Mazungumzo Kati ya Mungu na Nabi Musa (a.s)

Kutoka wikishia

Mazungumzo Kati ya Mungu na Nabi Musa (a.s): ni yale mazungumzo yaliokuwa yakijiri baina ya Mwenye Ezi Mungu na Nabii Musa (a.s), ambayo yanasemekana kuwa yalifanyika moja kwa moja bila ya kupitia Malaika fulani au mfikishaji fulani wa ujummbe wa Mwenye Ezi Mungu. Suala hili la mazungumzo baina ya Mwenye Ezi Mungu na mja wake bila ya kutumika Malaika fulani, linahisabiwa kuwa ni sifa na hadhi maalumu kwa Nabi Musa peke yake. Suala hili limezungumzwa wazi ndani ya baadhi ya Aya za Qur'ani, miongo mwa Aya za Qur'ani, zilizo nukuu suala hili ni ile Aya ya 164 ya Suratu al-Nisa. Nabi Musa husifika kwa sifa ya Kalimullah (yule ambaye Mungu alisema naye) ambayo ni mahususi kwa Nabi Musa (a.s), na Mayahudi walimtabua kwa jina “Kalimi” kwa kutokana na sifa hii. Baadhi ya wanazuoni wa Kishia kama vile Sheikh Tusi, wanaamini kwamba; mazungumzo yaliokuwa yakipita kati Mwenye Ezi Mungu na Nabi Musa, yalikuwa ni halisia yanayo fanana na mazungumzo ya kawaida. Katika Hadithi, maneno ya Mwenye Ezi Mungu yamezingatiwa ni maneno yanayozaliwa bila ya kutumia mdomo na ulimi. Kuna maoni tofauti kuhusiana na uhalisia wa maneno yenye sifa kama hizi: Baadhi ya wafasiri wa Shia wanaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu aliumba mawimbi ya sauti na maneno katika anga au katika vitu fulani. Baadhi ya wafasiri wengine wanaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu hakutaja wala hakutufahamis jinsi ya usemaji huo ulivyotimia, nasi hatuna mashiko yoyote yale kutoka katika Qur'ani, kuhusiana na namna halisi ya usemaji huo wa Mwenye Ezi Mungu. Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba; pamoja na Musa (a.s) pia Mwenye Ezi Mungu lizungumza moja kwa moja na Mtume wa Muhammad (s.a.w.w).

Nabi Musa (a.s) Kupata Sifa ya Kalimullah Kwa mujibu wa Aya ya 164 ya Suratu al-Nisa, ni kwamba Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Musa (a.s), Mwenye Ezi Mungu katika Aya hiyo Anasema: "کَلَّمَ الله مُوسی تَکْلیماً", Maana yake ni kwamba; "Na Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Musa kwa mazungumzo". [1] Pia mazungumzo haya baina ya Mwenye Ezi Mungu na Nabi Musa yametajwa katika Aya ya 144 ya Suratu A'raf. [2] Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu [3] na Mayahudi [4] wanayachukulia mazungumzo aina hii, kuwa ni makhususi na maalum kwa Nabii Musa (a.s) peke yake. Hivyo basi wao wamelirodhesha jambo hilo katika orodha ya sifa maalumu za Nabi Musa (a.s). [5] Wao wamesema kwamba Sifa ya Kalimullah ni makhususi kwa Nabi Musu, [6] na wakasema kwamba; sifa hiyo hiyo ya Nabii Musa ndiyo iliwafanya Mayahudi kuitwa “Kalimi.” [7] Baadhi ya wanazuoni wa Kiislamu wanaamini kwamba Mwenye Ezi Mungu pia alizungumza na Mtume wa Muhammad (s.a.w.w) katika safari yake ya Miraji, pia wamedai kuwa kuna Hadithi maalumu zinathibitisha usemi wao huo. [8] Wanazuoni hawa wanaamini kwamba; mawasiliano ya moja kwa moja na Mwenye Ezi Mungu, yalikuwa ni mahususi tu kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na Musa (a.). [9] Mazungumzo ya Mwenye Ezi Mungu yamezingatiwa kuwa; ni namna ya kunena bila kutumia na mwili; Kwa sababu kunena kwa kutumia ulimi na kwa njia ya sauti, ni dalili ya kuwa na kiwiliwili, hali ya kwamba Mwenye Ezi Mungu hana mwili. [10] Imamu Ali (a.s.), kwenye moja ya vipengele vya hotuba zake, akizungumzia suala la mazungumzo baina ya Nabi Musa na Mola wake, ameyasifu mazungumzo hayo ya Mungu, kuwa ni mazungumzo na matamshi yasiyo haihitaji aina yoyote ile ya nyenzo au viungo vya kiwiliwili. [11] Pia Imamu Redha (a.s) alizingatia unenaji huo wa Mungu, kuwa ni unenaji uliojiri bila ya kutumia mdomo na ulimi, jambo ambalo ni tofauti kabisa na mazungumzo ya viumbe. [12]

Mazungumzo ya Moja kwa Moja na Bila ya Kiunganishi Kulingana na nadharia za wanazuoni wa Kiislamu, ni kwamba; Mazungumzo yaliojiri kati ya Mwenye Ezi Mungu na Nabi Musa (a.s) yalifanyika kwa njia ya moja kwa moja [13] na bila mwasilisha -ambaye ni Malaika-. [14] Tabarsi, mwandishi wa tafsiri ya Majma’u al-Bayan, akitoa ufafanuzi kuhsiana na tofauti kati ya mazungumzo ya Mwenye Ezi Mungu na Nabi Musa (a.s) na manabii wengine, ameeleza ya kwamba; Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Nabi Musa (a.s) moja kwa moja bila kupitia mwasilishaji. [15] Katika aina hii ya mazungumzo, ujumbe hufikishwa kwa mkusudiwa (msikilizaji), huku mzungumzaji akiwa hawaonekani; hii ni kutokana na uwepo wa pazia maalumu la kiroho au kizuizi kinachozuia kumuona mzungumzaji huyo. [16] Sheikh Tusi aliona kwamba; Mazungumzo ya Mwenye Ezi Mungu na Nabi Musa (a.s) ni mazungumzo yenye sura ya mazungumzo halisi kabisa. [17] Baadhi ya wafasiri wakizingatia neno “takliman تَکْلیماً” lililoko katika Aya isemayo “وَ کَلَّمَ الله مُوسی تَکْلیماً” “Na Mwenye Ezi Mungu alimzungumza na Musa kwa mazungumzo”[18] wamedai ya kuwa neno hilo ni ushahidi wa kwamba Mwenye Ezi Mungu amezungumza kwa mazungumzo halisi kabisa, na wakasema kwamba; haiwezekani kutafsiri mazungumzo hayo kuwa ni ya “kimajazi” au kitamthili. [19] Kulingana na maelezo ya Allama Tabataba’i, mwandishi wa tafsiri ya al-Mizan, kuzungumza huko kwa Mwenye Ezi Mungu na Musa kulikuwa katika mfuma wa mazungumzo halisi kabisa na kulikuwa na athari sawa na mazungumzo ya kawaida, kama vile kufahamisha na kufikisha makusudio yake kwa wengine; lakini mazungumzo hayo yalikuwa ni tofauti na mazungumzo ya kawaida, na kwamba mazungumzo hayo hayakuwa kupitia njia ya ulimi au koo. [20] Jinsi ya Mungu alivyozungumza na Nabi Musa (a.s) Makarim Shirazi, ambaye ni mwanazuoni na mfasiri wa Kishia, anaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu alizungumza na Nabi Musa (a.s) kwa kutuma mawimbi ya sauti angani au kwenye vitu fulani. [21] Sheikh Tusi pia ameandika akisema kwamba; Mwenye Ezi Mungu huzalisha maneno katika umbo (kiwiliwili) fulani ili kufikisha lengo lake kwa viumbe vyake. [22] Baadhi ya wafasiri wengine pia wameeleza kuwa; Mwenye Ezi Mungu aliumba sauti na maneno, na Musa akayasikia maneno hayo yatokayo kwa Mola Wake. [23] Kwa upande mwingine, Allama Tabataba’i anaamini kwamba Mwenye Ezi Mungu hajataja ni jinsi yeye alitima mazungumzo yake hayo, na wala sisi hatupati maelezo yale juu ya jinsi hiyo ya uzungumzaji kutoka katika Qur’ani Tukufu. [24] Muhammad Jawad Maghniyyah, mfasiri wa Kishia, yeye pia anaamini kwamba; Mwenye Ezi Mungu amekaa kimya bila ya kusema chochote kile kuhussiana na jinsi ya mazungumzo hayo. Hivyo basi sisi pia tunakaa kimya katika suala hili, na hatusemi chochote kuhusiana na asili ya maneno na mazungumzo hayo yalivyo. [25]