Al-Hakim al-Shar’i

Kutoka wikishia
(Elekezwa kutoka Mtawala wa Kisheria)

Al-Hakim al-Shar’i (Kiarabu: الحاكم الشرعي) au Mtawala wa sheria ni Mwanachuoni wa masuala ya Fiq'hi aliyetimiza masharti na vigezo vya kuhukumu katika mizozo na hitilafu baina ya Waislamu. Kuchukua na kubeba jukumu la Hakim Shar’i ni wajib Kifai (huu ni wajibu ambao wakitekeleza baadhi basi unawaondokea watu wengine yaani sio wajibu kwao kutekeleza), na kwa mujibu wa hili, faqihi mmoja akitoa hukumu juu ya jambo fulani, faqihi mwingine hawezi kulipinga. Wakati wa kutokuwepo kwa Imamu wa Zama (Imamu Mahdi), mafaqihi wanachukua nafasi ya mtawala wa Sheria kwa niaba ya Imamu maasumu.

Kuhusiana na mipaka ya mamlaka ya mtawala wa Sheria kuna mitazamo tofauti; baadhi ya mafakihi wamewekea mipaka mamlaka ya mtawala wa Sheria katika masuala kama usimamizi wa mayatima na kuchukua uamuzi kuhusiana na mali za wasiokuweko na mkabala wao, kundi la Maulamaa linasema kuwa, mamlaka ya mtawala wa sheria ni kama mamlaka ya Maasumina.

Ili kuthibitisha mamlaka ya kisheria ya mafaqihi, kunatumiwa kama hoja hadithi ambapo hadithi kama Maulamaa ni warithi wa Mitume, watunza amana (waaminifu) wa Mtume au warithi wake ni miongoni mwazo. Kadhalika hoja ya kiakili (kulinda nchi, nidhamu katika masuala ya dini na dunia ya waja na ijma'a) navyo vimetumika kwa ajili ya kuthibitisha mafaqihi kuwa ni watawala wa sheria.

Utambuzi wa maana

Al-Hakim al-Shar’i ni faqihi aliyetimiza masharti anayetoa hukumu katika mizozo na hitilafu baina ya Waumini. [1] Kwa muktadha huo, faqihi aliyetimiza masharti mbali na kutoa fat'wa akiwa kama Marjaa Taqlidi, ana jukumu la kutoa hukumu pia akiwa kama mtawala wa sheria [2] na kuchukua na kubeba jukumu la Hakim Shar'i (mtawala wa sheria) ni wajib Kifai [3] (huu ni wajibu ambao wakitekeleza baadhi basi inawaondokea watu wengine yaani sio wajibu kwao kutekeleza). Ni wajibu kufuata hukumu ya mtawala wa sheria. [4] Istilahi hii iliingia katika vitabu vya fiq’h kuanzia zama za Allama Hilli. [5]

Imam Khomeini baada ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran aliitumia istilahi ya mtawala wa sheria kwa makadhi (mahakimu) ambao wanajishughulisha na utoaji hukumu katika maeneo mbalimbali. [6]

Hoja ya kwamba, mafakihi ni watawala wa sheria

Katika vitabu mbalimbali vya Fiqhi kunazungumziwa suala la mafaqihi kuwa ni watawala wa sheria katika zama za ghaiba ya Imamu Mahdi (a.t.f.s), [7] hoja hizi zimetegemea hadithi ambazo zinabainisha kwamba, Maulamaa ni warithi wa Manabii, [8] watunza amana (waaminifu)[9] wa Mtume au warithi wake (viongozi baada yake). [10]

Mbali na hoja za hadithi, kuna hoja za kiakili za kuthibitisha kwamba, mafaqihi ni watawala wa sheria katika zama za ghaiba; mafaqihi wanaamini kwamba, akili ileile ambayo imeona kuna ulazima wa Imamu kuteuliwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kulinda nchi, na kuleta nidhani katika masuala ya dini na dunia kwa waja wa Allah, basi ndio akili hiyo hiyo ambayo inahukumu kwamba, kuna ulazima Imamu awe na mrithi katika zama za ghaiba yake. [11] Ili kuthibiutisha hilo, kumetumiwa pia ijma'a. [12]

Mamlaka

Mafaqihi wametofautiana kuhusiana na mipaka na mamlaka ya mtawala wa sheria. Baadhi wanasema kuwa, mamlaka yake yanahusiana na masuala ambayo yamebainishwa na Qur’ani na katika hadithi; kama masuala yanayohusiana na mayatima na mali ambayo wenyewe hawapo (hawajulikani).[13] Baadhi ya wengine wanaamini kwamba, mamlaka yake ni mamlaka yale yale ya Maimamu. [14]

Mgongano baina ya watawala wa sheria

Mafaqihi wanaamini kuwa, kwa kuzingatia kuwa, mafaqihi waliotimiza masharti ni watawala wa sheria, endapo mmoja atatoa hukumu kuhusiana na jambo fulani, haijuzu na hata ni haramu kwa mafaqihi wengine kupinga hilo; kwa sababu kwanza kabisa kuwa mtawala wa sheria ni wajibu kifai na kama mtu atalifanya hilo kwa usahihi kama ilivyo kwa wajibu zingine ambazo ni wajibu kifai haijuzu kupinga, pili upinzani wa marajii wengine kwa hukumu ya mtawala wa sheria yumkini hilo likapelekea kuvurugika nidhamu (katika jamii) na kuleta mizozo na mivutano jambo ambalo bila shaka Mwenyezi Mungu hataliridhia. [15]


Rejea

  1. Taasisi ya Ensaiklopidia ya Sheria ya Kiislamu, Farhang Fiqh, 2007, juzuu ya 3, uk.198-199.
  2. Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1, uk. 389-395; Rahman Sataysh, Rasa'il fi Wilayat al-Faqihi, 1425 AH, kitabu kizima.
  3. Shaheed Thani, Al-Rudah Al-Bahiya, 1412 AH, Juz. Rouhani, Fiqh al-Sadiq, 1412 AH, juzuu ya 16, uk. Qomi, al-Dalael, 1423 AH, juzuu ya 4, uk. 357-356.
  4. Sadr, al-Fatavi al-Sharraha, 1403 AH, uk. 632.
  5. Kafi, "Hakim (1)", uk. 423.
  6. Imam Khomeini, Sahifa Noor, 1389, juzuu ya 11, uk.378; Juzuu ya 20, uk.285; Juz. 18, uk.36; Juz. 14, uk.466; Buku la 16, ukurasa wa 398.
  7. Kwa mfano, angalia Hakim, Nahj al-Fiqahah, Qom, uk. 299-303.
  8. Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1, uk.350; Bahrani, al-Hadaeq al-Nadrah, 1405 AH, juzuu ya 13, uk.564; Rahman Sataysh, Rasail fi Wilayat al-Faqih, 1425 AH, uk. 116.
  9. Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1, uk.354; Bahrani, al-Hadaeq al-Nadrah, 1405 AH, juzuu ya 13, uk.566; Rahman Sataysh, Rasail fi Wilayat al-Faqih, 1425 AH, uk.118.
  10. Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1, uk.355; Bahrani, al-Hadaeq al-Nadrah, 1405 AH, juzuu ya 13, uk.566; Rahman Sataysh, Rasail fi Wilayat al-Faqih, 1425 AH, uk. 118.
  11. Kashif Al-Ghita, Al-Noor Al-Sate, 1381 AH, Juz.1. uk. 343; Heydari, Wilayat al-Faqih, tarehe na misingi, 1424 AH, uk. 221.
  12. Tazama Bahrani, al-Hadaiq al-Nadrah, 1405 AH, juzuu ya 13, uk.563; Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1, uk.348; Rahman Sataysh, Rasail fi Wilayat al-Faqiyya, 1425 AH, uk.115; Heydari, Wilayat al-Faqih, tarehe na misingi, 1424 AH, uk. 220.
  13. Heydari, Wilayat Al-Faqih, Historia na Misingi, 1424 AH, uk. 226-228; Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1. uk 341,379; Maraghi, Al-Anawin al-Fiqhiyyah, 1417 AH, juzuu ya 2, uk. 562-569.
  14. Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1, uk. 341; Maraghi, Al-Anawin al-Fiqhiyyah, 1417 AH, juzuu ya 2, uk. 562-569.
  15. Kashif al-Ghita, Al-Noor al-Sate, 1381 AH, juzuu ya 1, uk. 389-390.


Vyanzo

  • Imam Khomeini, Seyyed Ruhollah, Sahifa Noor, Tehran, Taasisi ya Uchapishaji ya Imam Khomeini, 1389.
  • Bahrani, Yusuf bin Ahmed, al-Hadaiq al-Nadrah fi Haqam al-Utrah al-Tahirah, Qom, utafiti na marekebisho ya Mohammad Taqi Irwani na Seyyed Abd al-Razzaq Mokaram, Qom, Ofisi ya Machapisho ya Kiislamu yenye uhusiano na Jumuiya ya Seminari ya Qom. ya Walimu, 1405 AH.
  • Taasisi ya Ensaiklopidia ya Sheria ya Kiislamu, utamaduni wa sheria kwa mujibu wa dini ya Ahlu al-Bayt, Qom, Taasisi ya Encyclopaedia ya Sheria ya Kiislamu, toleo la pili, 1394.
  • Hakim, Seyyed Mohsen Tabatabai, Nahj al-Faqaha, Qom, 22 Machapisho ya Bahman.
  • Heydari, Mohsen, Wilayat al-Faqih, tarehe na misingi, Beirut, Darulula Lalprinta va Nashar va al-Tawzee, 1424 AH.
  • Rahmansataish, Mohammad Kazem, Rasail fi Wilayat al-Faqih, Qom, Machapisho ya Ofisi ya Propaganda ya Kiislamu ya Seminari ya Qom, 1425 AH.
  • Shaheed Thani, Zain al-Din bin Ali, al-Rawda al-Bahiya fi Sharh al-Lamaa al-Damashqiya, Sharh Sultan al-Ulama, Qom, Machapisho ya Ofisi ya Propaganda ya Kiislamu ya Qom Seminari, 1412 AH.
  • Sadr, Seyyed Muhammad Baqir, Al-Fatawa al-Hazara kwa mujibu wa dini ya Ahlul-Bayt, amani iwe juu yake, Beirut, Dar al-Taarif kwa Waandishi wa Habari, 1403 AH.
  • Qafi, Hossein, "Mtawala (1)", Encyclopaedia of Islamic World, Juzuu 12, Tehran, Islamic Encyclopaedia Foundation, toleo la 1, 1387.
  • Qomi, Seyyed Taqi, Al-Dalael fi Sharh Munqab al-Masal, Qom, duka la vitabu la Mahalati, 1423 AH.
  • Rouhani, Seyyed Sadiq, Fiqh al-Sadiq, Qom, Dar al-Kitab - Shule ya Imamu Sadiq (amani iwe juu yake), 1412 AH.
  • Maraghi, Seyyed Mir Abd al-Fattah bin Ali Hosseini, Al-Anawin Al-Faqhiyyah, Qom, Ofisi ya Uchapishaji ya Kiislamu yenye uhusiano na Jumuiya ya Walimu ya Seminari ya Qom, 1417 AH.
  • Kashif al-Ghata, Ali bin Muhammad Reza bin Hadi, Al-Nur al-Sata’ fi fiqh al-nafi, Najaf, Al-Adab Press, 1381 AH.