Kukusanya baina ya Sala mbili

Kutoka wikishia

Kukusanya Baina ya Swala Mbili (Kiarabu: الجمع بين الصلاتين) maana yake ni kuswali Swala za Adhuhuri na Alasiri na swala za Magharibi na Isha kwa pamoja katika wakati wa kushirikiana. Ili kujuzisha kukusanya baina ya Swala mbili kumetumiwa kama hoja Sunna za Bwana Mtume (s.a.w.w) na sira ya Maimamu (a.s). Maulamaa wa Ahlu-Sunna wao hawaamini kuhusiana na wakati wa kushirikiana wa Swala mbili, kwa msingi huo wanaona inajuzu kukusanya baina ya Swala mbili katika mazingira maalumu tu kama ya kuwa safarini au ugonjwa.

Kumeandikwa vitabu mbalimbali kuhusiana na maudhui ya kukusanya baina ya Swala mbili ambapo kitabu cha: Al-Jam’u baina al-Salatayn Alaa Dhaui al-Kitab wal-Sunna kilichoandikwa na Ja’afar Sobhani ni miongoni mwa vitabu hivyo.

Utambulisho

Kukusanya baina ya Swala mbili ni istilahi ya kifikihi ambayo inaashiria suala la kuswali kwa pamoja Swala za Adhuhuri na Alasiri na vilevile Magharibi na Isha kwa pamoja wakati wowote katika wakati wa kushirikiana. Hii ni kwa mujibu wa madhehebu ya Shia[1], na kwa mujibu wa madhehebu ya Ahlu-Sunna kila Swala ina wakati wake makhsusi.[2] Kikawaida Mashia huswali kwa pamoja Swala za Adhuhuri na Alasiri kama ambavyo huswali kwa pamoja (kwa kukusanya) Swala za Magharibi na Isha. Lakini Waislamu wa Kisunni wao huswali Swala moja moja bila kukusanya.[3]

Katika vitabu vya fikihi suala la kukusanya baina ya Swala mbili hujadiliwa katika mlango wa nyakati za Swala.[4] Kadhalika katika milango ya tohara[5] na Hija pia hili limezungumziwa.

Hoja ya Kisheria

Kwa mujibu wa Shahid al-Awwal ni kuwa, kwa mtazamo wa mafakihi wa Kishia inajuzu kukusanya baina ya Sala mbili.[6] Kwani kwa mujibu wa hadithi, Mtume (s.a.w.w)[7] na Maimamu Maasumina (a.s)[8] waliswali Sala za kila siku kwa kukusanya na kwa kutenganisha katika mazingira na hali ya kawaida na isiyo ya kawaida (kama vita, woga safari, mvua na kadhalika). Mtume (s.a.w.w) amebainisha kuwa, sababu ya kukusanya Sala mbili katika mazingira ya kawaida ni kuzuia na kuondoa ugumu na taabu kwa umma wake.[9] Hata hivyo, mafakihi wa Kishia wanasema kuwa, hatua ya Mtume ya kuswali Swala mbili kwa kutenganisha ilitokana na hilo kuwa mustahabu[10], na vilevile kuweko kwa wakati wa kushirikiana.[11]

Akthari wa mafakihi wa Ahlu-Sunna wanaona kuwa, haijuzu kukusanya baina ya Sala mbili katika mazingira ya kawaida[12] na wanaona hilo linajuzu tu katika mazingira maalumu na yasiyo ya kawaida kama kuweko udhuru kama wa safari, maradhi, mvua na kadhalika.[13] Kadhalika wanaamini kuwa, hadithi kuhusu sunna ya Mtume ya kukusanya baina ya Sala mbili katika mazingira ya kawaida kwa mtazamo wao zinafanyiwa taawili katika mazingira ya udhuru.[14] Hata hivyo mafakihi wa madhehebu zote za Kiislamu wanasema kuwa, inajuzu kukusanya baina ya Sala mbili za Adhuhuri na Alasiri katika masiku ya ibada ya Hija katika viwanja vya Arafa na kukusanya Swala za Magharibi na Isha huko Muzdalifa.[15] Ijapokuwa Muhammad bin Idris Shafii, tofauti na mafaqihi wengine wanne wa Kisunni wanaoichukulia Hija na Umra kuwa ndio sababu ya kuruhusiwa kukusanya baina ya Swala mbili, katika hali hii, yeye anaona safari kuwa ndiyo sababu ya kuruhusiwa kukusanya baina ya Swala mbili.[16]

Sababu ya Tofauti Baina ya Mtazamo wa Shia na Sunni

Kuwa tofauti mtazamo wa Shia na Ahlu-Sunna ni kwa sababu ya kuweko tofauti ya kimtazamo baina yao kuhusiana na wakati wa Swala za kila siku.[17]Kwa mujibu wa Aya isemayo:

أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا
Simamisha Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur'an ya alfajiri, hakika Qur'an ya alfajiri inashuhudiwa daima[18]

wanazuoni wa Kishia wanaamini kupitia Aya hiyo juu ya suala la kuweko wakati wa kushirikiana, wakati wa fadhila na wakati makhususi kwa ajili ya Swala za Adhuhuri na Alasiri na vilevile Magharibi na Isha.[19] Lakini wanazuoni wa Kisunni wao wanaamini kwamba, kila Swala ina wakati wake makhsusi,[20] na hawakubaliana na suala la kuweko wakati wa kushirikiana kwa Swala za kila siku.[21] Kwa muktadha huo wanaamini kwamba, endapo mtu ataswali kwa kukusanya baina ya Swala mbili, moja ya kati ya Sala mbili hizo itakuwa imeswaliwa nje ya wakati wake na kuswaliwa katika wakati mwingine ambao sio wake. Hii ni katika hali ambayo, kwa mujibu wa mafakihi wa Kishia, haijuzu kuswali Swala fulani katika wakati makhususi wa Swala nyingine na inajuzu kuswali Swala fulani katika wakati wa kushirikiana na katika wakati wa fadhila.[22] Baadhi ya wafasiri wa Ahlu-Sunna wanatambua nyakati tatu za (Asubuhi, Adhuhuri na Usiku) kuwa ni thabiti kwa ajili ya Swala za wajibu za kila siku.[23]

Bibliografia

Kumeandikwa vitabu mbalimbali kwa lugha za Kiarabu na Kifarsi kuhusiana na kukusanya pamoja baina ya Swala mbili na miongoni mwa vitabu hivyo ni kitabu cha: Al-Jam’u baina al-Salatayn Alaa Dhaui al-Kitab wal-Sunna kilichoandikwa na Ja’afar Sobhani, mmoja wa Marajii Taqlidi wa Kishia ambacho kilichapishwa na kusambazwa 1388 Hijria Shamsia na Taasisi ya Imam Swadiq (as) [24]. Katika kitabu hiki kumetajwa Aya na hadithi ambazo zinaeleza na kubainisha suala la kujuzu kukusanya baina ya Swala mbili.

Miongoni mwa Vitabu Vingine ni:

  • Al-Jam’u baina al-Salataynn” kilichoandikwa na Abdul-Latif Baghdadi.
  • Al-Jam' bayn al-Salatayn fi al-Safar, mwandishi: Muqbil Wada'i.
  • Jam' bayn al-Salatayn va hudud-i an, kilichoandikwa na: Sayyid Muhammad Reza Mudarrisi.
  • Al-Jam' bayn al-Salatayn, kilichoandikwa na: Najm al-Din 'Askari.

Rejea

  1. Tazama: Subhani, ((Jamu'u miyan do namaz az dideghah kitabu wa sunna)), uk. 66.
  2. Jaziri, Fiqh Alal-madhahib al-Arba, 1424 H, juz. 1, uk. 438.
  3. Subhani, ((Jamu'u miyan do namaz az dideghah kitabu wa sunna)), uk. 45.
  4. Ibn Idris Hilli, Asarair, 1410 H, juz. 1, uk. 198.
  5. Sheikh Ansari, Kitab al-Tahara, 1415 H, juz. 4, uk.70.
  6. Shahidu Awal, Dhikr al-Shia, 1419 H, juz. 2, uk. 331.
  7. Sadouq, Ilal as-sharaih, 1385 S, JUZ. 2, uk. 322; Bukhari, Sahih Bukhari, 1401 H, juz. 1, uk. 138; Muslim, Sahih Muslim, 1374 H, juz. 1, uk. 489, H. 705.
  8. Kuleini, al-Kafi, 1407 H, juz. 3, uk. 286-287.
  9. Sheikh Sadouq, Ilal as-sharaih, 1385 H, juz. 2, uk. 322; Muslim, Sahih Muslim, 1374 H, juz. 1, Babu al-jamu'u baina Swalatein fil-Hadhar, uk. 490, H: 705.
  10. Shahid Awali, Dhikr al-shia, 1419 H, juz. 2, uk. 335
  11. Ibn Idris Hilli, Asarair, 1410 H, juz. 1, uk. 198.
  12. Sarkhisi, Al-Mabsuut, 1414 H, juz. 1, uk. 149.
  13. Tazama: Nawawi, Sherh bar Sahih Muslim, 1392 H, juz. 5, uk. 218, h: 212.
  14. Tazama: Nawawi, Sherh bar Sahih Muslim, 1392 H, juz. 5, uk. 218.
  15. Mousavi, Jam kati ya sala mbili, 2014, p. 34; Subhani, Aqidatu al-islamiya ala dhwaui madrasatu Ahl al-Bayt, 1419 H, juz. 1, uk. 340.
  16. Jaziri, Fiqh Alal-Madhahib al-Arba, 1424 H, juz. 1, uk. 419.
  17. Tazama: Shahid Awal,dhikr al-Shia, 1419 H, juz. 2, uk. 336.
  18. Surat al-Israa, aya: 78
  19. Subhani, Al-Insaf, 1381 S, juz. 1, uk. 291.
  20. Sarkhisi, Al-Mabsuut, 1414 H, juz. 1, uk. 149.
  21. Tazama: Shahid Awal, dhikr al-Shia, 1419 H, juz. 2, uk. 323.
  22. Subhani, “Jamu'u miyan do namaz az didegh kitab wa sunnah”, uk. 67.
  23. Tazama: Alousi, Ruh al-Ma'ani, 1415 H, juz. 8, uk. 127.

Vyanzo

  • Ālūsī, Maḥmūd b. ʿAbd Allāh al-. Rūḥ al-maʿānī fī tafsīr al-Qurʾān al-ʿaẓīm. Edited by ʿAlī ʿAbd al-Bārī al-ʿAṭiyya. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1415 AH.
  • Ḥillī, Ibn Idrīs al-. Kitāb al-sarāʾir al-ḥāwī li taḥrīr al-fatāwī. Qom: Daftar-i Intishārāt-i Islāmī affiliated to Jāmiʿa-yi Mudarrisīn-i Ḥawza-yi ʿIlmīyya-yi Qom, 1410 AH.
  • Bukhārī, Muḥammad b. Ismāʿīl al-. Ṣaḥīḥ al-Bukhārī. Beirut: Dār al-Fikr li-Ṭibāʿat wa al-Nashr wa al-Tawzīʿ, 1419 AH.
  • Jazīrī, ʿAbd al-Raḥmān. Al-Fiqh ʿalā al-madhāhib al-arbaʿa. Beirut: Dār al-Kutub al-ʿIlmiyya, 1424 AH.
  • Subḥānī, Jaʿfar. Al-Inṣāf fī masāʾil dāma fīhā al-khilāf. Qom: Muʾassisa Muʾassisa Imām Ṣādiq, 1381 Sh.
  • Subḥānī, Jaʿfar, Jamʿ bein-i du namāz az dīdgāh-i kitāb wa sunnat (Performing two prayers together on the light of Qur'an and Sunna). Faṣlnāma-yi Fiqh-i Ahl al-Bayt, No 45, Spring 1385 Sh.