Nyumba ya Imamu Ali (a.s) mjini Kufa

Kutoka wikishia
Nyumba ya Imamu Ali (a.s) mjini Kufa

Nyumba ya Imam Ali (a.s) huko Kufa (Kiarabu: بيت الإمام علي (ع) في الكوفة) ni mahali panapohusishwa na Imam Ali (a.s), ambaye anajulikana kuwa aliishi hapo wakati wa ukhalifa wake. Nyumba hii iko upande wa kusini-magharibi wa Msikiti wa Kufa na imeunganishwa na kasri ya Dar al-Imarah ya Kufa. Kuhusu muundo wa ndani wa nyumba, vyumba na sehemu zinazonasibishwa kwake na watoto wake, na mahali ambapo Imamu alifanyiwa ghusli, kuna nukuu zilipokewa kuhusiana na hayo ambazo zimekosolewa na watafiti wa historia na hadithi.

Utambulisho

Nyumba ya Imam Ali (a.s) iko katika kona ya kusini-magharibi ya msikiti wa Kufa na imeunganishwa na kasri ya Dar al-Imarah [1] Nyumba hii imefanyiwa ukarabati mara kadhaa, na ukarabati wa mwisho ulifanyika baada ya kuanguka utawala wa Baath nchini Iraq. [2]

Ndani ya nyumba hiyo, kuna vyumba na sehemu zinazonasibishwa na Imamu Ali (a.s) na watoto wake; [3] upande wa kulia wa mlango, chumba cha Imamu Hassan (a.s) na Imamu Hussein (a.s) na upande wa kushoto, chumba alichofanyiwa ghusli Imamu Ali (a.s) na mihrabu. [4] Pia kuna vyumba vingine vinavyonasibishwa na Zainab (a.s), Ummu Kulthum na Umm Al-Banin.[5]

Mwishoni mwa nyumba kuna kisima cha maji ambacho inaelezwa kuwa kilichimbwa na Imamu Ali (a.s) na wafanyaziara hunywa maji ya kisima hicho kwa lengo la kutabaruku. [6]

Shaka ya kuwa sahihi kunasibishwa nyumba hiyo na Imamu Ali (a.s)

Baadhi ya watafiti wana shaka juu ya usahihi wa kunasibishwa kwa nyumba hii na Imamu Ali (a.s): [7] Miongoni mwa shaka hizo ni kuwa, ingawa kitovu cha serikali ya Imamu Ali (a.s.) kilikuwa Kufa mwishoni mwa maisha yake, [8] lakini kuna tofauti za rai na mitazamo kuhusu mahali alipoishi Imamu na nyumba yake, [9] ingawa eneo la sasa linajulikana kama sehemu ya nyumba ya Imamu Ali. [10] Kwa upande mwingine, kujengwa upya kwa nyumba hiyo mara kadhaa, ikiwa ni pamoja na katika mwisho wa utawala wa Saddam na baada ya kuanguka utawala wake ni mambo ambayo yameongeza shaka kama kweli hiyo ilikuwa nyumba ya Imamu Ali (a.s). [11]

Pia, kwa kuzingatia itikadi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia juu ya kwamba, Hassan na Hussein (a.s) ni Maimamu na wana elimu kutoka kwa Mwenyezi Mungu na hawakuwa na haja ya kujifunza, hivyo kutengwa sehemu maalumu kwa anuani ya maktaba ya Hassan na Hussein ni jambo lisilo la kimantiki, [12] au hawakubaliani na kutolewa maana ya maktaba kuwa ni sehemu ya kufundishia kwa sababu nyumba ilikuwa ndogo na isingeweza kutumika kama sehemu ya kufundishia au ofisi. [14] Imebainika pia kwamba, Imam Hassan (a.s.) na Imamu Husein (a.s.) wakati wa utawala wa baba yao huko Kufa, wao walikuwa wakijitegemea kimaisha na kuwa na maktaba kama hiyo katika nyumba ya baba yao hakuwezi kuhalalishika. [15]