Kujibari na washirikina

Kutoka wikishia

Kujiweka mbali na washirikina (Kiarabu: البراءة من المشركين في الحج) ni miongoni mwa mambo ambayo hufanywa na mahujaji wa Kiirani katika ibada ya Hija. Katika marasimu hayo, mahujaji sambamba na kutoa nara dhidi ya Marekani, Israel na kuwataka Waislamu kuungana na kuwa kitu kimoja huandamana pia.

Kujibari na washirikina (kujitenga na washirikina) ni amali ambayo chimbuko lake ni Qur’an tukufu na ina msingi wa kifikihi na kwa mara ya kwanza ibada hiyo ilifanywa baada ya Fat’h Makka (kukombolewa Makka) ambapo kwa amri ya Mtume (s.a.w.w), Imamu Ali (a.s) alisoma Aya za Baraa (za kujitenga na washirikina). Katikka zama hizi, kujibari na washirikina kwa mara ya kwanza kulifanyika mwaka 1358 Hijiria Shamsia sambamba na ujumbe wa Imamu Khomeini. Serikali ya Saudi Arabia ilikuwa ikipingana na suala la kufanyika marasimu haya ambapo mwaka 1366 Hijiria Shamsia washiriki wa ibada hiyo walishambuliwa na vikosii vya usalama hatua ambayo ilipelekea kuuawa na kujeruhiwa idadi kubwa ya mahujaji wa Kiirani.

Umuhimu na asili yake

Marasimu ya kujitenga (kujibari na washirikina ni ada ya kidini na kisiasa ambayo hufanywa kila mwaka wakati wa msimu wa ibada ya Hija. [1] Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran daima amekuwa akisisitiza juu ya kutekelezwa amali hii ili upande wa kisiasa wa ibada ya Hija uhifadhiwe na kubakia. [2]

Marasimu haya hufanyika kwa lengo la kutangaza kujibari na kujiweka mbali na siasa za kibeberu za makafiri na washirikina na kulingania umoja wa Waislamu kwa minajili ya kukabiliana nao. [3] Suala la kuwakataa washirikina na kujitenga nao limeashiriwa katika Aya kadhaa za Qur’an zikiwemo: Aya ya 4 Surat al-Mumtahinah, [4] Aya ya 1-3 katika Surat Tawba na Aya ya 19 Surat al-An’am. Aya hizi zinaashiria vyema jambo hilo. [5]

Kwa mara ya kwanza kujitenga na washirikina kulifanyika baada ya Fat’h Makka (kukombolewa Makka). [6] Baada ya Mwenyezi Mungu kushusha Aya za Baraa (kujiweka mbali) yaani Aya ya 1-10 za Surat Tawba alimtaka Mtume (s.a.w.w) atangaze kujibari na kujitenga na washirikina. Imamu Ali (a.s) alifikisha ujumbe wa Aya hizi katika msimu wa ibada ya Hija wa mwaka wa 9 Hijiria. [7] Imeelezwa kuhusiana na sababu ya kushuka imeelezwa kwamba, washirikina walikiuka mkataba wa makubaliano katika Suluhu ya Hudaibiya waliofikia na Mtume (s.a.w.w) kwamba, wangewaachia wazi Waislamu mji wa Makka kwa muda wa siku tatu kwa ajili ya kutekeleza ibada ya Hija. [8] [9] Katika Tafseer Nemooneh suala la washirikina kukiuka mara kadhaa mkataba limezungumziwa. [10]

Ili kupata taarifa zaidi kuhusiana na haya angalia: Kufikishwa Aya za Baraa (kujitenga).

Namna ya kutekeleza

Baina ya miaka ya 1358 mpaka 1366 Hijiria Shamsia, mahujaji wa Kiirani na baadhi ya mahujaji wa mataifa mengine, walikuwa wakikusanyika katika sehemu maalumu mjini Makka kabla ya kuanza ibada na amali za Hija na baada ya kusikiliza hotuba ya tathmini ya matukio ya ulimwengu wa Kiislamu na matukio ya sasa ya dunia walikuwa wakiandamana. [11]

Kuanzia mwaka 1380 Hijria shamsia na kuendelea, marasimu ya kujibari na washirika hufanyika asubuhi ya siku ya Arafa katika makao ya biitha ya Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika jangwa la Arafa, [12] kwa kupigwa nara kama “Mauti kwa Israel”, “Mauti kwa Marekani”, (یا ایها المسلمون اِتّحدوا اِتّحدوا) yaani “Enyi Waislamu! Unganeni, unganeni, na mfarakano na hitilafu ni kumfuata shetani”. Marasimu haya hufanywa na mahujaji wa Kiirani na wa mataifa mengine na hufuatiwa baada ya kusomwa Aya za Qur’an na katika kuendelea, mkuu wa biitha ya mahujaji wa Kiirani, husoma ujumbe wa Kiongozi wa Jamhuri ya Kiislamu kwa mahujaji kwa lugha mbili za Kifarsi na Kiarabu. Mwishoni mwa shughuli hiyo, husomwa azimio na mahujaji hupiga takbira kila baada ya kipengee kimoja na hivyo kuunga mkono. [14]

Msingi wa kifikihi

Inaripotiwa kwamba, katika ibada ya Hija katika vipengee vyake mbalimbali kuna marasimu ya kutangaza kuwakataa na kujitenga na washirikina. Ramiu al-Jamarat na Talbiya (kutamka labayka) ni miongoni mwa amali na ibada za dhahiri za marasimu haya ambapo ndani yake kuna kujitenga na kujibari na washirikina. [15] Imamu Khomeini (r.a) katika kubainisha kujibari na washirikina anaitambua marasimu hii kwamba, ina mtindo tofauti tofauti ambapo hutekelezwa kulingana na zama. Ni kwa msingi huo, ndio maana anaona kuwa katika msimu wa Hija na katika Haram ni wakati na eneo bora kabisa la kutekeleza ibada hii ya kujibari na washirikina, kwani katika hali hii jambo hili litakuwa na taathira zaidi. [16] Imamu Khomeini anatumia hoja ya tawalli (Kumtawalisha Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul-Bayti wake watoharifu) na Tabarri (kujiepusha na kujitenga na adui zao) kama nukta za kuthibitisha hilo. [17]

Baadhi ya Ahlu-Sunna wanatilia shaka marasimu ya kujitenga na washirikina kwa kuzingatia kupigwa marufuku suala la mjadala katika Hija na mkabala wake, mafakihi wa Kishia wanaitambua ibada hjii ya kujibari na washirikina na muundo wake jumla kwamba, sio mjadala ambao unapelekea kuibuka hasama kwa Waislamu. [18]

Historia yake kwa ufupi

Imeripotiwa kwamba ada hii haikuwa ikitekelezwa katika ibada ya Hija kabla ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran. [19] Imam Khomeini ametajwa kuwa muhuishaji wa ada na sunna hii ya kujibari na washirikina katika msimu wa Hija ambaye alitekeleza ibada hii katika msimu wa Hija. [20] kwa muktadha huo, Imamu Khomeini anatajwa kama muanzilishi wa siku ya kujibari na kujitenga na washirikina. [21]

Hija ya damu

Makala kuu: Hija ya damu

Serikali ya Saudi Arabia imekuwa mpingaji wa kufanyika kujibari na kujitenga na washirikina katika vipindi tofauti. [22] Mnamo mwaka 1366 Hijiria Shamsia, baada ya mahujaji kupanga kuondoka kwenye marasimu ya kujibari na washirikina na kwenda kwenye Msikiti wa Makka, walishambuliwa na polisi na vikosi vya usalama vya Saudi Arabia. Katika tukio hili, zaidi ya mahujaji 500 waliuawa na wengine mia saba walijeruhiwa. [23] Baada ya tukio hili kuanzia mwaka 366 Hijria Shamsia, marasimu haya yalizuiwa kufanywa hadi 1369 Hijiria Shamsia; lakini tangu 1370 Hijria Shamsia marasimu ya kujibari na kujitenga na washirika yamekuwa yakifanyika Mina na Arafa. [24]

Monografia

  • Kitabu cha “Mabani Dini Va Siyasi Baraat az Moshrikan (Misingi ya Kidini na Kisiasa ya Kujibari na Washirikina) mwandishi: Javad Varei. Kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha ya Kiajemi. [25]

Rejea

Vyanzo