Lahad

Kutoka wikishia
Picha inayoonyesha Lahad

Lahad (Kiarabu: اللحد) ni kukata na kuchonga ukuta wa Qiblani kiasi cha urefu wake na kwa upana kiasi cha kuweza kukaa maiti. Falsafa ya kuchonga mwanandani ni kuzuia udongo kuufikia mwili.

Mafakihi wa Kiislamu wanasema kuwa, ni mustahabu kuziba mwanandani na Mafakihi wa Kishia wanasema, ili kutilia nguvu hilo (kuziba mwanadani) wameusia kuweka matope na udongo na kusoma dua maalumu wakati wa kuweka mawe. Hata hivyo, kwa mujibu wa fat’wa ya mafakihi wa Madhehebu ya Shia ni kwamba, kama ardhi ni laini, mwanandani hauchimbwi kwenye ukuta; bali unachimbwa chini upande wa Qibla, uchimbwe kiasi cha kuweza kukaa mtu na ubao unamfunika juu.

Utambuzi wa maana

Lahad ni kukata na kuchonga ukuta wa Qiblani kiasi cha urefu wake na kwa upana kiasi cha kuweza kukaa maiti. [1] Dekhoda anaarifisha na kutoa fasili na maana ya Lahad kwa kusema: Ni upenyo kando ya kaburi. Upenyo wa urefu ambao maiti anatosha hapo. [2]

Kitu ambacho ni kigumu, jiwe au mfano wa hicho ambacho kinafunika mwanandani, kinafahamika kwa jina la jiwe la mwanadani. [3]

Hukumu ya kifiq’h

Kwa mujibu wa mafakihi wa Kishia, ni mustahabu kuchimba au kuchonga mwanandani kwa ajili ya kumzika maiti. [4] Kama ardhi ni laini, mwanandani hauchimbwi kwenye ukuta; unachimbwa chini upande wa Qibla, uchimbwe kiasi cha kuweza kukaa mtu na ubao unamfunika juu. [5]

Kwa mujibu wa fiqhi ya Shia, inapendekezwa kufunika mwanandani kwa udongo.[6] Falsafa yake ni kwamba mchanga usimfikie maiti. [7] Inajuzu pia kutumia vitu vingine kama jiwe, mbao na kitu kingine chochote ili kuzuia mchanga usimfikie maiti. [8] Hata hivyo, Muhammad Hasan Najafi (aliyefariki 1266 Hijiria), mwandishi wa kitabu cha Jawahir al-Kalam, anaona ni bora kuziba mwanandanikwa udongo. [9] Kwa mujibu wa riwaya katika Kitabu cha Tahdhib, Imam Ali (a.s) pia aliwausia Hassan na Hussein kufunika mwanandani wake kwa udongo.[10] Kwa mujibu wa hadithi nyingine, Imam Ali (a.s) alifunika mwanandani wa Mtume (s.a.w.w) kwa udongo.. [11] Kwa upande mwingine, kwa mujibu wa Sayyid Muhammad Saeed Hakim (1354 Hijiria) mmoja wa Marajii Taqlidi ni kwamba, kinachopendekezwa na ambacho ni mustahabu ni kuliimarisha kaburi, hata kama halitokani na udongo [12].

Baadhi ya mafakihi wa Kisunni wanaona kuwa ni makuruhu kutumia mbao na tofali la kuchoma kwa ajili ya kuzibia mwanandani. [13]

Adabu

Mafakihi wa Kishia [14] wakitegemea hadithi wamesema [15] ili kuimarisha jiwe la mwanandani wameusia kuweka udongo na kusoma dua maalumu wakati wa kufunika mwanandani. Imeusiwa kusoma dua hii:

اللَّهُمَّ صِلْ وَحْدَتَهُ، وَ آنِسْ وَحْشَتَهُ، وَ أَسْکِنْ إِلَیْهِ مِنْ رَحْمَتِکَ رَحْمَةً تُغْنِیهِ عَنْ رَحْمَةِ مَنْ سِوَاکَ

Mungu! Muokoe kutokana na upweke na uwe mshirika wake katika khofu yake na mpe amani kwa rehema yako ili asihitaji rehema za asiyekuwa wewe.[16]

Kwa mujibu wa Qutb Ravandi, mtaalamu wa hadithi na mwanachuoni wa Kishia wa karne ya 6 Hijiria amenukuliwa akisema: Mashia huanza kupanga mawe ya mwanandani kuanzia kichwani. [17] Kwa mujibu wa Muhammad Hussein Najafi (aliaga dunia 1226 Hijiria), mwandishi wa kitabu cha Jawahir al-Kalam, sababu ya hili ni kwamba kichwa ni muhimu zaidi kuliko viunge vingine vya mwili. [18]

Rejea

Vyanzo

  • Fāḍil Hindī, Muḥammad b. Ḥasan. Kashf al-lithām ʿan qawaʿid al-aḥkām. Edited by Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1383 Sh. Qom: Muʾassisat al-Nashr al-Islāmī, 1416 AH.
  • Ḥakīm, Muḥammad Sa'īd,al-. Miṣbāḥ al-minhāj. [n.p]: [n.n], 1417 AH.
  • Ḥillī, al-Ḥasan b. Yūsuf al-. Muntahā al-maṭlab fī taḥqīq al-madhhab. Introduction by Maḥmūd Bustānī and Ṣafā al-Dīn Baṣarī. Edited by Majmaʾ al-Buhūth al-Islāmiyya, Qism al-Fiqh. Mashhad: Majmaʾ al-Buhūth al-Islāmiyya, 1412 AH.
  • Ibn Zuhra al-Ḥalabī, Ḥamzat b. ʿAlī. Ghunyat al-nuzūʿ ilā ʿilmay al-uṣūl wa al-furūʿ. Qom: Muʾassisat al-Imām al-Ṣādiq, 1417 AH.
  • Ibn al-Barrāj, al-ʿAzīz b. Niḥrir. Al-Muhadhdhab. Introduction by Jaʿfar Subḥānī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1406 AH.
  • Ibn ʿĀbidīn, Muḥammad Amīn b. ʿAbd al-ʿAzīz. Radd al-muḥtār ʿalā al-durr al-mukhtār. Beirut: Dār al-Fikr, 1412 AH.
  • Ibn Qudāma, Muḥammad ʿAbd Allāh b. Aḥmad. Al-Muqnīʿ fiqh al-Imām Aḥmad b. Ḥanbal al-Shaybānī. Edited by Maḥmūd Arnaʾūt and Yāsīn Mahmūd al-Khaṭīb. Jeddah: Maktabat al-Suwādī, 1421 AH.
  • Khomeinī, Sayyid Rūḥ Allāh. Taḥrīr al-wasīla. Tehran: Muʾassisa-yi Tanẓīm wa Nashr-i Āthār-i Imām Khomeinī, 1392 Sh.
  • Kulaynī, Muḥammad b. Yaʿqūb al-. Al-Kāfī. Edited by Dār al-Ḥadīth. Qom: Dār al-Ḥadīth, 1429 AH.
  • Mūsawī ʿĀmilī, Muḥammad b. ʿĀlī. Madārik al-aḥkām fī sharḥ al-mūkhtaṣar sharāyiʿ al-Islām. [n.p]. [n.d].
  • Muḥaqqiq al-Karakī, ʿAlī b. al-Ḥusayn al-. Jāmiʿ al-maqāṣid fī sharh al-qawāʿid. Edited by Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth. Qom: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1414 AH.
  • Mufīd, Muḥammad b. Muḥammad al-. Al-Irshād fī maʿrifat ḥujaj Allāh ʿala l-ʿibād. Edited by Muʾassisat Āl al-Bayt. Qom: Kungira-yi Shaykh al-Mufīd, 1413 AH.
  • Nūrī, Ḥusayn b. Muḥammad Taqī. Mustadrak al-wasāʾil wa musṭanbit al-wasā'il. Edited by Muʾassisat Āl al-Bayt. Beirut: Muʾassisat Āl al-Bayt li-Iḥyāʾ al-Turāth, 1408 AH.
  • Najafī, Muḥammad al-Ḥasan al-. Jawāhir al-kalām fī sharḥ sharāʾiʿ al-Islām. Edited by Ustādī, Riḍā and others. Beirut: Dār Iḥyāʾ al-Turāth al-ʿArabī, [n.d].
  • Shahīd al-Thānī, Zayn al-Dīn b. ʿAlī. Ḥāshiya mukhtaṣar al-nāfiʿ. Edited by Markaz al-Abḥāth wa al-Dirāsāt al-Islāmiyya. Qom: Markaz al-Nashr al-Tābiʿ li-Maktab al-Aʿlām al-Islāmī, 1380 Sh.
  • Ṭabāṭabāʾī Yazdī, Muḥammad Kāẓim al-. Al-ʿUrwat al-wuthqā wa al-taʿliqāt ʿalyhā. Qom: Muʾassisa al-Sibṭayn al-Ālamīyya, 1388 Sh.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Mabsūṭ fī fiqh al-imāmīyya. Edited by Muḥammad Bāqir Bihbūdī and Muḥammad Taqī Kashfī. Third edition. Tehran: al-Maktaba al-Murtaḍawīyya, 1387 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Al-Amālī. Edited by Muʾassisa al-Baʿtha. Qom: Dār al-Thiqāfa, 1414 AH.
  • Ṭūsī, Muḥammad b. al-Ḥasan al-. Tahdhīb al-aḥkām. Edited by Sayyid Ḥasan al-Khirsān. Tehran: Dār al-Kutub al-Islāmiyya, 1407 AH.