Nenda kwa yaliyomo

Kumait bin Zaid al-Asadi

Kutoka wikishia

Kumait bin Zaid Al-Asadi Taarifa Zake Jina Kamili Abū Mustajil Kumait bin Zayd Al-Asadi Harakati Zake Ushairi wa kuwasifu Ahlul Bait (a.s) Mahali alipoishi Iraq Mahali alipozikwa Kufa, Mava ya Bani Asadi Aliyeishi naye Imamu Sajjad (a.s), Imamu Baqir (a.s) na Imamu Sadiq (a.s) Madhehebu Shia Diwani ya Mashairi Mkusanyiko wa mashairi Sababu ya Umaarufu Mshairi wa kusifu Ahlul Bayt (a.s) Kumait bin Zaid al-Asadi (aliyeishi baia ya mwaka 60 na 126 Hijria): alikuwa ni mshairi mashuhuri wa Kiarabu na mfuasi wa madhehebu ya Shia. Yeye ni miongoni wailiobahatika kuishi enzi moja na Imam Sajjād, Imam Bāqir, na Imam Sādiq (s.a). Miongoni mwa kazi zake andishi mashuhuri, ni diwani ya mashairi inayojulikana kwa jina la “Al-Hāshimiyyāt”, ambayo ilihusiana na mada nyeti na zenye umuhimu mno, kama vile fadhila (sifa) za ukoo wa Bani Hāshim, tukio la Ghadīr, kuuawa kwa Imamu Ḥussein (a.s), pamoja na masuala yanayohusiana na utawala wa Bani Umayya na athari zake kwa jamii ya Kiislamu. Mashairi haya yalitungwa kati ya mwaka w 15 hadi 20 baada ya tukio la mauaji ya kikatiki ya Karbala. Kumait alipata heshima kubwa mbele ya Imamu Sajjād na Imamu Bāqir (a.s), ambao ni Maimamu wa nne na wa tano wa madhehebu ya Shia, heshima hii ilitokana na mashairi yake yenye mwelekeo wa kiitikadi. Pia kuna masimulizi ya Riwaya fulani yanayosema kwamba; Maimamu hao walimuombea dua kwa juhudi za mchango wake katika kujenga hamasa za kidini. Hata hivyo, inadaiwa kwamba, ili kujilinda dhidi ya madhara ya watawala dhalimu wa wakati huo, aliwahi pia kuandika kutunga mashairi ya kuwasifu Bani Umayya. Nafasi na Umuhimu wa Kumait bin Zaid Al-Asadi Abu Mustahal Kumait bin Zaid al-Asadi, kama alivyoelezwa na Abu al-Faraj al-Isfahani, alikuwa mshairi mahiri wa Kiarabu, mtaalamu wa lugha na msamiati wa Kiarabu, na mwenye maarifa makubwa kuhusiana na historia ya Waarabu. Aidha, alikuwa ni mkiritimba na mwenye kufadhilisha kabila la Bani Mudhirr juu ya kabila la Waqahtan. Kumait bin Zaid al-Asadi al-Adnān, alipambanuka kwa ustadi wake katika mashindano yake ya ushairi dhidi ya washairi wengine mashuhuri wa zama zake. [1] Mashairi yake yaliyomo katika diwani iitwayo Al-Hāshimiyyāt, yanachukuliwa kuwa ni miongoni mwa kazi bora zaidi alizozitunga maishani mwake, yakibeba maudhui yenye uzito wa kihistoria, kiitikadi, na kisiasa. [2] Inasimuliwa kuwa aliandika zaidi ya beti elfu tano za mashairi, [3] ingawa sehemu kubwa ya kazi zake zimepotea na hazipatikani tena katika maandiko yaliyohifadhiwa ndani ya maktaba mbali mbali. [4] Kama ilivyoelezwa hapo mwanzo kwamba; Kumait bin Zaid al-Asadi al-Adnān, alikuwa na upendeleo mkubwa kwa kabila la Bani Mudhirr ukoo wake wa Adnān katika mashairi yake, ambapo mara kwa mara alionekana kuwashambulia washairi wa makabila mengine Yemen (Waqahtan), mtindo ambao aliendelea nao katika maisha yake yote. [5] Hata hivyo, kwa mujibu wa maelezo ya Abu al-Faraj al-Isfahani, anayenukuu vyanzo vya kihistoria, ni kwamba; sababu hasa ya Kumait kuyahambulia makabila mengine ya watu wa Yemen haikuwa ikitokana na chuki ya kikabila, bali ni mwitikio kwa mshairi wa Yemen, aitwaye Hakim bin Ayāsh al-Kalbī, ambaye alikuwa ni wa karibu wa Bani Umayya, aliyemdhihaki Imamu Ali bin Abi Tālib (a.s) na ukoo wa Banu Hāshim. [6] Kwa hivyo, ili kuepuka lawama na ghadhabu kutoka kwa utawala wa Bani Umayya, badala ya kuwatetea moja kwa moja Imamu Ali (a.s) na Banu Hāshim, Kumait alichagua kuonyesha hasira zake na kumjibu mshairi huyo, kwa kuwashambulia watu wa Yemen kwa njia ya kifasihi. [6] Mkakati huo ulimwezesha kufanikisha azma yake ya kujibu mashambulizi dhidi ya Ahlul Bait bila kusababisha madhara ya moja kwa moja kutoka kwa watawala wa wakati huo. [7] Kumait bin Zaid bin Khunais bin Mukhalid al-Asadi alizaliwa mwaka wa 60 Hijria. [8] Naye alikuwa ni mpwa wa Farazdaq, ambaye ni mshairi mashuhuri wa enzi za utawala wa Bani Umayya. Kumait aliishi zama moja na Sayyid Himyari, mshairi maarufu na mmoja wa wafuasi wakuu wa madhehebu ya Shia. [9] Kumait alifariki dunia akiwa katika mji wa Kufa, mnamo mwaka wa 126 Hijria, katika zama za ukhalifa wa Marwān bin Muhammad, ambaye alikuwa ni khalifa wa mwisho wa nasaba ya Bani Umayya. [10] Inasemekana kuwa yeye ndiye alikuwa mtu wa kwanza kuzikwa katika makaburi (mava) ya Bani Asad. [11]

Uhusiano wa Kumait bin Zaid na Ahl al-Bait (A.S) Kwa mujibu wa Riwaya mbalimbali, Kumait bin Zaid al-Asadi, alikuwa ni mshairi mashuhuri aliyetumia fani yake ya ushairi katika kuwasifu Ahl al-Bait (Watu wa Nyumba ya Mtume), katika enzi za utawala wa Bani Umayya, jambo lililomfanya kupata heshima kubwa kutoka kwa Imamu Sajjād, Imamu Bāqir, na Imam Sādiq (a.s). Kuna masimulizi ya Riwaya fulani yanayoeleza kuwa Maimamu hawa walimuombea dua kutokana na ujasiri wake wa kuwatetea na kuwaenzi kupitia mashairi yake. [12] Aidha, inasemekana kwamba; Kumait hakupokea zawadi yoyote ile kidunia kwa mashairi yake ya kuwasifu Ahl al-Bayt (a.s). Badala yake, alikuwa akihimidiwa kwa msimamo wake wa kiitikadi, na wakati mwingine aliomba tu mavazi kwa nia kupata baraka, kutoka kwa Imamu Sajjād au Imam Bāqir, akiamini kuwa mavazi ya Maimamu ni yenye baraka na neema kubwa kwake yeye. [13]

Mashairi ya al-Hāshimiyyāt Mashairi ya al-Hāshimiyyāt, yaliyotungwa na Kumait bin Zaid al-Asadi kuanzia mwaka wa 15 hadi wa 20 baada ya tukio la Karbala, yanachukuliwa kuwa ni miongoni mwa kazi zake mashuhuri na zenye athari kubwa katika historia ya ushairi wa Kiislamu. [14] Mashairi haya yamekusanywa katika kasida nane, yakibeba maudhui ya kiitikadi, kihistoria, na kisiasa yanayohusiana na Ahl al-Bayt (Watu wa Nyumba ya Mtume). Ndani ya al-Hāshimiyyāt, Kumait alieleza kwa ustadi wa kishairi fadhila za ukoo wa Banu Hāshim na Ahl al-Bait (a.s). Pia katika maishiri haya alisimulia tukio mengine kadhaa, kama vile; tukio la Ghadīr Khum na madai ya haki ya Imamu Ali (a.s.) ktika sulala la ukhalifa, mauaji ya Imamu Ḥussein (a.s) na ukatili wa watawala wa Bani Umayya, pamoja na mateso waliyoyapata Ahl al-Bait (a.s) na wafuasi wao. Aidha, mashairi haya yanazungumzia mauaji ya Zaid bin Ali, mjukuu wa Imamu Ḥusein (a.s), na madhila yaliyowakumba watu wa ukoo wa Hāshim chini ya utawala dhalimu wa Bani Umayya. [15] Hata hivyo, inasimuliwa kuwa ili kulinda maisha yake kutokana na ghadhabu za watawala wa Bani Umayya, Kumait alitunga baadhi ya mashairi ya kuwasifu kuhusika wa nasaba hiyo. Inadaiwa kuwa kabla ya kufanya hivyo, alipata ruhusa kutoka kwa Imamu Bāqir (a.s). [16] Mfano wa Mashairi ya Al-Hāshimiyyāt kwa lugha ya Kiarabu: وَ مِنْ أکْبَرِ الأحداثِ کانَتْ مُصیبَهً عَلَیْنا قتیلُ الَأدعیاءِ المُلَحَّبُ قتیلٌ بِجَنْبِ الطَّفِّ مِنْ آلِ هاشمٍ فیالک لحماً لَیْسَ عَنْه مُذَبِّبُ و مُنْعَفِر الخَدَّیْنِ مِنْ آل هاشم أَلا حَبَّذَا ذاكَ الجبینُ المترَّبُ[17] Tafsiri yake Kwa Kiswahili Adhimu kweli adhimu msiba leo tufikia * wanaharamu hasimu mwiliwe kuurarua Pembeni mto furati mwana Hashimu kauliwa * Damu ya muadhamu hiana wa kutetea Vumbi mashavuye pakazwa mwana wa Hasimia * Mtukufu ulioje uso dongo lobobea [18]