Sheikh Mufidu

Kutoka wikishia
Kaburi la Sheikh Mufid katika Haram ya Kadhimein

Muhammad bin Muhammad bin Nu’uman, maarufu kama Sheikh Mufid (alizaliwa mwaka 336 au 338 kufariki 413 Hijiria). Sheikh Mufid alikuwa mwanatheolojia na mwanazuoni wa Kiimamiyya katika karne ya nne na ya tano Hijiria. Yasemekana kuwa; Sheikh Mufid alivumbua njia mpya ya ijitihad baada ya kutunga fani ya elimu ya usul al-fiqh, ambayo ilikuwa njia ya wastani kati ya mtazamo wa mkali wa kiakili uliopita budi na mtazamo iliotegemea Riwaya kavu bila kuzingatia akili. Sheikh Saduqu, Ibn Junayd Iskafi, na Ibn Qulawaihi walikuwa miongoni mwa walimu maarufu wa Sheikh Mufid. Sheikh Tusi, Sayyid Murtadha, Sayyid Razi, na Najashi pia wanahesabiwa kati ya wanafunzi wake maarufu. Vitabu maarufu kama vile; Al-Muqni’ah katika elimu ya fikh, Awail al-Maqalat katika elimu ya kalam (theolojia), na al-Irshad katika uchambuzi juu ya Maimamu wa Kishia, ni miongoni mwa kazi maarufu za Sheikh Mufid.

Asili na maisha

Muhammad bin Muhammad bin Nu’man alizaliwa tarehe 11 Dhul-Qa’idah mwaka wa 336 au 338 Hijiria katika kitongoji cha Ukbari karibu na mji wa Baghdad nchini Iraq. [4] Baba yake alikuwa mwalimu jambo ambalo lilipelekea Sheikh Mufid kujulikana kama ni “Ibn al-Mu’allim” (mwana wa mwalimu). [5] Ukbara na Baghdadi pia ni miongoni mwa majina yake mengine ya umaarufu. [5] Kuhusiana na uhalisia wa yeye kuitwa jina la Mufid, imeelezwa kuwa; katika mjadala uliofanyika baina yake na Ali bin Isa al-Rumani, ambaye ni mwanazuoni wa upande Mu’utazila, Sheikh Mufid alifanikiwa kubatilisha hoja za mpinzani wake. Baada ya hapo, al-Rumani akamwita Muhammad bin Muhammad bin Nu’man kwa jina la “Mufid” (mwenye kufidisha). [6] Katika vyanzo vya kihistoria, inasemekana kuwa Mufid alikuwa na watoto wawili; Abu al-Qasim Ali na binti mmoja ambaye jina lake Halikulikana. Binti huyo ndiye aliye kuwa mke wa Abu Ya’ala Ja’afari. [7] Sheikh Mufid alifariki siku ya Ijumaa, tarehe 2 au 3 Ramadhani mwaka wa 413 Hijiria. [8] Sheikh Tusi ameelezea kuhusisna na msongamano mkubwa wa watu kutoka madhehebu mbali mbali waliohudhuria kwa ajili ya kumsalia na kuomboleza kifo chake, Sheikh Tusi amelisifu tukio hilo kuwa ni tukio lililokuwa na msongamano kupita kiasi. [9] Kwa muda wa miaka kadhaa kaburi lake lilikuwa nyumbani kwake kabla yeye kutolewa na kusafirishwa kwa ajili ya kuzikwa kwenye makaburi ya Maquraish, karibu na kaburi la Imamu Jawad (a.s). [10]

Sifa zake kimaadili

Yasemekana kwamba Sheikh Mufid alikuwa ni; mwingi wa kutoa sadaka, mnyenyekevu, msalihina na mwenye kufunga sana. Pia imeelezwa kuwa yeye alikuwa na kawaida ya kuvaa nguo chakavu, hadi kufikia hatua ya watu kumpa jina la Sheikh wa Mashaikh wa Kisufi (شیخ مشایخ الصوفیه) au kwa kwa lugha nyengine ni (Mwalimu wa Mawalimu wa MaSufi). [11] Abu Ya’la Ja’fari, ambaye ni mkwewe, aliripoti akisema kuwa; Sheikh Mufid alikuwa na kawaida kulilala sehemu ndogo tu wakati wa usiku na alitumia muda wake mwingi katika amali za; kusoma, kusali na kusoma Qur’an, au kufundisha. [12] Katika barua ambayo Imam Mahdi (a.s) alimwandikia Sheikh Mufid, alimtaja baruani humo kwa majina ya “Sayyid” (imara na mwaminifu) na “Waliyyun Rashidun” (kiongozi mwongozaji au aliye ongoka na kuzinduka). [13]

Elimu yake

Mufid alipata elimu ya Qur'an Kareem na elimu ya msingi kutoka kwa baba yake. Kisha alifuatana na baba yake kwenda Baghdad na akajifunza kutoka kwa wanazuoni wa fani tofauti, wakiwemo; mutakallimuna (wanatheolojia), na wanazuoni wa fani ya fiqhi mashuhuri wa madhehebu ya Shia na Sunni. [14]

Sheikh Saduq (aliyefariki mnamo mwak 381 Hijiria), Ibnu Junaid Askafi (aliyefariki mnamo mwaka 381 Hijiria), Ibnu Qulawaih (aliyefariki mwano mwaka 369 Hijiria), Abu Ghalib Zarari (aliyefariki mnamo mwaka 368 Hijiria), na Abu Bakar Muhammad bin Omar Ja’abi (aliyefariki mwaka 355 Hijiria), amabo ni miongoni mwa wanazuoni mashuhuri wa Shia, ni miongoni mwa walimu aliojifunza kutoka kwao. [15] Sheikh Mufidu alijifunza elimu ya kalamu (theolojia) kutoka kwa Hussein bin Ali alBasri, maarufu kama Ju’al, ambaye alikuwa ni mwanazuoni mkubwa wa upande wa madhehebu ya Mu’utazila. Pia Sheikh Mufid alikuwa ni mwanafunzi wa mutakallim (mwanatheolojia) maarufu aitwaye Abu Ya’asir. Pia, kwa mapendekezo ya Abu Yaasir, alishiriki katika vikao mafunzo ya elimu chini ya taaluma iliyotolewa na Ali bin Isa al-Rumani, mwanazuoni mashuhuri kutoka upande wa madhehebu ya Mu’utazila. [16] Kuanzia umri wa miaka takriban 40, Sheikh Mufid alikuwa ndio kiongozi wa shia katika fani ya fiqhi, kalamu (theolojia) na hadithi. Yeye katu hakuwa nyuma katika vikao vya kielimu, mara kadhaa alijihusisha katika majadiliano ya kujadiliana na wanazuoni wa madhehebu mengine kuhusiana na imani za shia. [17]

Nafasi ya elimu

Kaburi la Sheikh Mufid katika Haram ya Kadhimein

Sheikh Tusi, katika kitabu chake Al-Fihrist, anamtambulisha Mufidu kama ni mtu mwenye ufahamu wa mkali mno, mwenye uwezo wa kujibu maswali kwa haraka, na ni mtu wa mbele kabisa katika elimu ya kalam (theolojia) na fiqhi. [18] Ibn Nadim anamtaja Sheikh Mufidu kama kiongozi na bingwa wa elimu ya theolojia wa upande wa madhehebu ya Shia, na anamsifu kwa kuwa mbeleni katika fani hii kalamu (theolohjia) kuliko wengine, akiendelea katika kumsifu kwake, amesema kwamba yeye hana mpinzani katika fani hiyo. [19]

Sheikh Mufidu anachukuliwa kuwa mwakilishi wa fani ya kalam (theolpjia) mjini Baghdad, na yasemekana kwamba yeye alikuwa ni mwanazuoni maarufu aliye jishughulisha sana katika uchambuzi na ukosoaji wa mawazo ya kitheolojia kutoka shule ya kalam (kitheolojia) ya Qom. [20] Inasemekana kuwa shule ya fikra (kifalsafa na kitheolojia) ya Baghdad ilifikia kilele chake kupitia msaada wa Sheikh Mufid katika zama hizo. [21] Pia yasemekana kuwa; Sheikh Mufid hakuwa ni mfuasi wenye msimamo mkali wa kufuata akili wala mfuasi wa wenye msimamo mkali wa kufuata Hadithi kavu, bali alikuwa na mtazamo wa wastani na wenye fikra mseto za kati na kati. [22]

Sheikh Mufidu alikuwa ni mwalimu wa wanafunzi wengi, ambao baadhi yao walikuwa ni wanazuoni mashuhuri wa upande wa madhehebu ya Shia. Baadhi yao ni: [23]

Sheikh Mufidu katika mlolongo na jopo la wanazuoni wa madhehebu ya Imaamiyya, si tu mwanatheolojia na mwanazuoni mkubwa na maarufu wa Kishia, bali ni zaidi ya hayo. Yeye ndiye mwanzilishi na kiongozi wa mtiririko wa elimu uliokuwa na mchirizi wa bonde la maendeleo, ambao hadi leo unaendelea kutiririka katika uwanja wa elimu fani ya kalamu (theolojia) na fiqhii katika vyuo vikuu vya Kishia. Licha ya kila zoni tamaduni zake maalumu kihistoria, kijiografia, na kifikra, bado fikra zake zimebaki kuwa ni fikra msingi katika pande mbali mbali ulimwenguni. Sheikh Mufid alikuwa ni kete katika kudumisha uwelewa na ufahamu huru wa madhehebu ya Ahlul Bait (a.s), katika kuweka msingi wa muundo sahihi wa elimu ya fiqhi ya Shia, na kuunda njia ya iliokushana kimantiki kati ya akili na maandiko (Qur’ani na Hadithi) katika uwanja wa fiqhi na kalamu (theolojia).

Kazi za Sheikh Mufidu

Shiekh Mufidu aliandika kazi nyingi ambazo kulingana na orodha iliyo sajiliwa katika kitabu kiitwacho Al-Fahrast cha Najashi, idadi ya tasnifu na vitabu vyake ni 175. [25] Inasemekana kuwa nusu ya kazi hizi ni kuhusiana na mada ya Uimamu. [26] Kazi maarufu zaidi ya Sheikh Mufidu katika fiqhi ni Al-Muqni’a, na katika elimu ya kalam ni Awailu al-Maqaalat, na katika wasifu wa maisha ya Maimamu, ni Al-Irshad. [27]

Mlolongo wa kazi zilizoandikwa na Sheikh Mufidu umechapishwa katika seti ya vitabu 14 chini ya jina la Musannafat Sheikh Mufid. Mlolongo huu ulichapishwa mnamo mwaka 1371 Shamsia (1992 Miladia) kwa ajili ya Kongamano la Kimataifa la Sheikh Mufid. [28]

Mbinu mpya za kifiqhi

Sheikh Mufidu alianzisha njia tofauti za katika fiqhi ya Shia, ambazo zilikuwa ni mpya kabisa ukilinganisha na zama zilizopita kabla yake. Kulingana na maelezo ya Jafari Subhani na Gurji, ni kwamba; kabla ya kuja kwa Sheikh Mufidu, kulikuwa na njia mbili za kifiqhi zilizokuwa maarufu katika zama hizo: njia ya kwanza ilikuwa imejikita sana katika Riwaya na katu haikuzingatia vya kutosha uhakiki wa sanad (hati halali) na umakini wa maandishi ya Riwaya. [29] Njia ya pili haikutilia maanani Riwaya bali ilizingatia sana kanuni za akili bila ya kujali umuhimu wa Riwaya, bila kutilia maanani maandiko ya kidini. [30] Sheikh Mufidu alichagua njia ya wastani na akabuni njia mpya ya kifiqh ambapo kwanza, kanuni na misingi ya kufikia hukumu zilikuwa zinajengwa kwa kutumia akili. Kisha, kwa kutumia kanuni hizo za kimantiki, hukumu za kifiqhi zikawa zinachukuliwa au kuzaliwa kutoka kwenye maandiko ya kidini (Qur’ani na Hadithi). [31] Sababu hiyo ndiyo iliyo mfanya yeye ktambulikana kama ni mwanzilishi wa elimu ya usul al-fiqh. [32]

Baada ya Sheikh Mufidu, wanafunzi wake ambao ni; Sayyid Murtadha katika kitabu chake Al-Dhari’ah ila Usul al-Shari’ah na Sheikh Tusi katika kitabu chake Al-'Uddah fil -Usul, waliendeleza njia hii. [33]

Kushiriki kwake katika majadiliano ya kielemu

Kitabu cha Al-Irshad kilichoandikwa na Sheikh Mufid

Katika kipindi cha Sheikh Mufidu, kulikuwa na kawaida ya kufanyika majadiliano ya kielimu kati ya wanazuoni wakubwa wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu huko Baghdad. Majadiliano mengi yalifanyika mbele ya Makhalifa wa utawala wa Bani Abbas. Sheikh Mufidu naye alikuwa na kwaida ya kuhudhuria mikutano hiyo na kujibu hoja zinazohusu madhehebu ya Shia. [34]

Nyumbani kwa Shaeikh Mufidu, pia kulikuwa na vikao vya mjadala mbali mbali, ambapo wanazuoni wa madhehebu mbalimbali ya Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Mu’utazila, Zaidiyya, na Ismailiyya, walishiriki ndani yake. [35]

Hadithi ya kurekebishwa kosa katika fat'wa

Kulingana na ripoti fulani, imedaiwa kwamba; Sheikh Mufidu alifanya kosa katika kutoa fatwa fulani na Imam Mahdi (a.s) akamsawazisha. [36] Inasemekana kuwa chanzo cha zamani zaidi cha ripoti hii ni kutoka katika chanzo cha miaka 150 iliyopita. [37] Udhaifu wa chanzo, kutofautiana kwa fatwa hiyo na Hadithi sahihi, kupingana kwake na fatwa za wanazuoni maarufu, tuhuma za kutokuwa na elimu au haraka katika kutoa fatwa alizotuhumiwa nazo Sheikh Mufid kwani ripoti hiyo, ni miongoni mwa sababu zilizotolewa katika kupinga ukweli wa tukio hilo. [38] Pia tukizingatia ukweli wa kwamba; Sheikh Mufidu, katika kitabu chake cha fiqhi, kiitwacho Al-Muqni'a, amethibitisha na kutoa fatwa juu ya suala hili kulingana na fatwa za wanazuoni maarufu, Jambo ambalo linaendana kinyume na madai yeye kutenda kosa kama hilo. Ni Dhahiri kwamba; madai hayo yamefanana sana na hadithi za uwongo. [39]

Kulingana na nukuu mashuhuri iliyotajwa kuhusiana na kisa hicho, ambayo imeweza kupenya na kuingia hata kwenya vyanzo hivi sasa, [40] ni kwamba; mtu wa kijijini alimwendea Sheikh Mufidu na kumuuliza ikiwa mwanamke mjamzito atafariki hali akiwa na kiumbe tumboni mwake kilicho hai, jee itabidi kukitoa kiumbe hicho au la? Sheikh Mufidu akamju kwa kuwambia mtu huyo kwamba; yabidi mwanamke kuzikwa bila kukitoa kiumbe hicho kutoka tumbo mwake. Wakati wa kurudi kwake, mtu huyo akielekea kijijini kwao, alikutana na mtu aliyeku amepanda farasi, ambaye alikuja kwa kumharakia, alipomfikia akamwambia; Sheikh Mufidu amesema muchane tumbo la huyo mwanamke, kisha mumtoe kiumbe huyo hai alieko tmboni mwake, na kisha mumzike mwanamke huyo. Baada ya muda, wakati mtu huyo wa kijijini alipomnukulia Sheikh Mufidu kisa cha tukio hilo, Sheikh Mufidu alishangaa, na kukanusha suala la yeye kumtuma mtu huyo kwa ajili ya kusahihisha fatwa yake ya kwanza, ila akagundua kuwa mtu huyo alikuwa Imamu Mahdi (a.f). Baada ya hapo Sheikh Mufidu alisitisha kutoa fatwa hadi alipopata ruhusa kutoka kwa Imamu Mahdi (a.f), kwa kuambiwa kwamba; yeye aendelee kutoa fatwa na Imamu Mahdi atasahihisho iwapo patatokea mapungufu yoyote. [41] [Maelezo 1]

Kazi kuhusiana na Sheikh Mufidu

Kuna kazi zilizofanywa kuhusiana na Sheikh Mufid, miongoni mwazno ni vitabu na makala kadhaa vilivyeo andikwa na kuchapishwa na watu mbali mbali. Baadhi yake ni:

  • Mufidu, Mshika Bendera ya Uhuru wa Mawazo (شیخ مفید پرچم‌دار آزادی اندیشه), cha Sayyid Ja'far Murtadha Amili
  • Fikra za kitheolojia za Mufidu (ندیشه‌های کلامی شیخ مفید), cha Martin McDermott
  • Sheikh Mufidu “شیخ مفید”, cha Ali Akbar Velayati
  • Mlinzi wa mpaka wa Ushia (مدافع حریم تشیع) ukaguzi wa maisha na kazi za Sheikh Mufidu (مروری بر زندگی و آثار شیخ مفید), cha Qasem Ali Kuchnani
  • Sheikh Mufidu Mwalimu wa Ummah (شیخ مفید؛‌ معلم امت), cha Ahmad Lukmani. [43]

Mnamo Machi 1993 (24 hadi 26 Shawwal 1413 Hijiria), lilifanyika Kongamano la Kimataifa la Maadhimisho ya Mufidu huko Qom. Katika kongamano hili, zaidi ya watu 250 kutoka nchi 23 duniani walishiriki katika uwasilishaji wa makala zichunguzazo mawazo na fikra za Sheikh Mufidu katika fani za; kikalamu (kitheolojia), kifiqhi, kihistoria na kihadithi. Makala hizi zilichapishwa kwa mfumo wa vitabu.

Pia, mnamo mwaka 1994 Miladia, kuliandaliwa mfululizo wa filamu ya televisheni kuhusiana na maisha ya Sheikh Mufidu uliitwa Jua la Usiku (“خورشید شب ). Mfululizo ulio andikwa na Mahmoud Hassaniy na kuongozwa na Sirius Muqaddami. Filamu hii ilionyeshwa kwenye chaneli ya pili ya televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran mwaka wa 1995 Miladia. [44]

Maelezo

  1. Baadhi ya watu wamekanusha tukio la kutolewa kwa fatwa kama hii kutoka kwa Sheikh Mufid, hii ni kwa sababu tatu zifuatazo:
    1. Kuwepo kwa Hadithi zinazokinzana na fatwa hii.
    2. Kupingana kwa fatwa hii na ijmaa (mawafikiano) ya wanachuoni.
    3. Kupingana kwa fatwa hii na hukumu ya akili inayosema ni lazima kulinda maisha ya binadamu.

Vyanzo

  • Gurjī, Abu l-Qāsim. Tārīkh-i fiqh wa fuqahā. Tehran: Intishārāt-i Samt, 1385 Sh.
  • Ibn Nadīm, Muḥammad b. Abī Yaʿqub Ishāq. Al-Fihrist. Edited by Riḍā Tajaddud. Tehran: 1350 Sh.
  • Ibn Taghrībirdī, Al-Nujūm al-zāhira fī mulūk Miṣr wa'l-Qāhira. Cairo: Wizārat al-Thiqāfa wa Al-Irshād al-Qawmī, [n.d].
  • Khaṭīb Baghdādī, Aḥmad b. ʿAlī. Tārīkh-i Baghdād. Edited by Muṣṭafā ʿAbd al-Qādir ʿAṭā. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmīyya, 1411 AH.
  • Khurshīd-i Shab dar IFIlM, Website of Dunyā-yi Cīnamā, visited in 11.7.2020.

Barzigar. Qom: Masjid Muqaddas-i Jamkarān, 1386 Sh.

  • Muḥammadī Ishtihārdī, Muḥammad. Haḍrat-i Mahdī furūgh-e tābān-i wilāyat. Qom: Masjid Muqaddas-i Jamkarān, 1387 Sh.
  • Najāshī, Aḥmad b. ʿAlī al-. Rijāl al-Najāshī. Edited by Sayyid Mūsā Shubayrī Zanjānī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī, 1407 AH.
  • Nahāwandī, ʿAlī Akbar. Al-ʿAbqarī al-ḥisān fī aḥwāl-i mawlānā Ṣāḥib al-Zamān. Edited by Ḥusayn Aḥmadī Qummī and Ṣādiq
  • Subḥānī, Jaʿfar. Mawsūʿat ṭabaqāt al-fuqahāʾ. Qom: Muʾassisat Imām al-Ṣādiq (a), 1418 AH.
  • Shubayrī, Muḥammad Jawād. Guzarī bar ḥayāt-i Shaykh Mufīd. in Persian articles of World Conference of the Millennium of al-Shaykh al-Mufid, 1372 Sh.
  • Shubayrī, Muḥammad Jawād. Nāguftahā-yī az ḥayāt-i Shaykh Mufīd. in Persian articles of World Conference of the Millennium of al-Shaykh al-Mufid, 1372 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Fihrist. Edited by Muḥammad Jawād Qayyūmī. [n.p]. Muʾassisa Nashr al-Fiqāha, 1417 AH.