Mazoezi

Kutoka wikishia

Mazoezi ya nafsi (Kiarabu: رياضة النفس) kuifanya ivumulie mambo magumu, aiche matamanio na kufanya ibada kwa ajili ya kuitakasa roho au nafsi ambapo katika baadhi ya maandiko ya Kiirifani jambo hili limetajwa kuwa ni jihad al-Akbar (jihadi kubwa) na Uislamu umeusia jambo hili. Kujinyima, kula kidogo (kwa kiasi) kukesha (kwa ajili ya kufanya ibada), kutozungumza sana, (kuongea kidogo) na kuchagua kujiweka faragha ni katika mambo ambayo yametambuliwa kuwa ni katika nguzo za mazoezi ya nafsi.

Kusamehe, ushujaa, ghera na kuwa na unyenyekevu mbele ya haki yametajwa kuwa ni matokeo ya kuifanyisha mazoezi nafsi. Katika Uislamu kumekatazwa mbinu zisizo halali za kuilea nafsi kama utawa (kuacha dunia na ladha zake kama kuoa, kula nyama na kujitenga na jamii).

Mulla Sadra ametambua kufanya mazoezi ya nafsi kabla ya kukamilisha maarifa na kufanyia kazi kikamilifu ibada za kisheria kuwa ni jambo la upotovu.

Utambuzi wa maana

Mazoezi au mazoezi ya nafsi ni kuifanya ivumulie mambo magumu, iache matamanio na kufanya ibada kwa ajili ya kuitakasa roho (nafsi) [1] ambapo katika Aya za Qur’ani Tukufu na hadithi za Maasumina zimeusia na kukokoteza jambo hili.

Mazoezi ya nafsi katika athari za Kiirfani yamekuja kwa maana tofauti tofauti; [3] miongoni mwazo ni kuifanyia mazoezi na kuizoesha nafsi ili maneno, vitendo na nia yake iwe kwa ajili ya Mwenyezi Mungu tu. [4] Mazoezi ya kinafsi yametambuliwa kuwa ni mithili ya jihadi kubwa na nguzo zake ni kula kidogo, kukesha kwa ajili ya kuomba dua na kufanya ibada, uchache wa maneno na kujiweka faradha. [5]

Athari na matokeo

Kuondoka ubakhili, husuda, kiburi na tamaa ya dunia ni miongoni mwa mambo yaliyotajwa kuwa ni matokeo ya kuifanyisha mazoezi nafsi; [6] kama ambavyo kufanikiwa kufikiwa sifa njema kama kusamehe, ushujaa, ghera na kuwa na unyenyekevu mbele ya haki ni matokeo mengine ya mazoezi ya nafsi. [7]

Baadhi ya Aya za Qur’ani Tukufu zinaonyesha na kudhihirisha maana ya mazoezi ya nafsi; [8] miongoni mwazo ni Aya ya 40 na 41 za Surat Naziat ambapo kwa mujibu wa Aya hizo, mtu ambaye "Na ama yule anaye ogopa kusimamishwa mbele ya Mola wake Mlezi, na akajizuilia nafsi yake na matamanio, Basi huyo, Pepo itakuwa ndiyo makaazi yake!" [9] Imamu Ali (a.s) amenukuliwa akisema: Kila ambaye daima ni mwenye kuifanyisha mazoezi nafsi yake atapata faida. [10]

Maeneo yalipokatazwa

Kumekatazwa kufanya mazoezi ya nafsi kutumia njia zisizo za kisheria [11] na ni kwa msingi huo ndio maana utawa kwa maana ya kuipa mgongo dunia na kuachana na kila kitu chake [12] ni jambo ambalo limekatazwa. [13]

Mulla Sadra ametambua kufanya mazoezi ya nafsi kabla ya kukamilisha maarifa na kufanyia kazi kikamilifu ibada za kisheria kuwa ni jambo la upotovu [14] na kwa msingi huo anaamini kuwa, madhali kungali na uzembe na hali ya upuuzaji katika masuala ya ibada za kisheria, hakuna nafasi ya ibada za kihekima na mazoezi ya kisuluki na kitabia; kwa sababu kufanya hivyo ni kuangamia na kuangamiza wengine. [15]

Vyanzo

  • Āmadī, ʿAbd al-Wāḥid b. Muḥammad al-. Ghurar al-ḥikam wa durar al-kalim. Edited by Mahdī Rajāʾī. Qom: Dār al-Kitāb al-Islāmī, 1410 AH.
  • Anwarī, Ḥasan. Farhang-i buzurg-i sukhan. Tehran: Sukhan, 1390 Sh.
  • Gulpāyigānī, Muḥammad Riḍā. Irshād al-sāʾil. Beirut: Dār al-Ṣafwa, 1413 AH.
  • Khātamī, Rūḥ Allāh. ;;Āyina-yi makārim. Tehran: Zulāl, 1368 Sh.
  • Mūsawī Tabrīzī, Muḥsin. Muqaddama-ī bar ʿirfān-i ʿamalī wa ṭahārat nafs wa shinākht-i insān-i kāmil. Tehran: Muʾassisa-yi Farhangī-yi Nūr ʿalā Nūr, 1387 Sh.
  • Qāsānī, ʿAbd al-Razzāq al-. Sharḥ manāzil al-sāʾirīn. Edited by Muḥsin Bīdārfar. Qom: Bīdār, 1385 Sh.
  • Shāhrūdī, Sayyid Maḥmūd al-. Farhang-i fiqh muṭābiq bā madhhab-i Ahl al-Bayt (a). Qom: Muʾassisat Dāʾirat al-Maʿārif-i Fiqh-i Islamī, 1389 Sh.
  • Ṭūsī, Naṣīr al-Dīn Muḥammad. Awṣāf al-ashrāf. Edited by Mahdī Shams al-Dīn. Tehran: Wizārat-i Farhang wa Irshād-i Islamī, 1369 Sh.