Madyan (kabila)

Kutoka wikishia

Makala hii inahusiana na kabila la Madyan. Kama unataka kuhafamu kuhusu mji wa Madyan, angalia makala ya Mji wa Madyan.


Madyan (Kiarabu: قوم مَدْيَن ) ni kaumu ya Waarabu ambayo Nabii Shuaib alitumwa na kuteuliwa kuwa Mtume ili akawaongoze, na Nabii Mussa (a.s) aliishi baina yao kwa miaka kadhaa. Baadhi ya wahakiki wamelinasibisha kabila hili na dhuria (kizazi) ya Midian, mtoto wa Nabii Ibrahim (a.s) na wengine wakilinasibisha na Nabii Ismail (a.s). Kabila hili lilikuwa likiishi katika mji wa Madyan karibu na Ghuba ya Aqaba. Kabila la Madyan lilikumbwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu kutokana na kutomuamini Mwenyezi Mungu.


Shajara (mtungo wa nasaba)

Madyan ni kabila ambalo asili na mbari yake ni Waarabu. [1] Neno Madyan limetajwa mara 10 katika kitabu kitakatifu cha Qur'an [2] ambapo baadhi ya maana yake limekusudiwa kabila la Madyan [3] na baadhi ni mji wa Madyan. [4] Kuhusiana na nasaba ya kabila la Madyan kuna hitilafu za kimitazamo:

Baadhi ya wahakiki na wanahistoria wamelinasibisha kabila la Madyan na mtoto wa Nabii Ibrahim (a.s) anayejulikana kwa jina la Midian. [5] Kwa mujibu wa ripoti ya Torati [6] na baadhi ya vyanzo vya Kiislamu, [7] baada ya Nabii Ibrahim (a.s) kufiwa na mkewe Sara, alioa mwanamke mwingine na mkewe huyo akamzalia watoto akiwemo Midian. Midian alimuoa binti ya Nabii Lut (a.s) na kwa njia hiyo kizazi chao kikaendelea. [8]

Kadhalika Ibn Kathir amelihesabu kabila tajwa kwamba, linatokana na kizazi cha Madyan bin Midian bin Ibrahim [9] na baadhi ya wahakiki wamekitaja kizazi hicho kwamba, kinatokana na kizazi cha Nabii Ismail (a.s). [10]


Makazi

Makala kuu: Mji wa Madyan

Raman ya mji wa Madyan

Kaumu ya Madyan ilikuwa ikiishi katika mji wa Madyan na jina la mji limechukuliwa kutoka katika jina la kabila hilo. [11] Mji huu kijiografia upo mashariki mwa Ghuba ya Aqaba [10] katika ukingo wa bahari na mji huo unahesabiwa kuwa na mandhari ya kijani kibichi. [12] Mji wa Madyan upo jirani na eneo la Tabuk [13] na vilevile jirani na mji wa kaumu ya Lut. [14] Sheikh Swaduq anasema, Madyan ni kijiji kidogo ambacho ndani hamkuwa na nyumba zaidi ya 40. [15]

Baadhi ya wahakiki wameuhesabu mji huu kuwa miongoni mwa miji wa Sham (Syria) [16] na wamesema kuwa, kuna uwezekano mji wa Maan ulioko katika nchi wa Jordan ]17] ndio uliojengwa mahali pake. [18] Baadhi ya wengine wanaamini kwamba, Madyan ipo katika Saudi Arabia ya leo. [19]

Mapigano na Bani Israil

Kwa mujibu kauli ya wazi ya Qur’an [21] na Torati [22] Nabii Mussa (a.s) baada ya kukimbia kutoka Misri alielekea Madyan na akiwa huko alioana na binti wa Nabii Shuaib (a.s) [23] na kuishi huko kwa miaka mingi na akiwa baina ya kabila la Madyan [24] na alikuwa akishughulisha na kazi ya kuchunga mifugo. [25]

Katika duru za historia yake, kabila la Madyan lilishuhudia mapigano baina yake na Bani Israil. Imekuja katika kitabu cha mahakimu moja ya vitabu vitakatifu vya Mayahudi visa vya mapigano ya kaumu ya Madyan na Bani Israil ambapo hatimaye baada ya miaka mingi ya kushindwa na kudhalilishwa, Bani Israil wakawashindwa watu wa kaumu ya Madyan. [26]


Radiamali kwa Utume wa Shuaib

Mwenyezi Mungu akiwa na lengo la kutoa hidaya na uongofu kwa kaumu ya Madyan alimteua na kumfanya Shuaib kuwa Mtume. [27]

Shuaib alikuwa akitokana na kabila la Madyan. [28] Nabii Shuaib (a.s) kwa miaka mingi alijishughulisha na kazi ya kuwafikishia watu wa kaumu yake risala na dini ya Mwenyezi Mungu; ambapo aliwalingania tawhidi (kumpwekesha Mwenyezi Mungu), [29] insafu (uadilifu) na ukweli katika muamala, [29] kujitenga mbali na ufisadi katika mgongo wa ardhi [30] na kuogopa adhabu ya Siku ya Kiyama. [31]. Katika Surat al-A’raf kumeashiriwa mazungumzo baina ya Nabii Shuaib na wapinzani wake. [32]


Adhabu

Akthari ya watu wa kabila la Madyan waliupinga na kuukata mwito wa Nabii Shuaib (a.s) na wakakumbwa na adhabu ya Mwenyezi Mungu. [33] Kwa mujibu wa Aya za Qur’an Tukufu, kaumu ya Madyan iliangamizwa kwa tetemeko la ardhi; [34] kwa namna ambayo kama vile hakuna mtu wa kaumu hiyo aliyeishi katika mji huo. [35].


Vyanzo

  • Balāghī , Sayyid ʿAbd al-Ḥujjat, Ḥujjat al-tafasīr wa balāgh al-iksīr, Qom: Hikmat Publications, 1386 AH.
  • Burūjirdī, Sayyid Muḥammad Ibrāhīm, Tafsīr Jāmiʿ. Sixth edition. Tehran: Sadr Publications, 1366 Sh.
  • Fakhr al-Rāzī, Muḥammad b. al-ʿUmar al-, Mafātīḥ al-ghayb (al-Tafsīr al-Kabīr). Third edition. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, 1420 AH.
  • Ḥusayni al-Shīrazi, al-Sayyid Muhammad al-, Tabyīn al-Qurʾan. Beirut: Dar al-'Ulum, 1423 AH.
  • Ibn Athīr, Ismaʿil b. ʿUmar, Al-Bidāya wa al-nihāya. Beirut: Dar al-Fikr, 1986.
  • Makārim Shīrāzī, Nāṣir, Tafsīr-i nimūna, Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmīyya, 1374 Sh.
  • Mawlawi, Diwān-i Shams-i Tabrīzī.
  • Qurashī, Sayyid ʿAlī Akbar, Qāmūs al-Qurʾ ān. Sixth edition. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, 1371 Sh.
  • Shaykh al-Ṣadūq, Muḥammad b. ʿAlī al-, Kamal al-din wa tamam al-ni'ma. Edited by Ali Akbar Ghaffari. Second edition. Tehran: Dar al-Kutub al-Islamiyah, 1395 AH.
  • Shubbar, Sayyid ʾAbd Allāh, Tafsir al-Qur ʿan al-karīm. First edition, Dar al-Balagha li l-Tiba'a wa al-Nashr, 1412 AH.
  • Ṭabarī, Muḥammad b. Jarīr al-, Jāmiʾ al-bayān fi tafsīr al-Qurʾān. Beirut: Dār al-Maʾrifa, 1412 AH.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥassan al-, Majmaʿ al-bayān fī tafsīr al-Qurʾān. Tehran: Naṣir Khusruw, 1372 Sh.
  • Ṭabrisī, Faḍl b. al-Ḥasan al-, Tafsīr-i jawāmiʾ al-jāmiʾ. 1st Edition. University of Tehran Press and the Centre for the Management of the Islamic Seminaries of Qom, 1377 Sh.
  • Yāqūt al-Ḥamawī. Muʿjam al-buldān, Second edition. Beirut: Dār Ṣādir, 1995.