Nenda kwa yaliyomo

Sa'd bin Hudhayfa bin Yamani

Kutoka wikishia

Sa'd bin Hudhayfa bin Yamani (Kiarabu:[[Arabic| سَعْد بن حُذَيفة بن اليمان}}) (kuuawa shahidi: 37 Hijria) ni mmoja wa masahaba wa Imamu Ali (a.s) na mmoja wa mashahidi wa Vita vya Siffin. [1] Hudhayfa ambaye ni baba wa Sa'd ni miongoni mwa masahaba wa Mtume (s.a.w.w) na mmoja wa masahaba wa Imamu Ali (a.s). Sa'ad na kaka yake Saf'wan walikuweko katika vita vya Siffin na walipigana upande wa Imamu Ali (a.s) na walifanya hivyo kwa mujibu wa wasia wa baba yao na kuuawa shahidi katika vita hivyo. [2] Katika baadhi ya vyanzo, jina lake limetajwa kuwa ni Said. [3] Inaelezwa kuwa, amenukuu hadithi kutoka kwa Sa'd bin Masoud. [4]

Imekuja katika Tarikh Tabari kwamba: Wakati wa kujiri harakati na mapinduzi ya Tawwabin, Sa'd bin Hudhayfa alikuwa hai na katika barua ya Suleiman bin Surad Khuzai kwake, alimtaka msaada na himaya na yeye akatangaza utayari wake. [5] Kadhalika Tabari ameandika kwamba, Mukhtar Thaqafi alimteua Sa'd bin Hudhaifa kuwa mtawala mji wa Hulwan. [6] Kwa msiingi huo,, Sayyid Mohsin Amini na baadhi ya watafiti wengine wameibua uwezekano kwamba Hudhaifa alikuwa na mtoto mwingine wa kiume aitwaye Sa'd, ambaye aliishi hadi wakati wa harakati ya Tawwabin na harakati ya Mukhtar.[7]

Rejea

Vyanzo