Nenda kwa yaliyomo

Kujifananisha na makafiri

Kutoka wikishia

Kujifananisha na Makafiri (Kiarabu: التشبُّه بالكُفّار) ni kitendo cha Waislamu kuiga desturi au mitindo ya maisha ya makafiri katika masuala ya kibinafsi au kijamii. Baadhi ya wanazuoni wa fiq’hi wameharamisha aina fulani za uigaji wa mitindo hiyo. Hata hivyo, kuiga makafiri katika masuala ya kielimu na viwanda hakuchukuliwi kuwa ni kujifananisha nao. Wengine wanaona kwamba hukumu ya kutojifananisha na makafiri imeegemea kwenye kanuni ya kifiq’hi inayotumika kufafanua hukumu za masuala mbalimbali ya kijamii na kitamaduni, na kuainisha yale yanayokatazwa na yanayo juzishwa miongoni mwa yale wanayoshikamana nayo makafiri.

Kuna maoni tofauti miongoni wanazuoni wa fiq’hi, kuhusiana na hukumu za kisheria juu ya kujifananisha na makafiri. Maoni haya ni pamoja na: uharamu wa moja kwa moja, makruhu (haipendekezwi) ya moja kwa moja, na uharamu katika masharti na mipaka maalum. Wanazuoni wa KiShia kwa kiasi kikubwa wanakubaliana na nadharia ya uharamu kujifananisha na makafiri kwa mipaka maalum. Inagwaje wanazuoni hawa wanakubaliana na ushahidi wa Qur’ani, Hadithi, na mantiki kuhusiana na uharamu wa kujifananisha na makafiri, lakini hawakubaliani ueneaji wa uharamu huo katika nyanja zote bila ya kuwepo mipaka maalumu.

Kuna dalili nne zililizo tumika ili kuthibitisha hukumu ya uharamu wa kujifananisha na makafiri. Miongoni mwa ithibati zinazotumika kuthibilisha hilo, ni kitabu cha Mwenye Ezi Mungu. Katika Qur’ani, kuna makundi matatu ya Aya, zinazoweza kutumika kama ithibati ya uharamu huo: Aya zinazopiga marufuku kujifananisha na makafiri kwa mfumo wa kijumla jamala (bila ya kuweka mipaka maalumu), Aya zinazo watahadharisha Waislamu dhidi ya kuwa chini ya utawala wa makafiri au kufanya urafiki nao, na Aya zinazopiga marufuku kujifananisha na makafiki katika nyanja maalum. Zaidi ya hayo, baadhi ya Hadithi zinakataza kujifananisha na makafiri kwa jumla lamala (bila ya kuweka mipaka maalumu), huku nyingine zikihusiana na kujifananisha na makafiri katika masuala maalum. Kwa upande wa kimantiki, kujifananisha na makafiri kunapelekea kuimarika kwa madaraka yao juu ya Waislamu katika nyanja za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, na kitamaduni, hivyo ni jambo linalopigwa marufuku.

Muktadha wa Kujifananisha na Makafiri na Umuhimu wa Kujadili Suala Hili

Kujifananisha na makafiri kunahusisha kufuata mitindo ya maisha ya makafiri katika nyanja mbalimbali za maisha, iwe ni maisha binafsi au maisha ya kijamii. [1] Kulingana maoni ya sheria za kiislamu, kujifananisha na makafiri ni jambo linalochukiza na lisolopendeza mbele ya sheria za Kiisamu, wala hakuna tofauti za maoni kati ya wanazuoni wa Shia na Sunni kuhusiana na ubaya wa suala hili. [2] Hata hivyo, kuna utofauti wa maoni kuhusiana na hukumu andamizi au tendaji (hukmu takliifi) za kisheria juu ya suala hili, pamoja na vipengele vyengine, kama elimu na nia katika kutekeleza hukumu hiyo. Kwa lugha nyengine ni kwamba je, mtu atakaye tenda sawa na makafiri bila yeye kuwa na elimu ya suala hili atakuwa amefanya haramu? Au iwapo mtu atatenda sawa matendo ya makafiri, bila yeye mwenyewe kuwa na nia ya kujishabihisha na makafiri, je, atakuwa amefanya dhambi? [3]

Imeelezwa na wanazuoni ya kwamba; kujifananisha na makafiri si suala linalohusiana na masuala ya kifiq’hi moja kwa moja, bali linahusiana na moja kanuni (kaida) ya kifiq’hi (kaida andamizi) inayotumika katika kuangaza hukumu za masuala mbalimbali katika nyanja tofauti za kifiq’hi kulingana na miktadha yake ilivyo. [4]

Wanazuoni wa upande wa madhehebu ya Shia Imamiyyah wamejadili zaidi suala hili la kujifananisha na makafiri katika muktadha unaohusia na masuala ya ibada, kama vile; mavazi ya waumini wakati wa sala, vitu vinavyo batilisha sala, na kutufu (kuzunguka Kaaba). Wanazuoni hawa hawakupanua tafiti zao katika maeneo mengine ya maisha ya kibinafsi na ya kijamii ya Muislamu. Wala suala hili halikuonekana kupewa kipau kipaumbele katika tafiti zao mbai mbali. [5]

Hukumu za Kisheria Juu ya Kujifananisha na Makafiri

Hukumu za kisheria kuhusu kujifananisha na makafiri zimetanda kwa namna mbalimbali miongoni mwa Waislamu wa Kishia na kisunni, ikianzia kwenye uharamu kamili (bila mipaka) hadi umakruhu kamili (bila mipaka):

Marufuku Kamili: Huu ndiyo mtazamo maarufu miongoni mwa wanazuoni wa Kisunni na baadhi ya wanazuoni wa Kishia. [7] Kwa mtazamo huu, ni haramu kwa Muislamu kujifananisha na wasiokuwa Waislamu —iwe ni makafiri, washirikina, Ahlul-Kitabu au hata Wamagharibi— bila kuwa na tofauti kati ya kujifananisha nao katika mtindo wa maisha kibinafsi au maisha ya kijamii. [8] Wafuasi wa mtazamo huu wanaamini kwamba; hakuna tofauti ya kwamba kitendo chenyewe ni halali au haramu, wala kujali dhamira ya mtu anayefanya kitendo hicho, au kwamba kitendo hicho ni mtu cha binafsi cha serikali ya Kiislamu. [9]

Makruhu Kamili (bila masharti au mipaka maalumu): Huu ni mtazamo wa baadhi ya Waislamu wa madhebu ya Kishafi'i [10] na baadhi ya wanazuoni wa Kishia, akiwemo Sheikh Mufidu, [11] Muhaqiq Hilli, [12] Allama Hilli [13] na Sheikh Bahai. [14] Kwa mtazamo wa wanazuoni hawa, ni kwamba; ni makruhu mtu kutenda matendo sawa na yale ya wasiokuwa Waislamu, [15] iwe ni kwa dhamira ya kujifananisha au kutokujifananisha na wasiokuwa Waislamu. [16]

Marufuku (haramu) yenye Masharti na mipaka maalumu: Wafuasi wa mtazamo huu, wengi wao ni wanazuoni wa madhehebu ya Shia. [17] Wanazuoni hawa wanakubaliana na vielelezo vyote vya Qur'ani, Hadithi, na mantiki, ambavyo hutumika katika kuthibitisha ubaya wa kujifananisha na makafiri, ila hawakubali upana na uenevu wa hukumu zilizomo ndani ya vielelezo hivi, bila kujali mipaka maalumu. [18] Kwa mtazamo wa wanazuoni hawa, ni kwamba; ni kuwepo masharti fulani, ili tendo fulani liingie katika mlolongo wa matendo ya kujifananisha na makafiri. Masharti hayo ni kama ifuatvyo: [19]

  • Kujifananisha na makafiri kwa nia ya kukuza mtindo wa maisha wa makafiri, kuthibitisha ubora wao, na kudhoofisha Uislamu. [20]
  • Kujifananisha katika mtindo wa maisha na tabia maalum za makafiri (kama vile kutumia msalaba), na si katika mambo yanayoshirikisha pande zote mbili kati ya makafiri na Waislamu. [21]

Misingi ya Kujifananisha na Makafiri

Mjadala wa kujifananisha na makafiri katika sheria za Kiislamu umechambuliwa katika nyanja mbili kuu, nazo ni kama ifuatavyo: [22]

Ibada: Nalo ni suala linahusina hali ya mtu kumwabudu Mwenye Ezi Mungu kwa njia inayofanana na taratibu au mavazi ya makafiri. [23] Pia kuna Hadithi zitokazo kwa Imamu Ali [24] na Imamu Baqir (a.s), [25] zinazo kataza kufanya vitendo vinavyofanana na mila za Wamajusi wakati wa sala.

Kujifananisha na Makafiri Katika Mtindo wa Maisha: Mjadala wa kujifananisha na makafiri katika mtindo wa maisha umezingatiwa katika maeneo matatu makuu; [26] Mavazi: Hili linahusiana na kufuata mavazi yanayofanana na ya makafiri. Kwa mfano, katika Hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s), waumini wametakiwa kuepuka kuvaa mavazi ya maadui wa Mwenye Ezi Mungu. [27] Kutokana na hilo, imekatazwa kuvaa baadhi ya mavazi yenye mapambo ya Kimagharibi, kama vile tai. [28]

Kujifananisha na Makafiri Katika mapambo (mitindo); Waislamu wanahimizwa kujiepusha na mitindo ya inayotokana na makafiri. Kwa mfano, bwana Mtume (s.a.w.w) aliwakataza wanaume wa Kiislamu kujifananisha na Wamajusi kwa kunyoa ndevu huku na kuacha masharubu makubwa. [29] Kujifananisha na Makafiri Katika desturi na mila; Hii inahusiana na kuiga desturi na kimila za makafiri. Kwa mfano, Imam Sadiq (a.s) aliwakataza Waislamu kula chakula kwenye nyumba za wafiwa, desturi ambayo ilikuwa ni ya kawaida kwa washirikina wa zama za ujahilia. Hivyo basi, pia Waislamu wanakatazwa kushiriki baadhi ya desturi za Kimagharibi, kama vile; kuadhimisha mwaka mpya [31] au Siku ya Wapendanao (Valentine’s Day). [32] Inasemekana kwamba; kutokana na ufinyu wa mada zilizotajwa katika vyanzo vya kidini kuhusiana na kujifananisha na makafiri, haiwezekani kupiga marufuku kufuata makafiri katika masuala ya sayansi na viwanda. [33]

Vigezo Aishi vya Kutambua Mifano Hai ya Kujifananisha na Makafiri

Kutambua na kukihukumu kitendo fulani kuwa ni kitendo cha kujifananisha na makafiri, kunategemea mila na desturi za jamii husika. Kwa hivyo, kitendo fulani kinaweza kuwa cha kitendo cha desturi za wasio Waislamu peke yao, ila kijamii kitendo hicho hakitambuliki moja kwa moja kama ni kitendo cha kujifananisha na makafiri. [34] Kwa mfano, ingawa sherehe za Nowruz (Mwaka Kogwa) zinahusiana na mila za Wazoroastria (Wamajusi), ila hakuna faqihi yeyote wa Kishia aliyewahi kusema kwamba kusherehekea Nowruz ni kujifananisha na makafiri. [35] Hata hivyo, hapo awali kunyoa ndevu, kuvaa tai, na kutumia kipaza sauti katika minasaba fulani ya kidini, vilionekana kama ni mifano ya kujifananisha na makafiri. [36] Ila wanazuoni wa sheria wamebaini kwamba; baadhi ya vitendo vilivyokuwa vikichukuliwa kama kujifananisha na makafiri hapo awali, baada ya kupita muda fulani, vimekuwa ni vyenye kukubalika ndani ya kijamii, nahatimae kuonekana kama vitendo vya kawaida vifanywavyo na Waislamu na wasio Waislamu. [37]

Nyaraka na Ithibati za Hukumu Juu za Kujifananisha na Makafiri

Katika kujadili suala la kujifananisha na makafiri, wanazuoni wa Kiislamu wamezingatia dalili nne kuu (Adillatu Arbaʿa), ambazo ni: Qur’an, Hadithi, Ijma (makubaliano ya wanazuoni), na Akili (mantiki). [38]

Qur’an na Hadithi

Kuna makundi matatu ya Aya za Qur’an zinazotumiwa kama msingi wa hukumu dhidi ya kujifananisha na makafiri:[39]

Hadithi Zinazohusiana na Kujifananisha na Makafiri:Hadithi zinazohusiana na suala la kujifananisha na makafiri zimeainishwa katika makundi mawili: Hadithi za jumla na Hadithi makhususi: [43]Hadithi za Jumla: Hadithi hizi ni zile zinatoa mwongozo wa jumla kuhusiana na kujifananisha na makafiri. Miongoni mwa Hadithi hizi ni zile Hadithi kutoka kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) [44] na Imam Ali (a.s) [45] ambazo zinaeleza kwamba; kila anayejifananisha na kundi fulani, huhisabiwa ni miongoni mwa kundi hilo. Hadithi Makhususi: Hizi ni zile Hadithi zinazozungumzia hali mbali mbali kuhusiana na maisha, kuanzia masuala ya ibada hadi maadili binafsi na maadili ya kijamii. Mfano wake ni: Hadithi kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) inayosema kwamba, yapaswa Waislamu kufyagia uwanja wa nyumba zao, ili kuepukana na kujifananisha Wayahudi. [46]

Ithibati Nyengine za Kisheria

Miongoni mwa Waislamu wa madhehebu ya Sunni, Ibn Taymiyyah (aliyefariki mwaka 728 H) amedai kwamba kuna ijmaa (consense) juu ya marufuku ya kujifananisha na makafiri. [47] Kwa upande wa hoja za kiakili, sababu zifuatazo zimeelezwa ili kutetea mtazamo huu:

  • Kujifananisha na makafiri kunaweza kuimarisha utawala wao juu ya Waislamu: Kwa mfano, hii inaweza kujumuisha nyanja za kisiasa, kijeshi, kiuchumi, na kitamaduni, na hivyo kuongeza ushawishi wao. [48]
  • Waislamu mara nyingi wamekuwa wakikumbana na madhara kutoka kwa adui zao: Kutojifananisha na makafiri ni njia ya kupinga athari zao na kuweka msimamo wa kinyume na wao, hivyo kulinda utambulisho wa Kiislamu. [49]

Baadhi ya kanuni za kifiq’hi, kama vile kanuni ya Nafyu Sabeel (Kukataa Njia) na Sadd al-Dharai’i (Kufunga Njia za Haram), zimekuwa miongoni mwa misingi ya kuhalalisha maoni dhidi ya kujifananisha na makafiri. Imeelezwa kwamba; maana ya "Sabeel" katika kanuni ya Nafy Sabeelni pana mno, ambapo ueneaji na kushamiri kwa tamaduni za makafiri kunachukuliwa kama ni miongoni mwa mifano ya Sabeel (njia) za utawala wa makafiri. [50] Aidha, marufuku ya kujifananisha na makafiri inaendana na kanuni ya Sadd al-Dhara’i, ambayo inalenga kufunga njia zinazoweza kupelekea vitendo vya haramu, kama vile utegemezi wa kuwategemea makafiri, kudhoofika, kudhalilishwa, na kupoteza hali ya kujiamini kwa Waislamu. [51]

Rejea

Vyanzo