Mdhaifu wa kifikra
Mdhaifu wa kifikra “Mustadh'af Fikriyyun / مُستَضعَف فکری": Ni yule mtu mwenye uwezo dhaifu wa kifikra ambaye hana uwezo wa kiakili wa kutambua au kutofautisha kati ya haki na batili au hakupata fursa na wala hakuwa na uwezo wa kufikiwa na ujumbe wa dini ya Kiislamu. Hata hivyo, “Mustadh'af Fikriyyun / مُستَضعَف فکری" anayekusudiwa katika ibara hii, ni yule mtu ambaye kama Uislamu ungelimfikia basi asingekewa na pingamizi katika kuupokea Uislamu huo. Kinyume chake, ni “Mustadh'af Fikriyyun / مُستَضعَف فکری""Mdhaifu Kimatendo". Naye ni yule mdhaifu anayefahamu uwepo na ukweli wa Uislamu, lakini mazingira yanamzuia na hayamruhusu kutekeleza maamrisho ya dini hiyo.
Mstadh'af Katika Qur’ani na Hadithi
Qur'ani Tukufu imeashiria hali ya watu wenye sifa hifa hii ya "Mstadh'af" kupitia Aya mbali mbali. Baadhi ya wafasiri wamesema kwamba maana ya Mstadh'af aliyekusudiawa katika baadhi ya Aya hizo, ni mdhaifu wa kifikra ambaye kiistilahi huitwa “Mustadh'af Fikriyyun / مُستَضعَف فکری". Vilevile, kuna hadithi kadhaa kutoka kwa bwana Mtume (s.a.w.w) na Maimamu (a.d) zenye kutoa maelezo kutaja sifa mbali mbali kuhusiana na hali za mdhaifu wa kifikra. Baadhi ya wanazuoni wengine wakimtambulisha mdhaifu wa kifikra, wamejaribu kumpa maana sawa samabamba na yule "mjinga asiye na uwezo wa kujifunza, ambaye katika istilahi hutambulika kwa jina la “Jaahilu Qaasirun / جاهل قاصر”.
Kuna mitazamo mitatu tofauti kuhusiana na hatima ya maisha ya Akhera kwa mdhafu wa kifikra:
· Adhabu ya Jahannam – Baadhi ya wanatheolojia wa Kishia wanaamini kuwa hatima yake ni kuingia Jahannam.
· Kuokolewa – Wengine wanaamini kuwa mdhaifu wa kifikra ataokolewa na ataepushwa na adhabu, hasa akiwa ametekeleza majukumu yake ya kidini kwa dhati kulingana na imani aliyokuwa nayo moyoni mwake.
· Kutoadhibiwa na Badala Yake Kupewa Malipo Mema – Wengine wanaamini kuwa; Mwenye Mungu hatamwadhibu mdhaifu wa kifikra na badala yake atamlipa thawabu na kumpa malipo mema.
Maana ya Mdhaifu wa Kifikra “مُستَضعَف فکری”
Katika muktadha wa fasihi za kidini, mdhaifu wa kifikra ni mtu anayeshindwa kutafautisha baina ya batili na sababu ya upungufu wa akili aliokuwa nao, au kuto kuwa na fursa ya kuufikia na Uislamu (yaani hakufikiwa na Uislamu). [1] Ila anayekubalika miongoni mwa wenye kukadiriwa kuwa na sifa hiyo, ni yule amabaye lau kama angefikiwa na ukweli huo (Uislamu), basi asingepingana nao wala kuukanusha na kwenda kinyuma nao. [2]
Mstadh'af wa kifikra hutafautishwa na mdhaifu wa kivitendo, ambaye ni yule anayefahamu haki ila kutokana na mazingira dhalimu humfanya yeye ashindwe kutenda kulingana na matakwa ya Uislamu. [3] Kulingana na maoni ya baadhi ya watafiti ni kwamba; Dhana ya mdhaifu wa kifikra ina maana sawa na dhana ya "mjinga asiye na uwezo wa kujielimisha", ambaye kiistilahi hujulikana kama “Jaahilun Qaasirun”. [4] Kwa mtazamo huu; mdhaifu wa kifikra hatokuwa na tafauti na "mjinga asiye na uwezo wa kujielimisha".
Nafasi ya Mdhaifu wa Kifikra Katika Qur'ani
Katika baadhi ya Aya za Qur'ani, kuna ibara zilizobeba ndani yake ufafanuzi au maelezo kuhusiana na mdhaifu wa kifikra, ambazo ndani yake mnapatika msamiati wa "Mustadh'af" (mdhaifu). Wafasiri wa Qur’ani wakifafanua Aya hizo wamesema kwamba; baadhi ya matumizi ya msamiati huo yanahusiana na mdhaifu wa kifikra. [5] Ila tukiangalia upande wa maelezo ya Hadithi mbali mbali, tutakutia kuwa; ibara nyingi za Hadithi zimetumia msamiati huu kwa maana ya mdhaifu wa kifikra. Kwa mfano, Imamu Kadhimu (a.s) katika moja ya Hadithi zake amesema kwamba; mdhaifu ni yule ambaye hajawahi kuoneshwa hoja au dalili za wazi juu ya ukweli wa dini, na wala yeye mwenyewe hana ufahamu wala welewa wowote ule juu ya tofauti kuhusiana na dini na madhehebu mbali mbali. Hata hivyo, pindi anapofahamu kuhusiana na uwepo wa tofauti hizo, basi hachukuliwi tena kuwa "Mustadh'af" (mdhaifu). [6]
Allama Majlisi, katika kitabu chake Bihar al-Anwar, katika sura yenye jina la "Al-Mustadh'afina wal-Murjauna li-Amrillahi," amekuja na hadithi alizozifafanua kuhiana na 37 dhana ya "Mustadh'af" (mdhaifu). [7]
Ni Akina Nani Wanaohisabiwa Kuwa ni Wenye Odhoofu wa Kiakili?
Sheikh Sadouq ametaja makundi matatu ya watu kama ni mifano ya wenye udhoofu wa kiakili, nayo ni kama ifuatavyo:
1. Wale ambao wamezaliwa wakiwa wamekosa neema ya akili amabo wanaishi maisha yao yote wakiwa katika hali hiyo. [8]
2. Watoto waliozaliwa hali wakiwa wamebahatika kupata neema ya kiakili, lakini hufariki kabla ya wao kufikia umri wa kuwa na uwezo wa kupambanua kati ya haki na batili.
3. Wale waliokuwa na uwezo wa kiakili, ila sharia na habari za utume ziliwafikia hali wakiwa wazee, kiasi ambacho uzee wao haukuwapa fursa wa kuelewa haki kutokana na ukongwe wa akili zao. [9]
Kwa mujibu wa imani za watafiti fulani, watu walio na akili, ila kutokana na sababu za kimazingira au propaganda fulani wakawa hawajawahi kufikiwa na ujumbe wa haki, nao pia wanaweza kuhesabiwa miongoni mwa wenye udhaifu wa kiakili.
Jaafar Subhani, mtaalamu wa fani ya theolojia ya Kishia, ameorodhesha mifano minne mikuu kuhusiana na wenye udhaifu wa kiakili:
1. Mtu aliyezaliwa katika eneo ambapo hakuna fursa ya kujifunza dini.
2. Mtu anayeishi katika jamii isiyo na mwanafiq’hi ndani yake, ambapo ukosefu wa mtaalamu kama huyo wa kidini mwenye maarifa tosha, kunafanya iwe ni vigumu kwake kuweza kutekeleza wajibu wake wa kidini ipaswavyo.
3. Mtu aliyelelewa katika familia ambayo mila za kidini za kurithi ambazo hupokewa na kukubaliwa na wanajamii bila kudadisiwa au kukosolewa.
4. Mtu ambaye kiasili ni mwenye udhaifu wa kiakili. [11]
Hatima ya Wenye Udhaifu wa Kiakili Siku ya Kiyama
Msimamo na namana ya muamala wa Mwenye Ezi Mungu kuhusiana na wenye udhaifu wa kiakili katika Siku ya Kiyama umeibua mitazamo tofauti miongoni mwa wanazuoni wa Kiislamu:
· Baadhi ya wanatheolojia wa Kishia wanaamini kwamba; Ifikapo Siku ya Kiyama, Mwenye Ezi Mungu atawakusanya wenye udhoofu kama na kuwaingiza Motoni. [12]
· Wafasiri na wanatheolojia wengine, wakitegemea Aya ya 98 na 99 za Suratu An-Nisaa pamoja na baadhi ya Hadithi kutoka kwa Maimamu, [13] wanasema kuwa; wenye uwezo mdogo wa kiakili ni miongoni mwa wale watakaookolewa na Mola wao Siku ya Kiama. [14] Aidha, wanaongeza wakisema kuwa; ikiwa mtu aliye dhaifu kiakili atatekeleza wajibu wake wa kidini kwa dhati kulingana na imani yake na uwezo wake, basi si tu kwamba yeye ataepukana na Jahannamu, bali pia atastahili kupata malipo mema. [15]
· Kundi jingine linaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu hatawaadhibu wenye udhoofu wa kiakili, lakini pia Yeye hawatawapa thawabu waja hao, kwani thawabu hutolewa kwa mujibu wa utekelezaji wa majukumu ya kidini. Ila hukumu yao ipo chini ya maamuzi ya huruma na fadhila za Mwenye Ezi Mungu. [16]
Murtadha Mutahhari, mwanafalsafa wa Kishia, akielezea suala la wenye udhaaifu wa ufahamu wa kiakili, amekuja na mitazamo miwili tofauti kuhusiana na suala hili. Mtazamo wa kwanza ni ule wa siasa kali na kupindukia mipaka, na wa pili ni mtazamo wa kuzorota na kutojali. Kwa maoni ya Murtadha Mutahhari, mitazomo miwili yote kwa pamoja na yenye kukinzana na mafunzo ya Qur’ani: [17]
1. Kwa mujibu wa mtazamo wenye kupindukia mipaka, ni kwamba; hakuna amali ya mtu yeyote yule itakayokubaliwa mbele ya Mwenye Ezi Mungu, isipokuwa amali za Mashia peke yao. Hivyo hata kama mtu atakuwa mdhaifu wa kiakili, hilo halitamfanya yeye kukubalika mbele ya Mola wake. [18] Msingi mkuu wa ndharia hii unatokana na imani isemayo kwamba; kukubalika kwa amali za mja kunategemea imani yake juu ya Ushia. Kwa maana ya kwamba asiyekuwa Shia hawezi kukubaliwa amali zake.
2. Katika mtazamo wa kuzorota na kubutuka makali, ni kwamba; Iwapo amali za mwenye mapungufu ya kiakili zitakuwa ni amali njema na zenye kheri ndani yake, bila shaka mja huyo atastahili kupata malipo mema, bila kujali imani yake. Yaani hata kama yeye atakuwa si Shia wala si Muislamu, hilo halitamfanya yeye kupoteza thamani za matendo yake. [19] Murtadha Mutahhari anaamini kwamba; Iwapo mwenye mapungufu ya kiakiali atakuwa si mpinzani wa kupingana na haki, wala kukataa ukweli, bila shaka mtu huyo atapata malipo na jaza njema kutoka kwa Mola wake. [20]
Historia na Vyanzo vya Utafiti Kuhusu Waliodhoofika Kiakili
Kwa mujibu wa maoni ya baadhi ya watafiti, hakuna makala au kitabu maalum kilichoandikwa kikamilifu juu ya mada ya wenye udhaifu wa kiakili. Badala yake, mada hii imetajwa ikiwa katika hali ya mparaganyiko katika vitabu mbali mbali vya tafsiri ya Qur’ani. Kwa hiyo tukipitia vitabu mbali mbali vya tafsiri ya Qur’ani, tutakutia mada hii imetajwa katika baadhi ya sehemu ya vitabu hivyo, hasa katika wakati wa kufasiri Aya zinazotaja neno "Mustadh’af au Mustadh’afuna" au maneno jengine linalotokana na mzizi wa neno hilo, au linalohisiana na mada hiyo. [21] Kwa mfano, Murtadha Mutahhari kitabu chake kiitwacho Uadilifu wa Mwenyezi Mungu (Adl-e Ilahi), alijadili suala la udhaifu wa kiakili katika mada inayohusiana na "matendo mema yatokanayo na wasio Waislamu". [22]
Makala nyingine zilizochambua mada hii ni pamoja na:
- Didgah Imam Khomeiniy dar Babaare Peirowane Adyan "Mtazamo wa Imam Khomeini Kuhusu Wafuasi wa Dini Tofauti" iliyoandikwa na Hussein Taufiqi. [23]
- Pluralisim Najat dar Andishe Islami "Wingi wa Wokovu katika Mawazo ya Kiislamu" iliyoandikwa na Mahdi Azizan. [24]
- Bar-resi Pluralisim Najat az Didgah Qur’an "Uchambuzi wa Wingi wa Wokovu kwa Mtazamo wa Qur’ani" iliyoandikwa na Ilqar Ismailzadeh. [25]
- Wadh’iyyate Mustadh’afane Fikri dar Qiyamat "Hali ya Waliodhoofika Kiakili Siku ya Kiyama" iliyoandikwa na Mohammad Ali Yusufizadeh na Qasim Jawadi. [26]
- Bar-resi Maahiyyat wa Aaqibat Ukhrawi Mustadh’afane Diniy ba Takiyye bar Ayat wa Riwaayaat "Uchunguzi wa Asili na Hatima ya Akhera ya Waliodhoofika Kidini kwa Kutegemea Aya na Hadithi" iliyoandikwa na Mohammad Hussein Naqizadeh na Samad Abdullahi Aabid. [27]
Maudhui zinazofungamana: Jaahili Qaasir, Jaahil Muqassir