Mir Shamsu al-Din al-Iraqi
Mir Shams al-Din al-Iraqi (Kiarabu: مير شمس الدين العراقي) (845-932) ni mmoja wa wajukuu wa Imamu Musa Kadhim (a.s) na ni mmoja wa waenezaji wa madhehebu ya Shia huko Kashmir na Baltistan.
Mir Shams al-Din al-Iraqi alifanya mahuburi ya Ushia huko Kashmir na kwa msingi huo, idadi ya watu na wakazi wa huko waliingia katika madhehebu ya Shia. Pia, aliandaa mazingira ya kutolewa hotuba kwa kusomwa majina ya Maimamu Kumi na Mbili wa Kishia katika Msikiti wa Jamia wa Kashmir. Ujenzi wa msikiti na Khangah (sehemu ya kufanyia ibada masufi) na kuharib nyumba ya sanamu zilikuwa miongoni mwa shughuli zake nyingine katika eneo la Kashmir.
Muhammad Ali Kashmiri aliandika kitabu Tuhafat Al-Ahbab kwa lugha ya Kiajemi kuhusu Mir Shams al-Din Iraqi na akaeleza wasifu wake na harakati zake katika kitabu hicho.
Maisha yake
Mir Shams al-Din Iraqi alizaliwa mwaka 845 Hijria katika kijiji cha viunga vya mji Arak. [1] Jina lake la asili ni Sayyid Muhammad, na nasaba yake inaishia kwa Imamu Musa al-Kadhim (a.s), Imam wa saba wa Kishia. [2] Baba yake Sayyid Ibrahim na mama yake wanatokana na ukoo wa masharifu wa Qazvin. [3] Nasaba yake ya Iraqi inahusiana na kuhusishwa kwake na Iraq ya Kiajemi moja ya miji ya Iran [4] ambao leo unajulikana kama Arak. [6] Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana baadhi wanamtambua na kumtaja kwa kiungishi cha Araki. [6]
Kulingana na shajara, mwaka wa kifo cha Mir Shams al-Din Iraqi ni 932 Hijria. Hata hivyo, kulingana na baadhi ya watafiti, hakuna chochote kuhusu hili kilichokuja katika vyanzo vya kale kama vile Baharistan Shahi, Tuhfah Al-Ahbab na Tarikh Malik Haidar Chadurah [8]. Pia, kuna tofauti ya maoni kuhusu kama Mir Sham al-Din alikufa kifo cha kawaida au aliuawa. [9] Katika mashairi ya maombolezo ya Mullah Said Ashraf, mpwa wa Muhammad Baqir Majlisi kumeashiriwa kuuawa kwake. [10] Baadhi ya waandishi katika Kashmir pia wana mtazamo huu. [11]
Mir Sham al-Din amezikwa Khanqah huko Jidibal jirani na Srinagar mji mkuu wa Kashmir. [12]
Harakati za Kiutamaduni
Mir Shams al-Din alifanya shughuli na harakati za kitamaduni huko Kashmir; inasemekana kwamba katika kipindi cha Shah Hassan wa ukoo wa Shah Miri (876-889 Hijiria), alipewa nafasi na cheo cha Shaykh-ul-Islam [13] na aliandaa mazingira ya kutolewa hotuba kwa kusomwa majina ya Maimamu wa Kishia katika Msikiti wa Jamia wa Kashmir na misikiti mingine. [14] Baadhi ya shughuli zake zingine za kiutamaduni huko Kashmir ni:
Kueneza Ushia Kashmir
Mir Shams al-Din alikwenda Kashmir mwaka wa 882 H kama balozi wa Sultan Hussein Bayqara (utawala: 911-875 H), mtawala wa ukoo wa Taymuri wa Khorasan, na akarudi Khorasan baada ya kukaa huko kwa miaka minane. [15]
Pia aliingia Kashmir mwaka wa 902 kwa ombi la Shah Qasim Nurbakhsh na akawalingania watu kwenye madhehebu ya Shia. [16] Mir Shams al-Din alizingatia machifu wa makabila na watu wenye ushawishi katika siasa na hivyo kufanya tablighi ya ana kwa ana nay a mtu hadi mtu badala ya kuhubiri hadharani. [17] Baba Ali Najjar, Sufi mashuhuri wa wakati huo, alikuwa mtu wa kwanza kutoa kiapo cha utii kwake. [18] Kisha Musa Raina, Waziri Mkuu, na Kaji Chak na Ghazi Chak (962-971 AH), miongoni mwa watu mashuhuri katika serikali, walikubali madhehebu ya Shia. [19] Ni kwa msingi huo ndio maana vyanzo vya historia vimezungumzia juu ya kuwa Shia ukoo wa Chak, ambao walikuwa na nasaba ya madhehebu ya Imamiya na waliokuwa wakitawala Kashmir katika miaka ya 962-994 H. [20] Inasemekana pia kwamba kwa himaya na msaada wa Musa Raina, Waziri Mkuu wa Kashmir, familia 24,000 za Kihindu zilingia katika madhehebu ya Shia [21] na idadi ya Mabudha wakazi wa Ladakh katika eneo la Baltistan pia waliingia katika madhehebu ya Shia [22].
Kujenga Msikiti na Khanqah
Mir Shams al-Din aliharibu na kubomoa nyumba za masanamu na badala yake akajenga msikiti na nyumba ya masufi mahali hapo. Vyanzo vimetaja nyumba 3943 za masanamu ambazo zilibomolewa naye. [23] Ni kutokana na sababu hiyo ndio maana alipewa lakabu ya Mukassir al-Asnam (mvunja-masanamu). [24] Miongoni mwa nyumba za watawa au masufi zilizojengwa na Mir Shams al-Din, ni ya Zadibal iliyoko kilomita 8 kutoka Srinagar mji mkuu wa Kashmir. [25] Pia, aliifanyia ukarabati Khanqah iliyojengwa na Sultan Sikandar mvunja masanamu (796 AH) kwa ajili ya Mir Sayyid Ali Hamdani. [26]
Kutuma wahubiiri (mubalighina) katika maeneo ya mbali [27] na kufufua utamaduni wa Jihadi ni miongoni mwa shughuli na harakati zingine za kiutamaduni zilizofanywa na Mir Shams al-Din. [28]
Harakati za Kielimu
Mir Shams al-Din alisoma kwa Sayyid Muhammad Nurbakhsh. [29] Pia alitumia muda fulani kusuhubiana na watu kama Shams al-Din Lahiji na Shah Qasim Nurbakhsh. [30] Alikuwa na wanafunzi wengi [31] na baadhi yao wametajwa katika Kitabu cha Baharistan Shahi.[32]
Monografia
Kitabu cha Tuhaf al-Ahbab, kilichoandikwa na Muhammad Ali Kashmiri, kinatoa wasifu na maelezo ya harakati za Mir Shams al-Din Iraqi. [33] Kitabu hiki kiliandikwa wakati wa utawala wa Sultan Hussein (utawala: 971-978 H) wa Shah Chak. [34] Kitabu hiki pia kimetarjumiwa kwa Kiurdu. [35]