa Mwenye Ezi Mungu, je, nimetimiza ahadi yangu?" Imam Hussein (a.s) akamjibu kwa kusema: "Ndio; umetangulia kungia Peponi kabla yangu". [15] Hawa ndio mashujaa walionyesha ujasiri wa kipekee na kujitolea kwa hali ya juu, wakijitahidi kwa kila njia kumlinda Imamu Hussein (a.s), walio akisi wa dhamira za nyoyo zao na misimamo yao ya kidini hata katika hali ngumu kama hiyo. Pia ifuatayo ni maana ya shairi la hamasa linalo nasibishwa naye;

Ewe Hussein, sogea uwe mbele kwani leo ndiyo siku ya kukutana na babu yako mteule wa Mungu na pia baba yako menye mkono mkunjufu na mkarimu. [16]

Rejea

Vyanzo