Kumi la Safar
Kumi la mwisho la mwezi Safar (Kiarabu: عشرة صفر) (Mfunguo tano) ni siku kumi za kuanzia tarehe 20 hadi mwisho wa mwezi. Arubaini ya mashahidi wa Karbala, hauli (kumbukumbu) ya Mtume (s.a.w.w), kumbukizi ya kuuawa shahidi Imamu Hassan al-Mujtaba (a.s) na Imamu Ali bin Mussa al-Ridha (a.s) ni matukio ambayo yaliyokea katika kumi hili la Safar. Katika kipindi hiki, Waislamu wa madhehebu ya Shia hufanya maombolezo.
Tarehe 20 Safar (Mfunguo Tano) inasadifiana na kumbukumbu ya Arubaini ya Imamu Hussein (a.s) na mashahidi wengine wa tukio la Karbala [1] Kadhalika tarehe 28 Safar, ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Bwana Mtume (s.a.w.w), kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imamu Hassan al-Mujtaba (a.s) [3] na siku ya mwisho wa mwezi huu (Safar) ni siku ya kumbukumbu ya kuuawa shahidi Imamu Ali bin Mussa al-Ridha (a.s). [4]
Siku ya kwanza ya kumi la mwisho la mwezi Safar (tarehe 20 Safar) ni mashuhuri kwa siku ya Arubaini. [5] Katika hadithi zilizopokewa na Waislamu wa madhehebu ya Shia, imeusiwa kusoma Ziyarat Arubain katika siku hii. [6] Kwa mnasaba huu hufanyika matembezi ya Arubaini na Waislamu wa madhehebu ya Shia kutoka katika maeneo mbalimbali huelekea Karbala kwa ajili ya kufanya ziara katika Haram ya Imamu Hussein (a.s) [7]
Nchini Iran, kumi la mwisho la Safar kama lilivyo kumi la mwisho la Muharram ni siku ambazo hufanyika hafla mbalimbali za maombolezo ya Muharram.
Rejea
Vyanzo