Ndoa ya Imamu Mahdi (a.f)

Kutoka wikishia

Kuoa Imamu Mahdi (a.t.f.s) (Kiarabu: زواج الإمام المهدي (عج)) Ni katika maudhui ambayo ina hitilafu kuhusiana na Hadhrat Imamu Mahdi (a.t.f.s). Waungaji mkono wa nadharia na mtazamo kwamba; Imamu Mahdi ameoa ili kuthibitisha nadharia yao hii wanategemea kama hoja za hadithi ambazo zinaashiria watoto wake. Kadhalika kwa mtazamo wao ni kwamba; ndoa ni sunna iliyokokotezwa na kutiliwa mkazo mno na Bwana Mtume (s.a.w.w) hivyo kwa msingi huo, Imamu Mahdi (a.t.f.s) bila shaka ameifanyia kazi Sunna hii muhimu. Wapinzani kwa upande wao wanasema kuwa, kuoa Imamu Mahdi (a.t.f.s) kunakinzana na falsafa ya ghaiba (kughibu) na kutoonekana katika upeo wa macho ya watu. Wengine nao wanaamini kwamba, hata kama kuna uwezekana kwamba, Imamu Mahdi huenda akawa ameoa, lakini haiwezekani kutoa kauli ya moja kwa moja kuhusiana na jambo hili.

Sayyied Muhammad Sadr, Sheikh Mirza Hussein Nuri Tabarsi (1254-1320 Hijiria) na Ali Akbar Nahavandi (aliaga dunia 1369 Hijiria) ni miongoni mwa wanaounga mkono nadharia ya kwamba, Imamu Mahdi (a.t.f.s) ameoa. Mjadala na mada hii kwa mara ya kwanza ilizungumziwa na kujadiliwa kwa sura ya uchambuzi na kitathmini katika kitabu cha Tarikh Ghaibat al-Kubra kilichoandikwa na Sayyied Muhammad sadr (aliyeaga dunia 1377 Hijiria).

Historia ya mada

Wanazuoni wa Kishia wana mitazamo na nadharia tofauti kuhusiana na suala la kwamba, je, Imamu Mahdi (a.t.f.s) katika kipindi hiki cha kuwa kwake ghaiba ameoa au la. Imekuja katika kitabu cha Ensaiklopidia ya Imamu Mahdi (a.t.f.s) kwamba, maudhui na mjadala huu ulizungumziwa zaidi katika katika karne ya 14 Hijiria,[1] na kitabu cha kwanza kilichozungumzia kiuchambuzi maudhui ya kuoa Imamu Mahdi ni Tarikh Ghaibat al-Kubra cha Sayyied Muhammad Sadr (aliyeaga dunia 1377 Hijiria).[2] Hata hivyo kabla yake maudhui hii ilizungumziwa pia katika vitabu vya Najm al-Thaqib[3] kilichoandikwa na Sheikh Nuri (aliyeaga dunia 1320 Hijiria) na al-Abqariy al-Hisan[4] cha Ali Akbar Nahavandi (aliyefariki dunia 1369 Hijiria) na maudhui hii inapatikana pia katika kitabu cha Bihar al-Anwar katika mlango wa “Khulafaa al-Mahdi Wauladuh wama yakun baadahu”[5]

Mitazamo

Kuna mitazamo mitatu kuhusiana na suala la kuoa Imamu Mahdi (a.t.f.s)

Waungaji mkono

Sayyied Muhammad Sadr,[6] Sheikh Mirza Nuri,[7] na Ali Nahavandi[8] wamekubaliana na nadharia kwamba, Imamu Mahdi (a.t.f.s) ameoa. Kadhalika katika kitabu cha Ensaiklopidia ya Imam Mahdi (a.t.f.s) imani hii imenasibishwa na Allama Majlisi.[9] Hoja za kundi hili ni:

  • Ndoa ni sunna iliyokokotezwa na kutiliwa mkazo mno na Bwana Mtume (s.a.w.w) hivyo kwa msingi huo, Imamu Mahdi (a.t.f.s) ni mtu mstahiki zaidi wa kuifanyia kazi Sunna hii muhimu.. Kwa msingi huo yeye ameoa na kutekeleza Sunna hii akiwa katika ghaiba.[10]
  • Kuna hadithi na ziyara zinazoonyesha kuwa, Imamu Mahdi (a.t.f.s) ana watoto. Katika kitabu cha Ensaiklopidia ya Imamu Mahdi (a.t.f.s) kumekusanywa humo hadithi 14 kuhusiana na maudhui hii.[11] Miongoni mwazo ni hadithi mashuhuri kwa jina la Hadithi al-Wasiyya ambayo kwa mujibu wake baada ya Imamu wa zama Mahdi (a.t.f.s) watakuja Mahdi kumi na wawili kutoka katika kizazi chake ambao watatawala.[12] Hata hivyo kwa mujibu wa Allama Majlisi, hadithi hii inapingana na lile ambalo ni mashuhuri. Kadhalika kuna uwezekano makusudio ya Mahdi kumi na wawili ni Mtume (s.a.w.w) na Maimamu 12 wa Kishia ukimuondoa Imamu Mahdi (a.t.f.s).[13] Miongoni mwa hadithi zingine zinazotumiwa na kundi hili kama hoja ni hadithi iliyopokewa kutoka kwa Imam Swadiq (a.s) ambapo ndani yake imeashiriwa makazi ya Imamu Mahdi, mke na familia yake katika msikiti wa Sahla.[14] Kwa mtazamo wa wale wanaopinga suala la kuoa Imamu Mahdi wanasema kuwa, tujaalie kwamba, tumezikubali hadithi hizi, mke na watoto wa Imamu Mahdi wanahusiana na kipindi cha baada ya kudhihiri.[15]
  • Kuna ripoti inayoonyesha juu ya kuishi familia ya Imamu Mahdi katika Kisiwa cha Khadhra.[16] Hata hivyo baadhi ya Maulamaa wa Kishia wanasema kuwa, kisiwa cha Khadhra ni kitu cha kutungwa na ni ngano.[17]

Wapinzani

Hoja za wapinzani wa kadhia ya kuoa Imamu Mahdi (a.t.f.s) ni:

  • Kukinzana na falsafa ya ghaiba: Falsafa ya ghaiba (kughibu) ni kutoonekana katika upeo wa macho ya watu na kutotambuliwa na watu na kwamba, kuoa ni jambo linalopingana na falsafa hii, kwani kuoa itakuwa sababu ya kutambuliwa.[18]
  • Kuna hadithi ambazo mafuhumu na maana yake zinaonyesha kuwa, Imamu Mahdi hana watoto.[19]
  • Kutoashiria manaibu na mabalozi wa Imamu mahdi (a.t.f.s): Kama Imamu Mahdi angekuwa ameoa, basi mabalozi na mawakala wake katika kipindi cha Ghaiba Ndogo wangeashiria kuoa kwake pamoja na watoto wake.[20]

Knyamazia kimya

Ilivyokuja katika kitabu cha Ensaiklopidia ya Imamu Mahdi (a.t.f.s) ni kwamba, hoja za waungaji mkono na wapinzani wa kuoa Imamu Mahdi zinapingana na hivyo haiwezekani kuzitumia kwa ajili ya hoja ya kuthibitisha na kuainisha na kutoa uamuzi kuhusiana na jambo la kihistoria.[21] Sayyied Ja’far Murtadha al-Amili (aliaga dunia 1441 Hijiria), mtafiti wa historia ya Uislamu anaamini kwamba, ni jambo la kutia shaka kama Imamu Mahdi ana mtoto na hivyo haiwezekani kutoa mtazamo wa moja kwa moja kuhusiana na jambo hili.[22] Kadhalika kwa mujibu wa Ayatullah Safi Golpeygani (aliyeaga dunia 1400 Hijiria Shamsia), mmoja wa Marajii Taqlidi ni kwamba, licha ya kuwa kuna uwezekano Imamu Mahdi akawa ameoa, lakini hakuna hadithi yenye itibari ambayo itapelekea kupatikan uhakika na yakini kuhusiana na jambo hili.[23]

Monografia

Kitabu cha Tahlil Mas’aleh Izdivaj Imam Mahd (a.t.f.s) kilichoandikwa na Muhammad Reza Fuadiyan, kinachungunza na kufanya tathmini kuhusiana na hoja na kauli mbalimbali kuhusiana na kuoa Imamu Mahdi na vilevile kuwa kwake na mtoto.[24]

Rejea

  1. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, uk. 56.
  2. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, uk. 45.
  3. Nūrī, Najm al-thāqib, uk. 402-407.
  4. Nahāwandī, al-ʿAbqarīyy al-ḥisān, juz. 6, uk. 537.
  5. Majlisī, Biḥār al-anwār ,juz. 53, uk. 145.
  6. Ṣadr, Tārīkh al-ghayba ,juz. 2, uk. 64.
  7. Nūrī, Najm al-thāqib, uk. 403.
  8. Nahāwandī, al-ʿAbqarīyy al-ḥisān ,juz. 6, uk. 537.
  9. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, uk. 46.
  10. Nūrī, Najm al-thāqib, uk. 403.
  11. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, uk. 46-51.
  12. Ṭūsī, al-Ghayba , uk. 150.
  13. Majlisī, Biḥār al-anwār ,juz. 53, uk. 148-149.
  14. Ibn al-Mashhadī, al-Mazār al-kabīr , uk. 134-135.
  15. Ṣāfī Gulpāyigānī, Pāsukh-i Dah Pursish , uk. 54.
  16. Nūrī, Najm al-thāqib, uk. 405.
  17. Kāshif al-ghitāʾ, al-Haqq al-mubīn , uk. 87.
  18. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, juz. 3, uk. 52-53.
  19. Ṭūsī, al-Ghayba , uk. 224.
  20. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, juz. 3, uk. 53.
  21. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, juz. 3, uk. 55-56.
  22. Muḥammadī Reyshahrī, Dānishnāma-yi Imām Mahdī, uk. 55.
  23. Ṣāfī Gulpāyigānī, Pāsukh-i dah pursish, uk. 54.
  24. Reviewed by Mohammad Reza Fu'adiyan; Is Imam Zaman (a) married and has children?(Persian)

Vyanzo

  • ʿĀmilī, al-Sayyid Jaʿfar al-Murtaḍā al-. Dirāsa fī ʿalāmāt al-ẓohūr. Qom: Muntadā Jabal ʿĀmil al-Islāmī Qism al-Ṭibāʿa wa l-Nashr, 1992.
  • Ibn al-Mashhadī, Muḥammad. Al-Mazār al-kabīr. Qom: Daftar-i Intishārāt-i wābasti bi Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1409 AH.
  • Kāshif al-Ghitāʾ, Jaʿfar. Al-Haqq al-mubīn fī taṣwīb al-mujtahidīn wa takhṭaʾat al-ʾkhbārīyyīn. Tehran: Aḥmad Shīrāzī, 1319 AH.
  • Majlisī, Muḥammad Bāqir al-. Biḥār al-anwār. Beirut: Muʾassisat al-Wafāʾ, 1403 AH.
  • Muḥammadī Reyshahrī, Muḥammad. Dānishnāma-yi Imām Mahdī. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1393 Sh.
  • Nahāwandī, ʿAlī Akbar. Al-ʿAbqarīyy al-ḥisān fī aḥwāl mawlānā ṣāḥib al-zamān. Qom: Intishārāt-i Masjid-i Jamkarān, 1386 SH.
  • Nūrī, Mīrzā Ḥusayn al-. Najm al-thāqib fī aḥwāl al-Imām al-ghāʾib. Qom: Intishārāt-i Masjid-i Jamkarān, 1383 SH.
  • Ṣadr, Sayyid Muḥammad. Tārīkh al-ghayba. Beirut: Dār al-Taʿāruf, 1412 AH.
  • Ṣāfī Gulpāyigānī, Luṭf Allāh. Pāsukh-i dah pursish. Qom: Daftar-i Nashr-i āthār-i Āyat Allāh Ṣāfī Gulpāyigānī, 2011.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Ghayba. Edited by ʿIbād Allāh Tihrānī and ʿAlī Aḥmad Nāṣiḥ. Qom: Muʾassisat al-Maʿārif al-Islāmīyya, 1411 AH.
  • به قلم محمدرضا فؤادیان بررسی شد؛ آیا امام زمان (عج) ازدواج کرده و فرزند دارد؟ (Reviewed by Mohammad Reza Fu'adiyan; Is Imam Zaman (a) married and has children?(Persian)). Accessed: 2023/06/03.