Nenda kwa yaliyomo

Mkopo:Dua ya Hamsini ya Sahifa Sajjadiyya

Kutoka wikishia
Dua ya Hamsini ya Sahifa Sajjadiyya
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa Mnamo Sha'ban 1102 AH.
Nakala ya Sahifa al-Sajjadiyah, katika hati ya Naskh ya Abdullah Yazdi, iliyoandikwa Mnamo Sha'ban 1102 AH.
MadaDua maalumu iombwayo na mja, pale anapojisikia khofu mbele ya Mwenye Ezi Mungu kutokana na makosa yake mbali mbali.
Ina Mapokezi au Haina MapokeziIna Mapokezi
Imenukuliwa Kutoka kwaImamu Sajjad (a.s)
MpokeziMutawakkil ibn Harun
Vyanzo vya KishiaSahifa Sajjadiyah
Dua ya Tawassuli • Dua ya Kumaili • Dua ya Nudba • Dua ya Samati • Dua ya Faraji • Dua ya Abu Hamza Thumali • Ziara ya Ashura • Ziara ya Jamiat Kabira • Ziara ya Warith • Ziara ya Aminu-Llah • Ziara ya Arobaini


Dua ya Hamsini ya Sahifa Sajjadiyya (Kiarabu: الدعاء الخمسون من الصحيفة السجادية) ni moja kati ya dua zilizonukuliwa kutoka kwa Imamu Sajjad (a.s). Nayo ni ile inayotumika wakati wa kukumbwa na hali ya wasiwasi na woga wa kumkhofu Mwenye Ezi Mungu kutokana na makosa ya kibinadamu tuyatendayo mara kwa mara kutokana na udhaifu tuliokuwa nao. Katika maombi haya, Imamu Sajjad (a.s) anamtaja Mola wake kwa sifa mbali mbali. Miongoni mwa sifa za Mwenye Ezi M ungu zilizomo ndani ya dua hii, ni pamoja na sifa ya; uanzilishi (katika uumbaji wake), sifa ya ulezi (unawirishaji), pamoja na sifa ya kuruzuku waja wake. Halikadhalika, dua yatoa msisitizo maalumu juu ya amali ya kuomba maghufira kutoka kwa Maenye Ezi Mungu, huku ikitambua kwamba; maghufira ndiyo chanzo msingi kijengacho fikra za matumaini ndani ya maisha ya wanadamu. Aidha, dua inalielezea ufahamu wa Mwenye Ezi Mungu juu ya tabia na udhaifu alionao mwanadamu, pamoja na kuelezea ukarimu wa Mola wetu katika kupokea toba za waja Wake.

Tafsiri fafanuzi ya Dua ya Hamsini, inapatikana katika vitabu mbali mbali vilivyotoa tafsiri chambuzi ya kitabu cha Sahifa Sajjadiya. Miongoni mwa vitabu vilivoandikwa kwa lugha ya kiajeme ni kitabu maarufu kiitwacho; Shuhud wa Shenakht, kazi ya Hassan Mamdouhi Kermanshahi. Pia kwa upande wa lugha ya Kiarabu, kitabu Riadh as-Salikina, kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu Sayyid Ali Khan Madani, ndiyo moja ya vitabu mashuhuri vilivyohudumia waumini pamoja na wahakiki mbali m bali watumiao lugha ya Kiarabu.

Mafunzo Yaliomo Ndani ya Dua ya hamsini

Dua ya Hamsini ni miongoni mwa dua tukufu zilizomo ndani ya Sahifa Sajjadiyya, nayo ni dua maalumu iombwayo na mja, pale anapojisikia khofu mbele ya Mwenye Ezi Mungu kutokana na makosa yake mbali mbali. Mfasiri wa kitabu cha Sahifa Sajjadiyya, bwana Mamduhi Kermanshahi, anabainisha akisema kwamba; Madhambi ndiyo chanzo cha hofu na woga katika moyo wa Muumini. Hivyo basi, dua hii inatotufunza kuwa; kumkimbilia Mwenye Ezi Mungu na kumtaka maghufira Allah (Subhanahu wa Ta'ala), ndiyo msingi mkuu wa uokovo, kwani Yeye ndiye kimbilio pekee lenye uhakika wa uokovu kwa Muumini.[1]

Miongoni mwa mafunzo maridadi yaliomo ndani ya dua hii adhimu ni kama yafuatayo:

  • Mwenyezi Mungu ndiye chimbuko la uwepo wa mwanadamu, mstawishaji wake na mpatiaji (mfadhili) wa mahitaji yake.
  • Woga na wasiwasi wa aibu inayotokana na maasi yaliyohifadhiwa ndani sajili ya vitendo vya mwanadamu.
  • Dhambi ni kichocheo cha uhafifishaji wa nguvu chanya za kibinadamu na ndio chanzo cha changamoto hasi.
  • Upatikanaji wa nafuu kutokana na hali ya kukata tamaa na kuvunjika moyo, kupitia bishara ya msamaha utokao kwa Mwenye Ezi Mungu.
  • Matarajio ya msamaha wa Mungu ni chanzo cha fikra za matumaini ndani ya maisha mwanadamu.
  • Ubatili wa dhana potofu kuwepo uwezekanao wa kukwepa mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Ungamo la kustahiki adhabu kwa mujibu wa makosa tuyatendayo.
  • Adhabu ya Mola ni kielelezo cha uadilifu wake.
  • Mwenye Ezi Mungu hana ulazima wala uhitaji wa kuwapa adhabu waja wake.
  • Kutowepo pazia la kuyastiri yaliomo mbinguni na ardhini mbele ya elimu ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Mwali wa moto wa jahanamu unazidi kiwango cha ustahimilivu na uwezo wa mwanadamu.
  • Ombi la kuomba rehema na msamaha kutoka kwa Mwenye Ezi Mungu.
  • Ungamo la kuungama na kukiri ukuu wa mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu na udumifu wake.
  • Utiifu na uasi havina athari, si katika uendelevu wala mapungufu ya mamlaka ya Mwenye Ezi Mungu.
  • Watu wasio watoharifu na wasio na dosari (a.s), ndiwo watu pekee wenye ufahamu wa majina maalumu ya Mwenye Ezi Mungu ylioko katika ghaibu Yake.
  • Mwenye Ezi Mungu ana ujuzi kamili wa asili na nyenendo za kila kitu.
  • Mwenye Ezi Mungu ni mwingi wa kukubali toba na ni Mwenye rehema kubwa mno kwa waja Wake.
  • Ufalme wa Mungu juu ya ulimwengu wa viumbe ni wa kudumu na hauna mwisho.[2]

Tafsiri Chambuzi za Dua ya Hamsini

Dua ya Hamsini ya Sahifa Sajjadiya imefasiriwa na kushereheshwa na wanazuoni kwadhaa waliofasiri dua za kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa kazi mbali mbali zilizoandikwa kwa lugha ya Kiajemi ni pamoja na; kazi maridadi ya Hussein Ansariyan ilioko katika kitabu chake kiitwacho Diare Asheqan,[3] kazi ya Muhammad Hassan Mamduhi Kermanshahi inayojulikana kwa jila la Shohud wa Shenakht,[4] pamoja na kazi maarufu ya Sayyid Ahmad Fahri, iliyoko katika kitabu chake kiitwacho Sharhe wa Tarjome Sahifa Sajjadiyye.[5]

Pia kuna waandishi mbali mbali waliotumia kalamu zao katika kutoa uchambuzi wa dua hii kwa lugha ya Kiarabu sambamba na dua nyengine zilizomo ndani ya kitabu cha Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa vitabu vya Kiarabu vilivyotoa huduma hii ni pamoja na; Riadhu al-Salikin cha Sayyid Ali-Khan Madani,[6] Fi Dhilali al-Sahifa al-Sajjadiyya cha Muhammad Jawad Mughniyah,[7] Riadhu al-Arifina cha Muhammad bin Muhammad Darabi[8] na Afaqi al-Ruh kilichoandikwa na Sayyid Muhammad Hussein Fadhlullah.[9] Aidha kuna juhudi maalumu zilizofanywa na baadhi ya wanazuoni katika kukusanya na kufasiri msamiati wa dua hii sambamba na msamiati wa dua nyengine zilizomo ndani ya Sahifa Sajjadiyya. Miongoni mwa kazi hizi zenye ufafanuzi wa kilugha ni pamoja na; Ta'aliqati ala al-Sahifati al-Sajjadiyya, kitabu kilichoandikwa na Faidhu Kashani[10] na Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyya, kazi ya Izz al-Din al-Jaza’iri.[11]

Matini ya Dua ya Hamsini Pamoja na Maelezo Yake kwa Kiswahili

Maandishi
Maandishi na Tafsiri
Tafsiri

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الرَّهْبَةِ

اللَّهُمَّ إِنَّكَ خَلَقْتَنِي سَوِيّاً، وَ رَبَّيْتَنِي صَغِيراً، وَ رَزَقْتَنِي مَكْفِيّاً

اللَّهُمَّ إِنِّي وَجَدْتُ فِيمَا أَنْزَلْتَ مِنْ كِتَابِكَ، وَ بَشَّرْتَ بِهِ عِبَادَكَ أَنْ قُلْتَ: «يا عِبادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلى‏ أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ، إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً» وَ قَدْ تَقَدَّمَ مِنِّي مَا قَدْ عَلِمْتَ وَ مَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، فَيَا سَوْأَتَا مِمَّا أَحْصَاهُ عَلَيَّ كِتَابُكَ

فَلَوْ لَا الْمَوَاقِفُ الَّتِي أُؤَمِّلُ مِنْ عَفْوِكَ الَّذِي شَمِلَ كُلَّ شَيْ‏ءٍ لَأَلْقَيْتُ بِيَدِي، وَ لَوْ أَنَّ أَحَداً اسْتَطَاعَ الْهَرَبَ مِنْ رَبِّهِ لَكُنْتُ أَنَا أَحَقَّ بِالْهَرَبِ مِنْكَ، وَ أَنْتَ لَا تَخْفَى عَلَيْكَ خَافِيَةٌ فِي الْأَرْضِ وَ لَا فِي السَّمَاءِ إِلَّا أَتَيْتَ بِهَا، وَ كَفَى بِكَ جَازِياً، وَ كَفَى بِكَ حَسِيباً.

اللَّهُمَّ إِنَّكَ طَالِبِي إِنْ أَنَا هَرَبْتُ، وَ مُدْرِكِي إِنْ أَنَا فَرَرْتُ، فَهَا أَنَا ذَا بَيْنَ يَدَيْكَ خَاضِعٌ ذَلِيلٌ رَاغِمٌ، إِنْ تُعَذِّبْنِي فَإِنِّي لِذَلِكَ أَهْلٌ، وَ هُوَ- يَا رَبِّ- مِنْكَ عَدْلٌ، وَ إِنْ تَعْفُ عَنِّي فَقَدِيماً شَمَلَنِي عَفْوُكَ، وَ أَلْبَسْتَنِي عَافِيَتَكَ.

فَأَسْأَلُكَ- اللَّهُمَّ- بِالْمَخْزُونِ مِنْ أَسْمَائِكَ، وَ بِمَا وَارَتْهُ الْحُجُبُ مِنْ بَهَائِكَ، إِلَّا رَحِمْتَ هَذِهِ النَّفْسَ الْجَزُوعَةَ، وَ هَذِهِ الرِّمَّةَ الْهَلُوعَةَ، الَّتِي لَا تَسْتَطِيعُ حَرَّ شَمْسِكَ، فَكَيْفَ تَسْتَطِيعُ حَرَّ نَارِكَ،! وَ الَّتِي لَا تَسْتَطِيعُ صَوْتَ رَعْدِكَ، فَكَيْفَ تَسْتَطِيعُ صَوْتَ غَضَبِكَ!

فَارْحَمْنِيَ- اللَّهُمَّ- فَإِنِّي امْرُؤٌ حَقِيرٌ، وَ خَطَرِي يَسِيرٌ، وَ لَيْسَ عَذَابِي مِمَّا يَزِيدُ فِي مُلْكِكَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ، وَ لَوْ أَنَّ عَذَابِي مِمَّا يَزِيدُ فِي مُلْكِكَ لَسَأَلْتُكَ الصَّبْرَ عَلَيْهِ، وَ أَحْبَبْتُ أَنْ يَكُونَ ذَلِكَ لَكَ، وَ لَكِنْ سُلْطَانُكَ- اللَّهُمَّ- أَعْظَمُ، وَ مُلْكُكَ أَدْوَمُ مِنْ أَنْ تَزِيدَ فِيهِ طَاعَةُ الْمُطِيعِينَ، أَوْ تَنْقُصَ مِنْهُ مَعْصِيَةُ الْمُذْنِبِينَ.

فَارْحَمْنِي يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ، وَ تَجَاوَزْ عَنِّي يَا ذَا الْجَلَالِ وَ الْإِكْرَامِ، وَ تُبْ عَلَيَّ، إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ‏.

وَ كَانَ مِنْ دُعَائِهِ عَلَيْهِ السَّلَامُ فِي الرَّهْبَةِ
Na (ifuatayo ilikuwa na) miongoni mwa dua zake, amani iwe juu yake, (aliyokuwa akiiomba) katika hali ya khofu (aliyokuwa nayo wakati wa kumcha Mungu).
اللَّهُمَّ إِنَّكَ خَلَقْتَنِي سَوِيّاً، وَ رَبَّيْتَنِي صَغِيراً، وَ رَزَقْتَنِي مَكْفِيّاً
Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika Wewe umeniumba nikiwa na maumbile kamili (yasio na upungufu), na ukanilea (ukanistawisha) nikiwa mdogo, na ukaniruzuku kwa kunitosheleza.
اللَّهُمَّ إِنِّي وَجَدْتُ فِيمَا أَنْزَلْتَ مِنْ كِتَابِكَ، وَ بَشَّرْتَ بِهِ عِبَادَكَ أَنْ قُلْتَ: «يا عِبادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلى‏ أَنْفُسِهِمْ لا تَقْنَطُوا مِنْ رَحْمَةِ اللَّهِ، إِنَّ اللَّهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعاً» وَ قَدْ تَقَدَّمَ مِنِّي مَا قَدْ عَلِمْتَ وَ مَا أَنْتَ أَعْلَمُ بِهِ مِنِّي، فَيَا سَوْأَتَا مِمَّا أَحْصَاهُ عَلَيَّ كِتَابُكَ
Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi nimekuta (bishara njema) katika kitabu (Chako) ulichokiteremsha, pamoja na zile habari njema ulizowabashiria waja kwa kuwaambia: 'Enyi waja wangu mliopindukia mipaka kujidhulumu wenyewe nafsi zenu, msikate tamaa ya kupata rehema za Mwenye Ezi Mungu, hakika Mwenye Ezi Mungu ni mwenye kusamehe dhambi zote.' Na hakika yametangulia kutoka kwangu yale unayoyajua, na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi. Ole wangu kwa yale yaliyoandikwa dhidi yangu katika kitabu chako (sajili Yako/rejesta Yako)!
فَلَوْ لَا الْمَوَاقِفُ الَّتِي أُؤَمِّلُ مِنْ عَفْوِكَ الَّذِي شَمِلَ كُلَّ شَيْ‏ءٍ لَأَلْقَيْتُ بِيَدِي، وَ لَوْ أَنَّ أَحَداً اسْتَطَاعَ الْهَرَبَ مِنْ رَبِّهِ لَكُنْتُ أَنَا أَحَقَّ بِالْهَرَبِ مِنْكَ، وَ أَنْتَ لَا تَخْفَى عَلَيْكَ خَافِيَةٌ فِي الْأَرْضِ وَ لَا فِي السَّمَاءِ إِلَّا أَتَيْتَ بِهَا، وَ كَفَى بِكَ جَازِياً، وَ كَفَى بِكَ حَسِيباً.
Lau kusingekuwepo masshiko ya matarajio ninayotaraji juu ya msamaha Wako uliotanda juu ya kila kitu, bila shaka ningekuwa ni mwenye kukata tamaa (ningekuwa miongoni mwa wenyekujiangamiza kwa mikono yangu). Na kama ingewezekana kwa yeyote kumkimbia Mola wake, basi mimi ningekuwa na haki zaidi ya kukukimbia. Hata hivyo, wewe ni yule ambaye hakuna kitu kinachoweza kujificha kwako, iwe ardhini au mbinguni, isipokuwa unakileta wazi. Unatosha kama mlipaji, na unatosha kama mhasibu.
اللَّهُمَّ إِنَّكَ طَالِبِي إِنْ أَنَا هَرَبْتُ، وَ مُدْرِكِي إِنْ أَنَا فَرَرْتُ، فَهَا أَنَا ذَا بَيْنَ يَدَيْكَ خَاضِعٌ ذَلِيلٌ رَاغِمٌ، إِنْ تُعَذِّبْنِي فَإِنِّي لِذَلِكَ أَهْلٌ، وَ هُوَ- يَا رَبِّ- مِنْكَ عَدْلٌ، وَ إِنْ تَعْفُ عَنِّي فَقَدِيماً شَمَلَنِي عَفْوُكَ، وَ أَلْبَسْتَنِي عَافِيَتَكَ.
Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika Wewe ndiye uninitafutaye pindi ninapotoroka (ninakutoroka), Nawe (ndiye) unayenidiriki pindi ninapo ponyokaka (ninapokuponyoka). Basi (tayari), mimi hapa niko mbele Yako, nikiwa mnyenyekevu (nikiwa katika hali ya unyenyekevu kamili), ni mdhalili, na mtiifu (niliye chini ya amri Yako). Ukinuadhibu, bila shaka mimi ni mwenye kustahili adhabu hiyo, na hilo, Ee Bwana (wangu), litakuwa linatokana na uadilifu utokao Kwako. Na ukinisamehe, basi msamaha Wako umekuwa ukinifunika tangu zamani, na (tokea mwanzo) ulinivisha afya Yako njema (ulikuwa ukinishushia kheri na hisani Zako adhimu).
فَأَسْأَلُكَ- اللَّهُمَّ- بِالْمَخْزُونِ مِنْ أَسْمَائِكَ، وَ بِمَا وَارَتْهُ الْحُجُبُ مِنْ بَهَائِكَ، إِلَّا رَحِمْتَ هَذِهِ النَّفْسَ الْجَزُوعَةَ، وَ هَذِهِ الرِّمَّةَ الْهَلُوعَةَ، الَّتِي لَا تَسْتَطِيعُ حَرَّ شَمْسِكَ، فَكَيْفَ تَسْتَطِيعُ حَرَّ نَارِكَ،! وَ الَّتِي لَا تَسْتَطِيعُ صَوْتَ رَعْدِكَ، فَكَيْفَ تَسْتَطِيعُ صَوْتَ غَضَبِكَ!
Ewe Mwenye Ezi Mungu, ninakuomba kwa mamlaka (hadhi) ya majina yako yaliyofichika na kwa utukufu wako uliositiriwa kwa sitara maalumu, uihurumie nafsi (hali yangu) hii yenye taharuki na kiwiliwili (changu) hichi chenye hofu kubwa. Kiwiliwili hichi hakiwezi kuhimili hata miale ya jua lako, ni vipi basi itaweza kustahimili ukali wa moto wako? Na iwapo hakiwezi kuvumilia ngurumo ya radi zako, kitathubutuje kukabiliana na mngurumo wa hasira Zako?
فَارْحَمْنِيَ- اللَّهُمَّ- فَإِنِّي امْرُؤٌ حَقِيرٌ، وَ خَطَرِي يَسِيرٌ، وَ لَيْسَ عَذَابِي مِمَّا يَزِيدُ فِي مُلْكِكَ مِثْقَالَ ذَرَّةٍ، وَ لَوْ أَنَّ عَذَابِي مِمَّا يَزِيدُ فِي مُلْكِكَ لَسَأَلْتُكَ الصَّبْرَ عَلَيْهِ، وَ أَحْبَبْتُ أَنْ يَكُونَ ذَلِكَ لَكَ، وَ لَكِنْ سُلْطَانُكَ- اللَّهُمَّ- أَعْظَمُ، وَ مُلْكُكَ أَدْوَمُ مِنْ أَنْ تَزِيدَ فِيهِ طَاعَةُ الْمُطِيعِينَ، أَوْ تَنْقُصَ مِنْهُ مَعْصِيَةُ الْمُذْنِبِينَ.
Basi nihurumie, Ewe Mola, kwani mimi ni kiumbe dhalili, na umuhimu wangu ni mdogo mno. Mateso yangu si jambo lenye kuongeza hata chembe ya thamani katika milki Yako. Na lau mateso yangu yangekuwa ni yenye kuongeza kitu fulani katika milki yako, basi kwa yakini ningekuomba ustahamilivu juu yake, na ningependelea hilo liwe kwa ajili Yako (yaani ningependelea Wewe uwe ndiye mwenye kufaidika badala yangu). Hata hivyo, mamlaka yako, Ewe Mola, ni adhimu zaidi, na ufalme wako ni wa milele zaidi ulioepukika na mapungufu kuweza kuongezeka kitu fulani kupitia utiifu wa wenye kutii, au kupungua kutokana na maasi ya wenye kukosea.
فَارْحَمْنِي يَا أَرْحَمَ الرَّاحِمِينَ، وَ تَجَاوَزْ عَنِّي يَا ذَا الْجَلَالِ وَ الْإِكْرَامِ، وَ تُبْ عَلَيَّ، إِنَّكَ أَنْتَ التَّوَّابُ الرَّحِيمُ‏.
Kwa hivyo basi, nirehemu, Ewe Mwingi wa rehema kuliko warehemevu wote. Na (nakuomba) uyafumbie macho makosa yangu, Ewe Mwenye utukufu na taadhima. Pia (nakuomba) unisamehe kwa toba Yako, kwa hakika Wewe ni Mwingi wa kupokea toba na Mrehemevu wa hali ya juu kabisa.

Na (ifuatayo ilikuwa na) miongoni mwa dua zake, amani iwe juu yake, (aliyokuwa akiiomba) katika hali ya khofu (aliyokuwa nayo wakati wa kumcha Mungu).

Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika Wewe umeniumba nikiwa na maumbile kamili (yasio na upungufu), na ukanilea (ukanistawisha) nikiwa mdogo, na ukaniruzuku kwa kunitosheleza.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika mimi nimekuta (bishara njema) katika kitabu (Chako) ulichokiteremsha, pamoja na zile habari njema ulizowabashiria waja kwa kuwaambia: 'Enyi waja wangu mliopindukia mipaka kujidhulumu wenyewe nafsi zenu, msikate tamaa ya kupata rehema za Mwenye Ezi Mungu, hakika Mwenye Ezi Mungu ni mwenye kusamehe dhambi zote.' Na hakika yametangulia kutoka kwangu yale unayoyajua, na ambayo Wewe unayajua zaidi kuliko mimi. Ole wangu kwa yale yaliyoandikwa dhidi yangu katika kitabu chako (sajili Yako/rejesta Yako)!

Lau kusingekuwepo masshiko ya matarajio ninayotaraji juu ya msamaha Wako uliotanda juu ya kila kitu, bila shaka ningekuwa ni mwenye kukata tamaa (ningekuwa miongoni mwa wenyekujiangamiza kwa mikono yangu). Na kama ingewezekana kwa yeyote kumkimbia Mola wake, basi mimi ningekuwa na haki zaidi ya kukukimbia. Hata hivyo, wewe ni yule ambaye hakuna kitu kinachoweza kujificha kwako, iwe ardhini au mbinguni, isipokuwa unakileta wazi. Unatosha kama mlipaji, na unatosha kama mhasibu.

Ewe Mwenye Ezi Mungu, hakika Wewe ndiye uninitafutaye pindi ninapotoroka (ninakutoroka), Nawe (ndiye) unayenidiriki pindi ninapo ponyokaka (ninapokuponyoka). Basi (tayari), mimi hapa niko mbele Yako, nikiwa mnyenyekevu (nikiwa katika hali ya unyenyekevu kamili), ni mdhalili, na mtiifu (niliye chini ya amri Yako). Ukinuadhibu, bila shaka mimi ni mwenye kustahili adhabu hiyo, na hilo, Ee Bwana (wangu), litakuwa linatokana na uadilifu utokao Kwako. Na ukinisamehe, basi msamaha Wako umekuwa ukinifunika tangu zamani, na (tokea mwanzo) ulinivisha afya Yako njema (ulikuwa ukinishushia kheri na hisani Zako adhimu).

Ewe Mwenye Ezi Mungu, ninakuomba kwa mamlaka (hadhi) ya majina yako yaliyofichika na kwa utukufu wako uliositiriwa kwa sitara maalumu, uihurumie nafsi (hali yangu) hii yenye taharuki na kiwiliwili (changu) hichi chenye hofu kubwa. Kiwiliwili hichi hakiwezi kuhimili hata miale ya jua lako, ni vipi basi itaweza kustahimili ukali wa moto wako? Na iwapo hakiwezi kuvumilia ngurumo ya radi zako, kitathubutuje kukabiliana na mngurumo wa hasira Zako?

Basi nihurumie, Ewe Mola, kwani mimi ni kiumbe dhalili, na umuhimu wangu ni mdogo mno. Mateso yangu si jambo lenye kuongeza hata chembe ya thamani katika milki Yako. Na lau mateso yangu yangekuwa ni yenye kuongeza kitu fulani katika milki yako, basi kwa yakini ningekuomba ustahamilivu juu yake, na ningependelea hilo liwe kwa ajili Yako (yaani ningependelea Wewe uwe ndiye mwenye kufaidika badala yangu). Hata hivyo, mamlaka yako, Ewe Mola, ni adhimu zaidi, na ufalme wako ni wa milele zaidi ulioepukika na mapungufu kuweza kuongezeka kitu fulani kupitia utiifu wa wenye kutii, au kupungua kutokana na maasi ya wenye kukosea.

Kwa hivyo basi, nirehemu, Ewe Mwingi wa rehema kuliko warehemevu wote. Na (nakuomba) uyafumbie macho makosa yangu, Ewe Mwenye utukufu na taadhima. Pia (nakuomba) unisamehe kwa toba Yako, kwa hakika Wewe ni Mwingi wa kupokea toba na Mrehemevu wa hali ya juu kabisa.

🌞
🔄
➖
➕

Rejea

  1. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 296.
  2. ↑ Mamduhi Kermanshahi, Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 4, uk. 296-305.
    Sherh Farzahaye Duaye Panjohom Sahife Az Site Irfan.
  3. ↑ Ansarian, Diyar Asheqan, 1373, juz. 7, uk. 587-599.
  4. ↑ Mamduhi, Kitab Shuhud wa Shenakht, 1388, juz. 3, uk. 293-305.
  5. ↑ Fahri, Sherh wa Tafsir Sahifa Sajjadih, 1388, juz. 3, uk. 535-539.
  6. ↑ Madani Shirazi, Riyadh al-Salikin, 1435 AH, juz. 6, uk. 297-330.
  7. ↑ Mughniyah, Fi Dhilal al-Sahifa, 1428 AH, uk. 637-640.
  8. ↑ Darabi, Riyadh al-Arifin, 1379 AH, uk. 699-705.
  9. ↑ Fadhlullah, Afaq al-Ruh, 1420 AH, juz. 2, uk. 592-600.
  10. ↑ Faydh Kashani, Ta'baqat al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1407 AH, uk. 101-102.
  11. ↑ Jazairi, Sharh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, 1402 AH, uk. 285-287.

Vyanzo

  • Ansarian, Hussein, Diyar Asheqan, Tafsir Jamii Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Payam Azadi, 1374.
  • Jazairi, Izu-Din, Sherh al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Beirut, Dar al-Taaruf Lil-Matbuat, 1402 AH.
  • Darabi, Muhammad bin Muhammad, Riyadh al-Arifin Fi Sherh Sahifa Sajjadiyah, Muhaqiq Hussein Dargahi, Tehran, Nashr Us-wah, 1379.
  • Fadhlullah, Sayyid Muhammad Hussein, A'faq al-Ruh, Beirut, Dar al-Malik, 1420 AH.
  • Fahri, Sayyid Ahmad, Sherh wa Tarjume Sahifa Sajjadiyeh, Tehran, Us-wah, 1388 S.
  • Faidh Kashani, Muhammad bin Murtaza, Taaliqat Ala Sahifa Sajjadiyah, Tehran, Muasase al-Bahth wa al-Tahqiqat al-Thaqafiyah, 1407 AH.
  • Mughniyeh, Muhammad Jawad, Fi Dhilal al-Sahifa al-Sajjadiyyah, Qom, Dar al-Kitab al-Islami, 1428 AH.
  • Madani Shirazi, Sayyid Ali Khan, Riyadh al-Salikiin Fi Sherh Sahifa Sayyid al-Sajidin, Qom, Muasase al-Nashr al-Islami, 1435 AH.
  • Mamduhi Kermanshahi, Hassan, Shuhud wa Shenakhte: Tarjume wa Sherh Sahifa al-Sajjadiyyah, Ba Muqadime Ayatullah Jawadi Amuli, Qom, Bostan Kitab, 1385 S.