Kuishi kinyumba

Kutoka wikishia

Kuishi kinyumba (White Marriage au Cohabitation) (Kifarsi: ازدواج سفید) ni aina ya mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanaume na mwanamke ambayo yako nje ya misingi na sheria za ndoa. Katika utamaduni wa Kiarabu aina hii ya mahusiano inafahamika kwa jina la "kuwa pamoja". Kwa mujibu wa wanazuoni wa fikihi wa Kishia aina hii ya mahusiano ni haramu na kisheria haihesabiwi kuwa ni ndoa; kwani hayajatimiza masharti ya lazima ya ndoa kama kusomwa tamko la kufunga ndoa na pande mbili hazina ahadi ya kufungamana na athari za ndoa ya kisheria kama urithi, kutoa matumizi na kukaa eda.

Katika mahusiano haya ya kuishi kinyumba kumetajwa matokeo yake kama kuongezeka khiyana (usaliti), kuongezeka mimba zisizo na mpango, kuava (kutoa) mimba na msingi wa familia kukabiliwa na tishio. Mazingira ya kutokea suala hili la kuishi kinyumba yameelezwa kuwa ni kama vile wazazi kutokuwa na usimamizi unaofaa na madhubuti kwa watoto wao na kuongezeka umri wa ndoa. Kumependekezwa pia mikakati ya kukabiliana na hili ambapo miongoni mwayo ni, kuandaa mazingira ya ndoa, kuandaa fursa za kazi na ajira na ndoa ya mut’a (ndoa ya muda).

Ndoa Nyeupe (Kuishi Kinyumba) au Kuwa Pamoja

Kuishi pamoja (cohabitation) au ndoa nyeupe (White Marriage) au kuwa pamoja ni aina ya mahusiano ya kimapenzi baina ya mwanaume na mwanamke ambayo hayachungi misingi na sheria za ndoa kama kusomwa tamko la kufunga ndoa. Aina hii ya mahusiano inajulikana pia kwa jina la «kuwa pamoja» na «uhawara» . [1] Katika utamaduni wa Kiarabu aina hii ya mahusiano inafahamika kwa jina la «kuwa pamoja» (cohabitation). [3]

Tofauti Yake na Ndoa ya Kisheria

Ndoa nyeupe au kuishi kinyumba ina tofauti nyingi na ndoa halali na ya kisheria. Kwa mfano kusoma tamko la kufunga ndoa, kuainisha mahari, kuchunga suala la eda, idhini ya Walii kwa ajili ya kuolewa binti ambaye ni bikira ni miongoni mwa masharti ya ndoa ya kisheria na ya halali ambayo hayapo katika ndoa nyeupe au kuishi kinyumba. [4] Kadhalika ndoa ya kisheria ina athari kama kurithiana mume na mke, mahari, kutoa matumizi na kadhalika ambayo hayya hayamo kwenye kuishi kinyuma. [5] Kadhalika katika nikaha ya Muatati pia tamko la nikaha halisomwi bali tangazo la ridhaa ya nikaha linaonekana kupitia masuala mengine kama kuandika au kuashiria. [6]

Historia Fupi

Kuishi kinyumba (White Marriage) kunakoshuhudiwa katika jamii za Kiislamu inaelezwa kuwa jambo hilo limeathiriwa na jamii za Kimagharibi. [7] Inaelezwa kuwa, mwishoni mwa muongo wa 1960 kulitokwa mabadiliko katika Ulaya na Marekani ambayo yaalifahamika kama «Mapinduzi ya Kijinsia» (sexual revolution) ambapo ndani yake kukapatikana uhuru wa kingono na kutokea upotofu mwingi. Kuwa pamoja au uhawara ni moja ya mambo yanayohesabiwa kuwa yaliibuka na kuenea hatua kwa hatua katika jamii zingine ikiwa ni taathira ya mapinduzi haya ya kingono. [8]

Hukumu ya Fikihi

Kwa mujibu wa nadharia na maoni ya wanazuoni wa fikihi wa Kishia, ndoa nyeupe au kuishi kinyumba ni haramu na ni zinaa. [9] kwa mujibu wa fat’wa iliyotolewa mwaka 1397 Hijiria Shamsia na Mrajii Taqlidi kama Khamenei, Makarim Shirazi, Noori-Hamedani, Ja’far Sobhani, Shubair Zanjani na Safi Golpaygani, waliiharamisha ndoa hii. [10]

Baadhi wakitegemea kifungu cha 1062 cha sheria ya kiraia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambayo ndani yake imebainishwa wazi sharti la tamko la nikaha katika ndoa, wanaitambua ndoa hii kuwa, si ya kisheria. [11]

Sababu, Matokeo na Mikakati

Hitajio la kukidhi matamanio ya kijinsia, kutokuweko usimamizi wa familia kwa mienendo ya watoto wao na kuwafukuza na kuongezeka umri wa ndoa kwa mabinti ni miongoni mwa mambo yanayotambuliwa kuwa sababu ya ndoa nyeupe au kuishi kinyumba. [12] Kadhalika kuishi kinyumba kuna matokeo ambayo yamebainishwa ambayo ni:

  • Kutishia misingi ya familia. [13]
  • Kuongezeka mahusiano haramu, mimba zisizo za kupanga na kutarajia na kuava (kutoa) mimba. [14]
  • Kupungua uzaaji na kutotambuliwa rasmi watoto watarajiwa na kuwa na hatima isiyofahamika. [15]
  • Kuongezeka takwimu za talaka. [16]
  • Madhara ya kinafsi kama uraibu. [17]

Kumependekezwa pia mikakati ya kukabiliana na hili ambapo miongoni mwayo ni, kuandaa mazingira ya ndoa, kuandaa fursa za kazi na ajira na ndoa ya mut’a (ndoa ya muda) ili kupunguza tatizo hili la kijamii. [18]

Rejea

Vyanzo