Mwaka 255 Hijria

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Mwaka 255 H)

Mwaka 255 Hijiria (Kiarabu: سنة 255 للهجرة) ni miaka 255 tangu kuhajiri Mtume (s.a.w.w) kutoka Makka na kwenda Madina kwa mujibu wa kalenda ya Hijiria. Imam Mahdi (a.t.f.s), Imam wa 12 wa Waislamu wa Kishia alizaliwa katika mwaka huo. Kadhalika mwaka huo unasadifiana na kipindi cha uongozi na Uimamu wa Imam Hassan al-Askary (a.s) (254-260), ambaye ni Imam wa 11 wa Waislamu wa Kishia.

Miongoni mwa matukio muhimu yaliyojiri na kutokea katika mwaka huu ni kuanza harakati na mapinduzi ya Ali bin Zayd na Issa bin Ja’afar (miongoni mwa wajukuu wa Imam Hassan al-Mujtaba (a.s) katika mji wa Kufa, shambulio la Ya’qub Layth al-Saffar dhidi ya mamlaka ya utawala wa Tahiriyan na kudhibiti maeneo ya Fars.

Utambulisho

Mwaka 255 Hijiria ulisadifiana na zama na kipindi cha Uimamu wa Imamu Hassan al-Askary (a.s) ([254-260). [1] Kadhalika katika kipindi hiki utawala ulikuwa mikononi mwa Mu’taz (252-255 Hijiria) na Muhtadi (255-260 Hijiria) miongoni mwa watawala wa Bani Abbas. [2]

Siku ya kwanza ya mwaka huu ilisadifiana na tarehe Mosi Muharram ambayo ni muafaka na 24 Disemba 868 Miladia, na siku ya mwisho ya mwaka huu inasadifiana na 29 Dhul-Hija ambayo ni sawa na tarehe 12 Disemba 869 Miladia.

Matukio

Mazazi

Vifo

  • Ali ibn Mahziar Ahvazi, mmoja wa maswahaba wa Imam Ridha, Jawad na Hadi (a.s) ambaye kifo chake kimetambuliwa kuwa kilitokea mwaka 254 au 255 Hijria. [12]
  • Muhammad ibn Saleh ibn Abdallah mmoja wa wajukuu wa Imamu Hassan Mujtaba (a.s) ambaye kipindi fulani katika zama za utawala na ukhalifa wa Mutawakkil alianzisha harakati na mapinduzi na kutiwa mbaroni na baada ya miaka mitatu akaachiliwa huru. [13]
  • Muhammad bin Karaam, muasisi na mwanzishi wa maktaba (fikra) ya kitheolojia ya Karamiyah. [15]
  • Abu Othman, Amru ibn Bahr ibn Mahbub Kanani, mashuhuri kwa jina la Jahidh, mmoja wa wanafasihi wakubwa wa Kkiarabu na mwanateolojia mahiri wa kundi la Mu’tazila. [16]
  • Ahmad bin Hamdun Nadim (mtambuzi wa lugha) ambaye alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa pamoja na wa karibu na Mutawakkil na Mustain Abbasi. [17]

Vyanzo

  • Abu al-Fida', Isma'il bin 'Ali, Tarikh Abi al-Fida' al-Musamma al-Mukhtashar fi Akhbar al-Basyar, Koreksi: Muhammad Diyub, Beirut: Dar al-Kutub al-'Ilmiyah
  • Abu al-Hassani, Rahim, Aleman-e Shieh, Majalah Syieh Syenasyi juz: 3 & 4, edit musim gugur dan musim dingin
  • Erbili, Ali bin Issa, Kashf al-Ghummah fi Ma'rifah al-Aimmah, Tabriz: Percetakan Bani Hashimi, cet. pertama
  • Husseini Khatun Abadi, Abdul Hussein, Waqayi' al-Sinin wa al-A'wam, Teheran
  • Ibn 'Abari, Gregoris bin Harun, Tarikh Mukhtashar al-Duwal, Beirut: Dar al-Masyriq
  • Ibn Atsir, 'Izz al-Din. Al-Kamil fi al-Tarikh, Beirut: Dar al-Shadir
  • Ibn Hamzah Thusi, Muhammad bin Ali, Al-Tsaqib fi al-Manaqib, Qom: Penerbitan Anshariyan, cet. ketiga
  • Ibn Khalkan, Ahmad bin Muhammad, Wafiyat al-A'yan wa Anba' Abna' al-Zaman, Qom: Al-Syarif al-Radhi
  • Ibn Taghra Bardi, Jamal al-Din Yusuf, Al-Nujum al-Zahidah fi Muluk Mishr wa al-Qahirah, Kairo: Kementrian Kebudayaan dan Bimbingan Masyarakat, Yayasan Umum Mesir
  • Isfahani, Abul Faraj Ali bin Husain. Maqatil al-Thalibin. Koreksi: Sayyid Ahmad Shaqar, Beirut: Dar al-Ma'rifah
  • Mufid, Muhammad bin Muhammad, Al-Irshad fi Ma'frifah Hujajillah 'ala al-'Ibad. Qom: Kongres Sheikh Mufid, cet. pertama
  • Qut'b al-Din Rawandi, Sa'id bin Abdullah, Al-Kharaij wa al-Jaraih, Qom: Yayasan Imam Mahdi afs
  • Spuler, Bertold, Tarikh Iran dar Qurun-e Nukhustin-e Islami, Terjemah: Abdul Jawad Falaturi, Teheran: Kantor Percetakan Ilmiyah dan Budaya
  • Tabari, Tarikh Tabari, Tarikh Umam wa al-Muluk, Beirut
  • Tabrasi, Fadhl bin Hassan, I'lam al-Wara bi A'lam al-Huda, Qom: Muassasah Al al-Bayt li Ihya al-Turats
  • Zirakli, Khairuddin, Al-A'lam, Beirut: Dar al-'Ilm li al-Malayin